Mama wa kwanza Salma Kikwete akimimina zege katika msingi wa jengo la mojawapo ya madarasa katika shule mpya ya sekondari inayojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na wananchi wa eneo la Nyamisati, Rufiji mkoa wa Pwani. mama pia aliongea na baadhi ya wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Mahege iliyopo Nyamisati,Rufiji Mkoa wa Pwani juzi wakati alipoitembelea shule hiyo kufuatilia maendelo ya Wanafunzi wa kike 11 anaowafadhili kupitia taasisi anayoendesha ya WAMA(Wanawake na Maendeleo).WAMA imetoa pia msaada wa Solar kwa ajili ya kuweka umeme katika shule hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mama wa kwanza ni mama yako mzazi Michu, wee mke wa JK hawezi kuwa mama yako wa kwanza. Usipende kufanya direct translations zisizokuwa na maana.

    ReplyDelete
  2. Yaani wewe anonymous hapo juu unakuwa kama humjua Michuzi bwana!!
    Michuzi hajaenda shule. Kwa hiyo ni wazi tu kuwa kiingereza kitampa chenga.
    teh...teh..teh...

    ReplyDelete
  3. Kwanini hanaitwa mama wa kwanza.

    ReplyDelete
  4. Chuki nichukiee! roho yangu niachie mwenyewe x2

    Jipe raha, Michuzi jipe raha, jipe raha na mimi nijipe zangu! x2

    Michuzi huyo anayechukia translation zako achana naye jipe raha mwenyewe translate wewe mwenyewe roho yako inapenda. Wengine tunafuata hiyo lugha yako humu ndani ya dinner ya mchana, my wife na picha. Mwenye kufanya utafiti wa Kiswahili aende Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Mlimani au BaKiTa.

    Aende akausikilize huo mwimbo wa Mzee Yusuf vizuri. Msomari huooooooooo!

    Tukirudi kwa Mama wa Kwanza kweli anastahili pongezi kwa kazi nzuri anayoifanya kupitia taasisi yake ukizingatia hayo maeneo ya delta ni kama vile yalikuwa yamesahaulika kabisa. Hongera mama wa kwanza siye tuliofika huko delta ya Rufiji tunadhamini mchango wako.

    ReplyDelete
  5. Hata mama wa kwanza pia si lazima awe mama mzazi inategemea babako ameaoa wake wangapi kama mama yako ni mke wa tatu au wa sita, basi mke wa baba yako wa kwanza ndio mama wa kwanza. Hata wewe hujui kiswahili! Acha kukandia watu kwa lugha za watu pia.

    Hongera mama wa kwanza kwa kazi zako za wanawake na maendeleo.

    ReplyDelete
  6. NAPENDA KUMTOA HOFU HUYU MDAU AITOA MAONI JUU YA MICHUZI KUMUITA FIST MAMAM WA KWANZA. KWA TAARIFA YAKO TANGU DUNIA IUMBWE HANA KITU CHOCHOTE AU JAWABU LA TATIZO IMEHAKIKISHWA KUWA SAHIHIKILA KITU UNACHOKIONA NI MAONI YA WATI WA VIZAZI MBAIMBAI NA HUBADILIKA KWA NYAKATI. KWA UPANDE WANGU KATIKA SHULE YANGU YA UGHA KUNAKITU NAKIITA TASFIRI YA MAANA NA TAFRISI YA MOJAKWA MOJA AMBAYO HAINA MAANA. MICUZI NI MSANII KWAHIYO TAFSRI YAKE LAZIMA IKAE KISANII NA HAJAKOSEA. KWA UPANDE WA MAANA TAFASIRI NI KAMA HUU MFANO MAANA YA NENO MAMA NI MZAZI WA KIKE AU MOTHER IS A FEMAEPARENT KWA BADILIKO LA MOJA KWA MOJA BIA TAFASIRI MAMA KWA KIINGEREZA NI MOTHER KWA HIYO UKI TAFASIRI NENO KWA MBADILIKO WA MOJA KWA MOJA NDIO INAKUWA MAMA MOTHER AKINI DIFINITIVE TRANSATION IS THE BEST KAIKA UKUMBI AMBAO UTAKIWI KUONYESHA USANII. HAYO NIMAONI YANGU WADAU ASANTENI

    TUMAINI GEOFREY TEMU

    ReplyDelete
  7. Kweli kabisa anonymous 2:25 pm
    kaka michuzi umetereza kidogo kumwita Mrs kikwete mama wa kwanza!imagine kama Bi mkubwa wako angekua anaikong`otea hii blog yako angekufikiliaje,maana najua alipo utandawazi mh!!!!
    then huyu mama unae mwita wa kwanza anafanya migizo,tena afadhali na ze comedy!zege linawenyewe cio huyo mambo safi,matawi ya juu aka ma-fisi-hadi selikalini! mcheki mdharendo wa tatu kutoka kulia anavyoona kazi yake inayo muweka mjini ikiingilia na kina "Malali"wakiume Balali.
    SALIM HASSAN

    ReplyDelete
  8. Wee Tumaini acha kuchemka, Michuzi sio msanii bali ni mpiga picha tu, mama wa kwanza ni yule aliyebeba ujauzito wako, mbona watu hamko proud na wazazi wenu kiasi hiki? Wawaaaa anony wa kwanza, good point.

    ReplyDelete
  9. Wote waongo na wanafiki wakubwa, ni mswahili gani na kiswahili cha wapi hicho kumwita mama yako mzazi mama wa kwanza? Haya tutafsirieni basi kwa kiingereza! Acheni kutunga maneno simply tu kwa kumchukia mtu bila sababu.

    Mimi mama yangu ni mama yangu tu, daraja yake ni mama yangu mzazi basi. Na ni ndicho kiswahili tunachokielewa na kukizungumza mitaani. Iwapo mama yako mzazi utamwita mama wa kwanza, mama wa pili atakuwa mama yako yupi?

    Hebu acheni uzungunaizesheni kutaka kuiga kila kitu. Mama mzazi ni mama tu haiwekewi daraja la kufananishwa na kupangishwa foleni na wengine. Mama ni mama, au mama mzazi basi, kama umelelewa na mama wa kambo, hayo mengine utakuwa na mama mzazi na mama wa kambo basi.

    Eti mama mzazi ni mama wa kwanza halafu mkeo ni mama wa pili, kimada ni mama wa tatu? Ati si ndio madaraja hayo mnayopanga. NO WAY DARAJA YA MAMA NI YAKE PEKE YAKE, MAMA MZAZI BASI HANA WA KUPANGWA NAYE HAPA DUNIANI.

    Hongera mama wa kwanza au Bibi wa Kwanza kwa kazi nzuri unayoifanya. Wenye chuki na husda zao watakufa siku zi zao.

    ReplyDelete
  10. HAWA WASOMI HASRA WAIOSEMESHWA WAKAWA NA KIBURI NA NYODO NAKUFURAHIA WENZAO AMBAO HAWAJAPATA HIYO NAFASI KWA SABABU MBALIMBALLI YA KIUCHUMI IKIONGOZA NAFIKIRI KWAO ADHABU YA KUWAFUNGA MAISHA NI MSAMAHA MKUBWA SANA MAANA HASARA WANAYOTUPA NI YA MILELE . BAHATI MMBAAYA WAKIPATA NAFASI YA KUNFUNDISHA MWANAO HALAFU MWANAO WA KIKE NA YEYE NI LECTURER HATAHAKIKISHA KWA MBINU ZOTE MMMMMMMMHHHH. NAFIKIRI HAYO YA KUMMMHHH MHHH NI KUJITAFUTIA LAANA. TAFADHALINI BADILIKENI TABIA NO TIME TO WAIT NO TIME TO WEST TIME IS NOW EDUCATION FOR ALL AND FREE. JENGO HALIITAJI ADA KITABU AKIITAJI PESA ILA MTUNZI NDIO ANAHITAJI PESA MTU AKITOSHEKA LAWAFUNGULIE WALALAHOI HII NI ILE INA JULIKANA KAMA FUNGULIA MBWA WAKATI WA MIPIRA YA KULIPIWA
    ( KWA KIFUPI MAANA USANII NI KUWEZA KUFANYA KITU CHOCHOTE KWA UWEZO BINAFSI)
    WENU

    ReplyDelete
  11. AZAFALI siku hizi kapunguza makekeke kidogo baada ya Kidume Slaa kuwa sheki kidogo.Nae tratbu ufisadi unampumlia kisogoni.
    Dokta kaza buti mkuu
    ©Majita

    ReplyDelete
  12. We Michuzi wacha ushamba.
    WAMA wametoa msaada wa SOLAR PANEL, na sio Solar.
    Solar ni JUA, sasa wakitoa msaada wa jua na kulishusha hapo toka juu patakalika hapo kweli?
    We vipi wewe!?!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...