pedejee amos ananisindikiza wakati naondoka ukerewe leo kurejea maskani baada ya shoping nzito ya krismasi wikiendi ilopita. ukweni nilishinda siku moja tu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Si unaona....nilijua wewe si mtu wa kukaa sana ukweni!!! Duh!! Lakini nasikia unarudi tena ukweni wakati wa sikukuu.. na sfari hii unakaa wili tatu tu.hizo habari nimezisikia muda si mrefu

    ReplyDelete
  2. Wewe chezea tu pesa upatazo sasa hivi.

    Wanawake wa Kiganda wanapenda shopping hasa nenda kote wanasifika kwa hilo.

    mimi nilioa huko uganda nikamtoroka mchana kweupe tukiwa tunafanya shopping wall street kule USA baada ya kuona VISA kadi yangu inakaribia zero kwa shopping zisizoisha.

    Atakupelekesha huyo hadi akupukute kila kitu kwa shopping za nguo na vinginevyo. Utakoma michuzi aliyekutuma ukaoe mwanamke wa kiganda

    ReplyDelete
  3. Kaka Michu sijakuelewa! ulienda shopping ya Xmas au Idd El Hajj!??
    Shemejio Jose Cameleon ana wimbo mzuuurii...
    "Anapenda vitu vya bei kali..." maliziaaaa

    ReplyDelete
  4. Mithupu nawe kutia chumvi hivi Ukerewe nako kuna London Buses,hiyo picha si ume piga East London hiyo au East Central

    ReplyDelete
  5. DAR TAMBARARE BWANA ...KWANINI UNAENDA LONDON KUFANYA SHOPING YAKO....? UNAWATAJIRISHA WENGINE BADALA YA KUSUPPORT YOUR PEOPLE...JUZI KIPANYA KAANZISHA NGUO ZAKE SASA WEWE USIPOSHOP KWAKE NANI ATANUNUA...SUPPORT YOUR LOCAL PEOPLE NDIO TUTAENDELEA...UCHUMI WA NCHI UNAJENGWA NA WANANCHI WENYEWE...UNATEGEMEA WATU WALONDON WAJE KUSHOP BONGO....?

    WEWE JUZI TU UMETOA MJADALA NA UMEULIZA TUFANYEJE NCHI IENDELEEE....?????? WELL, ONE OF THE REASON NI HII HATUTHAMINI VYA KWETU

    ReplyDelete
  6. Kaka Michu hivi ndivyo ulituambia weekend iliyopita,

    "wadau msione kimya. niko ukweni (UGANDA)kula krisimasi"
    Leo unasema

    " pedejee amos ananisindikiza wakati naondoka ukerewe(UK)leo kurejea maskani baada ya shoping nzito ya krismasi wikiendi ilopita. ukweni nilishinda siku moja tu"

    Halafu moja kwa moja kunakuwa na comments eti za kukuhurumia hivi kuwa wewe ni mtu wa matumizi sana na oh sijui Mganda atakumaliza mara oh nasikia utarudi na kukaa wiki tatu!!!

    WACHAMBUZI MAKINI TUNAKUWA NA WASIWASI JUU YA HIZO TUNGO NA HIZO COMMENTS ZAKO. AIDHA TU WACHACHE SANA TUNAOFAGILIA MTU ANAYEJIFAGILIA MARA KWA MARA KWA UFAGIO ULIO KATIKA DOMEINI YA UMMA KABLA YA KUFAGILIWA.
    ZAIDI YA YOTE, WATANZANIA (WENYE NAZO) WANAFANYA HIYO SHOPPING NZITO WAKIWA HAPO HAPO DAR KWA URAHISI BILA USUMBUFU NA KWA GHARAMA INAYOITA. KAMA HUJAJUA WASILANA NAMI NIKUTONYE MIUNDO MBINU.


    Samahani sana kama nimeongea vibaya pengine tofauti na mitizamo ya wengine. Kazi yako ya kutuhabarisha ni njema sana lakini nakuomba uzingatie kanuni za mahakama ya ustaarabu ambayo mara zote umhukumu ajisifiaye MARA KWA MARA kuwa ama hajiamini au ni limbukeni sifa ambazo naamini kabisa huzikustahili wewe. Sina haja ya kukwambia kuwa usiniminyie hii maana hujanifanyia hivyo.

    Nyakatakule Unyilisya Echalo

    ReplyDelete
  7. huyo Nyerere anageuka kwenye kaburi lake kusikia mmatumbi na mdengeleko anakwenda ulaya shopping!!!ajabu kwamba anazipata wapi hizo sanduko...au malaya wewe???

    ReplyDelete
  8. Anonymous wa Monday, December 17, 2007 10:23:00 PM EAT.....FYI Kwa lugha ya michuzi Ukerewe anamaannisha
    UK..

    ReplyDelete
  9. Thank you anon wa 2:31am for educating me nyie nae mna misamiati mingi duuuuuuuuuuuu!haya tutafika

    ReplyDelete
  10. Mshauri pedejee mwenzio kwamba koti la suti hufungi vifungo vyote kama shati la kulalia - pajama! Koti la vifungo vitatu sharti kimoja kiwe wazi cha juu ama chini; la viwili - cha chini. Mnakaa majuu msijue hata haya ya abc za uvaaji!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...