Michuzi,
Jana nimejenga hoja kuwa kama kweli wanataka kukomesha mtandao wa wahalifu katika ngazi mbalimbali za serikali na utumishi wa umma, hususan kuanza na BoT, wampe kinga ya kisheria (immunity) aliyekuwa Gavana wa Benki hiyo Bw. Daud Balali ili aweze kuwa shahidi na kutoa msaada wa kutambua kilichoendelea Benki Kuu bila hofu ya kile atakachosema kutumiwa dhidi yake katika mahakama.

Ni hoja ndefu, na kabla hujashtuka na kusema "kinga ya nini" tafadhali soma nilichosema halafu tuwe na mjadala mzuri. Angalia kwenye editorial ya KLH News. Na pia unaweza kuisoma kwenye Tanzania Daima toleo la Januari 22, 2008. Je, serikali watakuwa tayari kumpa kinga Balali? Je kumpa kinga kutasaidia kuwatambua watu wengine? Je kumpa kinga kutasidia kutuonesha fedha zetu ziko wapi?

Title: KLH News Episode: Balali apewe Kinga!
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2008-01-23T21_14_12-08_00
Enjoy!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

 1. Mimi naungana na wewe Mwanakijiji katika hoja yako. Kusema kweli hoja yako ni ya msingi sana, hasa ukizingatia kuwa Balali amekaa kimya kwa muda wote huu ambao sakata hili limekuwa likiendelea. Ukimya huu unaweza ukawa na maana zifuatazo

  1. Kuwa anakubaliana na shutuma na hana cha kusema kwa maana ya kujitetea, anaacha nature ichukue mkondo wake, si unajua Tanzania, watu wanaweza kupiga kelele wee, mwishowe wanasahau, au linatokea tukio lingine linawakumba na wanasahau, tumeshayaona mengi yamepita, tumeyasahau.
  2. Balali anakaa kimya kwa vile hajui hatima yake kama akisema chochote. Kuwa anawafaham watu wahusika wakuu wa sakata hili lakini anaogopa kwa vile akisema tu wanammaliza. Sio tu kusema hata kuonekana hadharani inakuwa issue.

  Kwa maana hiyo basi, akiwekewa Kinga, anakuwa na confidence na kuweza kueleza mwanzo hadi mwisho wa mchezo, na hapo ndo itakuwa rahisi kwa serikali kuwanasa wote wale waliohusika

  Hata hivyo itakuwa vigumu kwa serikali kufanya hivyo ikiwa kama kuna viongozi wazito waliohusika kwenye ufisadi huu

  Nawakilisha

  KAS

  ReplyDelete
 2. mdau uliyetoa propozo ya kinga mi nadhani unafurahisha baraza.umewahi kusikia neno'real politik'?ni neno la kijerumani by the way,tafuta maana yake.

  ReplyDelete
 3. NAFIKIRI NCHI ZILIZOENDELEA INAWEZEKANA KUMPA KINGA KAMA WALIVOFANYA WANAJESH WA MAJI MEUSI UKO GHUBA SHIDA SIO KUMFUNGA BALALI MUHIMU NI WAONGEE UKWELI WANANCHI WAWASAMEHE UFISADI UISHE HAINA MAANA AKIKAA GEREZANI ALAFU MBINU ZA UFISADI ZINABOREKA TUTAKUWA TUNACHZA MCHEZO PAKA NA PANYA.

  MWNA WA TAIFA TUMAINI GEOFREY TEMU AKA PROF DR ING

  ReplyDelete
 4. Hii katika kuthibitisha u milioni 3 wang

  ReplyDelete
 5. You right, hiyo itakua babu kubwa sababu balali hawezi kukubali kufa peke yake huku kuna watu wangine walishika mshiko mkubwa zaidi.

  ReplyDelete
 6. Mi nafikiri hakuna cha kinga wala nini,

  Kama ni hivyo basi wezi wote wa kuku Manzese na andale wawe wanapewa kinga ya kutoshtakiwa then ndo waeleze vizuri walivyoiba hao kuku.

  Huyu jamaaa akija akamatwe, awekwe ndani ili awe mshitakiwa, then yeye ndo ataeleza kama ni yeye au sie alieiba.

  ReplyDelete
 7. Jamani hii sio hoja muhimu wala maarufu. Kinga ya nini wakati alionyesha kiburi na hakutaka kutoa information yoyote alipohojiwa na waandishi. iweje leo awe ndio credible source na kupewa ulinzi. Suppose he is dead?
  Hana jipya? Kina Balali ni wengi mno. yeye ni 0.000001 ya mabalali waliomo ndani ya Bongo na wanapeta kwa jeuri bab kubwa. No one can do shit to them Balalis. Mahalu,Yona Mkapa,Jeetu wapo na kampuni zao zipo zinachota na zitachota bila kunaswa. Uchungu mwingi kaa huko ughaibuni au anzisha blog na kupiga kelele nyingi sana. Watu wanacheza na CCM. Inasemakana ni chama cha kuondoa umaskini kwa njia ya ufisadi. Big fish is eating small fish day by day.

  ReplyDelete
 8. sisi tunataka hizo dola kwanza.
  felma2001us2yhaoo.com

  ReplyDelete
 9. ninavyoliangalia hili sakata la BOT, ni kwamba BOT kama Bank ina customers mbao ni pamoja na serikali na commercial banks. Ili account ya serikali iwe debited, instructions zinatoka serikalini (wenye account). Hivyo wizara ya fedha, katibu mkuu wizara ya fedha, mhasibu mkuu wa serikali etc inabidi watoe instructions za malipo!
  kumuadibisha Gavana na labda management ya BOT ni kiini macho tu, maana inabidi uelewe kuwa BOT ni watekelezaji tu wa instructions ambazo zimetoka serikalini.
  Kitu ambacho mpaka sasa hivi hakijafanyika ni kuangalia huko instructions zinapotoka!!!!!!?.
  kwa analysis yangu ya haraka haraka ni kwamba Balali hawezi kuwekewa hiyo 'kinga' maana atavumbua yale ambayo hayatakiwi kujulikana!!!!
  Nachangia HOJA.

  ReplyDelete
 10. Michuzi mdau milioni tatu........chupu chupu niwe mimi, ila chuki binafsi kibao....mara oooh error # 10...kidogo nikawa wa 2,999,997 nafungua tena, error # 10...Nataka kupiga picha niwe na ushahidi wa kutosha kamera yangu ikaishiwa baterry.....

  Aisee wadau "wanaroga" hata mambo ya kuwa mdau wa milioni tatu....Mwenzao nimekesha ofisini leo ili nishinde hiyo dola 500 niongezee kwenye kodi ya nyumba....Anyway, hongera Michuzi kwa blogu yako kutembelewa na watu milioni tatu so far

  ReplyDelete
 11. Michuzi, mdau toka Japan hapa, nitakuwa nimelamba hiyo dola 500, kama mchezo unakwenda kwa HAKI bin SAWIA. Email yangu ni:
  ki0021ma@tiu.ac.jp

  Nakutumia uthibitisho dk 2 zijazo

  ReplyDelete
 12. MIMI NI MDAU WA MOSHI NLIKUWA WA 29999998 NA PIA 30000002 NAFIKIRI HUYU MDAU WA JAPAN MTANDAO WAKE SIO MCHEZO TUNAMUOMBA ATULETEE NYUMBANI MAANA TANZANIA KUANZIA MWAKA 2035 ITAKUWA NCHI YA KWANZA KUTUMIA SEREKALI YA MASAFA ILI KUEPUKA UKOSEFU MAARIFA WA SIKU ZA MWISHO UTAKAYOYAKABILI MATAIFA YA ULAYA AMBAYO SEREKALI ZAKE NA NAKAMPUNI MPAKA ZIWAONE WAFANYA KAZI KWA MACHO KWA HIYO KILA WMANANCHI ANAKUWA NA GARI MSONGAMANO ITAFIKA KIPINDI ITAANZIA KWEYE UZAMILI CHUMBA CHA KULALA(MASTERBEDROOM)TUNA TEGEMEA MALKIA WETU WA WAKATI HUO ATAKUWA ANAHUTUBIA KUTUMIA PICHA MWENDO MASAFA NAFIKIRI MAGARI YATATUMIKA KWA AJILI YA SUGHULI ZA UJENZI NA DHAULA KAMA KUMUONA MGANGA AU MGANGA KUNUONA MGONJWA. HII NI HABARI NJEMA WATANZANIA KWANI MAFUNZO KWA AJILI YA MFUMO HUO MPYA WA SERIKALI UTAANZIA NYUMBANI KAMA ILIVYO ADA. NINAHITAJI UTULIVU WENU WA HALI YA JUU ILI TUSIENDELEE KUUKALIA UCHUMI WETU. ENU KATIKA UJENZI WA DUNIA

  TUMAINI GEOFREY TEMU AKA PROF DR ING

  ReplyDelete
 13. Nadhani hii sasa ni ya ushindi.
  rdor7819@hotmail.com

  ReplyDelete
 14. Hamna lololte aadhibiwe tuu kwani hakimu akikupa hukumu anasema iwe mfano kwa wengine anmaanisha nini ?
  Na hivi wanavyomchelewesha anaweza akavuta halafu ushahidi wote ukapotea na mfana usiwe
  hili ni fundisho kwa woote

  ReplyDelete
 15. mimi ni mshindi wa dola 500, nifahamishe kupitia simu yangu ya ofisini 2185009-hellen

  Thax

  ReplyDelete
 16. Wazo zuri sana ila ni kama kesi ya........, kumpelekea........! Kwa kiingerezaz wanasema Good idea for nothing!

  We Mwanakijiji bongo yetu unaijua vema, na unajua fika hii shutuma/ufisadi Big fishes (Waliopo serikarini) wanahusika moja kwa moja, then ETI hao hao wampe protection aweze kuwataja hadharani? Hivi hii kweli inawezekana jamani? Hii kitu haipo bwana, na vile haiwezekani Mi naona huyu jamaa (Mshikwa na ngozi), ashtakiwe kivyake, wakipakitanaga wengine Ishaalah. Asipewe cha kinga wala Kingo. Atatupotezea muda tu.

  Michuzi mimi ndo yule mdau wa $ 500, cheki fresh hiyo tuk tuk yako.

  ReplyDelete
 17. i sayyyyyyyyyyyyyyyy

  ReplyDelete
 18. Mh, huyu Mwanakijiji si ana blog yake jamani, kwa nini hii Mada asiiweke huko kwake wadau tutaenda kuchangia huko huko?

  Au na yeye anawania USD 500? Tuambiane Mwanakijiji, au wadau hawatembelei blog yako vile unabania comment zao wametimua nini?

  Michuzi blog JUU, JUU, JUU ZAIDI. Inafunika eh?

  Na we michuzi usiibanie comment yangu. Na kwa taarifa mi ndo mdau wa hiyo USD 500.

  ReplyDelete
 19. Mdau masaki hii ni ajabu leo asubuhi nami nilipata hiyo namba 2999997. Mbona hiyo counter noma?

  na katika kubonyeza tena ikawa error #10 zikaja

  Michuzi tangaza mshindi basi aliyeshinda najua ilikuwa 8 twenty something am UK time

  sema kitu basi, umeshatumiwa evidence?

  ReplyDelete
 20. hello friends. just dropping in, searching for 'tanzania'. this is the first time i read an african language in a blog.

  great site. keep on blogging. greetings from malaysia. :)

  ReplyDelete
 21. michuzi mimimdau helsink nimeshinda

  ReplyDelete
 22. Hakuna cha kupewa ulinzi wala nini. Ye akamatwe huko alipo na afikishwe mahakamani ashitakiwe kama wezi wenzake (wengine).

  Hatutaki ushirikiano wake kuwapata hao wengina. Na wao watapatikana bila msaada wake kama alivyopatikana yeye.

  "Ukipata mihogo, utavuna mihogo na sio mahindi ebo"!

  Michuzi $500 ni yangu.

  jina_langu@yahoo.com

  ReplyDelete
 23. Anaweza kupewa kinga, lakini lazima aonje adhabu ya aliyoyafanya, then we can negotiate and make him a hostile witness.

  ReplyDelete
 24. Anatakiwa ashitakiwe na kama atapatyikana na hatia ahhadiwe kupewa hiyo kinga (au hata chanjo) kama atatoa ushirikiano na Polisi. Offering immunity at the very beginning would be good news for any culprit - in his shoes, I would welcome it and just walk into the Dar High Court to state that I did nothing wrong.

  I think people like Balali (or is it Dalali?) should be ashemed of themselves and how they bring professionalism into disrepute. I bet Idrissa will be laughing...

  ReplyDelete
 25. waliodhinisha akiwemo pay master general (if u knw wat i mean) ni PS G MGONJA ambaye bado ni MJUMBE wa bodi MPYA YA BOT ILIYOAMBIWA IRUDISHE IMANI KWA WATZ je? hii iko sawa kweli wadanganyika wenzangu?

  ReplyDelete
 26. UNAJUA SISIS NI WACHEKESHAJI WAKUBWA SANA.SASA SERIKALI ITAMKINGAJE MTU AMBAYE ANATA KUWAUMBUA? KASHIFA YA SERIKALI NDIO IMEHUSIKA KWENYE SWALA LOTE ,SERIKALI HIO HIO UNATAKA IMLINDE HUYU BALALI? SASA NA HIO SUMU INAYOSEMEKANA KAPEWA BALALI ILIYOSABABISHA YEYE KULAZWA KAEKEWA NA NANI? MNATANIA WAKUBWA HILO SOO JINSI SIKU ZINAVYOKWENDA NDIO USHAIDI UTAKAVYO POTEA NA TUTAONA MWISHO WAKE.HIO SKENDO UKISEMA DR.BALALI ASIMAME LEO ATOE USHAIDI SERIKALI ITAUMBUKA VIBAYA SANA. HAYO NDIO NA WAAMBIA NA NAKUOMBA KAKA MICHUZI HUWEKE HII WATU WASOME INAONESHA KUNA HOJA NZITO SANA UNAZIKUEPA NAJUA UNAFANYA KAZI SERIKALINI LAKINI NDIO KAZI YAKO SASA KUWEKA HOJA HUMU BILA KUANGALIA INALENGA UPANDE GANI.

  ReplyDelete
 27. mimi naona huyu Balali kama anaona ameonewa basi afanye hata teleconference na waandishi wa habari wa hapa then aseme ni nini kilitokea.Kwasababu kama ataendelea kukaa kimya itakuwa anaonyesha kuwa anahusika moja kwa moja na kashfa hii. Na kwa taarifa yake huku nyumbani watanzania wengi hawataki kuamini kama ni yeye ndie muhusika mkuu wa haya mambo kama viongozi wa serikali wanavyotaka watz waamini kwa sasa.Mimi binafsi kwa jinsi navyofahamu system ya serikali yetu namuonea huruma sana mh. Balali kwani tupende tusipende huyu bwana kafanya mambo mengi sio Tz tu bali duniani kote.Na sitaki kuamini kuwa mh. Balali anaweza kukubali ujuzi,elimu,uzoefu wake alioujenga kwa miaka yote mwenyezi mungu aliyompa hapa duniani upotee kirahisi unless sababu iwe ni kwamba amehusika binafsi kuifisadi nchi yetu.
  kwa system ya uendeshaji nchi yetu ni rahisi sana kukolimbwa kabla hujafanya chochote cha kuisaidia nchi,mifano ipo!
  So mh. Balali,nikiwa bado ni miongoni mwa watz ambao tunaamini kuwa tunachoelezwa na serikali yetu si ukweli hasilia wa kilichotokea BOT,naomba utoe neno!Otherwise nitafuta imani yangu niliyokuwa nayo kwako,ambayo nina uhakika kuwa itaniathiri sana kwa sababu mimi bado ni mwanafunzi na nilikuwa na admire the steps you followed in your life.

  ReplyDelete
 28. nimefuarahi mambo mawili:
  1. Wadau wa UGAIBUNI NJAA KAlI wataka ponea kwa Michuzi
  2. Michuzi kaikwolaizi, kugawa ushindi home ili wadau wa home waache kuchonga

  ReplyDelete
 29. Fisadi mkuu apewe kinga ili ataje mafisadi wenzake?! Na Patel nae apewe kinga? Na wale watoto 17 BOT wa vigogo nao wapewe kinga ya kutotimuliwa au kushtakiwa kwa rushwa ili wawataje waliohusika na ajira zao? Na Mr. na Mrs Kiwira nao wapewe kinga ili wawataje waliowauzia mgodi?

  Mafisadi wengi wanajulikana na kupata ushahidi na wengine zaidi sio ngumu kiasi hicho. Tuwe serious na tuwachukulie hatua kali. Watu wengi wamekufa kwa kukosa huduma muhimu kwa sababu ya ulafi wao!

  ReplyDelete
 30. Michu huyu fala mwanakijiji anapenda sifa na kujitangaza sana akiandika kitu anatuma kila mahali usimkubalie tena kuweka utumbo wake balali na mafisadi wenzake hamna kinga wala nini

  ReplyDelete
 31. Itakua kosa na kebehi kwa mfumo wa sheria kumpa kinga Balali.
  Kuhusu swala wa kuwataja inawezekana kuwataja kama atakata ziko njia za kumlazimisha muhalifu kutaja nikimaanisha kutumia nguvu (torture).Kama wanavyo fanyiwa wahalifu wengine
  Kuhuibia TANZANIA ni kuwa torture msikini walio wengi vijijini (wakulima)kwahiyo na yeye anastahili.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...