Sir,
I write to request for your assistance in the form of linking me with any football agent in the Republic Of Tanzania.

My name is Julius Chakupewa (in red and white above). I was born in Zimbabwe and my late father was a Tanzanian national who migrated to Zimbabwe in 1975. I thus have decided to relocate to Tanzania at the beginning of 2008 and wish to link up with any footbaall agent who may assist me in finding a Soccer Club in Tanzania.

I have played soccer in Zimbabwe's Premier Soccer League for the years 2004-2006 and had recently been playing in Division one. I am an attacking midfielder and is also comfortable playing as a striker.

Your assistance in this regard will be highly appreciated.

I would also appreciate if you could link me directly with any Soccer Club.

Thank you in advance.
Yours truly

Julius Chakupewa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Yakhe Chakupewa,Hilo ulichopewa kipaji cha kusakata dimba basi lichukue pengine labda Sauzi au Uarabuni kwani hapo bongo mjomba ni dhiki tuu,kiwango chetu kidogo na viongozi wa vilabu vikubwa kujishughulisha na migogoro,ufisadi,rushwa n.k.
    Sasa baada ya nasaha yangu,bado unataka kuja,basi timu yangu ya Wanajela wa Mbeya...tunakukaribisha!!!

    ReplyDelete
  2. huyo kijana anamkimbia mugabe!karibu kwetu au niseme karibu kwenu

    ReplyDelete
  3. Well, surely there are relations that will be able to match your story that are still alive in Tanzania. It would probably be a good idea if your Mother or someone could give you more insight as to who your relations are and where they may be from exactly in Tanzania. Once you have managed to get this information the next step would be to convince the authorities.... after that it will be "Karibu nyumbani" (Welcome home). All the best.

    ReplyDelete
  4. Mpeleke Jangwani dogo huyo nenda kwa wakweli Hapo jangwani

    ReplyDelete
  5. mr michuzi huyu anakimbia ukata wa zimbabwe, anataka kuja kujilipua bongo, ama kuitumia bongo kama daraja kwenda anakotaka, ogopa sana watu wa aina hii, na matapeli wakubwa kuliko hata wale wanaigeria wanaokesha wakituma email za pesa mingi wakati hawana hata pa kulala, hii ni aina mpya ya wizi, kaa chonjo mkuu!!

    ReplyDelete
  6. kasheshe za zimbabwe ndio zinataka kumrudisha tanzania huyo wanatafuta njia yoyote ya kutoka nchini kwao sasa hivi njaa kweli

    ReplyDelete
  7. kaka michuzi kazi hio tumekuachia wewe manake wewe ndio mkuu hapa mjini kijana anatka kuja kucheza soka akikisha asiangukie kwenye mikono ya matapeli na utu update umemsaidia vipi na mmefikia wapi.anaweza kuwahi mzunguko wa pili au unasemaje kaka? aje kufanya majaribio.

    ReplyDelete
  8. CV mona haiko kamili. Premier ya Zimbabwe alichezea timu gani na alishinda nini? Akija aanzie kujenga jina mchangani kabla ya kupanda timu kubwa. Soka la bongo sio rahisi kama wengi ambavyo wanapenda kutupotosha humu ndani.

    ReplyDelete
  9. Huyu njaa tu inamsumbua maana wa zim wengi sana wanakimbia kwao kuna mmoja nilikutana nae SA anasema harudi tena kwao amekuja south na manguo na vitu vyake vyote..bro michu sasa huyu kijana alikuwa wapi mda wote mpka iwe kipindi hiki hali ya uchumi imeyumba ndo anakumbuka baba yake aliyekuja kusaidia ukombozi wa Zim!

    ReplyDelete
  10. Chakupewa karibu nyumbani, huna haja ya kuomba chochote kuwa mtanzania. Hata kama baba yako asingekuwa mtanzania wa kuzaliwa, kama wewe ni mwafrika mweusi basi wewe pia ni mtanzania. Don't ask for anything just take it, as long as you don't break the law of the land.

    Afrika is one.

    ReplyDelete
  11. Waswahili wanasema hujafa hujaumbika. Nikiwa mwanafunzi na damu inadai nilifika Harare mwaka 1988 nikitokea Ulaya. Maisha niliyoona pale - kama mbongo niliyekuwa nimetoka kwetu some four years earlier kukiwa hakuna hata unga - yalikuwa sawa na maisha ya Ulaya. Miaka minane baadaye nilikwenda tena Harare na kukuta bado kunadai. Leo hii kijana wa watu kazaliwa pengine hakujaliwa kuyaona mema ya Zimbabwe - kwa nini asifikirie kumtafuta babu yake popote alipo. Anayesema Bongo njaa hajaona wala hajui njaa.

    ReplyDelete
  12. Jamani nyie watu mnaomsema kijana wa watu eti anakimbia shida. Kwani hata kama ni hivyo kuta tatizo gani? Yeye amejiemeza kuwa baba yake ni Mtanzania, kwa hiyo na yeye pia( by implication). Kwani kati yenu ni nani ambaye anaishi pale alipozaliwa? Dunia ya leo ni ku-move kule kwenye opportunities.

    To Julius:
    Please visit http://www.yangatz.blogspot.com/ and post what you need there. You will be directed to contact the Jangwani club for trials.

    Good luck and welcome home.

    ReplyDelete
  13. Go Julius goooooooooo!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...