Vijana wote wa sanaa wa Tz hasa wale mlio pitia Bwagamoyo, mpo hapo? Jana usiku katika pitapita zangu maeneo ya mji wa hapa Cesena katika shamlashamla ya kuikaribisha sikukuu ya x-mas, niliona onyesho hili la mwanadada huyu, mara moja nilikumbuika Bongo-Bagamoyo.
Moyoni nilisema nyie wazungu mmetuzidi mambo mengi ya sayansi na teke linalo kuijia, lakini kwenye swala hili nikasema hata kwetu wapo hapa hamtuzidi, wapo vijana shupavu kwa sanaa.
Ila huyu dada alizungusha moto mpaka niliogopa, watu walichanganyikiwa kwa furaha na kumshangilia kwa nguvu, ni hodari sana, lakini hata sisi tupo. Baada ya onyesho niliweza kuongea nae na kumhadisia kuwa hata kwetu wapo vijana kama yeye, alifurahi sana na kutoa salamu nyingi kwa wasanii wote wa Kibongo.
Basi nawafikishieni salamu zenu popote pale mlipo, tuendeleze sanaa kwa wingi na kujivunia nchi yetu Tz.
Salamu sana Wasanii wote Bongozzzzzzzzzzzz
Kutoka kwa Mdau
Cesena-Italy.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...