RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini leo mchana kwenda Addis Ababa, Ethopia, kuhudhuria kikao cha 10 cha Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Kikao hicho kinaanza kesho (31 Januari) na kumalizika Jumamosi Februari 2, 2008.
Ajenda kuu ya kikao hicho cha mwaka huu ni “Maendeleo ya Viwanda katika Afrika”, mada inayolenga kuchochea mawazo mapya miongoni mwa mataifa wanachama wa AU kuhusu jinsi gani maendeleo ya Afrika yanavyoweza kusukumwa mbele kwa kutumia uzalishaji wa viwandani.
Kikao hicho pia kitamchagua Mwenyekiti mpya wa Umoja huo.
Kwa kawaida Mwenyekiti wa Umoja huo hupatikana kwa njia ya mzunguko wa kikanda (geographical rotation). Kwa mujibu wa utaratibu, Mwenyekiti huyo mpya anatakiwa kutoka nchi za Mashariki mwa Afrika.
Eneo hilo linazo nchi 14 ambazo ni Burundi, Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, Sudan, Tanzania na Uganda.
Mbali na kuchagua Mwenyekiti wa AU ambaye huwa ni mkuu wa nchi mojawapo wanachama wa Umoja huo, mkutano huo utamchagua pia Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Afrika.
Wagombea sita wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ambayo inaachwa wazi na Alpha Omar Konare wa Mali, ambaye anamaliza muda wake na pia kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Miongoni mwa ripoti zitakazowasilishwa na kujadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na ile ya Kamati ya Mawaziri iliyopewa jukumu la kutoa mapendekezo kuhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja ya Afrika.
Ujumbe wa Rais kwa ajili ya kikao hicho unamshirikisha Mama Salma Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Wengine ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Basil Mramba; na Waziri wa Biashara, Viwanda, Masoko na Utalii wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Samia Suluhu Hassan.
Rais na ujumbe wake atarejea Dar es Salaam Februari 3, 2008
Uenyekiti apewe Mheshimiwa Kagame. Maana Vasco Dagama wetu ana majukumu mengi mno! Iam sure Kagame is best for this role! Akiongezewa na hilo la uenyekiti ndo atahamisha ofisi kabisa na kwenda kuishi Addis!
ReplyDeleteGo Kagame....
Kweli bwana!!! Kuna mdau alitabiri humu kuwa "VASCO DAGAMA" ataelekea Ethiopia muda si mrefu baada ya kuteua balozi wa Tanzania huko!Alisema kuwa jamaa huwa haendi mahala ambapo hatuna Balozi. Kweli mdau nimethibitisha maneno yako.
ReplyDeleteSasa kule Addisibaba watapiga gumzo gani jamani?mie naona watacheza bao na karata na pia watalinganisha masuti kwamba nani kavaa more expensive!!!
ReplyDeleteNAKUMBUKA KAISTORIA KANGU NILICHOSOMA BABA WA TAIFA NA WENZAKE WALIJIUNGA KUZIKOMBOA NCHI ZA AFRICA KUTOKA UKOLONI. KABLA YA HAPO WASHIKAJI WALITUPIGA BAO BAADA YA KUFANYIWA KAZI BURE NA WATUMWA. SASA WAMETAJIRIKA KWA NGUVU ZA WATUMWA. SASA KAMA SISI TUNATAKA TUENDELEE KAMA WAO TUTAPATA WAPI WATUMWA WA KUWADOZIA. INAWEZEKANA WADAU INA INA BIDI TUFANYE KAZI KWA CHAKULA NA MALAZI NA NGUO YAANI BASIC NEEDS HILI VITUKUU VYETU VILE KUKU KAMA BAADHI YA NCHI KULE BARA ASIA
ReplyDeleteKuna Mdau alitabiri juzi tu kuhusu ule uapishaji wa balozi mpya Ethiopia.Ama kweli duniani kuna kuna mambo!
ReplyDeleteJK mkifika huko mkutanoni please mwekeni kiti moto Mwai kibaki kwa kutoa amri ya kuua wananchi wake. Na ikiwezekana mfukuzilieni mbali asihudhurie kikao hicho anatuharibia sifa waafrica.
ReplyDelete