abijo kama ilivyokuwa inajulikana simba enzi hizo, kabla ya kuitwa sunderland na baadaye simba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hao walikua simba teyari waliompiga yanga 6-0. pichani nawakumbuka hassan mlapakolo,shaban baraza, mohamed kajole, haidari abeid, omari gumbo, athumani bin juma, abdallah kibadeni, mohamed kajole, abasi dilunga, sadi ali enzi hizo akiitwa (watakiona) na wengine siwakumbuki vizuri.

    ReplyDelete
  2. wee fala hapo juu hata hujui mpira mida hiyo ulikuwa huko kwenu kaishozi unasikiliza mpira kwenye radio chapa mbao 277.Simba iliyoipiga Yanga 6-0 golini alikuwa Omar Mahadhi Bin Jabir,Na hat- trick alipiga Nicodemus Njohole,wengine walofunga ni Thuwein Ally na Abdallah Kibaden.hao unaowataja hapo hawakuwepo.Pole.

    ReplyDelete
  3. Hao simba unaowataja hapo juu waliitoa Hearts Of Oak ya Ghana na kufungwa na Mehalla El-Kubrah ya Egypt kwenye club bingwa ya Africa na sio kuifunga Yanga 6- 0.Ok.

    ReplyDelete
  4. Wee ndio fala cha chandu acha uzushi, thuweni ally na abdallah kibadeni hawajacheza pamoja na wala simba ya akina nico haijawahi kuifunga yanga 6-0, wakati kikosi hicho hapo cha kina kibadeni kinacheza simba wee bado uko kaitaba unanyonya.

    ReplyDelete
  5. michuzi hebu sawazisha mambo angalia kwenye kumbukumbu zako nani mkweli.maana huyu jamaa wa kaishozi naona anachemka.

    ReplyDelete
  6. Nyote hapo juu hamjui kabisa,

    Hiyo ndio simba iliyotinga fainali 1993 kombe la CAF na kufungwa na Stellah Abdijan kwa mabao ya Boli Zozo.

    Namuona Abdul Mashine, Mohamed Mwameja, Nteze John, Kssongo Athuman, George Masatu, Godwin Aswile

    ReplyDelete
  7. Jamani tusaidieni,je kuna mpenzi yeyoto hapo ambaye anaweza kukitaja hicho kikosi kamili bila ya makosa au udanganyivu...Nadhani Gumbo,Kibadeni na Mohamed Tall badi ni active katika ulimwengu huo wa kandanda...labda watusaidie?

    ReplyDelete
  8. Kaka Michuzi.. Ukiisha kutazama ni nani mkweli naomba ubadilishe hilo jina.... Sio Abijo, hata kama ikiwa ni kwa Kiswahili. Ilikuwa inaitwa abijan, kwa kiswahili na Kwa Ki Ivory coast ni Abidjan. AU?

    ReplyDelete
  9. ...kwa mujibu wa kumbukumbu nilizonazo, hicho ni kikosi cha Simba kilichokuwa Mwanza mwaka 1974
    kwenye klabu bingwa ya taifa na kutolewa na Yanga kwenye fainali kwa goli 2-1. hapo ilikuwa ni mechi ya pili ama ya tatu.
    Hapo walikuwa ni akina Adam Sabu,Haidar Abeid, Saad Ally, Khalid Abeid, Kessy Manangu, Abas Dilunga, Aloo Mwitu,Mohamed Kajole, Shabani Baraza na 'Mawe' mengine dizaini hiyo...
    Hapo kulikuwa hakuna cha Nico Njohole wala Thuweni Ally...

    ReplyDelete
  10. kulia waliosimama m.tall bakari,haidari omari,aloo mwitu,m.kajole,idd salum,omar shaaban gumbo,ismail aden,dan mwalusamba,hassan mlapakolo.waliochuchumaa kulia ni kessi manangu,cassim mensah,hassan sakuru,athmani juma, saad ally,hamisi askar,abdallah kibadeni na abbas dilunga. hii siyo timu iliyofunga yanga 6-0, picha hii ni mwishoni wa 1975. 6-0 was 1977 at that time haidari alikuwa na nyota nyekundu. mambosasa hapa hayupo alikuwa anachezea yanga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...