Home
Unlabelled
kcb
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mimi sina uchoyo wa mawazo wacha nitoe mawazo yangu kwa faida ya yeyote.
ReplyDeleteKuanzisha benki nje ya nchi rahisi mno ili mradi uzalendo uwepo.
Utafiti unaotakiwa ni tu kujua kwanza raia wengi wako mji gani na nchi gani?
Labda nitoe mfano wewe ni mhindi unataka kuanzisha benki ya India nchini Uingereza unachotakiwa kufanya ni ubalozi wa India au viongozi wa jumuiya za wahindi kuhamasisha wahindi na kampuni zao walioko Uingereza kuweka pesa kwenye hiyo benki ya India inayofungua tawi Uingereza.
Ukitaka pia kuanzisha benki ya Kenya nchnini Tanzania unaanza na wakenya walioko Tanzania na kampuni za Kenya zilizoko Tanzania kuzisghawishi kuanza kuweka pesa zao kwenye hiyo Benki ya Kenya halafu wengine watafuata bwenki inavyojitanua.
Tanzania ina watanzania wengi nchi nyingi tu na wenye makampuni huko nje.Kinachotakiwa benki ka CRDB iongee nao kupitia balozi za Tanzania iamshe uzalendo na kuwashawishi lifunguliwe tawi la CRDB kwenye hizo nchi na wao wawe uzalendo kwa kuweka pesa kwenye hizo benki.
Mtaji wa benki yoyote ile inayotaka kufungua tawi nchi nyingine ni Raia wake walioko kwenye hiyo nchi na makampuni ya raia wake walioko kwenye hiyo nchi.Hivyo unapokuwa na Raia na makampuni mengi ya raia wako nje ya nchi ndipo unapojiweka kwenye nafasi kubwa zaidi kwenye mfumo wa fedha na kibiashara wa kimataifa maana raia wako waweza pata mitaji zaidi kupitia mabenki ya nchi zao yaliyoko huko .Unashika biashara ya nchi ugenini kupitia raia wako,makampuni ya raia wako na benki zako.
Sidhani kama sheria tulizo nazo zinahamasisha watanzania kuanzisha biashara nje ya nchi.Nyingi zinahamasisha watu wa nje ya nchi kuanzisha biashara ndani ya nchi.Baadaye tutakuta nchi imejaa watu wa nje na vitega uchumi vyao na sisi waswahili tutaishia kuwa vibarua kwenye makampuni ya wageni.
Sheria zetu za kuwekeza ni za kikoloni zikiwemo za pesa za kigeni maana zinahamasisha wakoloni wa biashara na benki toka mataifa mengine waje wakati hazituhamasishi na sisi wazawa tukawe wakoloni wa kwenda kutawala nchi nyingine kwa kufungua mabiashara kwenye nchi zingine ikiwemo kununua hisa na kufungua mabenki,n.k huu ni uvunjaji haki za binadamu.Uwekezaji siyo one way traffic.Serikali imehamasisha sana wawekezaji toka nje ihamasishe sasa watanzania kwenda nje kuwekeza pia kwa kupitia marekebisho ya sheria zinazozuia hilo.
Hakuna uhamasishaji wa Watanzania kuanzisha biashara nje ya nchi kunakofanywa hivyo kwa nguvu iwe ya bunge,serikali au mahakama.
Hivi watanzania ni lini tutaruhusiwa kununua hisa nje ya nchi tukiwa nchini kwetu kwenye makampuni yenye faida ya kimataifa kisheria?
Michuzi tunashukuru blogu yako kuhamasisha benki zetu kufungua matawi nje ya nchi.Uwezo upo,raia nje wapo kinachosubiriwa sikijui.
Labda Mkurugenzi Mkuu wa CRDB DR.KIMEI atusaidie kama hilo linaezekana au haliwezekani kwa CRDB kufungua tawi walau moja nje ya nchi.Tungefurahi akitujibu kupitia blogu hii kama inawezekana.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
koloboi@yahoo.com
Hilo bango lao linatangazo kuhusu "an old customer of our new bank" hio inawezekana vipi?
ReplyDeleteKAMA WANAKUJA KUZIVAMIA BENKI ZETU HUKU HUKU SASA TUKIWAPELEKEA HUKO KWAO SI NDIO ITAKUWA BALAA ZAIDI. NADHANI ITACHUKUA MUDA SANA KWA BENKI ZETU KUWA CONVICED KUFUNGUA BRANCHES KWAO.JAMAA INABIDI WADHIBITI MAMBO YA MAJAMBAZI KWANZA.
ReplyDeleteKAKA MICHUZI GAZETI LA OFISINI KWAKO LINA SHIDA GANI LEO NI SIKU YA TATU NADHANI SI LIONI HABARI LEO ONLINE NA HATA HII YA DAILY NEWS PAGE YAKE INAONEKANA NI YA ZAMANI AU KUNA SHIDA KWENYE KU LI PUBLISH?
ReplyDeleteAnon 11.11 Acha kuuliza mambo ya ajabu,inaonakna una lack of knowledge ya markerting strategy.Adverstisement huwa zina slogan zake za kuwagfanya watu wavute attention,sasa kama wewe unaanza kuhoji Mh!!!!! unaonyesha udhaifu wako wa kwenda na wakati
ReplyDeleteHATA MIMI HUWA NAJIULIZA HIVI HII SHERIA YA KUZUIA CAPITAL FLIGHT INAMBANA NANI HASA? ISIJE KUWA NDIO SHERIA ZILIZOTUNGWA KUWALENGA WAHINDI WASIHAMISHIE FEDHA CANADA NA SASA ZINATUUMIZA WOTE?
ReplyDeleteNA SWALI KUBWA NI KWAMBA HIVI KWELI UNAWEZA KUMZUIA MTU ASIHAMISHE FEDHA ZAKE AKIAMUA??
MI NAONA NI SHERIA YA KISHAMBA
Na kweli NMB, CRDB, NBC LTD, KUWA KENYA, UGANDA NK, MMH WAZO ZURI
ReplyDeleteWaneshajua Dar kuna soko kubwa ndio maana wameweka..nahisi competition itakua kubwa kwa hiyo mtu ukifanya hapo unalipwa hela ya madafu au pombe ya mnazi. Yaani kwa mwendo wa mapenny na ndururu. Na wafanyakazi wanatokakenya au ni wa nchi yetu...isijekua wanaona visa za kufanya kazi zinaisha soon wanaanza kuhamisha maofisi yao na kuhire watu wao tu nchini mwetu
ReplyDelete