Home
Unlabelled
marubani kwenye nondozzz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Unaposema kapteni na mwenzie una maana gani?Mwenzie ni nani? Halafu, kwenye cockpit kama hiyo, captain anakaa upande gani? Yupi Captain na yupi mshika break hapo?
ReplyDeletehongera sana waTZ. wa kujifunza udereva wa kukendesha ndege.
ReplyDeleteWe Anony hapo juu 11:44pm, ujumbe muhimu hapo ni kuwa Ndege mpya zilizoagizwa na kukua kwa shirika letu la ndege.
ReplyDeleteMichuzi anajitolea kutupa taarifa, hayo maelezo unayotaka unaweza kubofya mtandaoni na kuyapata.
Usisome kwa lengo la kukosoa huyu jamaa anajitahidi kutuhabarisha, na wewe unaweza anzisha blog yako kama nyingine nyingi tu!
Dash 8 iatisaidia sana ATC kwenda mikoa ambayo viwanja vyake sio tambarare kwa sana.
ReplyDeletesasa hivi mchuano wa makampuni ya ndege unaanza kuzaa matunda kwa wananchi.
sasa hivi bei tiketi za ndege zinazidi kushuka kila kukicha.
Kila la kheri ATC lakini mkae mkijua Precision na Community Airlines wana exist na wanakimbiza ktk kupunguza gharama. kazi kwenu Madenti
mungu ibariki Tanzania
hello emmanuel, nakuona mtamboni hapo!
ReplyDeleteMwenzie captain anaitwa "first officer" au rubani msaidizi ambaye baada ya muda nae pia huja kuwa captain.
ReplyDeleteBreki ziko upande zote mbili yaani kushoto na kulia.
Captain kwenye ndege anakaa kushoto.
Big up Airtanzania naona kweli wamedhamiria this time....tunangoja mboreshe huduma zenu...tena nasikia wana mpango wa kuwarudisha wakongwe kina Capt.Willilo na wengineo wenye uzoefu wa miaka mingi ili kulifufua shirika kwa kasi mpya
ReplyDeleteImetulia wadau mambo yenu si mchezo..
ReplyDeleteAna maana co-pilot wewe au hujui maana ya kapteni na mwenzie? Huyo mwenzie siyo mshika breki kwa taarifa yako ana kazi sawa na huyo kapteni. Hapa Bongo kuna wazungu hawapandi hizi ndege kama hazina makapteni wawili kwa sababu za safety. Wanakwambia incase kapteni mmoja akiumwa ghafla huko juu kama kupata heart attack na ndege ina kapten mmoja inakuwaje?
ReplyDeleteNadhani Lilla na mwenzake huwezi kuwaita Kapteni mpaka wapate nondooz.Swali la kizushi: hivi mganga (Dr.)anaanza kuitwa hivyo baada ya kuhitimu au akichungulia tu madirisha ya yunivesti of medisin.....?
ReplyDeleteWewe zuzu kweli. Kapteni(Lilla) yuko mkono wa kushoto na msaidizi wake (mshana)upande wa kuume. Hujui kusoma nini?rudi shule ukasome hata elimu ya watu wazima.
ReplyDeleteNifuraha yangu kumwona brother Jaffary Lilla na mwenzie wakiongeza ujuzi kwani nimepata petesi kuwa abiria wengi wa kibongo wanahofia ndege za shirika la watani wetu wa jadi (KQ) sijui kunani lakini ntaendelea kudodosa vyanzo vyangu vya habari, Samsingi wangu kahofia kupanda wakati akienda Afrika Magharibi kuleni tizi ili tuwe tunaruka kutoka dizim mpaka pwani ya pembe au kwa Obasanjo .
ReplyDeleteWe unaeambia watu warudi shule kusoma, jamaa kauliza tu na kuuliza sio ujinga, anayetakiwa kurudi shule ni wewe, you don't have manners.Jibu swali au shush.
ReplyDeletehi uncle Lilla habari za siku, mwisho kukuona ulipokuja mwz miaka ya 97/98 vp aunt Hindu hajambo? vp kids wamekua sasa? huku hawajambo pia. Tunafuraha tukiona bado unajitahidi kuliendeleza libeneke la angani bro.
ReplyDeletenduguzako Bank mwz.
Kibiriti acha uzushi hao ni tayari wameajiriwa na ATC na hiyo sio shule ya kurusha ndege kha!! Ingekuwa wako Aviation school sawa hebu somaga mesage uilewe kwanza ndio ukurupuke kukoment. Acha dharau ndio maana ukajiita kibiriti!!
ReplyDeleteWewe kibiriti.
ReplyDeleteHao jamaa walianza kuyavurumusha hayo madege kitaambo!, hawajaanzia hapo.
Hiyo wanayofanya hapo ni additional type tu.
Kwani huyo dokta wako aliyefuzu na kufanya kazi tuseme miaka 12 au miaka mitatu akirudi chuoni kuongeza ujuzi in a particular field UTAENDELEA KUMUITA DOKTA AU?
Dear Kibiriti, Jamani hao ni marubani kamili tayari, hizo ni refresher courses wanapataga from time to time, haimaanishi eti hapo ndio wanajifunza upya.
ReplyDeleteMimi kwanza nataka kuwajibu watu wote mlionishambulia. Mimi ni annon number moja hapo juu. Nilipouliza maswali yangu nilikuwa nina maana.
ReplyDeleteKwanza, ingawaje wote huwa tunapanda ndege lakini hatunaga idea ya kwenye cockpit wale jamaa wawili wanafanyaje kazi! Boss anakaa upande gani na mwenzake wapi! Je inapotokea huko hewani wakakorofishana, mmoja akafunga break na mwenzake kukata kona ghafla inakuwaje? Au wakaamua kuzichapa tu kwa sababu moja au nyingine!
Pili, issues za Lilla au Mshana mimi hazinihusu wala sihitaji kuwajua! Ni sawa sawa na kuniuliza kama namfahamu dereva wa daladala niliyopanda, utawajua wangapi na kwanini?! Kwa hiyo wewe unayesema mimi zuzu kwa kutowajua hao unaowajua wewe, mimi naweza juwa nawajua wengi kuliko unavyodhani. Hukuwa na comments, kwa hiyo si lazima uandike. Soma tu. Inatosha.
Mwisho, naomna tena kuuliza, hivi pilot na captain tofauti yake nini? Juzi juzi nilipanda Cathy Pacific jamaa akasema your PILOT CHENG speaking! British airways wansema your Captian ,... speaking! Hivi yupi ni yupi?! Na je mwenzake hasa anaitwaje? Kama ni first officer kama mmoja anavyosema, second, third, fourth ... officers ni wakina nani humo kwnye ndege? wanaweza wote rusha machine iwapo itatokea issue kama ndege ya Turkey marubani walipozimia wote kwa kukosa hewa!?
Naomba wataalamu wajibu swali. Asanteni
kaaaazi kweliweli pale kila mtu anapokuwa mjumvi.
ReplyDeletecaptain ndio boss kwenye ndege.ana-command the crew.he's like a CEO in a company.
first officer huyu ndo huwa anarusha ndege kwa kufata instructions za captain.usione ndege zinapaa,ukitaka kujua kinachoendelea kwenye cockpit wkt wewe unasumbua hostess wakupe kahawa,ingia youtube afu muvuzisha kwenye search 'cockpit videos' utaijua shughuli yake.nadhani mtakuwa na adabu na hao masela.
ndege zipo models zaidi ya 100 na kila moja moja in settings tofauti ktk cockpit.kabla ya kurusha ndege lazima uwe trained kurusha aina hiyo ya ndege kama wanavofanya hao masela hapo.wanajiandaa kurusha dash8q300.kuna pilots wanaendesha b737 tu,wengine 777 tu etc..may be niseme specialization for simplicity.nadhani hapo mtakuwa mmnipata wadau mnaopenda kujua vitu.
anon wa kwanza tatizo lako maswali yako umeyauliza kibabe, na imedhihirisha zaidi kwenye comments yako ya pili paragraph ya tatu, hiyo hasa mimi imenitibua nyongo, nikaanza kuhisi kuwa hapa kauli zako kidogo zinaanza kuwa za kifedhuli,hasa ulipoleta issues za daladala nikaanza kuelewa kwa nini wadau walikushambulia kabla kama ulivyodai. Kuweko nje isiwe sababu ya kutotaka kuwajua wazawa wenzio. Na inaonyesha umeshalowea huko uliko kiasi huwatambui hata hutaki kuwajua hata ukiletewa hawa hapa wajue basi.Heeh hiyo "Hasada basi"!
ReplyDeletebytheway "GET TO KNOW THEM. GET TO FEEL FREE AND EASY. GET TO LIKE THEM. AND GET TO FEEL THEM LIKE YOU."
anyway conclusion yako imeyeyusha ghadhabu uliyoanza kuipandisha.
mza.
Mwisho, naomna tena kuuliza, hivi pilot na captain tofauti yake nini?---
ReplyDeletePilot na Captain ni kitu kimoja, ISIPOKUWA kwenye ndege za marubani wawili sio kila pilot ni Captain, Captain ni "pilot in command", yaani chochote katakachotokea, ataulizwa yeye, pia maamuzi YOTE anafanya yeye baada ya kushauriana na wenzake yaani First officer na PURSER (mkuu wa wahudumu ndani ya ndege). First officer in "second in command". Huyu first officer hajawa captain bado kutokana na flying hours zake yaani experience.
Juzi juzi nilipanda Cathy Pacific jamaa akasema your PILOT CHENG speaking! British airways wansema your Captian ,... speaking! Hivi yupi ni yupi?!---
Wachina ENGLISH sio lugha yao, huyo mchina hakufafanua hapo, inawezekana alikuwa ni Captain speaking AU First officer speaking. Muingereza kwa kuwa english ni LUGHA YAKE alikuwa more specific.
Na je mwenzake hasa anaitwaje? Kama ni first officer kama mmoja anavyosema, second, third, fourth ... officers ni wakina nani humo kwnye ndege?
Mwenzake Captain ni First officer. Second officer ni yule straight from pilot school akaenda fanya TYPE RATING in that particular aircraft akaanza kuruka in that airline, ni most junior among FLIGHT CREW. Hawa ma second officer huwa hawaruki, wanaangalia tu operations, mpaka wanapokuja kuwa ma First officer baada ya muda fulani ndipo wanapokaa kiti cha kulia na kuanza kuruka...HAKUNA third, fourth etc officers.
wanaweza wote rusha machine iwapo itatokea issue kama ndege ya Turkey marubani walipozimia wote kwa kukosa hewa!?
Wote wanaweza kurusha ndege, kawaida mmoja akirusha kwenda mwanza (kwa mfano) mwingine anarusha kurudi Dar. Ikitokea WOTE wazimie (under most unlikely event)...TOO BAD.
Naomba wataalamu wajibu swali. Asanteni
Je imetosha?, if not, get a pilot if you can atakufahamisha.
Mambo ya ndege kidogo yanahitaji ufahamu zaidi, kuna mambo mengi.
Asante sana Deleva. Unaonekana si kwamba unajua tu, ila ni mwalimu mzuri. Asante sana kwa ufafanuzi. Ndo maana hatuondoki hapo kwenye hii blog. Mavituvitu ni mengi sana.
ReplyDeleteIla we annon mza 11:53 sijui una nini na mimi?! Mimi sikuhitaji kumjua Mshana wala Lilla. Wewe kama unawajua ni shauri yako huko huko. Mimi nilitaka kujua majibu kama alivyotoa Mr. au Mrs (Miss). Deleva hapo juu.
Asante sana Deleva na pole sana mza
Asante sana anon: wa kwanza nimefurahi kuona kumbe unajua kusema pole na asante pia. kumbe ukifanikiwa kupata unalohitaji unakuwa muungwana? Haina shida na karibu tena, na sina kitu nawe kama ulivyo hoji, ila nilitaka kukuelewesha tu kama ulivyolalamika kwa nini wadau walikua wanakushambulia.
ReplyDeleteSiku njema
mza.
Kila mtu ananamna yake ya kutaka kuelewa/kuelimika kuna wanaotafuta elimu kwa Nguvu zote hata Bunduki ikiwezekana na wakiipata ni watulivu kwenye kuitumia na wanaoitafuta kwa utulivu wakiipata wanaitumia hata kwa Bunduki.... Anon wa Kwanza kwangu hujakosea maswali yako ndio changamoto ya elimu fupi tuliyoipata kwenye hizo post juu.
ReplyDeletedereva hapo naona umeaelimisha wengi wasio jua kuhusu ndege nauongozaji wake kwa jumla. wale wapo kupata type rating za ndege hiyo dash 8 300, na sio wako shuleni,na captain ni mtu anakaa kushoto kwenye ndege siku zote na yule wa kulia ni first officer yaani co- pilot. wote wanarusha ndege lakini mmoja lazima awe kiongozi kama kwenye mpira wote ni wachezajilakini captain ni muongozaji mwenye kauli ya mwisho,na mkitaka mengi kuhusu urubani tafuta rubani atakuelezea vizuri
ReplyDeletemaana mimi najua mambo hayo kidogo,
Kwetu sie madaktari Surgeon huwa anasimama upande wa kulia wa operating table na msaidizi wake anasimama kushoto. Kumbe haya mambo tafauti sana. Kila mtu na kazi yake ati!
ReplyDelete"Kwetu sie madaktari Surgeon huwa anasimama upande wa kulia wa operating table na msaidizi wake anasimama kushoto."
ReplyDeleteFacing which direction?, at the patients feet facing the patients head? OR at the patients head, facing the patients feet. (this makes me remember ile presheni ya mguu akakatwa kichwa na wa kichwa akakatwa mguu hehee)
Knowing this is important for orientation