kwa wanaoangalia mbele watajua nini maana ya posti hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Samahani, naenda nje kidogo ya mada inayohusiana na post hii.

    Nataka kusema Kwa mara ya kwanza nimesoma habari (ippmedia) ya kiongozi aliyesema ukweli kabisa unaohusiana na hali halisi ya RUSHWA NA UFISADI. Ni vyema kila mwana jumuiya akaisoma. Nanukuu ...


    ''Vita dhidi ya rushwa unafiki mtupu - Askofu

    2007-12-25 11:14:34
    Na Simon Mhina


    Vita dhidi ya rushwa na ufisadi itaendelea kuwa ngumu, kwa vile wengi wanaodai kuipiga vita ni wanafiki na ndio hao hao wanaoidhoofisha.

    Hayo yalielezwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, alipokuwa akitoa salamu za Krismasi na mwaka mpya kwa Watanzania, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

    Alisema inashangaza kuona kila kiongozi na kila mwananchi anahubiri kupiga vita rushwa na ufisadi, lakini siku zinavyozidi kwenda ndivyo rushwa za kila namna zinavyozidi kukua na kujichimbia katika jamii yetu.

    ``Mimi nashangaa sana, kwani kila mtu anadai kupiga vita rushwa, kila kiongozi anaposimama anakemea rushwa na kudai kuchukizwa nayo.

    Hivi sasa ukitembelea ofisi nyingi utakuta mabango mengi ya kupinga rushwa. Sasa kama ni hivyo, hao wanaotoa na kupokea rushwa ni kina nani? Mbona kila mtu anadai hahusiki?`` Alihoji kiongozi huyo.

    Askofu Malasusa alisema kutokana na rushwa kukua siku hadi siku, huku watu wengi wakidai kupambana nayo ni ishara tosha kwamba kuna unafiki wa wazi katika vita hiyo.

    Alisema katika vita yo yote hakuna kitu kibaya kama unafiki, kwa vile matokeo yake ni usaliti.

    Alisema serikali haina budi kuchukua hatua za haraka ili kuwabaini wanafiki katika vita dhidi ya rushwa, vinginevyo juhudi zote zitakuwa bure.

    ``Kama mko pamoja kwenye vita, halafu mwenzenu, anaenda kinyume nanyi, itakuwa vigumu kushinda vita hiyo, hilo ndilo linalotokea kwenye rushwa, inakuwa vita ngumu kwa vile wapiganaji wenzetu wengi wao ni wala rushwa,`` alisema.

    Askofu Malasusa aliwataka Watanzania kusherehekea sikukuu ya Krismasi kwa amani na kujiepusha na vitendo vya uhalibifu, kama ulevi na magomvi.

    Alisema Kristo ambaye amezaliwa siku ya Krismasi, lengo la siku hiyo ni amani, maelewano na upendo.

    Alisema katika kipindi cha mwaka ujao, KKKT itaendelea kushirikiana na serikali, katika kuwaletea wananchi maendeleo.
    Alisema kanisa litaendelea kujikita katika kuendeleza huduma za jamii, kama shule na afya.

    ``Tunafanya hivi kwa vile mahitaji ya jamii ndiyo yale yale mahitaji ya kanisa. Kanisa halina watu wake wa pekee, bali watu wanaounda KKKT ni wale wale wanaoishi katika jamii yetu,`` alisema.

    Katika hatua nyingine Askofu Malasusa aliwataka Watanzania kutumia kipindi cha Krismasi, kuombea uchaguzi mkuu wa Kenya.

    Alisema Kenya ni nchi jirani na yenye changamoto nyingi za kisiasa, hivyo ni vema ikiombewa.

    Alisema Watanzania hawawezi kuepuka matatizo ya ghasia iwapo yatatokea nchini humo''. (mwisho wa kunukuu'' Huu ndio ukweli wenyewe. Ni kweli hii vita ni ngumu kwa sababu kuna mamuluki. Sasa nani atawabaini na kuwaondoa???

    ReplyDelete
  2. jamani mmeona kuanzia tar 25/12/2008 hadi 29/12/2008 watu wanakula maisha tuu...na pia tar 1jan 2009 watu wanapumzika tena..tar 2 na tar 3 na tar 4 duuuuuuuuuuu balaaaaaa

    ReplyDelete
  3. 7+7=14+7=21+7+28
    Lizzie

    ReplyDelete
  4. Kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi sana, x-mas ya mwakani imekaa vema kweli kweli! Safi sana.

    ReplyDelete
  5. the date starts on monday 1st to sunday the 7th and vice versa for the rest of the month. This means first day (1) is monday , second(2) tuesday ..... to sunday(7)

    ReplyDelete
  6. MANAKE HAMNA MWAKA 2009. MWISHO WA DUNIA, ANGALIA HAMNA TAREHE BAADA YA 31 DEC

    ReplyDelete
  7. The point here is: People will have several days to stay at home since the X-Mas falls on Tuesday, then Boxing Day then week-end. The problem is, this is a bogus calendar trying to move Sunday from being the first day of the week to the last day of the week.

    ReplyDelete
  8. 9:50pm have your glasses on .....it is not Tuesday but Thursday....and who told you Mon, or Sun is the first day or the second...etc...those are the myths and everyone has the right to call whatever day they want as their first day they want their first day....other people don't believe on whatever you believe or what you have been tought and brain washed....

    ReplyDelete
  9. mlevi bwana hataki kuulizwa swali. kwani lazima ujibu wewe? tangu uchumbie mkritso basii ahaaa uislamu umeutia kapuni. wala sikuonei huruma jahannam inanukia babake.

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli Michuzi nimetumia nguvu nyingi sana lakini sijaelewa kitu hapa! Naona Calenda tu hapa! Nifungue macho, bila na ya wengine!

    ReplyDelete
  11. We anon wa December 25, 2007 9:50:00 sio bogus calender hiyo. It's real.

    Check vizuri, calender uliyonayo wewe ndio inaweza kuwa bogus.

    Kama huamini check hapa http://www.timeanddate.com/calendar/index.html?year=2008&country=1

    ReplyDelete
  12. ama kweli wadau wengine mahoka kweli.hamuoni kwamba hii ni ratiba ya matumizi ya vidonge vya majira?

    ReplyDelete
  13. XMAss itakua kesho mwakani simple..

    ReplyDelete
  14. Inaonyesha Uzazi wa mpango a.k.a Nyota ya kijani. Hizo tarehe nyekundu hatari sana, ruka ama subiri (vumilia), vinginevyo umeliwa! Hizo zingine tambarareeeeeeeeeeee, kujiachia tu kwa kwenda mbele.

    ReplyDelete
  15. It shows that, 2008 ni MWAKA MREFU(LEAP YEAR).
    From Mdau wa Marangu- BIG up Marangu!!!

    ReplyDelete
  16. Hivi huyo anayeita hii kalenda bogus nani alikwambia siku ya kwanza ni Jumapili? Au siku ya saba ni Jumamosi.....Haya mambo ya kusoma na kukaririr tu TZ tutaishia wapi? fanya uchunguzi soma na jitahidi kuelewa.

    Kama unaimani yako just keep it lakini ukweli ni kuwa mwanzo wa siku ni Mungu mwenyewe anajua.... Hizi historia za waegypty na warumi ndio tunafuata ulimwengu mzima lakini kuna siku umeshajiuliza historia ya mtu mweusi ilirekodiwa wapi???? walivyoonaga lile fuvu la mtu wa kwanza kule olvai huyo mtu alikua nani....wanavyoona wahindi wekundu walikua miaka mingi sana wao mwanzo wao ni wapi?

    je wanavyoanza kuona kuwa kuna uhai kwenye Mars siku wakiweza kufika huko wakakuta watu je utawaambia leo ni siku ya kwanza au huku kwetu leo ni jumapili wakikukatalia wakakueleza vingine wanavyobelieve wewe utasema nini?

    Mambo haya sio ya kumbishia mtu au kumjudge mtu what you believe it is up to you....

    ReplyDelete
  17. Mhhh aisee, mwaka ujao umekaa vizuri sana michuzi,

    Manake mtu ukitoka nyumbani Jioni ya tarehe 24 jumatano, huonekani offisini mpaka jumatatu ya tarehe 29, hapo ukito ani karibia siku 5 nzima.

    Kana kwamba hiyo haitoshi, yaan ukitoka kazini siku ya tarehe 5 Jioni, huonekani kazini mpaka tarehe 10.

    Duh aisee, hii imekaa vizuri sana kaka, tumshauri kikwete kila mwaka ukae hivi hivi, nyie mnaodai kua hizo ni siku za mwanamke inaelekea mnamaindi sana chini, sasa endeleeni hivyo hivyo wacha sie wapenzi wa viti virefu pale jiran na kona tufurahie mpangilio mzuri wa mwezi wa 12 mwakani, maana itakua ni kujiachia tu na glass kadhaa,

    Duh, aisee

    ReplyDelete
  18. bro. michu sema ishallah kwanza. mambo ya kesho kayajua nani? usiifurahie kesho kabla hujaiona .Ila mwanawane tukijaaliwa tutakula pepo siku zote hizo? ni full kujiachiaaaa.

    ReplyDelete
  19. mi naona hapa kwenye kalenda ya upande uliyojificha inainesha ya mwezi wa nov 2008 kila siku ya jumapili(sund)inafanana na kila siku ya jumanne (tue) ya wezi dec 2008. imependeeeeza kweli si kweliiiii?

    nayma

    ReplyDelete
  20. Naona kuna jamaa humu huwa wanawashwa midomo yao na mijadala inayo husu dini,wanatafuta kila njia ili kila wakati tuwe tunajadili udini katika forum hii,tunaomba wawe wanfikiria kabla ya kuanza kuandika mambo hayo

    ReplyDelete
  21. Michu hiyo sio tight period ya English Premier League?? Manake najua bwawa la maini mnaangalia mwakani, mwaka huu mmeshachemsha tena.

    ReplyDelete
  22. Siku za kufanya kazi Tanzania ni 19 tu katika mwezi Desemba 2008.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...