NAWATAKIA KRISIMASI NJEMA WADAU WOTE WA GLOBU HII YA JAMII POPOTE MLIPO DUNIANI KWA MTUNDIKO WA SNEPU HILI LA KATIKATI YA JIJI LA DAR.
WAAMA, NAPENDA PIA KUTOA SHUKURANI KWA WADAU WOTE MNAOWASILIANA NA NDUGU NA JAMAA NA MARAFIKI KUPITIA HUMU, NIKIWAAMBIA MSISITE KUITUMIA GLOBU HII AMBAYO NI YENU HIVYO ITUMIENI MTAKAVYO, BORA ITIFAKI IZINGATIWE.
VILE VILE NAPENDA KUWAPONGEZA WADAU WOTE WACHANGIAJI KWANI SASA LUGHA YA KISTAARABU IMESHIKA MKONDO WAKE NA MANENO YA KUKATISHANA TAMAA YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA KUBWA KIASI YA KWAMBA INATIA RAHA, INGAWA KUNA WAWILI WATATU AMBAO BADO VING'ANG'ANIZI KATIKA KUTAKA KUCHAFUA HALI YA HEWA. NAMI NITAPAMBANA NAO KWA KUPIGA CHINI MICHANGO YAO AMBAYO HAISAIDII KITU KATIKA JAMII YA GLOBU HII.
MWISHO NAAHIDI KUENDELEZA LIBENEKE NA PIA KUWAWEKA WADAU MKAO WA KULA KWANI HIVI TUNAVYOONGEA MDAU WA MILIONI 3 ANAKARIBIA, NA PANAPO MAJAALIWA MAMBO YA ZAWADI KWA MDAU HUYO YATAANDALIWA...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Shukrani nyingi kwa salamu za Xmas.Sisi pia tunapenda kukutakia wewe binafsi,familia yako,wasomaji na watembeleaji wote wa blog hii Xmas Njema na maandalizi mema ya kuupokea mwaka mpya wa 2008.

    Pia tunakutakia kila la kheri katika kazi zako na jitihada hizi za kupasha habari na kuelimisha jamii.Kila la kheri.

    ReplyDelete
  2. MICHUZI Merry x-mas! kuna huyu mchngiaji SINA MAKOSA huwa haeleweki sometimes anaongea vitu mantiki some times anakuwa negative sana.Ila si wakukatisha tamaa kwani jamaa huwa anatoa comments nzuri kwa kiasi fulani na ni wa kudumu.Japokuwa alisha niponda humu ila nampa MERRY X-MAS pia.

    ReplyDelete
  3. kwenye maoni ndugu yangu unatumia UFASHISTI hiyo kubali au kataa lakini ukweli ukubali.
    laiti ungeishi ughaibuni ungejua maana ya demokrasi ya kinywa nini.
    umekuwa ukikalia sana maooni ya watu kwa kile unachotaka kujifanya msamaria mwema wa kuandika mazuri.
    kuna WADAU na heshima zao humu wanauliza mambo ya maana kuhusu maisha, jamii na hata siasa lakini ukiona vinaelemea IKULU, unazima!
    Mtu gani wewe usokubali kukosolewa au kuwapa watu fursa kuchangia mada HUKU UKIJIDAI BLOG wa wajamaa.
    Ukibanwa na shida UNAJITUTUMUA KIFUA Mbele na kutembeza BAKULI.
    Ungeweka angalau SUMMARY ya matukio muhimu yaliyokithiri kwenye BLOG hii mwaka huu ikiwa pamoja na;
    i)Kifo cha Amina Chifupa,
    ii)Ndoa ya Mpakanjia
    iii)Kuzama na kuibuka kwa BLOG hii
    iv)Msaada(bakuli) la Said la CMR
    v)Bakuli lako
    vi)Kipigo cha STARS CAN (GS)
    vii) Kashfa ya BOT na BILALI
    viii)MATAPELI wa CARGO UK/BONGO
    ix)Kung'oka kwa MAHITA na mengine kibao tuuuu.

    ReplyDelete
  4. Hallo Michuzi!!Kila la heri ya X-Mas na Boxing Day,huku Italy ni siku ya Saint Stefano.
    Hatutamaliza kukushukuru kwa kuianzisha hii Blog ambayo imekuwa ikitufanya tujisikie karibu zaidi na Bongo!!
    HAPPY HOLLIDAYS kwako na waBongo wote popote walipo!!

    Vicenza,Italy.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...