HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI LEO IMEWASIMAMISHA KAZI MADAKTARI 7 NA WAUGUZI 3 KWA TUHUMA ZA KUSABABISHA UPASUAJI TATA WA WALE WAGONJWA WAWILI WA KICHWA NA MGUU AMBAPO MMOJA WAO ALIFARIKI DUNIA NA MWINGINE YUKO NJE KWA MATIBABU ZAIDI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mimi napenda kuchangia hii habari kwa mtazamo wangu ambao najua unaweza kutofautiana na wengi hapa. ndio huu uzembe ulifanyika katika kuwaandaa na kuwafanyia upasuaji hawa jamaa hilo ni kosa, lakini wasishikie sana bango kwamba mgonjwa mmoja alifariki (hapa natoa pia pole kwa wafiwa wote), ukweli ni kwamba mgonjwa aliyefariki, alifariki kutokana na ugonjwa aliokuwa nao, ni kwamba ule ugonjwa ulichelewa sana kutibiwa kutokana na foleni ya kusubiri tiba katika ile hospital ya rufaa (Muhimbili). ndo kusema huu uzembe unawahusu wengi kuliko inavyoweza kufikiriwa, maana serikali ndo mzembe mkuu katika hili, kwani hospitali ya rufaa kama muhimbili ambako wagonjwa wote walioshindikana katika hospital zingine wanaletwa hapo halafu wao wana chumba kimoja tu cha upasuaji, unategemea nini hapo, ni lazima kutakuwa na foleni ndefu sana ya kusubiri matibabu na ndo kilichosababisha mgonjwa akachelewa kufanyiwa upasuaji na hatimaye ule ugonjwa aliokuwa nao ulifikia point ambayo huwezi kuutibu tena. hebu fikiria hospital ya taifa inakosa vyumba vya kutosha kwa kazi kama hii ya upasuaji, kuna majengo pale muhimbili mimi nilianza kuyaona yanakarabatiwa muda mrefu sana, sijui jamaa walikula pesa, maana ni muda mrefu sana, japo nimeona kuna jengo moja limekabidhiwa jana, lakini hilo nalo limechukua muda mrefu sana kukarabatiwa, sasa jambo kama hili badala ya kulichukulia juu juu, tulichukulie kwa undani zaidi kwanini wagonjwa wetu wanapofika muhimbili hawatibiwi kwa wakati, na hapo ndo tutakuwa tumeweza kuanza kuliondoa tatizo ikiwa ni pamoja na kufanya masahihisho madogo madogo ya uzembe kama huu, lakini niwaambie makosa kama haya yaliyotokea muhimbili huwa yanatokea sehemu nyingi sana, hivyo sio kitu kigeni japokuwa tunasema tusishabikie makosa.

    Pia kuna watu kibao zaidi wanakufa kwa magonjwa mengine kwa sababu hakuna dawa huko waliko lakini watu wanakula (mafisadi) tu pesa za nchi, hao ni wabaya zaidi kuliko hao madaktari waliosimamishwa, kwani wao wanasababisha vifo vingi zaidi kuliko hicho kilichosababishwa na hao wa muhimbili.hapo hapo hao mafisadi wakiugua kidogo tu, wanakimbizwa nje ya nchi kwa pesa ya walipa kodi tena, hivi kwanini wasiitengeneza hiyo muhimbili iwe ya viwango wanavyoviona huko wanakoenda kutibiwa? pesa zote wanazotumia kutibiwa huko na hizo wanazoiba si tungekuwa mbali?
    nina mengi ya kuandika, lakini naomba kuwasilisha haya machache na niwaachie wengine pia.

    ReplyDelete
  2. Bro Michu mbona hutuambii ni nani wamesimamishwa, kambale au dagaa??? hebu lete maneno yaliyokamilika kaka.....

    ReplyDelete
  3. Makosa yameshatendeka na wangesamehewa tu hawa wajifunze kutoka na makosa waliyoyafanya...

    Kama tunafukuza brain surgeons mhhhhh.....bongo....hiyoooooo..... hao watu ujue vichwa kweli ....brain surgeons?????!!!!! Na mda waliotumia kupata ujuzi wao tunawatupia majirani zetu.

    Kosa sio lao wenyewe system yao labda ipo so bad. Kufuta maovu yao wanafukuza waganga wenye ujuzi. Hao waliowaprep hao wagonjwa ndio wakufukuzwa...

    Tunawafaidisha nchi nyingine tu hapa. hao tumewangharamikia elimu yao wataenda nchi nyingine waaajiriwa vizuri na kulipwa hela nyingi tu...

    ReplyDelete
  4. Makosa yameshatendeka na wangesamehewa tu hawa wajifunze kutoka na makosa waliyoyafanya...

    Kama tunafukuza brain surgeons mhhhhh.....bongo....hiyoooooo..... hao watu ujue vichwa kweli ....brain surgeons!!

    Na mda waliotumia kupata ujuzi wao tunawatupia majirani zetu.

    Kosa sio lao wenyewe system yao labda ipo so bad. Kufuta maovu yao wanafukuza waganga wenye ujuzi. Hao waliowaprep hao wagonjwa ndio wakufukuzwa...

    Tunawafaidisha nchi nyingine tu hapa. hao tumewangharamikia elimu yao wataenda nchi nyingine waaajiriwa vizuri na kulipwa hela nyingi tu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...