
mangariba wakiapa kuachana na ukeketaji
vifaa vya ukeketaji vya ngarbia walioacha shughuli hiyo...
Kwako Bwana Michuzi,
Nimefurahi sana kuona picha yako na wanaharakati wa kupiga vita Ukeketaji, na nimefarijika sana kuwa kumbe upo nasi katika gurudumu hili la kutokomeza mila hii. Masikitiko yangu ni kwa wadau ambao wanasema "ukeketaji ni mila tuwaache wenye mila waendelee".
Mimi napenda kujulisha kuwa hadi sasa idadi kubwa ya mangariba, wamesharudisha zana zao kama hizi ninazokuletea hapa.Naomba wadau tuzidishe mapambano hali bado ni mbaya Tanzania - 15% ni aibu sana.
Takwimu za nchi zinaonyesha;
Mkoa wa Manyara - 81%,
Dodoma - 68%,
Arusha- 55%,
Singida-43%,
Mara-38%,
Kilimanjaro- 25%,
Tanga -23%,
Iringa-23%,
Morogoro-18%,
Tabora-3%,
Pwani-2%,
Lindi-1%,
Mtwara-1%,
Ruvuma-1%,
Mbeya-1%,
Kigoma-1%,
Shinyanga-1%,
Mwanza-1%,
Kagera-1%,
Dar es Salaam - 1%,
Rukwa-1%.
Kuna madhara mengi sana yatokanayo na mila hii. Kwa sababu ni jambo la sehemu za siri ni vigumu watu kuanika hadharani lakini ninapicha moja inayoonyesha kuota kwa "Keloid" uvimbe sehemu ya siri pale palipokatwa, uvimbe kama ule wa watu wanaotoboa masikio nadhani unaujua. Naogopa kuweka hiyo picha kwenye blog isije ikaleta soo kwa wanaharakati wengine wa maswala ya wanawake kuwa namdhalilisha mwanamke mwenzangu. Hiyo picha ni ya kweli na huyo muathirika alifanyiwa upasuaji kwani sehemu hiyo ilikuwa inakuwa siku hadi siku. Na tunapokea kesi kama hizo sana na tunawasaidia kwenye upasuaji.
Wadau wanaopenda kusoma vitabu, wasome "Do they hear you when you Cry", Desert Flower na vingine vingi nitawaandikia siku nyingine.
Mdau mpigavita ukeketaji



Kaazi kweli kweli. Ndio maana baadhi ya nchi za jirani wanatuonea gere. Mfano Congo wakati wao wanahangaika kukusanya silaha toka kwa waasi sisi tunahangaika kukusanya vifaa vya ukeketaji toka kwa mangariba.
ReplyDeleteHeheheheee.. Tanzania utaipenda tu!
Jamani Michuzi naomba niwasiliane nao kwani kazi wanayofanya tunahitaji kuwa nao bega kwa bega
ReplyDeleteMbona bibi zetu walikeketwa na hakukuwa na matatizo yoyote?
ReplyDeleteuliotoa coment no.3 huna huruma au ujui nini maana ya kukeketwa,mambo hayo yashapitwa na wakati,zaidi kutesa tu watoto za watu,hata ktk uzazi wanawake waliokeketwa wanapata shida sana.ni vizuri sana hizo mila zifutwe.hazina maana.
ReplyDeleteDu! sikujua Tanga nao wako juu namna hiyo, ila inawezekana waliohesabiwa wamekuja na mila hizo toka pengine!!! inasikitisha.
ReplyDeleteTatizo ni kwamba wanaopinga kukeketwa hawana sababu za msingi za kupinga zaidi ya kusema ni mila mbaya na imepitwa na wakati. Na athari wanazotoa kwa mfano hiyo ya kuvimba kama yule anayetoboa skio inatokea kwa nadra sana na kwa mtu mmoja mmoja sana.
ReplyDeleteHakuna kitu kisichokuwa na side effect lakini kama side ifekti za kukekete ni za kujitungia, hii haisaidii wana harakati wala wakeketwaji. Kama kutoboa maskia kunasababisha uvimbe kwenye maskio mbona huko kutoboa maskio hakupigwi vita? Jamani enendeni pole pole na tamaduni za watu.
Nilishasema kwene bulogi zingine nitasema hapa pia kwenye kukeketwa kinachofanyika sio kukekete tu, kuna vitu vingine vinafanyika huko. Kwa wakurya kwa mfano ukikeketwa manake ndio umevuka utoto kwenda utu uzima. Ndio mana wanaita jando na unyago! huko wanaume wanafundishwa kutunza familia zao na akina dada halikadhalika. sasa unapowaaambia watu wastop kukeketa manake unawaambia wastop hio yoote.
Fanyeni risechi kabla ya kudandia mambo, wapeni mbdala wakutimiza malengo yao, wapeni kilichobora kuliko wanachokifanya sasa ivi, wasaidieni kusomesha watoto wao, the more educated they get the easier it will be not to practice some stuff! sasa zaidi ya kuwaaambia wasikekete ni kitu gani mmewafanyia zaidi ya dharau tu????
Tatizo ni kwamba wanaopinga kukeketwa hawana sababu za msingi za kupinga zaidi ya kusema ni mila mbaya na imepitwa na wakati. Na athari wanazotoa kwa mfano hiyo ya kuvimba kama yule anayetoboa skio inatokea kwa nadra sana na kwa mtu mmoja mmoja sana.
ReplyDeleteHakuna kitu kisichokuwa na side effect lakini kama side ifekti za kukekete ni za kujitungia, hii haisaidii wana harakati wala wakeketwaji. Kama kutoboa maskia kunasababisha uvimbe kwenye maskio mbona huko kutoboa maskio hakupigwi vita? Jamani enendeni pole pole na tamaduni za watu.
Nilishasema kwene bulogi zingine nitasema hapa pia kwenye kukeketwa kinachofanyika sio kukekete tu, kuna vitu vingine vinafanyika huko. Kwa wakurya kwa mfano ukikeketwa manake ndio umevuka utoto kwenda utu uzima. Ndio mana wanaita jando na unyago! huko wanaume wanafundishwa kutunza familia zao na akina dada halikadhalika. sasa unapowaaambia watu wastop kukeketa manake unawaambia wastop hio yoote.
Fanyeni risechi kabla ya kudandia mambo, wapeni mbdala wakutimiza malengo yao, wapeni kilichobora kuliko wanachokifanya sasa ivi, wasaidieni kusomesha watoto wao, the more educated they get the easier it will be not to practice some stuff! sasa zaidi ya kuwaaambia wasikekete ni kitu gani mmewafanyia zaidi ya dharau tu????
Unayesema "bibi zetu walikeketwa" Please speak for yourself. Bib yangu hajakeketwa na wala hii haipo kwa jamii ya wengi. Ni wachache wanaokeketwa na maddhara kama anavyosema huyo hapo juu watu hawaeki hadharani. Na pia wanawake wengi wanakufa wakijifungua na kwa vile ni vijijini hamna anayesema kilichosababisha mtu huyo asijifungue. Inakua hamna takwimu maalumu.
ReplyDeleteKama alivyosema huyo hapo juu ni muhimu kuwasupport hawa watu wanaojitahidi kuzuia haya mambo.
We anony wa juu, umekatwa, kama dume basi dada zako au mamio amekatwa, au wewe ni tasa, wacha kuzidi kuharibu watu wakati wenzako wanafight kuwaelimisha.
ReplyDeleteUnajua kama, hata watoto wanasoma hapa kwa Michuzi.
INAONEKANA HUKO KASKAZINI WASICHANA WENGI WEMEKEKETWA NIKIANGALIA REKORD HAPO HALI INATISHA SANA DAH.
ReplyDeleteHii mila mi naisapoti maana dada zetu nyege zimewazidia. Hii mila inaweza kupunguza kasi ya kuenea ukimwi.
ReplyDeleteSidhani kama mila inatelekezwa kwa kura!
ReplyDeleteCulture is a function of time. Ziache tu zitaisha zenyewe.
Mimi pia naisupport hii mila kwa asilimia 100%. Kwa kweli tunakoelekea dada zetu wanakuwa promiscuous kama mabinti wa ulaya. Kisa ni nini? Nyege zinawazidi. Cha hatari zaidi ni mazingira yetu ya ngono sio salama na maambukizi yanakuwa kibao na watu wanakufa wakiwa bado vijana. Wakikeketwa wanakuwa wavumilivu zaidi. Mbona Bibi na Mama zetu walikeketwa na wametuzaa bila matatizo - tena wengine tumezaliwa hata kumi na ndoa zao zimedumu hadi leo. Siioni sababu ya msingi ya kufuta hii mila.
ReplyDeletendoa za bongo zinadumu sababu ya uvumilivu "ujinga" wa wanawake kukubali kila utumbo mwanaume anafanya bora tu analeta mkate nyumbani.
ReplyDeletewith time itakwisha
Naanza na wewe unayesema BIBI YAKO HAKUTAHIRIWA???Are you crazy??Una uhakika gani au ulimchungulia wapi na siku gani.Acheni mambo msiyoyajua.UKEKETWAJI NI JAMBO BORA SANA NA LINA FAIDA KUBWA KWA JAMII HUSIKA.
ReplyDeleteWewe unayesema ukikeketwa una sababisha vifo na ndo maana wazazi wengi waliokeketwa ufa wakati wa kujifungua,UNA UHAKIKA???Angalia rekodi hapo juu.Mikoa inayoongoza kwa vifo vya kina mama wakati wa kujifungua ni Shinyanga,mtwara,Lindi na Rukwa.Mbona kwa idadi ya ukeketwaji mikoa hiyo ina asiimia 1 tu???Yani ina maana HUJUI SABABU ZINAZOSABABISHA KINA MAMA KUFA WAKATI WA KUJIFUNGUA???
Ok kama ni maumivu,ni yupi anaepata maumivu makali zaidi kati ya hawa,aliyetoga KITOVU,ULIMI,MDOMO WA CHINI,KWENYE NYUSI,PUA,ACHA SIKIO NA aliyekeketwa???NB siku hizi hata hicho kiharagwe kinachokatwa nacho hutogwa na kuvishwa hereni.Sasa tusemeje???
Mnaopinga ukeketaji tupeni sababu za kupinga kwenu siyo kupiga kelele tu.
Mimi nasapoti ukeketaji uendelee.
jamani sasa hawa watu wanaokwenda mamtoni na kujiripua eti wamekimbia kukeketwa sasa sijui watadanganya vipi ikiwa haya mambo yapo wazi haya kazi kwao!!!!!!
ReplyDeletenakuunga mkono mtoa maoni hapo juu Monday, October 15, 2007 11:56:00 PM EAT.
ReplyDeleteHEBU ANGALIENI HIZO STATISTIC HAPO JUU NA ANGALIA NI WAPI AU MIKOA IPI WANAPENDA SANA NGONO.UTAGUNDUA KUWA ILE MIKOA YENYE ASILIMIA NDOGO YA KUKUKETWA NDIO WANAWAKE WAO WANAPENDA SANA NGONO YAANI HATA UKIOA UJUE WATAKUCHAPIA TU.NADHANI MILA YA KUKEKETWA INASAIDIA KUPUNGUZA NYEGE WANAWAKE JAPO INAMADHARA KWA UPANDE MWINGINE.MIMI NADHANI HII MILA INGEBORESHWA TU BADALA YA KUPIGWA VITA MOJA KWA MOJA.
MKE WANGU AMETOKA KULE "WANAONGOZA KWA...".
MICHAEL MWAKALITOLO,
DOHA, QATAR
kukeketa soo, sasa hawa mabinti uloda wataupatia wapi wakipigwa kipala?
ReplyDeleteHAPA WAATAALAM WALITAKA KUUZA MIKASI NA DAWA ZA HOSPITALINI,ILI WATUTAHIRI SISI WANAUME..KWAHIYO WAGANGA WA JADI WAKAKOSA DILI..HOO NYUMBA ZA MAKUTI SIO NZURI MBONA HOTELI ZINAEZEKWA KWA MAKUTI...TUWE MAKINI JAMANI KUNAWIMBI LA "..GREEN ENERGY(GO GREEN).." SIO BAYA LAKINI TULIANGALIE KWA MAREFU NA MAPANA "..KUMBUKENI KWAMBA NCHI NYINGI MASKINI ZIMEGUNDUA MAFUTA NA WATU WAMESHA JANJARUKA WANATAKA MAENDELEO YA KWELI.." NDIO MAANA WANAHUBIRI "...GREEN ENERGY (GO GREEN).." KILA KUKICHA.. WAO WASHATUMIA SAANA NA WAMEENDELEA KUTUTAWALA BILA "..GREEN ENERGY(GO GREEN).." UKITAKA UWACHOKOZE WAAMBIE TANZANIA TUNAMPANGO WA KUWA NA NYUKLIA KWA MATUMIZI YA UMEME (ENERGY) WEWE..UGOMVI BWELELE NA MISAADA YOTE WATAFUNGA..UKAME UKITOKEA TU, UMEME WA MGAO TUNARUDI KULEKULE NA VIBATARI VYA MOSHI. "GO GREEN" ...TH!$ !$ B**$H!T.
ReplyDeletekweli lakini, wanatafuta gear tu ya kuingilia, watakuambia usiweke ndonya ni kinyume na haki za binaadamu and so and so......
ReplyDeletekukeketa ina madhara yake teana mabaya.Mwanamke kila siku nimechoka;hana hamu ya kutoa penzi(na ni mke ktk ndoa hivyo).Mpaka na ngumi anaweza akakutandika ilimladi usimguse.Mwanaume utakuwa wa msimu mpaka siku mwanamke ajisikie mwenyewe kufanya tendo la ndoa.Mkavu kama mti,analala tu hapo kama gogo. Mwanaume lijali umeumia ukikutana na aliekeketwa na ndoa itakuwa na mifarakano.Aliekeketwa asilimia kubwa wanapata hata matatizo ya kufunguka njia wakati wa kuzaa inaishia wajifungue kwa "operation". Sasa iweje msapoti kukeketwa jamani,elimikeni manaosupport hii ujinga.
ReplyDelete