Hi Michuzi,

Vipi "weak end" inakwendaje?

Je wadau wanajua maana ya neno "Pedejee" au "Pedeshee"?

Hili jina linatokana na cheo cha PDG (ambayo hutamkwa "Pe-De-Zhee" kwa kiFaransa) ambalo kwa kirefu ni Président Directeur Général. Hiki ni cheo cha kiongozi mkuu wa kampuni au shirika. Ni sawa na CEO (Chief Executive Officer kwa Wamarekani) au MD (Managing Director kwa Wakerewe na sisi waBongo).

//Fred

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. waambie bwana.

    sio watu kazi kuvalia suruali kifuani wakadhani ndio u-PDG

    ReplyDelete
  2. Aisee! mimi nilikuwa najua mtu ukiwa na pesa harafu uvae suruali hadi tumboni yaani mundende ndio anakuwa predejee kumbe sivyo Asalamaleko walahi

    ReplyDelete
  3. Bon mon freur, Uko sawa kabisa ila kimatamshi umekosea sio "zhee" ni "jhee" na ndivyo herufi "g" inavyotamkwa (kwa kifarnsa) "en la langue francaise"

    ReplyDelete
  4. Na wa chini yake huitwa De-Zhee (Directeur Général). (dRU dACHI)

    ReplyDelete
  5. KIINGEREZA CHAKO KIGUMU. SIJUI TUTAFSIRI MWISHO DHAIFU, SIJUI UNA MAANA GANI KAMA MWISHO WA WIKI NI WEEK END. WANASIAASA WETU HAWATAKI NASI TUKAJUA KIINGEREZA HII NDIYO TAABU.

    ReplyDelete
  6. Anon wa 6:50PM EAT umiteleza kiduuchu ni hivi "Bon mon frère" na chini ndani ya mabano (kwa kifaransa) na mwisho ni "en langue française" viji-maandishi vile vya lugha yenyewe.. uwage unacheki na babelfish ya altavista mwanawane... (dRU)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...