Bwana MICHUZI,
habari ya siku nyingi.
Mimi ni Kiongozi, na mwanzilishi wa huduma nzuri ya Western Union Money Transfer, Tanzania. Tuna zaidi ya Miaka 10 kwenye huduma hii hapa Tanzania. Habari hii ni ya KUSIKITISHA NA IMELENGA KUPOTOSHA ukweli kwa wanaotajia kutumia huduma hii baadae.
Wale waliokwisha itumia, IKIWA NI PAMOJA NA BWANA MICHUZI, watakubaliana na Mimi kuwa MPOKEAJI HATA SIKU MOJA haombwi KITAMBULISHO cha Mtumaji.
Mpokeaji huhitajika kufanya MAMBO MATANO yafuatayo ili apokee hela.
1)Awe na kitambulisho halishi chenye picha,
2)Ajue jina la mtumaji,
3) Ajue kiasi kilichotumwa angalau +/-10%ya kiasi alichotumiwa,
4)Ajue hela zimetoka nchi gani, na
5) Ajue jibu la swali ambalo mtumaji amemtungia.
Haya yote Bwana Mwakidila naamini aliambiwa na Ofisi alipoenda kutuma hela afanye nini ili Mama apokee hela baada ya kutuma, na nakala yake anayo. Hata kama alipata taizo, alipaswa aende alipotumia hela ili kujua ukweli wake muda ule ule.
Hata hivyo, anaweza kupata uhakika kupitia kituo chochote che Western Union au website hii www.westernunion.com .angalia taratibu za kutuma au kupokea hela "Tanzania".
Kila nchi imetoa taratibu zake, ambazo hazifanani kwa nchi moja na nyingine...hasa ukilinganisha nchi za mabara mengine na Africa...CHUNGUZA.
USHINDANI. Bwn Michuzi dunia ya sasa ni ya ushindani, isije ikawa inalenga kitu kingine zaidi.Huduma ya KUTUMA na KUPOKEA hela Kupitia Western Union na MoneyGram kwa Tanzania MASHARTI na TARATIBU ni zile zile, kimsingi.
Wote ni MABENKI na tunaongozwa ni SHERIA za fedha chini ya Benki Kuu ya Tanzania. Hivyo,alichokieleza Bwana Mwakidila hakipo katika taratibu za kupokea hela kupitia huduma hii.
OMBI: Namuomba Bwana Mwakidila atusaidie kujua undani wa jambo hili kwa kuwasiliana nasi moja kwa moja, au atupe namba ya simu ya Mama hapa Dar es salaam, ilituweze kulifanyia kazi kwa manufaa yetu wote. Labda ni kitu kingine kimejificha hapa!!!!!
Kisha atueleze kama Mama alilipwa au nini kilifuata baada ya hapo.
HITIMISHO: Namuomba Bwana Mwakidila awasiliane nasi kupitia namba za ofisi alikotumia hela, ziko nyuma ya fomu aliyopewa, au kwetu (Tanzania) moja kwa moja.
Nawaomba WA-TZ wote mtume hela nyumbani, tusaidie ndugu, jamaa, rafiki na familia zetu, na Taifa letu changa la TANZANIA, KUPITIA HUDUMA NZURI YA WESTERN UNION.
TAWA,
KPR
PS: GLOBU YENU HII YA JAMII INAKARIBISHA VIMEO KAMA HIVI ILI TUSAIDIANE KUTOA YALIYO MOYONI NA IKIWEZEKANA KUPATA UFAFANUZI WA KINA KAMA ALIVYOTUSAIDIA MDAU HUYU WA WESTERN UNION AMBAEO NAMPA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA TANGAZO HILI LA UBWETE


Michu inabidi uwe mwaangalifu,uenda hapa kuna kaujanja ka KUJITANGAZA kweny blog yako bila kulipa pesa.
ReplyDeleteMaana najua kwa MITUNDIKO hiyo basi western union tayari imejiongezea leo wateja.
Chonde usibane maoni yangu,hata kama michu unahusika katika ILI TANGAZO la western Union..tee tee bongo akili mukichwa....oooohh
Sifa yetu ukimwachia mTZ kuongea au kujitetea Utahachwa njia panda.Ndiomahana watani wetu kenya UG uwa makini sana kutupa mudauo.Huyu jamaa kutuandikia utaratibu wakutuma Pesa kila mtu anajua lakini bongo haisaidii iyo..
ReplyDeleteUmefanya kazi nzuri sana kaka michuzi tunakushukuru sana sisi ndugu zako waughaibuni .Rais kikwete alisema tuchume ugenini tupeleke nyumbani
ReplyDeleteMichuzi pamoja na kuwa out of point naomba kukumbusha kwamba kuna waandishi wa Mwnahalisi wameshambuliwa na hakuna lolote kwenye Blog yetu muhimu.Naomba tupe news zao.
ReplyDeleteHabari?
ReplyDeleteNamuunga mkono mdau aliyeleta malalamiko kuhusu Western Union. Hili suala ni la ukweli kabisa kwa sababu lilishawahi kunitokea. Mtu kuna mambo yanayojieleza kwenye fomu zao lakini eti wao wanadai wanataka kucontrol hili na lile. Mbona huku ughaibuni hawana masharti wakati wa kutuma na kupokea hela? Huko Tz ndio wanajifanya kudhibiti ubadhilifu wakati ndio kumeoza? Hebu wasituletee zao za kutaka sijui namba za Mama sijui nini,wao wakubali tu kuna hako kamtindo kachafu.
Wajirekebishe haraka iwezekanavyo na waache ubabaishaji wao huko.
Wasalaam.
Nyie western union gharama zenu kubwa na mambo kama haya. Mie kuanzia sasa ni Money Gram tu. Nawaambia watu wote wanaotumia Western Union kuachana nayo na Kuanza kutumia Money Ghram ni bei nafuu na hakuna usumbufu.
ReplyDeleteBWANA TAWA, MAELEZO YAKO HAYAJATUAIDIA SANA, KWASABABU HAYANA JIPYA. TATIZO NI KWAMBA BWANA MWAKIDILA ALITAKIWA ATUME UKURASA WA PASSPORT YAKE, SWALI UNALOTAKIWA KUJIBU NI JE, HUO NDIO UTARATIBU MPYA? JE KUNA CIRCUMSTANCES ZOZOTE AMBAZO MNAHITAJI PASSPORT YA MTUMIAJI SIKU HIZI? KAMA HAMHITAJI UNDER ANY CIRCUMSTANCES, HILI LA PASSPORT LIMETOKA WAPI? TUFAHAMISHE HILI.
ReplyDeleteMimi nadhani tuwe wepesi wakuelewa.Huyu Bwana Tawa nina hakika maelezo yake yakidhi haja ya muuliza swali.Katika jibu lake bwana huyu amefafanua kwa kina taratibu ambazo mpokeaji fedha anapaswa kuzifuata.Sasa mtu anaposema hajajibu swali mimi simuelewi.Katika maelezo yake hajagusia kabisa suala kuwepo kwa utaratibu wa kuhitajika kwa nakala ya pasi ya kusafiria ya mtumaji.Hii kwa mtu makini na mwenye upeo mpana wa kuelewa mambo ina maana kwamba hakuna kitu kama hicho.Na bwana Tawa ameenda mbali zaidi kwa kumtaka mdau aliyekumbwa na mkasa huo kuwasiliana na wahusika kujua tatizo liko wapi.Sasa mdau unapodai maelezo yake hayatusaidia sana na kwamba hayana jipya,mimi nadhani wewe ndio mzito wa kuelewa na kama sio hivyo basi ni mpenda ubishi usiokuwa na manufaa.Na huyu mdau anayepigia debe huduma za Money Gram lazima utambue kwamba huduma hiyo haijasambaa sehemu nyingi za nchi.Mimi nikitaka kumtumia pesa ndugu yangu wa kule Tukuyu, Mbeya(sio Tokyo,Japan kama michuzi avyopenda kuita)sitaweza kufanya hivyo kupitia huduma hiyo ya Money Gram.Lakini naweza kufanya hivyo kupitia huduma za Western Union ambayo ina mtandao mkubwa karibu asilimia 95 ya Wilaya zote za Tanzania.Kwa hiyo ni vema kuangalia urahisi wa huduma yenyewe kabla ya kuipigia debe.Naomba ieleweke kwamba sina ubia wowote na Western Union,lakini ninachotaka kusema ni ukweli na ubora wao kutokana na uzoefu wangu wa kutumia huduma tangu nilipokuwa nyumbani Tanzania na kwa muda wote niliokaa hapa Marekani.
ReplyDeleteMr Tom,Ohio-USA
Bwana Tawa,tunaelewa kuwa ni wajibu wako, kama kiongozi mwingine yeyote wa bongo,kukanusha lolote ambalo linaelekea kukuharibia ulaji wako.Kwa hiyo wimbo wako ni "santuri ya kale".
ReplyDeleteSiamini kwamba sisi wote tumwtunga suala hili,for what?
unataka namba ya simu ya mama Mwakidila ya nini,kwa nini usiombe location, siku na muda wa ofisi husika vinatosha?
Anyway,hayo mambo ndio yanatukatisha tamaa wengine kuhusu nchi yetu.
Sam.
I TOTALLY AGREE WITH MR. MUSHI. HONESTLY, MR. TAWA SOUNDED MORE DEFENSIVE THAN ACTUALLY TRYING TO ANSWER THE QUESTIONS ASKED BY MWAKIDILA, BASICALLY. SECONDLY, HE HAS FROM THE VERY BEGINNING SHOWN THAT WESTERN UNION IS ENTIRELY CLEAN AND THE MOST RELIABLE ONE AS HE SAYS, AND I QUOTE:
ReplyDelete"Mimi ni Kiongozi, na mwanzilishi wa huduma nzuri ya Western Union Money Transfer, Tanzania. Tuna zaidi ya Miaka 10 kwenye huduma hii hapa Tanzania. Habari hii ni ya KUSIKITISHA NA IMELENGA KUPOTOSHA ukweli kwa wanaotajia kutumia huduma hii baadae....."
THIS IS REDICULOUSLY OVERSTATED. ARE YOU THE ONE TO EMBRACE US ABOUT HOW GOOD THE SERVICE IS, OR DO WE ACTUALLY HAVE TO FEEL IT THE WAY WE ARE SERVED? I HAVE A DOUBT WITH YOUR LEADERSHIP OR ADMINISTRATIVE PRINCIPLES YOU APPLY. A GENUINE PERSONNEL WOULD HAVE TRIED TO INVESTIGATE THE ISSUE ON BOTH SIDES OF THE COIN. AND YOU EVIDENTLY ARE A FAILURE ON THAT ASPECT.
THE OTHER THING WHICH YOU SOUNDED TOO GENERAL WAS ABOUT THE REQUIREMENTS FOR A PERSON RECEIVING MONEY SENT THROUGH WESTERN UNION. AS FAR AS I KNOW, YOU DO NOT HAVE TO PRESENT ALL OF WHAT YOU LISTED SO AS TO GET THE MONEY. THE SITUATION IS A LITTLE FLEXIBLE OR RATHER FUZZY. THE RECEIVER MAY OR MAY NOT PRESENT ALL OF THE THINGS YOU MENTIONED, DEPENDING ON WHAT THE SENDER REQUIRES. TEST QUESTION AND ANSWER ARE NOT A MANDETORY PART OF THE PROCESS TO SEND MONEY BUT AN OPTIONAL ONE. I HAVE SENT MONEY WITHOUT IT, BUT THE THING IS THAT THE RECEIVER MUST HAVE AN ID.
HAPA MNAWACHEZEA WATU AKILI. MNAFANYA MATANGAZO YA BIASHARA BADALA YA KUJADILI MATATIZO. MAJIBU YAKO YANGEKUWA MURUA ENDAPO UTAFITI UGEFANYWA, NA HUYU ALIYELALAMIKA AKAONEKANA ALIONGOPA. LAKINI HUNA UTAFITI, HUNA HAKI YA KUONGEA ULIYOSEMA HAPO JUU.
Mwisho......
Tanzania bwana longolongo haliishi. Alichokisema bwana Tawa ni utaratibu uliopo wa kupokea pesa hapo Tanzania. Huo utaratibu wote tunaufahamu. Alochokosea ni kusema kuwa mlalamikaji ni mwongo. Yeye alitakiwa azungumzie tukio hili na sio kuja na ngonjera zake hapa. Hii tabia ya kutetea uozo haitatufikisha mbali. Yeye angeomba radhi kwa usumbufu uliompata jamaa na kuahidi kulifuatilia hili suala. Kama kawaida yetu waTanzania hatupendi kukubali makosa na pia HATUPENDI KUKOSOLEWA.
ReplyDeleteHuyu jamaa wa western union naomba atoke nje ya nchi kidogo atembelee wenzake wa western union ulaya aone jinsi wanavyoheshimu wateja.
ReplyDeleteYaani wewe mteja analalamika badala ya kumuomba radhi na kutatua tatizo lake mara moja unathubutu kumtuhumu kwa kosa ambalo huna uhakika amefanya? ulikuwepo huko musoma wewe? unajuaje jinsi mfanyakazi wenu wa musoma alivyofanya kazi?kama wewe kibosile hujui thamani ya wateja je yule wa musoma atajua?
Zingatieni shule mlizoenda bwana, kwani lazima mtu asome ulaya ndo ajue jinsi ya kum-treat mteja?hii si tunaweza tu kuivumbua Tz pia ukizingatia sisi ni wakarimu?
Lakini nimefurahi kuwa jamaa yake yule mteja amepata hela at last.
Bwana Muchuzi
ReplyDeleteHaya mambo ya Western Union ni sawa na Mabenki mengi ndani na nje, saa kadha huboa tu wateja. Waweza kwenda bengi hii na ukayakuta hivoivo. LA MAANA HAPA NI KWAMBA. KWA UJUMULA WAKE WESTERN UNION TANZANIA WAMETUTOA KUBAYA NA SASA TWAPELEKA ELA KUJENGA TAIFA LETU----POA SAAAAAAAAANA.
Aya majambo madogo madogo...Bwana Tawa awaambie wenzake wayarekebishe, naamini sana yanarekebika...bila kutumia jaziba mingi. Mimi nachojua VYOMBO VYA FEDHA DUNIA KOTE WANA MAJINA---YA FANNANAYO NA MAJINA AMBAO HUCHUNGUZWA KWANZA NA MABENK ILI KAMA SIYO VIPI NDIO HUKUBALIWA KUTUMA AU KUPOKEA ELA...MAJINA KAMA MOHAMED ABDALLAH, ABDALAH AHMED, ALI AHMED;;;;;N.K. AWA WENYE JINA HIZI NI WENGI MUNO DUNIANI, SI KAMA MAJINA KAMA "Mchuzi MBOGA", "MADENGE Machomi". Hivyo kuyachunguza, tangia Septemba 11, na hata kabla hapo...Vyombo vya Fedha hufanya. Ukiwa umeambiwa upeleka utambulisho, basi ni hiyo sababu. Na waliohusika ndio hukasirika na uchelewaji huu. Hii aina namna, ni utaratibu wa sheria ya fedha ya Mataifa yote....sio kwa hawa ndugu zetu ya TZ.
KWA IYO...WESTERN UNION kwa ujumla ake imetusaidia saaaanaaaaaa WATZ. Muwe tu wakweli jamani. Madogodogo haikosekani, LAKINI BRAVOOOO!!!!!!!WESTERN UNION-TANZANIA. ONGEZENI UBORA NA MAENEO MENGI---WILAYANI--ASA KUSINI NAKO KUENDELEEE!!!
MUDAU!!