
siku mwili wa baba wa taifa ulipokuwa unarejeshwa nchini toka london alikofia siku kama ya leo, niliamua kujibanza juu ya daraja la manzese ili kupata picha ya msafara pamoja na wadau waliosimama barabarani. nashukuru azama yangu hiyo ilifanikiwa. je mdau unakumbuka ulikuwa wapi siku hii na ulikuwa unafanya nini?


Wengine tunamkumbuka Mwalimu kwa mchango wake mkubwa katika kuongoza serikali (kabla ya/na kufuatia uhuru), hususani katika sekta ya elimu nchini wakati huo.
ReplyDeleteIsingekuwa yeye kuona mbali, pengine, wengi wetu tusingeweza kupata bahati tuliyo nayo leo. Kwa mfano:
Kaondoa ubaguzi wa rangi na dini mashuleni hata kabla ya uhuru.
Katoa Mtihani wa Darasa la Nane (Territorial Standard Eight) ili wanafunzi wengi waingie sekondari.
Karuhusu wanafunzi wa Darasa la Saba kujaribu Mtihani wa Darasa la Nane na washindapo waingie sekondari.
Kapunguza miaka ya Elimu ya Msingi kuwa saba badala ya minane ili wanafunzi wengi waingie sekondari.
Kaongeza “streams” mbili kwa kila darasa la shule ya sekondari (za serikali).
Katoa Mtihani wa Darasa la Kumi (Territorial Standard Ten) ili wanafunzi wengi waingie Darasa la Kumi na Moja.
Karuhusu wanafunzi wa Darasa la Kumi na Moja kujaribu Mtihani wa Darasa la Kumi na Mbili (Cambridge School Certificate - Ordinary Level) ili washindapo waingine High School.
Karuhusu wanafunzi wa Darasa la Kumi na Mbili kujipima kwa Mtihani wa “Mock” ili wawe tayari kwa Mtihani wa Darasa la Kumi na Mbili (Cambridge School Certificate - Ordinary Level).
Kapunguza karo ya shule kwa elimu ya sekondari kuwa 960/-.
Karuhusu wanafunzi wenye akili wamalizao Darasa la Kumi na Mbili wasingojee matokeo ya Cambridge School Certificate - Ordinary Level (mwezi wa Februari) waingie moja kwa moja (pre-selection) kuanza masomo shule za sekondari zifunguliwapo mwezi Januari.
Karahisisha wanafunzi wa High School (Cambridge School Certificate - Ordinary Level) kuingia Chuo Kikuu kama wameshinda “Principal” moja na “Subsidiary”.
Kaendeleza elimu ya watu wazima (kisomo cha ngumbaru).
Kaleta Jeshi la Kujenga Taifa.
Kajenga chuo kikuu cha kwanza (Dar es Salaam University College) ingawa hakikuwa na majengo yake, TANU ilitoa jengo lake hapo Lumbumba Street kuwa "campus" ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwalimu, mtoto mpendwa wa Tanzania na Afrika, hadithi yako itabaki siku zote!
Endelea kupumzika hapo nyumbani Mwitongo, huku ikifikiria jinsi ulivyokuwa unawataifisha kwa manufaa ya umma wahujumu wa uchumi na wakiukaji wa maadili ya uongozi!
mithuo hujambonji kalale bwana ,mainanihii anaveitiii!!!
ReplyDeletekaka Michuzi
ReplyDeleteMimi nakumbuka siku ya kumuaga kanisani, mjini London nikiwa masomoni wakati huo, Mwalimu wa Taifa letu alipokuwa amelala katika nyumba yake ya milele. Kwa kweli sitamsahau, isitoshe mie ni mmoja wa watu tulioishi karibu nae huko Mikocheni/msasani tangu miaka ya 80s. Enzi hizo tukisema twaishi huko watu walikuwa wanatuonea kama mmhh hawa watu wapo nje ya mji sasa ni the hot hot hot area in dar. U name it kipo. Nafurahia kuwa eneo letu limekuwa kama city fulani, natumaini ataangalia na kuchekelea akiona jinsi eneo letu lilivyoendelea
MAY HIS SOUL REST IN PEACE
R.I.P AMEN
ReplyDeleteNakumbuka siku hiyo nilikuwa nyumbani kama sikosei ilikuwa weekend au ilikuwa siku ya mapumziko ili kupokea mwili wake. Nilikuwa nikifuatilia kupitia TV muda wote ghafla TV ikapata shoti nilichanganyikiwa kidogo ila msafara wake haukuwa mbali na nilikuwa naishi maeneo ya Ubungo Bakwata karibu kabisa na kituo cha daladala basi nikajisogeza barabarani. Jua lilikuwa kali sana ia watu walikuwa wengi wamesimama kandokando ya barabara wakiimba 'parapanda italia'.
ReplyDeletePunde gari lililobeba mwili wa Marehemu Nyere likapita vilio vilitanda barabarani sijawahi kuona maana si kina mama waliokuwepo bali hata kina baba waliangua vilio. Ilinisikitisha sana ila utafanyaje, ya Mungu mengi. Na niliporudi nyumbani nikajaribu kuwasha TV na likawaka mpaka leo sijui nini kilitokea ila ninachojua I am technologically challenged.....yawezekana TV ilienda kwenye standby basi mshamba nikahangaika weeeee!!! ikabidi nishule barabarani tu. anyway life always has humour to something sad.
"...Zidumu Fikra Sahihi za Mwenyekiti wa CCM"
ReplyDeleteNilikuwa likizo Tanzania siku ambayo nilikuwa nikirudi shule london ndio nilipata Taarifa wakati niko Saloon natengeneza nywele nikasikia habari ilisikitisha sana nchi nzima ilikuwa na uzuni
ReplyDeleteNakumbuka siku hii vizuri sanaa, nilikuwa Tambaza high school, tuliitwa wote na mwalimu mkuu Mr Kaaya enzi hizo akatuambia tunatakiwa kwenda karibu na salander bridge mitaa ya ocean road...huko tulikutana na shule zote zilizo jirani na wanyewe walikuwepo kama shabaan robert ,azania, muhimbili...ilikuwa inatilisha huruma sanaa, wanafunzi wengi walijawa na nyuso za huzuni na wengine kulia+ wengine walikuwa na viji redio walitoka navyo nyumbani ili wafwatilie habari za mwalimu.Sitaisahau hii siku..na sijawahi kuona mkusanyiko wa watu kama huuu....kwa kweli baba wa taifa ...alikuwa ni zawadi kutoka kwa mungu..
ReplyDeleteRest in Peace mwalimu.
Nakumbuka mbali kweli kipindi hicho nipo chuo kikuu nakunguta mwaka wa pili pale Solomon Mahalangu campus, ndani ya unit 2 sijuhi baso wanazihita units (hostel) au la? Kipindi hicho tukiwa tunafaidi matunda ya Taifa kwa kupewa hela nafikiri 1500 kwa siku huku tukilamba mikwanja ya faculty requirements, long field practicals, stationaries etc sasa nasikia kuwa wadogo zangu hawapewi hela! Ndugu yangu we acha tu.....hii yote ilikuwa ni falsafa ya Nyerere ya Elimu kwa woote! sasa JK na timu yake wanaona upuuzi mtupu, huku wakiimiza shule zaidi zijengwe za sekondari, sasa hao wahotimu wataenda wapi? au ndo elimu ya watanzania itakuwa ni kuishia sekondari huku University ikionekana kituo cha police ahaha!
ReplyDeleteYangu macho!
Duh umenikumbusha mbali kidogo Issa. Kipindi hicho cha msiba nilikuwa ndio namalizia form six Kibaha Sec. Basi nilitafuta muda nikakamata Kipanya toka Tumbi hadi Ubungo ambako kwa bahati nikakutana na huo msafara wa Mwalimu ukipita kuelekea Uwanja wa Taifa. Mi nikamuagia hapo hapo. Ilikuwa siku maalumu pia kwangu kwa sababu ni junction hiyo hiyo ya Mandela Rd na Morogoro Rd ambapo nilimuona Mwalimu laivu kwa mara ya Kwanza mwaka 1990 alipopita na Mzee Mandela kufungua bara bara ya Mandela.
ReplyDeleteAlale pema peponi, Amina.
Michuzi,
ReplyDeleteI was on my fancy balcony in Urafiki flats along Morogoro road...the city was completely and deadly silent as the motorcade was slowly crwaling to Msasani!...You could hear even the heartbeat of a distant person...it was really realy a sad and sorrowful moment I had ever witnessed!
Tanzania has lost a great man in its history!
Nilikuwa hapa the greater London,nakumbuka hata hospitali nienda kumuangalia katika siku zake za mwisho tukiwa na watoto wake Madaraka na Makongoro.
ReplyDeleteRIP JKN-Utakumbukwa daima na watanzia wote.
CHA CHANDU- UK
Michuzi,
ReplyDeleteWith tears in my eyes
I still remember, when I got my form-one joining instruction without a follow-up in a remote area though I lived hundreds of kilometres from the nearest post office
I still remember that my poor parents were not obliged to pay anything like a school fees or any other expenses whatsoever except the pair of uniforms instructed to be bought,
I still remember that I had not to carry my own mattress to school,
I still remember free exercise and text books in the library and how we worked hard without tuitions and photocopy machines,
I still remember the warrants I used to travel with to and from a boarding secondary school in a far end of the country from where I was born,
I still remember the train wagons and buses booked for students during the terminal and annual holidays,
I still remember the unity existed among the school students regardless of the family status, religion, race and social background as I was not aware of the difference between John and Abdallah,
I still remember how we were proud of our beautiful country and sang a lot of songs of praises,
I still remember the colouful inter-school sporting events from the primary level to the secondary level, form which many young men and women became champions in out country,
I still remember a lot!
Well, time has changed and people too!...all changes are inevitable in any process of development in a society, but let us ask ourselves, are we changing to the positive side of negative side?...The answer is obvious!
To some of us Mwalimu will always remain in our hearts forever and ever and we have to convey the massage loud and clear to the next generation!
Our leaders should, therefore, understand that the cost of forgetfulness is too high to be paid by our grandchildren!
Kimori
Hakika ilikuwa siku ya uzuni kiasi sina maneno mazuri yakuelelezea tukio hilo.
ReplyDeleteNakumbuka nilikuwa nipo Musoma.Nakumbuka mji ulikuwa na uzuni sana.
Kwa kuwa nilikuwa masomoni nakumbuka,nilisitisha masomo na kuingia maeneo ya bara bara ya mkendo ndio nilikuwa natazama tukio kwenye Runinga katika moja ya hotel.
Hakika mwalimu aliliza watu.Nilishuhudia watu wakibubujikwa machozi wakati tukitazama tukio la mwili kuwasili.
Hakika mwalimu alikuwa mtu wa watu.
Leo hii umebakia unafiki wa wanasiasa kujifanya wanamuezi wakati hawaendani kabisa na yale aliyokuwa anaamini.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya hayati baba wa Taifa mahali pema peponi.Amina
Dear Michuzi,
ReplyDeleteWako wengi ambao hawajui uchungu ilikuwa siku mbaya mno kwa sisi tuliokuwa nyuzirum manake ni lazima uwapatie watu kitu ambacho kweli ni histori na uhakika wa histori kwa kuwa tulikuwa tunatengeneza history. Here comes the great stateman, lying in a coffin.. To people who loves him, who knows him it was real sad; and to us he is still living... I wish our leaders today can look back and say Hi guys we are moving out of the tracks.. God please mweke mahali pema peponi na kama umeshaingia peponi please tuombee hapa moto unawaka ingawa hatuungui kubaki majivu,watawala si tu wanapaniki wanatuwashia moto unaoweza kutuletea madhara wamelitupilia mbali azimio la arusha,hasa kipengele cha kiongozi kutochuma utajiri.wanapata wapi mapesa yote haya katika nchi ambayo ni maskini?
mimi mdau nisiyependa jina langu litoke lakini nipo dar
Hii kitu ilinichelewesha kula pipa la kuja huku dah,im still remeber this day when wr were told to wait for the msafara wa marehemu baba wa taifa na mimi nataka nikamate ndege.
ReplyDeleteIlikua tabu sana maana si mnajua tena utamu wa ulaya.
Nilikua naona kama nachelewa mbingu.
Mlazeni baba yetu maala pema peponi one day we gonna meet again but that day i was goin mtoni baba nisamehe.
Thank.