Serikali inakusudia kuifanya Aprili Mosi kila mwaka kuwa siku ya kupanda miti nchi nzima, Kutokana na ukweli kwamba katika kipindi hicho mvua zinakuwa zimechanganya nchi nzima.

Rais Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti kitaifa, zoezi ambalo yeye na Mkewe Mama Salma Kikwete walilifanya leo katika viwanja vya Ikulu, jijini. Januari mosi ya kila mwaka ni siku ya upandaji miti kitaifa.

“ tunajipanga vizuri na wizara ninazohusika, nataka aprili mosi, wakati nchi nzima mvua zinakuwa zimechanganya tufanye zoezi la kupanda miti kwa wingi nchi nzima.

Pamoja na wazo lake hilo la kuitaka aprili mosi kuwa siku ya kupanda miti nchi nzima, rais alieleza kuwa januari mosi bado itaendelea kuwa siku ya upandaji miti na hasa kwa ukanda wa pwani.

“hii ya tarehe mosi januari inaweza kufaa zaidi kwa ukanda wa pwani kwa sababu ndio wakati wa masika, lakini hata kwa ukanda wa pwani, januari mvua zinakuwa zimepungua. Ilikuwa imewekwa huko nyuma tutaendelea kupanda January lakini tutafute siku nyingine na kwa kweli fikra zangu ni kuwa tupande Aprili moja wakati kuna mvua nchi nzima.

Akafafanua kuwa kuanzia sasa hadi mwezi huo wa april utakuwa ni muda wa kujitayarisha na hasa kwa kuzingatia kwamba mwaka huu ni mwaka wa sayari dunia, mwaka wa kutafakari mazuri na mabaya, kuendelea yale mazuri na kufukia yale mabaya.

“ ni mwaka ambao tunatakiwa kutafakari namna gani tutafanya dunia iwe mahali pazuri pa kuishi. Na moja ya jambo ambalo watanzania tunatakiwa kulifanya ni kupanda miti kwa wingi na hasa ukizingatia kwamba watanzania tumekata sana miti na kuchoma sana” akasititiza.

Akizungumzia hoja ya kwamba kupanda kwa bei ya umeme kunaweza kuathiri dhana nzima ya upandaji miti na uhifadhi wa mazingira.

Rais amesema ingawa ni kweli kwamba bei ya umeme bado ni kubwa,lakini kuna ukweli pia kwamba ni asilimia kumi tu ya watanzania ndio inayopata au kutumia umeme nchi.

“ ukweli ni kwamba katika nchi hii ni ni asilimia kumi tu ya wananchi ndio wanaopata huduma ya umeme na waliobakia wanatumia nishati nyingine, tunazungumza tu kwa maana hiyo, lakini kwa kweli na katika mazingira yetu haya si watu wengi wanatumia vifaa vya umeme kwa kupikia kwa miaka mingi watu wanatumia mkaa, wanatumia mafuta ya taa kwa kupikia. Lakini bado ni kweli umeme bei ni juu.
Mama Salama Kikwete akizungumza baada ya kupanda mti wake, naye amewahimiza wananchi na hasa wanawake kujitokeza na kupanda miti kwa wingi.

Akasema kama inavyoeleweka akina mama ndio wanaoathirika wakubwa, kwa hiyo jambo kubwa na la msingi ni kupanda miti kwa wingi katika maeneo yote husika

“tupande miti ya kuni na miti ya mbao, ile ya kuni tutatumia kwa kuni na ile ya mbao pamoja na kuvuna mbao lakini wakati huo huo tutakuwa tunahifadhi mazingira” akasema mama salma.

Mama Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwatakia Kheri ya mwaka mpya watanzania wote na kuonyesha matumaini yake kwamba mwaka 2008 utakuwa wenye kheri na mafanikio kwa kila mtanzania.

Rais na Mama Salma walipanda mti maji (Trichilia Emetica)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Huyu naye mbabaishaji sana. Anadai bei ya mafuta itaendelea kutuumiza, mboa mjirani wetu hawalalamikii bei ya mafuta licha ya kwamba sisi na wao hatuna machimbo!

    Apunguze trips za nje tu. Kwa kweli tumechoka sana. Lakini hatuna la kufanya kwa hakika.

    ReplyDelete
  2. Anony hpo juu hujakosea hata kidogo,hapa hatuna rais ni ubabaishaji tu ingawa yeye ni makini ila tu ni kwamba kazungukwa na wasanii ndo wano mdanganya na it seems anawaogopa!sasa hivi hata hayo mafuta kidogo yaliyopo tunauziwa mifafa tu mafuta machafu balaa,EWURA wapo hakuna wanachofanya zaidi ya kutikisa kiberiti,vituo almost vyote vinauza mafuta machafu sasa hivi!Apunguze trips za nje aokoe hili jahazi.

    ReplyDelete
  3. Hivi kweli president yuko serious na hii issue,leo unahimiza watu wapande miti ya kuni!Maisha bora kwa kila Mtanzania ndo yatapatikana kwa kupikia kuni?Gas yote ya Songosongo tutaipeleka wapi?tatizo hapa ni matumizi mabovu ya hazina ya Taifa,eg ununuzi wa rada,ndege ya rais,mikataba mibovu kama vile IPTL Richamond,Kiwira,Meremeta na mengine mingi tu,right kwamba tungelikuwa makini hayo mapesa tuliyopoteza kungelitengeneza project ambayo watu wote mpaka vijijini wangeliacha kutumia kuni,mbona hakuna hata nyumba moja ambayo kwa siku haitumii mafuta ya taa kama nishati vijijini?That means kama kila kaya kijiji kwa siku inatumia mafuta ya taa then hata gas ingeliwezekana tu.

    ReplyDelete
  4. Michuzi kinachosikitisha hapa kwetu Bongo kila kitu ni kampeni nina shaka kuna siku Kikwete atakuja kutangataza itakuwa siku ya kujenga barabara.
    We subiri siku hiyo fulana zitatengenezwa kwa gharama kubwa kuliko hata hiyo miche itakayo pandwa. We kama unataka kujua labda muulize kiongozi mmoja wa serikali kama ana fulana ngapi za kampeni kuhusu kitu chochote hapa bongo kwanza atakuwa hakumbuki.
    Jamani Kikwete lete maendeleo achana na porojo za kampeni nchi haiendi hivyo jamani

    ReplyDelete
  5. Hivi jamani hamjashituka kwamba April Mosi ni siku ya ....ahhh hebu nikumbusheni nimesahau.Mapombe ya new year eve na mwaka mpya wenyewe yameharibu brain.Kesho nitakumbuka lazima.

    ReplyDelete
  6. SIKU YA WAJINGA DUNIANI.

    Mmmmh sijui vizuri kwa nini imechaguliwa hii siku kwa ajili ya kupanda miti.Nahisi watu hawatajitokeza kupanda miti kwani siku hii nayo imekaa vibaya ukizingatia ndo siku watu huwa wanadanganyana na kuongea UONGO.
    Haya ngoja tusubiri siku ya wajinga kuwa siku ya kupanda miti Tanzania.
    Majita

    ReplyDelete
  7. Hata hiyo gas ya SongoSongo pia inahitaji miundombinu kuisambaza kwa sababu ni natural gas na si kama hizi gesi mnazotumia kupikia majumbani za Oryx. Ukishaingizwa hiyo gharama ya mabomba ya kupeleka gesi asilia ya Songo Songo katika bei ya kununua hiyo gesi ni watanzania wangapi wa vijijini wanaweza kumudu kulipia hiyo gesi ili wapikie? Kulonga mbali na kutenda mbali sio ili mradi tunasema tu. Tuache kujidanganya kuwa wananchi walioko vijijini wataacha kupikia kuni kwa ushabiki wa kisiasa wakati hali halisi inajulikana, Iwapo 10% tangu wakati wa uhuru mpaka leo ndio wanatumia umeme na asilimia 90% bado wanaishi katika giza je unategemea hiyo asilimia 90% ghafla hii watapata uwezo wa kununua gesi ya kupikia.

    Safari bado ni ndefu wala tusijidanganye kwamba kuna mwanasiasa ambaye angeweza kuondoa umaskini uliopo na kuwezesha hiyo 90% kuweza kutumia umeme na gesi ndani ya miaka 2 ya utawala wake, huu ni ushabiki wa kisiasa, hata hizo MDGs zenyewe zaambiwa ziko too ambitious kwa muda walioweka wa kuondoa umaskini. Tunahitaji waliochukua resources zetu tangu enzi kabla ya ukoloni na wakati wa ukoloni waturudishie mali zetu na vile vile huu mfumo wa mpya (new world order/globalization) tupambane nao ili wasiendelee kupora utajiri wetu kwa kushirikiana na wenzetu wachache.

    Tunahitaji kutumia rasilimali zetu kuboresha maisha yetu, kuhakikisha kuwa elimu, afya, lishe, na miundombinu vinapatikana. Mazingira ya vijijini yanaboreshwa na wanachi wanashiriki katika kuboresha hali zao kwa kusaidiwa na serikali, sio kukaa kusubiri serikali itufanyie kila kitu. Tunahitaji na sie tulioko mijini kubadili tabia zetu za uvivu na utoro makazini, wizi na ufisadi (hapa wote wanaojifanya wanakula sehemu yao ya kazi haijalishi kuwa ni mwanasiasa au mwananchi wa kawaida) na ulipaji kodi kwa wafanyabiashara ili kuiwezesha hiyo serikali kutekeleza majukumu yake. Huko mliko mnafaidi matunda ya kodi za wenzenu ambao wanatoa katika serikali zao. Tunahitaji uwajibikaji kote kote kwa raia na serikali kuanzia ngazi ya afisa mtendaji wa kijiji mpaka ngazi ya juu kabisa hapo ndio tunapoweza kuona maendeleo ya kweli.

    Kila siku serikali itufanyie itufanyie sie tumefanya nini ili kuiwezesha hiyo serikali itufanyie hayo tunayotaka tufanyiwe? Tunalipa kodi kiasi gani mpaka tukichanganya na hayo madini tutakuwa na sisi kama Brunei?

    ReplyDelete
  8. Hivi hamjui wengine hii siku ni sikukuu yetu sie tuliopungukiwa uwezo wa kufikiri? Sasa kuifanya siku ya kupanda miti ni nini...!! Michu wewe upo karibu na Jk mshauri aibadilishe aweke hata tarehe mbili basi...hii siku ina wenyewe jamani...!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...