Nakupongeza kwa mafanikio makubwa sana ya gulobu yako hii ambayo hata huku kijijini tarime tunaipata.
Kaka yangu Magabe Kibiti amekula nondozz ya masters ya economics kutoka St Cloud State University huko Marekani. Naomba sana uweke picha hizi kwenye gulobu yako ili kumpongeza kwa kumaliza shule.
Ujumbe ni kuwa familia ya mzee Kibiti inamuombea Magabe ili aendelee na kumaliza Phd ya economics. Ombi ni kumtaka arudi nyumbani akimaliza masomo yake ili afundishe wadogo zake hapa Tarime. Mwisho nakutakia wewe na wanagulobu wote mwaka mpya mwema wenye mafanikio.
Asante.
Mariam


Hongera kaka!!!! heri ya mwaka mpya pia!
ReplyDeleteMariam, wewe umemwandikia mtu ambae kapata digrii kubwa kiasi hicho, halafu unakosea, sijui bahati mbaya, hujui au nini. Hii ni BLOG na sio GLOBU. Badilika mwanamke, jifunze!
ReplyDeleteSiyo gulobu tafadhali, ni BLOG, sawa mama? Rudia tena, tena, tena, enheeee swadakta bila shaka hutakosea tena.
ReplyDeleteJamani jamani,
ReplyDeleteHongera sana kaka Kibiti. Yaani nimekuwa excited ajabu kuona habari zako hapa mtandaoni. Dada Mariam ubarikiwe sana. Yaani huyu kaka tumemiss sana hapa kanisa la chuo kikuu mlimani. Imenikumbusha ulivyokuwa unaimbuisha ile kwaya yetu ya kanisa.
Naomba ninukuu sehemu ya wimbe aliokuwa anaupenda sana na alituimbisha kwa furaha yote:
Sing sing Halellujah to the Lord Almighty, .......
Unakumbuka enzi hizo kaka Magabe?
Yaani tunakumiss sana na tumefurahi sana kwa hatua uliyoipiga kimasomo. Kweli Mungu hujibu maombi tumwombapo.
Dada Mariam naomba unipe email yake ili nimwandikie ananifahamu sana nikimwandikia na ninadhani atafurahi pia kusikia habari za chuo Kikuu mlimani.Naomba unitumie kupitia salumayu@yahoo.co.uk.
Ubarikiwe kwa hatua hii.
Ninakutakia pia mafanikio tele hapo Tarime, uende mbali lakini usipotee.
Hongera Mr Petroliii, You will understand what I mean bse I still remember how we went through tough times together as DARUSO leaders in the October 2000 strike/extended meeting.
ReplyDeleteohhh Jamani,
ReplyDeletehongera sana magabe kwa mafanikio haya. maliza shule urudi nyumbani usizamie huko kwa wazungu mzee
umenikumbusha sana maisha ya mlimani na DARUSO.
Hongera
mkitaka majina ya utani marekani sio tarime,marekani paiteni tabora kwani ni kwa wanyamwezi.mdau wa kwa gulity.
ReplyDeleteHongera Magabe! Amang'ana. I am very proud of you. Yeah tunaitaka hiyo PHD ipelekwe Tarime, Keep it up. Mwirege wa Wisconsin
ReplyDeleteKeep it up Mr.Maasa. You are ma' hero......I will always adore you...Hongera sana....Men!!!You deserved it....Goodluck and have a merry x-mass.........
ReplyDelete