ukioa ama kuolewa uchagani lazima ujifunze kucheza ringi. tatizo wakwe zetu hawa hawajatoa kibao kingine toka ile singo yao ya sherehe itoke miaka hiyoooo....hapo ni usiku kuamkia leo tunakula 'kinaaaateeee kinaguruma...'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Zipo nyingi labda DJ alikuwa hana kuna ile Singo ya Mariale alikuwepo,Chuwa alikuwepo...cc wachagga tupo juu... Na kwa taarifa yako Reggae zote ni za kichaga...

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha!!!!
    Bro Michu unajua chanzo cha ringi,Hawa wenzetu ni watu wa fedha sana,hivyo wana yale mawazo ya kwamba kila hela ni yao,kwa hiyo ukisipofanya hivyo inakuwa matokeo kama yale ya wenzetu kipindi ile Twanga pepeta mikono juuuu ukishusha simu zote hakuna mfukoni,nao wachaga ukicheza bila ringi utakuta mifuko yako yote mitupu ,si unajuwa tena arawaa!!!

    ReplyDelete
  3. We Michuzi hao jamaa wana singo nyingi sana kupitia kwa mastaa wao kama JUDY BOUTCHER, LUCKY DUBE, SOPHIA GEORGE NA wengineo wengi ati zikiwemo zile zilizowahi kupendwa za RTD especially ile SIGTUNE ya kukaribisha wasikilizaji katika kipindi cha UGUA POLE CHA RTD.

    ReplyDelete
  4. Dr confusion haika monoko i mean asante mwanawane nimecheka sana umenikumbusha kisa cha massawe alokufa akafika lango la dhahabu la kuingia mbinguni, akamkuta malaika mikaeli na kitabu cha kuingilia mbinguni,akatafuta jina la massawe hakuliona akamwambia massawe jina lako halipo kwenye tarehe ya leo ngoja nikamuulize sir god tupate uhakika, looo malaika kurudi ili ampe jibu masawe kua arudi bado siku yake amefika pale kimakosa,alikuta massawe ameshatimua vumbi na gate la dhahabu halipo tena,

    ReplyDelete
  5. wachagaaaaaaaaaaaaaaaaaa oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  6. iringi ni muziki bila jasho...arawa akitoka kutafuta pesa yake ameshavuja jasho tayari sasa kwanini na mziki acheze kwa fujo? Huwa wanafanya kitu roho inapenda.....

    ReplyDelete
  7. hiyo harusi ilikuwa cheap sana

    ReplyDelete
  8. Hala hala kaka Michu,
    Mambo ya kuvaa suti harusi za watu uache bwana .
    Unaweza kumfofyuzi bi harusi Bwashe akatoa sime bure!
    Na mambo ya vibao vipya kila siku nani anataka.
    ....Kinate Kinanguruma !.....
    Oye oye Kinate kinangurumaaaaaaa
    Tembelea
    www.chagga.com
    kwa habari zaidi !

    ReplyDelete
  9. SASA HIYO SHUGHULI NI YAKO MICHUZI AU NI YA HAO WACHAGA UNAOCHEZA NAO? MAANA UNAONEKANA KAMA NDIO MOAJI WAKATI HAO WENZANGU WACHOVU TU KAMA MAMA, JAPO WAMETINGA TUTAI TWA UONGO NA UKWELI. fEZA NDIO INAZUNGUMZA, HAMNA CHA UCHAGGA WALA NINI. MWENYEWE UNAJIONEA HAPO UNAVYOONEKANA BOSS!

    ReplyDelete
  10. Kuna mchagga alikuwa anatayarishwa kufanyiwa upasuaji wa tumbo.Manesi wakampa nusu kaputi ili alale na baada ya sekunde chache akalala tayari kwa upasuaji.Kwenye harakati za kutayarisha mikasi na bandeji basi kwa bahati mbaya mkasi ukaanguka na kutoa mlio.Mchagga akaamka na kusema "msee kama ni pesa ni sa kwangu" Wakamjibu ni mkasi akarudi kulala.

    ReplyDelete
  11. Hivi ni kweli??Nimesikia ukitaka kujua kama kaburi ni la mchagga au hapana.Dondosha sarafu kama ni la mchagga utaona kaburi linatingishika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...