Home
Unlabelled
klynn
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
michuzi hivi wewe unalala lini na saa ngapi? We unajua kujituma I'm telling you kwa bidii yako ungekuwa majuu ungekuwa mbali sana. I really adire you, keep up with your spirit. We ni mtu muhimu kwa kutupasha habari sisi wabeba box, hahaha.
ReplyDeleteNasikia Rich alijimuvuzisha nao wote wawili...kwasasa jamaa yupo kempiski kwa muda,,,kwenye breakfast hawakuonekana, yani ni thooooooooo
ReplyDeletemmmmmhh!mimi sisemi chochote hapo,yaani no comment!
ReplyDeleteKama BBR II, ni hivyo..wanawake kede wa kede, hiyo Dola laki itakwisha mara mmoja!! Richadi ukiona kila picha yuko na mikonozzz!
ReplyDeleteAnastazia Anyimike
ReplyDeleteHabariLeo; Saturday,November 17, 2007 @00:08
“NIMESHITUKA kukuta nimekuwa maarufu kupita kiasi. Nilijua nitakuwa maarufu lakini si kwa kiasi hiki,” ndivyo anavyoanza kusema Richard Bezuidenhout katika mahojiano maalumu na gazeti hili juzi.
Richard, kwa sasa ni maarufu kama anavyosema mwenyewe, na hii inatokana na kuzitwaa dola za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh milioni 100) kwa kuibuka mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2 lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita Afrika Kusini.
Mtanzania huyo aliwabwaga washiriki wenzake Offuneka Molokwu wa Nigeria na Tatiana Durao wa Angola alioingia nao fainali.
Anasema, alipoingia kwenye shindano hilo alikuwa mtu wa kawaida lakini sasa amekuwa maarufu, kitu ambacho hakutegemea.
“Nimekuwa tofauti, ningependa kujirusha na washikaji (marafiki) lakini hilo kwa sasa haliwezekani. Nataka mambo haya yaishe na nirudi katika maisha yangu ya kawaida,” anasema.
Richard, alikuwa kati ya washiriki 12 walioshiriki kwenye shindano hilo lililoanza Agosti 5, wengine ni Offuneka, Tatiana walioshinda tiketi ya kushuhudia fainali za Kombe la Dunia 2010.
Wengine ambao walitolewa mapema ni Bertha (Zimbabwe), Kwaku (Ghana), Lerato(Afrika Kusini), Maureen (Uganda), Code (Malawi), Jeff (Kenya), Maxwell (Zambia), Justice (Botswana) na Meryl (Namibia).
Ushindi wa Richard haukuwa rahisi, alilazimika kukaa kwenye jumba la shindano kwa siku 98 huku akiwa anamulikwa na kamera 25, vipaza sauti zaidi ya 20 na hakuwa na mawasiliano yoyote kutoka nje.
Richard ana mengi ya kusimulia kwenye jumba hilo, lakini pia ana siri nyingi zilizomfikisha kwenye ushindi.
Katika maisha ya ‘kisiwa’ kwa miezi mitatu Richard anasema alipita katika mabonde na milima, kwani aligombana na kujenga urafiki miongoni mwa washiriki wenzake.
Richard akizungumzia siku yake ya kwanza kwenye jumba hilo, anasema alipata shida kuishi ndani ya jumba hilo na alikuwa akimkumbuka mkewe. “Kama uliniona kwa wiki moja nilikuwa mpole na nilikuwa namkumbuka sana mke wangu lakini baadaye, nikazoea”.
Watanzania zaidi ya 200 walijitokeza kuwania nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo, lakini Richard ndiye aliyefanikiwa kupeperusha bendera.
Richard anasema, maisha ndani ya jumba hilo ni magumu kutokana na kutokuwa na mawasiliano na watu.
“Kile nilichokifanya sikupanga. Najua hakuna atakayenielewa labda Mwisho (Mwampamba) ambaye ameshapitia maisha ya mle ndani,” anasema.
Mwisho aliiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo mwaka 2003 na kuibuka mshindi wa pili nyuma ya Cherise wa Zambia aliyekuwa mshindi.
Siri gani ya ushindi nyuma ya ushindi wake?
Anasema: “Nilipoingia sikuwa na mbinu yoyote ya kufanya ili nishinde. Na uhusiano wangu na Tatiana haikuwa mbinu, imetokea tu kwa vile ni hali ya kibinadamu. Yanayotokea hayapangwi ila yanatokea. Mimi sikujua kama ningekutana na Tatiana mle ndani.”
“ Kuna ugumu sana maana nilizoea kulala na mke wangu kwa miezi mitatu, sasa najikuta nalazimika kulala na watu wengine nisiowajua kabisa. Watu wenye kelele, wanaokoroma, wadokozi au hata vikojozi. Yalikuwa maisha mapya kwangu na nilimkumbuka sana mke wangu,” anasema Richard.
Anasema kuwa alijipa imani kuwa atashinda. "Nilikwenda kule kushinda na ndivyo ilivyotokea. Na nilipotangazwa kuwa mshindi nilikuwa kama nimezimia na kama uliniona nilikuwa natetemeka...
“Nakumbuka tulipobaki na Offuneka nilimkejeli kuwa yeye ni mshindi baada ya kuniambia anasikia watu wa Nigeria wakimshangilia na ndio maana ulimuoana alikuwa na furaha, lakini moyoni nilijua kuwa hata Watanzania wanaweza kushangilia hivyo.
Richard anasema kuwa alikuwa akimhofia mshiriki mmoja Maxwell kutoka Zambia na kuwa Ofunneka hakuwa tishio kwake ingawa alionekana kuwa mkweli na kuishi maisha yake ya kawaida.
“ Nilikuwa na wasiwasi sana na Max nilijua kabisa kuwa anaweza kushinda, lakini baada ya wiki mbili nikaona anatoka nje ya mstari kutokana na kuwa na tabia ya kujisifia sana, hapo nikajipa imani kuwa nitashinda ingawa haikuwa kwa asilimia 100. Na niliponusurika kutolewa mara ya tatu hapo nikajua kuna kitu na mimi nikaanza kuishi katika kuhakikisha nashinda...
“Washiriki wengine wote walikuwa wanajisifia sana na kutembea kifua mbele za kamera, lakini mimi nilikuwa mpole. Ukitaka kufanikiwa siku zote lazima ujishushe na usiwe juu ya watu,” anasema.
Nini kilimkera kwenye jumba hilo? “Kuna kubwa lilonikera sikupenda washiriki wengine waliojipachika jina la ‘Untouchables’ waniseme seme, lakini niliweza kuwashughulikia nilivyotaka, pamoja na wao kuwa na miili mikubwa na videmu vyao. Walikuwa wanakerwa na kuona wivu uhusiano wangu na Tatiana wakati wao nao walikuwa na mahusiano na wasichana wengine”.
“Mikwaruzano iliyotokea imeshapita na ule ni mchezo na sina kinyongo na mshiriki yeyote na natamani kukutana na washiriki wote katika siku za usoni,” anasema.
Anamzungumziaje Mwampamba? “Mimi na Mwisho ni watu wawili tofauti na yeye ana sababu za kuishi hivyo anavyoishi. Kujikweza ndiko kunakowaangusha watu, ila mimi sitakuwa juu ya watu,” anasema akieleza kuwa umaarufu wake hautamfanya abadili tabia yake.
Pamoja na ushindi huo, Richard ambaye aliondoka akiwa mwanafunzi wa shule ya kutengeneza filamu amepitia matatizo mengi, ikiwamo mtafaruku uliotokea kati yake na mkewe Ricki baada ya kuwa na uhusiano wa mshiriki mwenzake Tatiana.
“Nimejiandaa kwa lolote najua kuna watu watanisifia na wengine wataniponda. Changamoto ni kwa wale watakaoniponda na changamoto kubwa ni mke wangu. Yale yaliyotokea yametokea najua wengine watapinga kwa sababu hawajui ugumu wa kufungiwa ndani ya jumba lile”.
“Ingawa mpaka sasa (Alhamisi) sijapata nafasi ya kuzungumza na mke wangu, najua haitokuwa kazi rahisi, kwa sababu nimemuumiza kwa kile nilichokifanya, ila nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha narudiana naye, ninampenda sana mke wangu,” anasema.
Richard anasisitiza kuwa uhusiano wake na Tatiana ambao ulisababisha mashabiki wao kuwaita Richiana haukuwa wa kukusudia bali ilitokea kibinadamu.
Uhusiano huo ulimuudhi mkewe Ricki na kusababisha kutokwenda Afrika Kusini kumlaki mumewe.
Richard alifunga ndoa na Ricki mwenye miaka 29, ambaye alikuja nchini kwa ajili ya kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Anapoulizwa kama shindano hilo linavunja maadili kwa jamii, Richard anasema, “halivunji maadili maana mtu anayeshiriki ni maamuzi ya mtu husika na kuwa hata jukumu la kuangalia ni la familia husika, kwani unaweza usiangalie”.
Akizungumzia mipango yake ya baadaye, Richard anasema kuwa amepanga kuendelea na fani yake ya utengenezaji filamu na angependa kujikita katika kupambana na ugonjwa wa malaria na dawa za kulevya.
“Bado sijajua nitafanya nini, lakini pamoja na kuendelea na fani yangu napenda kuisaidia jamii na kuisaidia nchi yangu kwa vyovyote vile na hasa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria na matumizi ya dawa za kulevya,” anasema.
Walipokuwa kwenye jumba hilo, Tatiana alisema endapo angeibuka na ushindi, angegawana fedha hizo na Richard, Richard analizungumziaje hilo?
“Sijapanga lolote juu ya fedha nilizopata kama nitampa Tatiana ama vipi,” anasema.
Richard anasema kuishi na watu wenye tabia na tamaduni kumemfundisha mambo mengi na kama angepewa nafasi ya kushauri waandaaji, basi angewaambia kuwapo na mawasiliano na watu wa nje.
“Nimejifunza mengi na siku moja moja nilikuwa nazungumza na Maureen Kiganda kama chauna (binti), Olotya (mambo) lakini haikuwa ni lugha rasmi ya mazungumzo katika shindano hilo.”
Je, alikutana na Big Brother ana kwa ana? “Nimekutana naye, baada ya kutoka nimekutana na Big Brother na akaniambia katika washiriki wote, mimi nilimpa shida sana kwa sababu nilikuwa nabishana naye kila ninapoitwa kwenye mahojiano”.
Richard anasema kuwa yeye ni mpenda michezo. Na ni mpenzi mkubwa wa mchezo wa soka. Vile vile hupendelea kucheza mpira wa kikapu, pool table na mpira wa wavu.
Richard alizaliwa Agosti 10, 1984, Dar es Salaam na akiwa mtoto wa nne wa familia ya Vincent na Mtanzania Mariam Muhammed ambaye ni Mzaramo.
Vincent alizaliwa Uganda na babu yake Richard Corleleus Petrus aliyetokea Uholanzi na kuhamia Tsavo National Park nchini Kenya mwaka 1930, akiwa amejikita katika kuua simba waliokuwa wakiwamaliza watu waliokuwa wakijenga reli ya Mombasa na baadaye alihamia nchini Uganda akitafuta maisha.
Mwaka 1968, Vincent ambaye anatokana na uzao wa Mholanzi Corleleus Petrus na binti wa mfalme wa Rwanda, Mutara Rudahigwa, alimuoa mwanamke wa Kitanzania, Mariam aliyekuwa akisoma Uganda.
Mwaka 1969 familia ya Vincent ilipata mtoto wa kike Brenda aliyefuatiwa na Linda aliyezaliwa mwaka 1972 ambao wote walizaliwa Tanzania pamoja na kuwa wazazi wao walikuwa wakiishi Uganda.
Wakati utawala wa Iddi Amin alipopindua utawala wa Milton Obote mwaka 1972, na sera yake ya kunyang’anya mali na kulazimika kuwekwa kizuizini mji wa Nakuru, Vicent alishawishiwa na mkewe kuhamia Tanzania na familia hiyo ilihamia Tanzania mwaka 1976 na kuishi Ilala na baadaye kuhamia Makumbusho ambako ndiko alipata watoto wake Edward, Richard na Louis.
Richard alianza elimu ya msingi katika shule ya Makumbusho mwaka 1990 ambako alisoma mpaka mwaka 1993 na mwaka 1994 alihamia katika shule ya msingi Mashujaa ambako hakumaliza mwaka na mwaka 1995 alijiunga na shule ya msingi ya Vincent Alex, iliyopo Kampala, Uganda.
Mwaka 1998 Richard alijiunga na shule ya sekondari ya Makerere iliyopo karibu na Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, ambako alisoma kwa miaka miwili na mwaka 2000 alihamia shule ya Jinja ambako alihitimu elimu yake ya kidato cha nne.
Mwaka 2002 alijiunga na kidato cha tano katika shule ya Makerere na mwaka 2003 alirejea nchini baada ya kumaliza masomo yake.
Hiyo ndiyo siri aliyokuwa nayo Richard, ambaye kwa hakika ameitangaza Tanzania na kuiweka juu.
Huyu kijana ananiangusha sana mimi kama mwaname mwenzie
ReplyDeletehuyu alitakiwa akishatoka tu kwenye lile jumba angeenda kumtafuta mkewe straight badala ya kufanya ma press conferences yasiyo na kichwa wala miguuu
baada yakuongea kwa kina na mkewe ndipo angerudi kwa hao akina Baraka shelukindo sasa tazama...na kama yule mwanamke anakinyongo naye then tumuangalie maendeleo yake 6 months from now
Richard fanya hima umtafute mkeo na kama ikiwezekana panda ndege nenda Canada ukaongee naye pesa zako zikishaisha hata michuzi hatokutoa hapa kwenye hii blog kama huamini muulizE JEKI PEMBA
Mmh...!! Huyu demu Jackie yupo,dah....alisoma magogoni sio?
ReplyDeleteDemu mmh.....hajatuliaaaaaaa....!!! Big Up lakini naona umeangukia kwa BBA II sio mbaya!
Wacha nikabebe maboksi mimi.
Ciao!!!
Ha ha haaaa! Nilijua tu Majambazi hawa hawatakuachia. Hawa Golddigger ukiwa huna kitu hata salamu hupati. Sasa hivi wanajua una zaidi ya milioni 100 utawachoka. Hawana huruma hata kidogoooo, subiri ziishe uone
ReplyDeleteNakubaliana 100% na anonymous was Saturday, November 17, 2007 12:44:00 PM. Press conference hazimsaidii anabaki kuexpose personal life yake tuuuuuu, kujichoresha. Nina uhakika kuna mwanaume mwenzake anatumia weakness za huyu jamaa kujichukulia Mcanada kimoja. Akistukia mchezo, too late. Tatiana jamaa yake ana mpango wa kumrudia ila alimwambia rafiki wa karibu atamrudia kisha amtose vibaya sana. Nina mitandao Angola ndivyo inavozungumza..
ReplyDeleteKalagabaho we Mzaramo, ngoja ngoja huumiza matumbo na utakosa au ushakosa mwana na maji ya moto.
Huyu Jackie ni yule alikuwa anafanya Computer Center?..Ndio kazi zile zile ndogo ndogo madem wa Dar wanazofanya cos hawataki kusoma.Uzuri hauliwi..Brains ukiwa nazo utafika far...
Michu usibanie maoni..Ni hayo tuuuuuuuuuuuu!
Huyu namkumbuka Tulisoma nae Tambaza longi anaitwa Baraka Juma siyo shelukindo
ReplyDeleteJacky ntuya(klyn) badili hair style au msusi hizi nywele hazikupendezi bwana zinaonekana too artificial
ReplyDeleteMbona habari zinaandika vingine na mwenyewewanasema vingine. Richard alisema ana miaka 25 sasa kama alizaliwa August '84 Ndio ame turn 23 kama tunajua kuheasabu sasa sijui nani mkweli hapo?
ReplyDeleteAnd then mbona tunaambiwa tu umri wa hao watatu wengine niaje, kama unaeleza habari maliza yote...uandishi wa habari huu wa udaku?
Hizi news na press za kwetu ni umbea tu. Zinaandika mavitu zinazoona watu wana question...we need birth certificate to proove Linda amezaliwa '72.....Kama ni hivyo basi apunguze make up zinamzeesha sana
Nyie mnaopiga kelele eti Richard kamvunjia mke wake heshima, ni kwa vile mke ni mzungu ndio maana mnajipendekeza kwa wazungu ignorant wakubwa sana nyie washamba kupindukia ndio maana wazungu wanawaita niggers.
ReplyDeletehuyo mke wa richard alikuwa anajua big brother africa ni nini, na pili reaction yake imetokana tu na watu kupiga kelele zisizokuwa na maana haswa propaganda za wazungu, racist shit. Kama ricki angekuwa mweusi kila mtu angenyamaza tena i believe wangemlaani huyo mkewe basi kwa jinsi gani waswahili tulivo na akili finyu kubabaikia wazungu.
it is a shame richard bado ni mdogo let him do him, he has a lot to go for, ni kwa nini aanze kujinyima chance za maisha hivi hivi.
Stop hating
mi hii idea nzima ya big brother in africa si agree nayo, first sio maadili yetu, mtu amewadhalilisha wanawake na mke wake live halafu bado wakina jackie nampa mikonozzz ina maana wanamuunga mkono kwa kudhalilisha wanawake wenzao? second hii ni show ya first world ambako hamna shida ni raha tu na hamna adabu kwa sababu pesa ipo na si kwa taifa letu ambalo ndo tunajikongoja na full of respect(that wat i think) nawashangaaaaa watu wanaomshangilia au ni hizo laki hizo zitaongeza nini ni hela ya breakfast tu hiyo
ReplyDeleteRichard kafanana sana na Klynn.Au ni ma cousins?
ReplyDeleteHuyu Jacque alisoma Magogoni kweli, hajatulia kabisa yeye na Co. yake wakina Salome, naona mwenzake Salome ana duka(container la nguo pale Legho.
ReplyDeleteKama Richard aliishia kuondoka nao wote wawili sitoshangaa kwa maana huyo Jackie alishindwa kujizuiwa hapo studio, alijigonga live yaani mpaka huruma. Bora Kylinn alikuwa anazuga kiaina. kweli kunguru ni kunguru tu hata siku moja hawezi kuwa njiwa mzee wa peace!!!
ReplyDeleteBWANA MDOGO RICHI ACHANA KABISA NA HAO VIRUKA NJIA WA BONGO NI WEZI WAKUBWA KUKUONA UMEPATA PESA WANAANZA KUJINGONGA KWAKO HAO.HAO HAWANA USHAURI WOWOTE KWAKO ZAIDI YA KUKUAMBIA MTUMIE PESA NA ZIKIISHA WANAKUTOSA. MWANGALIE MWENZAKO MWISHO WALIVYO MTEMA.TAKE CARE BWANA MDOGO.TULIA FANYA VITU VYA MAANA UWE MFANO KWA WENGI.
ReplyDelete