majumba makuukuu mengi hapa yatabomolewa na kujengwa mapya makubwa na marefu zaidi. hii imakaaje wadau?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Yaani kuna watu wanaudhi sana!!!Hizo hela za kujenga maghorofa marefu zaidi si zingetumika kuwapa wakazi(wale wazalendo wanaoishi hukooooo) wa jiji hilo makazi yaliyotulia,maji,umeme na hata usafiri uboreshwe na mabarabara yaeleweke!!!
    Maghorofa,maghorofa,maghorofa, hali ya maisha ya asilimia kubwa ya wazalendo aaahh!!!

    ReplyDelete
  2. Yabomolewe kisha zijengwe parking lot, kama mtu anataka kujenga jengo refu au ghorofa apewe kiwanja nje ya mji kama Mbagala, gongo la mboto, kawe, bunju, kimara, kigamboni. Hapa mjini pamejaa jamani

    ReplyDelete
  3. MAJUMBA MAKUUKUU MENGI YA ZAMANI KUBOMOLEWA NA KUJENGWA MAPYA MAREFU! SIDHANI KAMA NI VYEMA SANA,NA TUJARIBU KUFIKIRIA KWA KINA ! BAADHI YA MAJENGO HAYO YANAYOITWA MAKUUKUU NI MAJENGO YA KALE SANA NA YANAA KUMBUKUMBU MUHIMU NA NZURI SANA KTK HII MIJII YETU YALIKUWEPO KABLA YA UHURU WA TAIFA LETU ! NA MENGINE KWA KWELI ARCHITECTURE YAKE NI NZURI INAYOJARIBU KUONNYESHA ARCHITECTURE YA KALE YA ZAMANI YA HAPA PWANI YETU YA TANZANIA NA HILI KTK MIJI MBALIMBALI DUNIANI AMBAKO WENYE MIJI YAO NA WENYE KUIPENDA MIJI YAO WAMEYAHIFADHI KWA USTADI MAJENGO YAO NA NI MOJA YA VIVUTIO VIKUBWA VYA UTALII KTK MIJII YAO. WATALII HAWAWEZI KUJA HAPA KUANGALIA MODERN ARCHITECTURE ! KTK NCHI YETU ASILANI ! HIVYO VITU VIKO KWAO NA WAMESHA VICHOKA WANATAKA KUONA TOFAUTI NA ASIKWABIE MTU VYA KALE NI DHAHABU.HAYA NI MAPUNGUFU MAKUBWA WALIYO NAYO WENYE MAMLAKA YA KUANGALIA HII VITU HASWA HAYA MAJENGO WAO HUFIKIRIA JINSI YA KUANDA MIRADI YENYE GHARAMA KUBWA KUBWA ILI NAO WAPONE HUMO HUMO BADALA YA KUANGALIA NA UPANDE WA PILI ! NA HAWA WAWEKEZAJI WANAOTAKA KUJENGA HAYO MAGHOROFA MAREFU BASI ANGALIENI UPANDE MWINGINE WA MJI KUNA MAENEO MAKUBWA NA MAZURI SANA NA MIONDO MBINU IPO VYEMA ANGALAU AIJAKAMILIKA LAKINI NAFASI IPO YA KUWEZA KUINDELEZA BILA YA GHARAMA KUBWA SANA SABABU HAKUNA UENDELEZAJI MKUBWA ULIOISHA FANYIKA.TUANGALIE HASA SUALA LA DRAINAGE KWA KWELI WALIO DESIGN MJI WETU MWANZO WALIWEKA MIONDO MBINU TOKANA NA UKUBWA WA MJI ULIVYO NA SI KAMA SASA ILIVYO ! NA BARABARA PIA ! NDIO MAANA TUNAJIKUTA TUNA MISURURU MIKUBWA SANA YA MAGARI INAYOINGIA MJINI NA KUTOKA LAKINI KAMA HAYA MAGHOROFA YANAYOTAKA KUJENGWA YANGEJENGWA NJE YA MJI AMBAKO KUNA VIWANJA VYA MIRADI VIMEPIMWA KUSINGEKUWA NA SABABU YA KILA MTU KUJA MJINI ! KWA MFANO JARIBU KWENDA PALE MAKUMBUSHO MILLENIUM TOWERS ! KUNA HUDUMA NYINGI SANA ZINAPATIKANA PALE NA UKIENDA UTAKUTA WATU MBALIMBALI KUANZIA WAFANYAKAZI ,BIASHARA ,WANAFUNZI,WASANII, WATALII WOTE KWA UJUMLA HUJA KUPATA HUDUMA AMBAZO ZAMANI ILIKUWA LAZIMA UENDE MJINI ! HAPO UTAJARIBU KUONA KUWA KUNA IDADI YA WATU FULANI IMEPUNGUWA KUINGIA MJINI.NA VILE VILE NI KUUPANUWA MJII ZAIDI KWA MPANGILIO.YAPO MAJENGO MACHAKAVU KWELI LAKINI TOKANA NA THAMANI YAKE KTK JAMII YETU NI MAKOSA MAKUBWA SANA KUYAVUNJA HATA HUKO KWA WENZETU KUNAOLD TOWN ! NA BASI TUYAWACHE JAMANI ILI TUWEZE KUIFADHI KUMBUKUMBU NZURI YA KWETU ! NA WENYE MAMALAKA WAACHE JEURI ZAO ZA KUTOTAKA SIKIA MAWAZO YA WENGINE NA WAANZE KUWAELEKEZA HAO WAWEKEZAJI WAENDE NJE YA MJI NA WAWEKEZE KWELI BADALA YA KUHARIBU ZAIDI !

    Mzushi

    ReplyDelete
  4. PaMBAAAFUU,badala ya kwenda kuwajengea wananchi vijijini nyumba nzuri za kuishi wanakazania kujenga Dar tuuu.Ama kweli sie ni kichwa cha mwendawazimu.

    ReplyDelete
  5. Hio sio noma, kwani hayo makuukuu hayako kwenye orodha ya majumba ya kumbukumbu kwenye dunia. tutawatoa makoo kama watayavunya yale ya stone town Zanzibar.
    Kubomoa majumba makuukuu nakujenga mapya na marefu zaidi hata Ulaya ipo
    Wacha wajenge waweke mandhari nzuri.

    ReplyDelete
  6. Bw.Michuzi hii imekaa kwamba siku hizi bongo ukata umeanza kutokomea taratibu miongoni mwa wanajamii ndio maana unaona hayo magorofa yanaibuka tu kama vichuguu kila uchao.

    Hiki ni kipimo tosha kwamba uchumi wetu umepanda na maisha bora kwa kila mtanzania tayari yashapatikana.Wenye kuendelea kuosha vinywa kwamba hakuna lolote lililofanyaika hadi sasa kazi kwenu.

    ReplyDelete
  7. amen.....duh, hii mipango miji kweli imekuwa kitendawili nchi yetu ya Tanzania...Hatukatai watu kujenga majumba marefu katikati ya jiji lakini parking hakuna, barabara kapa....kuweka parking pekee sio tija bali hata barabara za kufika huko mjini nalo ni tatizo.
    mimi nimeshachanganyikiwa kwa sababu kuna baadhi ya majengo yalijengewa parking lots ambazo la kushangaza zaidi ni pale wamiliki walipoamua kugeuza parking kuwa sehemu ya majengo (PPF Towers etc).
    haya jamani, kaazi kweli kweli....
    Mungu Ibariki Tanzania na watu wake...

    ReplyDelete
  8. pumbafu badala ya kuwekeza kwenye project za kuzalisha maji kwa wakazi wa jiji wanawekeza kwenye kujenga maghorofa kama si ujinga ni nini?Halafu hawa wapanga miji wana akili kweli wanatowa viwanja vikubwa vya kujenga majumba na kuacha nafasi ndogo kwa barabara huu ni ujinga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...