kampuni ya ndege ya abiria ya binafsi ya precision air inayosadikiwa kuwa ndiyo bora ist afrika mashariki na kati inaendelea kudunda bila kelele wala mikwaruzo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hongera sana Precision.Nadhani siku hizi ndege zao hazikorofi kama zamani.maana nakumbuka unaweza panda ndege ikagoma kuwaka wala sio mara moja wala mbili tu!
    Lakini sio wao tu,hata wenzetu huku majuu nao wanachemsha,kama mimi jana naingiza timu hapa Atlanta tayari kwa safari ya Bongo nakuta eti KLM wamecancel ndege bila hata ya kutupa taarifa!!ingekua sie wangedai wabongo(weusi)lakini kwao haka kimya!Inabidi leo ndio tuondoke tena waiopenda waliwekwa kwenye ndege nyingine za kupitia London,sie tusiopenda kupita huko na mizigo yetu akhaa!!tunasubiria leo

    ReplyDelete
  2. Kaka wacha hizo kaka, nimekustukia.
    Hapo ulikuwa unataka kutuhabarisha kuhusu Precision Air kweli au ulikuwa unataka "Tucheki Salio" la huyo anti hapo?
    Tehe teh tee!
    Asante Kaka.

    ReplyDelete
  3. Michuzi usiwasifu bure,ubora ni hizo rangi za kijani au hali halisi ya ndege,nimezitumia ndege zao hii miaka ya karibu nimekuja huko 2004,2005 na 2006,kwanza mbanano,pili air conditioning sawa na zero,tatu mizigo expect the next day,nazungumzia kwa sababu hiyo ndio service niliyo pata wanashirikiana na Kenya Airways kutoka UK mpaka hapo Jomo Kenyatta service it's very good but from Nairobi to Dar or Zanzibar or Kilimanjaro it's terrible,kwahiyo usiwasifu bure they have to work even harder to be the best service provider.

    ReplyDelete
  4. nilienda kukata ticket air tanzania wakanikalisha ooh subiri customer service mbovu nikawaambie warudishe hela nikaenda precision, Good customer service ingawa ni kwa kiwango cha bongo within 15 minutes nikaondoka na ticket yangu nimesafiri na kenya airways poa tu mizigo nimeshuka nayo ingawa rubani alikuwa anafanya bwebwe zisizo namaana kwenye kona. Ila kwa tanzania thats the only choice, ATC- no no bora nipande basi.

    ReplyDelete
  5. Kila mtu na uchambuzi wake;
    Wakati Perez yeye kaona MAKALIO, mimi naona kuwa suala ni UJIO AU ULINGANIFU WA COMMUNITY AIRLINES KWA PRECISION AIR!!

    Precision Air ina sifa ya jumla ya kila ndege ya kutufikisha tunakokwenda kwa haraka zaidi kuliko usafiri mwingine uliopo. Lakini kama alivyosema ANONY wa 10:52 nami naifahamu Precision Air kama ifuatavyo:-

    1. Kukaa ndani mwake ni sawa na kuwekwa kwenye pre-heated Microwave with 40-50 degrees Celcius. Ama mtengeneze hizo airco au leteni ndege mpya maana mmeahidi hili toka zamani!

    2. 'Precision on time' ni agenda inatakiwa kuwa katika kila kikao chenu cha Bodi kama mnataka kuendelea kuwa na jina hilo la Precision.

    3. Mizigo kupotea na au kupelekwa kituo kingine ni kero inayotakiwa kukaripiwa kwa nguvu zote na pengine utafiti ufanywe na idara ya huduma kwa wateja ili kujua chanzo chake na namna ya kudhibiti.

    4. Suala la Vinywaji na vitafunwa linaweza kuimarishwa kwa kuwa na aina mbalimbali za vyakula. Sio tu vi Ham & Chicken bread slices vya baridi tuuu. Pandisha gharama kidogo tu tupe misosi ya nguvu uone!

    4. Hamuwezi fanya chochote kuhusu mbanano kutoka kiti hadi kiti na pia kuwa na vikebini vidogo visivyotosheleza mizigo ya mikononi maana bado mnatumia ndege za kizamani. Suluhu ni kununua ndege zenu wenyewe!

    Kwa wastani marubani na cabin crews ni watanashati na wana lugha nzuri. Lakini wahudumu wa mawakala wenu kama wa Zanzibar na Musoma wanahitaji semina ya kukata na shoka!

    Otherwise tunawakaribisha sana Community Airlines kuleta ushindani mzuri kwa ajili ya ubora wa huduma kwa wateja.

    Michuzi kabla sijakimbia kufanya booking, NAOMBA NIMALIZIE KWA KUSEMA KUWA HUDUMA ZA NDEGE LAZIMA ZIENDANE SAMBAMBA NA ZA VIWANJA VYA NDEGE. KWA NINI VITU VINAVYOWEZEKANA KUBORESHWA BILA SHIDA KAMA UPATIKANAJI WA CHAKULA NA VINYWAJI VYA HUAKIKA NA HATA KUBADILISHA FEDHA NI ALMASI KUPATIKANA KATIKA KIWANJA CHA NDEGE MUSOMA????? TUNAOMBA WAHUDUMU WAKE WAVAE UNIFORM NA NAME TAGS ILI TUWAFAHAMU NA WAJITAHIDI KUSAWAZISHA MABONDE KWENYE RUNWAY MAANA INABIDI RUBANI AUME MENO KABLA YA KUTUA!

    Alhaji Obwatasyo

    ReplyDelete
  6. Katika mashirika ya ndege yaliyoko hapa bongo, precision yaongoza na haina mfano.

    Nimetumia ndege zao mara nyingi tu na kwakweli kwao kujali kwanza customer satisfactory ni namba moja then masuala mengine pembeni.

    Hembu mtu aniambie ni shirika gani hapa bongo ndege ikiaihirishwa hata kwa nusu saa tu kama ni mchana, passenger wanapelekwa hotelin pale first floor na kupewa misosi na ma-bufee ya nguvu bila extra cost??
    Hiyo ni moja tu lakin kama ni usiku watu wanapelekwa hotel yenye hadi na ishanitokea mimi.
    Ukweli hakuna na sijawahi kuiona zaidi ya Precision Air pekee tu.

    ReplyDelete
  7. nawafagilia precision kwani wamejitahidi sana katika usafiri wa anga hapa bongo....live long precision air

    ReplyDelete
  8. Huyo hapo juu ya Cyber yuko correct kabisa ila tu amesahau Flamengo Hotel pale 1st floor. Mi nlishapelekwa pale siku ilipotokea delay na pia si mara kwa mara.

    Rafiki yangu alishapigiwa simu na wafanyakazi wa Precision Air kuarifiwa kama ndege itachelewa kwa masaa mawili. Ni kitu ambacho sijakiona kwa mashirika mengine kupoteza gharama ya kumpigia kila mtu juu ya uchelewaji wa masaa mawili tu.
    Wengine ndege inafutwa kabisa na unakuja kujulia ushafika kiwanjani na mabegi yako.

    Precision wana ndege za kuanzia asubuhi na mapema. asubuhi ya saa tano yaan mpaka usiku.
    kwa kweli hua nasafiri na ndege zao mara kwa mara na muda wowote ndege zipo.
    lakin pia tusisahau ndilo shirika lililoajiri wafanyakazi wengi zaid kwenye sekta ya usafiri wa anga.
    hii pia imepunguza tatizo la ajira kwa nchi yetu.
    Binafsi nawapenda sana Precision na naomba wasomaji wangu wa blog hii tuiunge mkono.

    Aisee Michuzi wacha niwahi kukata ticket niishie zangu Moshi kula X-mass maana jinsi ndeghe zao zinavyogombaniwa, waweza kukosa nafasi.

    Shark, Arusha

    ReplyDelete
  9. Mh, wenzangu basi mna bahati na Precission Air.

    Binafsi ninaishi Arusha, ana ni msafiri wao mzuri tu, ila sio kila mara wanakuwa sahihi.

    Kwa Arusha, kwa mara zote kukiwa na delay (labda nikiwepo mimi mwenye gundu sijui), tutakaa pale pale uwanjani kusubiri, hatupewi cha sandwich wala koka kola!, na sometimes wakiona abiria ni wachache, basi mtapandishwa kadege kadogo hako, sio kuyumba huko angani, na vile hakana vyoo, hakuna che kupewa msosi wala nini, (imenitokea mara mbili)
    Haya, kuna siku nikaipanda toka Mwanza to Dar, niwahi Ethiopian Airlines, huwezi amini kulikuwa na delay ya 3hrs, tumekaa Airport hatuambiwi chochote, tunashangaa shangaa tu, wakumuuliza hakuna, well baadae tulifanikiwa kuondoka kufika Dar nimechelewa ndege ipo lakini Check in muda umepita na luggage belt zimefungwa!.
    Hasira ni pale tumeongea na macabin crue wajulishe ofisi zao ili wajulishe ethiopian airlines, tukadanganywa kila kitu kimeshakuwa arranged, tukifika tu tutaenda moja kwa moja kwenye ndege na vile mizigo yetu imechekiwa Mwanza hakuna shida itaingia ndani, mzozo kufika Dar jamaa wakaturuka kwamba they have done their part kutufikisha, suala la Ethiopian haliwahusu. Sasa kwa nini walitudanganya kwamba kila kitu kimeandaliwa?
    Any way, tulifanikiwa kuondoka kesho yake kwa gharama za hotel toka mifukoni mwetu.

    Precissional, Jirekebisheni vimakosa vidogo vidogo kama hivi, haipendezi kabisa. Hii ilitokea Dec 2006, nina hakika mnakumbuka.

    ReplyDelete
  10. jamani mimi ndo kwanza leo nataka kuwasifia hawa precision air tanzania,hawa jamaa wanajitahd japo wakati mwingine wanachemsha kiaina,pongezi zangu nazipeleka kwa wahudumu wa ndani ya ndege,kwakweli wahudumu hasa wanaume wanajitahidi sana kudeliver customer care,kuna jamaa mmoja ambaye mimi namjua kwa jina la Mukama ,huyu jamaa nilianza kumuona mwezi wa nne mwaka huu hasa baada ya kuwa nimerejea kutoka majuu kwa masomo yangu,kijana anajitahd sana kufanya kazi,anaongea vizuri na abiria,ansaidia kuweka mizigo namengine mengi,si kuwa namsifia huyu jamaa coz mi simfahamu na bila shaka hata yeye hanifahamu kwa sura,kwa kweli si yeye pekeyake awpo pia wavulana wengine bt huyu ni mfano tu.Hongera sana na zidisheni watu kama yeye na tena hasa wavulana,wadada nawapenda ila bado customer care inasuasua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...