Shikamoo kaka michuzi,
pole na kazi.mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili hapa chuoni,,napenda nikutaarifu kuwa tokea leo asubuhi tumegoma kutokana na matatizo mbalimbali kama ucheleweshwaji wa hela zetu za project na pia kuhusu kudahiliwa kama wanafunzi wa ardhi university wakati sisi tayari tulishadahiliwa kama wanafunzi wa university of dsm n.k
Kuna kituko kimoja kimetokea pale ambapo mshauri wa wanafunzi"dean of students" alipomkimbiza mpiga picha wa magazeti ya citizen na mwananchi kwa umbali upatao mita 200 na kutaka kumvunjia kamera yake ambayo ndio inamuweka mjini lakini wanaume wa shoka tulimsaidia mwandishi huyo mtetezi wetu na kumtoa mikononi mwa kiongozi huyo japo alimsababishia mikwaruzo kidogo mkononi.
tunampa pole mwandishi huyo ila huyo dean wetu kajiabisha sana,mtu mzima,mwanasheria na tai yake shingoni na miaka kibao ambayo kwa mimi nastahili kabisa kuwa mjukuu wake kukimbizana na mwandishi,kwa kweli kaka michuzi ningekuwa na kamera ningechukua picha yake ummuvuzishe kwenye blog yetu ya jamii, yani sisi tunadai haki zetu yeye anatuzuia na isitoshe ni mshauri wetu,whyyyyyyyyyyyy?????kwaniniiiiiii
mgomo bado unaendelea na utakuwepo mpaka kesho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wewe mwanafunzi lete hiyo picha acha kujifaragua hapa, yaani unashindwa kumpiga picha hata ya mbali, tafuta, sisi tuna kazi nae huyu, tunataka kumnyorosha!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Wanafunzi wenzangu wa Chuo cha Ardhi.
    Mimi sio mwanafunzi tena nilimaliza hapo miaka ya 90 mwanzoni. Nilishiriki na kuandaa baadhi ya migomo lakini ni mpaka nilipoondoka ndipo nilipoona mapungufu yake. Kila mgomo unapotokea, masomo husitishwa na muda wake uliopotea haurudi. Hii inapoteza sana ubora wa elimu itolewayo hapo chuoni. Ushauri wangu, SITISHENI MGOMO NA MJARIBU KUTUMIA NJIA NYINGINE AMBAZO ZITAFANYA MAHITAJI YENU YAJULIKANE BILA KUKOSA MASOMO. Kwa mfano; mnaweza kuandamana nje ya ofisi ya mkuu wa shule kila siku wakati wa mapumziko mkiwa na mabango yenu na kuita waandishi wa habari. Tumieni vyombo vya habari zaidi badala ya kuonyesha misuli yenu kwa kugoma kwani waathirika wa mgomo siku zote ni wanafunzi. Tuulizeni sisi tulioondoka. Mgomo mara nyingi sio wa lazima na wakati mwingi huja karibu na mitihani kwani kuna wanaotaka masomo yasimame kidogo wakijaribu kujiweka sawa na mitihani. Kuweni makini.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na Ex-Ardhi Grad alivyosema hapo juu, mi mwenyewe nilikuwa FOE miaka ya 1999-2003tuliendeleza sana libeneke la migomo lakini nikisngalia kwa sasa naona heri tungetumia mbinu nyingine ili kupunguza maumivu ya mda kupotea na washkaji kutoswa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...