msanii banana zahir ally zorro hatimaye amefunga pingu za maisha na wa ubani wake suzy na kufanya bonge la pati usiku wa kuamkia leo pale klabu cha new msasani ambapo kuna wakati alishika maiki na kumwimbia mai waifu wake nyimbo taamu ya mapenzi. kwa picha zaidi nenda www.michuzijr.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. wamependeza kweli ......mungu aidumishe ndoa yao.amin

    ReplyDelete
  2. KHERI YA MWAKA MPYA 2008 KWENU NYOTE!


    MDAU,

    NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO

    ReplyDelete
  3. Banana toa label kwenye suti..! Acha ushamba.

    ReplyDelete
  4. Those Tags Must Go
    It is common enough for us to forget to snip off tags and stickers that come with our clothing, but for more formal attire, such as suits and overcoats, a brand label may be sewn on near the sleeve. These tags are not meant to stay, so cut them off! Don’t forget to check for the little “x” sewn to keep the two flaps of a slit (such as at the tail of your jacket) neatly closed during shipping and packaging. These should also be removed. Labels on the inside of clothing should be kept.
    Mweh!

    ReplyDelete
  5. Banana:pressure,pressure,pressure ya nini na kutesatesa ya nini mbona Suzy huniamini.
    Suzy:vipi kuhusu Anita,yule binti wa moroko,acha yule rozi mwenye mtoto wako.
    Banana:kitanda akizai haramu,ile kweli damu yangu,kuhusu huyo Anita,Anita mbona simkumbuki.
    Suzy:Mbona kigugumizi.
    Banana:sababu waniona mwizi
    Suzy:mbona kigugumizi.
    Banana:mapenzi yamekwisha siku hizi.

    DADA YANGU INABIDI USTAHAMILI TENA MAJI USHAYAVULIA NGUO.......!MALALAMIKO YA NINI TENA.
    tehetehetehe

    ReplyDelete
  6. Hongera sana mmependeza sana, kila la kheri katika maisha mapya...
    NAOMBA NITOKE NJE YA HII TOPIC: Ninahitaji maelekezo ama ushauri, mimi ni mbeba maboksi, ama sijui mtoro wa nyumbani,kama mnavyotuita..ninahitaji vyeti vyangu vya form 4 na 6.. naomba mnipe maelekezo ya namna nitakavyovipata..
    1.Form 4 nilishagachukua, bahati mbaya nimekipotezea huku ugenini
    2. Form 6 nilichukuaga results slip tu,,
    please, naomba mnisaidie nikienda bongoland niende mashuleni kwangu ama wizara ya elimu ama baraza...mana nimejaribu sana kuagiza nikaambiwa sikuhizi hamna mambo ya kuchukuliana vyeti,,
    NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU..KHERI YA MWAKA MPYA 2008.

    ReplyDelete
  7. LABELZ LABELZ LABELZ '

    ReplyDelete
  8. Zaituni Hongera, yule dada yako? au ndugu yako alikuwa anaitwa Susana Mhina? yupo wapi?

    ReplyDelete
  9. Huu ushamba wa lebels kwenye suti mpya hatujaacha kumbe? Hata huyu bwana? Tusaidie kuelemishana jamani!

    ReplyDelete
  10. Banana na mkeo mmependeza tunawaombea ndoa yenu idumu,muondokewe na homa za alfajiri.Na husda za macho ya watu.

    ReplyDelete
  11. Anon wa 9:34 mie nitakufahamisha nilivyo fanikiwa mimi,nilirudia cheti changu 2004 au 2005 sikumbuki mwaka vizuri sijui kama mambo yamebadilika sasa na bwana wa nguvu mpya mambo mapya,kipindi nilicho kwenda mie nilienda shule yangu moja kwa moja,nikamtafuta mwalimu wangu kipenzi akanipeleka ofisi inayo hifadhi vyeti hapo shule, anae vihifadhi akadai miaka ni mingi sana,maana mie nimemaliza 1994 ina maana nimekirudia cheti changu baada ya miaka 10.Kwahiyo hata sijui nianzie wapi,akajifanya kutoka, mwalimu nilie mtumia kunisaidia akanambia inabidi umpe chochote japo ya chai ili akutafutie nikamkatia shs 10000 yake cheti within 2 minutes nikakabidhiwa NA LIVING CERTICATE YAKE JUU.Ninge kutajia na shule, lakini sijui nikiitaja shule atapata matatizo mama wa watu.Muhimu hapa ni ujiweke tayari na pesa ya chai pamoja wala vumbi wanasema bongo tambarare,hongo iko palepale kila mtu anataka pesa ya chai sijui chai na jua kali lililopo Tanzania wanainywa saa ngapi.Anyway GOODLUCK

    ReplyDelete
  12. Maarusi wamependeza. Ushauri: bibi arusi jitahidi kupunguza uzito. Kwa kasi hii si muda mrefu utakuwa si wa kitizama.

    ReplyDelete
  13. Lebel lazima tutajuaje kama suti mpya hongera sana kaka yangu banana kwa kuchukua jumla mungu awajaarie ndoa yenu idumu milele

    ReplyDelete
  14. Juzi nilimuona pale Kariakoo kwa Makoba akimuazima hiyo Suti.

    Sasa akitoa lebo kwenye suti za watu atajibu nini akiulizwa na Makoba?

    Au mnataka jamaa waistukie kwamba sio mpya ikirudishwa dukani??

    ReplyDelete
  15. asante anon wa hapo juu, mimi pia ni 1994 Jangwani, du kasheshe, basi itabidi niandae chochote kitu,,,then 1997 Tambaza, ila sasa Jangwani nilishakichukua ndo kimepotea, sasa sijui nirudi pale shuleni ama niende wizarani sasa...asante sana, kweli bongo tambarare......

    ReplyDelete
  16. Kaka banana usije ukamlengesha wife bwana,kuwa mume mzuri.Zaituni alishapoteza dada na mama yake,sasa usimlengeshe.Wanawake wengine achana nao ili muishi maisha marefu na furaha.Mmependeza sana.Heshimuni ndoa.

    ReplyDelete
  17. I HOPE HATUUDHI WAPENZI WA BANANA,MIE NI MPENZI WA BANANA VILEVILE,MAHARUSI WAMEPENDEZA.
    msg hii ni kwa sister wa Jangwani,nafikiri itakua rahisi ukienda shule kwanza uka ulizie endapo umepoteza cheti vipi utapata copy,labda rahisi wizarani kama unaijua number yako.all in all nenda shule kwanza kama nilivyo kwambia nyumbani pesa yako tuu,kila kitu kitaji set.Jambo lako liende kwa speed chai unataka lilale bania pesa yako.Usiingie pressure.Ila vile tumezoea system za nje rushwa hairuhusiwi unatamani umrushie mtu ngumi akiomba chai au haombi lakini vitendo vyake vina kwambia naomba pesa ya chai kwanza(yaani mtu ana kua kwenye slow motion).
    KHERI YA MWAKA MPYA KWA KAKA MICHUZI NA WADAU WOTE POPOTE MLIPO.

    MMasanja

    ReplyDelete
  18. Jamani tukumbukeni na masomo ya darasa la nne au tulikua tukiimba kama kasuku:- mithalimithali! mithali njoo Penye udhiaaaa..... penyeza rupiaaaa shost na hasa kwa uzembe wa kutupa vyeti ndo hapo ukiskia toa pesa upate haki yako au mtumikie kafiri upate haki yako.haki karne hizi hupatikana kwa pesa .ikiwa utaanzia shuleni au ikiwa wizarani, pesa mbele.

    Banana mmependeza sana na mkeo. sasa kilichobaki ni kutulia na kuunda familia bora, kila la kheri maharusa.

    ReplyDelete
  19. ooooo! bisumilahi nayo ya kwanza ya kuondokea, mwana anakwaoooo muenge engeee kama kioooo lyalyalyalyalya akbari shooo sho malikia umidaaaaa iyoooooooo. eeee akikuudhi umsameheee.akikuagaaaa mpe ruhusa. hiyo ni ilaaaa ya mwanamkeeee mara kwa mamaaaa. ah! nakumbuka tulicheza halaiki ya utamaduni Zenjy tukawa tunacheza ngoma ya kizenjy ya kurusha ndege (bomu) kwa wale wazenjy watauelewa ngoma ya maharusini wee yanaujumbe mzuri nilikua mdogo sana nilikua naimba kama kasuku tu ila sasa nimekua naelewa tafsiri ya wimbo huo nami namuwasa mzee wa pressure. mwana ana kwo huyo muengeenge kama kiyoo kukuvunjika huwa basi tena.Nawatakia maisha ya furaha msikilizane mvumiliane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...