leo ni vurugu tupu dar. benki zote foleni hadi nje na atm hazifikiki kutokana na wingi wa watu na uchache wa mashine hizo.l foleni barabarani ndo isiseme huku kijua kinawaka kama moto wa pasi ya mkaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. bongo tambarareeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. kwani wanagawa za bure???ah mie pesa zangu nazificha magodoroni!!!

    ReplyDelete
  3. Hiyo sio tambarare kabisa, yaani mtu pesa zake lakini lazima ahenye katika kuzipata, hapa nilipo ni karibu sa sita za usiku na nikihitaji fwedha zangu ninaingia benki yoyote na kadi yangu inafungua milango na fwedha nazipata mara moja kutoka kwenye money machine. Yaani unataka kusema hakuna utaratibu pale wakuweza kuwafanya hao watu wachukue pesa zao mara moja? Bongo jamani mteja si mfalme.

    ReplyDelete
  4. hiyo kali pesa zako mwenyewe tabu kuzipata,mnaosema bongo tambalale mnaishi wapi????hiyo ni aibu kubwa.

    ReplyDelete
  5. Naitwa Mike Mzee.

    Misururu hiyo mkubwa si siku za sikukuu tu, sema imezidi kuwa mikubwa katika sikukuu.

    Mimi huenda benki karibu kila kukicha, misururu ni hivyo hivyo. Inawezekana kuwa ni kwa sababu ya mambo kufanyika taratibu sana hasa wale wafanyakazi wanaokaa katika vile vidirisha.

    Lakini pia misururu huwa haiiishi kwa sababu kuna watu wanaojifanya kuwa ni wazoefu wa benki huzunguka mlango wa nyuma na kutoa tipu za hapa na pale ili wafanyiwe huduma chapuchapu bila ya kujali kuna watu wamepanga foleni tokea asubuhi.

    jamani tusiwaseme polisi tu tuwaangalie pia hawa wafanyakazi wa mabenki namna ambavyo wanavyowanyanyasa watu wanaotaka huduma katika benki zao.

    Juzi juzi tu kuna benki moja eti ilidai kuna moto unawaka hivyo kuwataka watu wote kutoika benki, kumbe ilikuwa mbinu yao tu ya kuwatimua watu kwani hata ATM mji mzima zilikuwa hazifanyi kazi.

    Inaniuma sana lakini sina la kufanya kwani hata nikihama benki nhii nikienda benki nyingine mambo ni hayo hayo tu.

    Tuwapeni vidonge vyao jamani hawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...