Jk akimkaribisha Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi katika uwanja wa ndege Mwanza leo mchana.Baadaye viongozi hao walifanya mazungumzo Ikulu ndogo ya Mwanza. Wakionge na waandishi wa Burundi na Bongo baada ya mazungumzo yao, viongozi hawa walionesha kuridhika kwao na maendeleo ya kurejesha makwao wakimbizi wa Burundi walio Bongo na kuwataka maafisa wahusika wahakikishe mstari mfu wa zoezi hilo unazingatiwa. Pia Jk aliwahakikishia warundi azama ya Bongo kuendelea kuweka wazi milango ya bandari ya Dar katika kupitisha mizigo ya huko ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wa huko. Kuhusu hali ya kisiasa na kijamii kwa watani wetu wa jadi viongozi hawa walielezea matumaini yao kwamba wapinzani na serikali watatafuta muafaka ili ukanda huu wa bara la afrika uendelee kuwa wa ustawi na amani. baada ya ziara hiyo fupi Mh. Nkurunzinza alirejea nyumbani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii ndo inaitwa 'flying visit...brekifasti Bujumbura...lanchi Mwanza...tea...tena Bujumbura!!!na sasa twangoja kwa hamu wapi Vasco Da Gama wetu ataelekea baada ya mapumziko ya masaa machache ikulu...labda Nairobi akawasuluhishe Mkikuyu na Mjaluo waanze kupatana!!!

    ReplyDelete
  2. JK naomba mfundishe Nkurunzinza kwamba koti la suti lenye vifungo vitatu kifungo chachini kabisa ni MWIKO kukifunga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...