1. Je, kuna haja ya kuuogopa jumuiya ya afrika masharikie eti, kwa mantiki kuwa ndugu zetu wa kenya na uganda watachukua kazi zetu?

2. Je, Mimi na wewe tutoe mchango gani, ili tuhakikisha kizazi kijacho kiepukane na ufisadi, rushwa, n.k?

3. Je, Watanzania tufanyeje ile nasi tupate meendeleo waliyopata Malaysia, ambao walikuwa masikini kama sisi miaka ya sitini?

Mdau Ronnie

"Mwalimu kasema it can be done, play your part..."


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

 1. siafiki swala la muungano wa afrika mashariki, hapa tulipo wenyewe twachechemea, bot scandals and all that, kenye ipo ho he ha he kwa sasa, vita kama hivyo, uganda not so good as well, nafikiri hadi tujijenge, na tukomae ndo tufikirie swala hilo. huu ni umaskini usiofutika sababu ya kurudishwa nyuma maendeleo na rushwa. watoto wetu tuendelee kuwapa elimu tu, ndo silaha kubwa, then tuwalete huku europe kwa masomo ya juu na ajira.

  ReplyDelete
 2. 1. ......... ndugu zetu wa kenya na uganda watachukua kazi zetu?
  __________________
  Kama wao wanavyoweza kufanya kazi Tanzania nasi pia tunaweza kufanya Kazi Kenya na Uganda...kwa hivyo tusiogope?

  2. Je, Mimi na wewe tutoe mchango gani, ili tuhakikisha kizazi kijacho kiepukane na ufisadi, rushwa, n.k?
  __________________
  Kwa kweli ni kuwaelimisha ndugu na jamaa kuhusu ubaya wa Rushwa hata hizi ndogo ndogo....kama kuhunga trafiki polisi; manesi hospitalini n.k. kwani si watanzania tutakapoacha kutoa rushwa basi pengine tuanza kujenge mila na maadili ya kuto kupenda Rushwa...njia nyengine pia ni kujihusisha ktk demokrasia na kusikiliza kwa karibu sera za serikali na vyama vingine na kufuatilia kwa karibu utendaji wao wa mambo wanayo ahidi...tumia kura yako kuwaweka watu waadilifu katika madaraka...(nimefurahishwa sana na Chadema zaidi Dr. Slaa kwa ufuatilizi wake wa ufisadi...watu pia kama kina Mtikila wanajaribu kusafisha udhaifu wa vyombo vya umma)...wananchi intakiwa waone yote hayo na wakati wa uchaguzi wakumbuke haya yote.

  3. Je, Watanzania tufanyeje ile nasi tupate meendeleo waliyopata Malaysia, ambao walikuwa masikini kama sisi miaka ya sitini?
  _______________

  Kwa kweli ni kazi kubwa lakini inabidi kama wananchi inabidi tushirikiane katika kujenga uchumi, kuelimisha jamii n.k.
  Inahitaji tuwe na mikakati katika jamii zetu ndogo (kutumia mfano wa wakati wa wajumbe wa nyumba kumi kumi),kila sehemu ijue idadi ya watu wake wanafanya shughuli gani? na wanawezaje kusaidiwa/ kujisaidia kujikuza kielimu/ kiuchumi? Inaitaji kusoma jinsi mwendo wa maendeleo wa nchi unapoeleke na kuwaweka vijana wetu katika mwendo huo....

  ...Hayo tu ni machache napenda kuyatoa kuchangia hoja hii!!

  ReplyDelete
 3. Maswali yaliyoulizwa ni ya msingi kweli.
  1.Kuhusu jumuia ya Africa mashariki ni kweli nadhani hofu ya watu wengi iko hivyo.Lakini nafikiri kwa upande mwingine wa sura hii ni kwamba hakuna sababu ya kuogopa kwamba sisi tutakuwa na nafasi za kufagia ndani ya jumuia.Hii ingekuwa ni changa moto kubwa kwetu kwelikweli.Kwani tukiogopa hilo je tumewasismamisha wakenya wasiendelee kusoma? hapana hatujawazuia,kwahiyo unakuta tuna hofu ya kijinga kabisa.Tujifunze toka kwa wakenya maana ni wenzetu.Mbona tunajifunza toka kwa wazungu!,mbona tuanungana na mazungu katika hata mambo amabyotungeweza kuyafanya wenyewe!.

  Ni kweli wakenya wamekwenda mbali katika nyanja nyingi.Mfano.Hapa Tanzania hatuna vyuo ambavyo vinaweza kutoa Degree za Criminal Justice,security Management,Criminal Investigation na elimu nyingine ya juu ya maswala ya uhalifu wakishirikiana na vyuo vingine vya nje kwa maana hiyo ukitangaza kazi kama za wapelelezi au maswala ya usalama utawakuta watanzania wengi hawatapta nafasi hizo maana hatuna vyuo hivyo na nafasi zikitangazwa zitakuwa zanawapa mataifa mengine nafasi zaidi kuliko watanzania.Hii ni kweli lakini ni kosa la nani? ni serikali yetu butu katika mambo haya ya usalama.Ikiwa nafasi zitagawiwa kwa nchi haizo tutapata lakini ikija kwa qualifications kama kwa mfano nilioutoa hapo juu utakuta hatutaweza kuingia au kugusa katika ushidani huo.

  Aidha hawa walioajiriwa katika nchi hizo amabo walibahatika hawapendi kuwaona wengine wakiwafuata huko maana hata akiona jina la mtanzania mwenzake ndo inkuwa sumu kabisa maana tumelewa sifa tu ili uitwe aa fulani fulani.Kwa hiyo tuna wivu wa kijinga hatupendi mtu mwingine apate.Sifa moja wa[po ya watanzania walionayo huku duniani ni ubanafsi na kutokusaidiana ili kuinuana.Sisi sio kama wakenya au watu wa west Africa.

  Serikali pia iruhusu kama kuna mfanaya kazi amepata kazi katika jumuia za kimataifa basi aruhusiwe aende kufanya kazi hiyo chini ya mkataba wa kurudi kazini (Secondment) huko wakaoenda wanajifunza mambo mengi na ujuzi mwingi amabo atawaambukiza wenzake wakati wa likizo na wakati akirudi kazini wenzetu wengi ndivyo wanavyofanya lakini kwa nchi kama Tanzania mameneja wakuu wa idara wanakuwa na sheria zao za wivu tu.Wakubwa hawafikirii hawa watu wakienda wataleta nini kwa upande wa utaalamu wa kazi, wao huangalia akirudi atakuja na nini bila kufikiria ujuzi atakaouleta.

  Wakubwa wengi hawapendi maendeleo ya wengine hupenda maendeleo ya wajomba na watoto wao ndio wayapate hayo.Huu ni ubinafsoi na ndio unatufikisha hapo tulipo.Tukibadilika tutaweza laikini kama hii gubu itaendelea hakuna kitu utaona na mafanikio ya matabaka machahche tu yataibuka.

  Mchango wangu ni huo.Hayo ni mawazo yangu na ndio ambayo nimeyaona kawa macho yangu na uzoefu wangu.

  ReplyDelete
 4. 1. ndio that federation itatunyakulia kazi zetu. wenzetu kila mtu ni college graduate na sisi kwetu kila mtu ni form IV graduate

  2. i have no clue about this

  3. tukiacha kutegemea kuexport kilimo na raw producs tutawafikia. wenzetu wana export finished products na technology goods

  badala ya kuexport kahawa ikiwa haiko kwenye packages tunge brand na kuship ready to use. hapo tunaengeza viwanda vya kuiprocess na kuipark. tunaiuza kwa hela nyingi na pia ajira zinaongezeka. Samaki, kahawa, sisal etc tungefanya the same.

  ReplyDelete
 5. 1. Hamna haja ya uoga. Kwani hamna mtu anaye iba kazi. Mtu mwengine anaweza pata kazi badala ya wewe kwa sababu ya vigezo vyake kielimu labda, au uzoefu nk....cha kufanya ni kujiandaa vyema ili kuchukua nafasi nzuri kwenye fani inayotuhusu

  2. Tunachoweza fanya ni kuishi kwa kutoa mfano. Kwani kama mtu binafsi anafanya vitendo fulani, vizazi vinavyokuwa na kumuona akifanya vile vitaona, au vitadhani kuwa ni sawa. Kwahiyo kilichobaki ni sisi kujitahidi kwa kufanya sawa, na kuongea juu ya vitendo visivyo sawa

  3.Kama quotation yako inavyosema , "it can be done, play your part"...
  ni kwamba ule uchungu hatuna..au ari hatuna ya kujiendeleza kama taifa. kila mtu anajiendeleza binafsi, ambayo ni muhimu na ndo mwanzo, lakini isiishie hapo. ni kwamba baada ya kusimama imara , nasi inabidi tunyanyue wale ambao hawajafika kiwango cha maendeleo. Ni lazima tuelewe kuwa sehemu ya kujiendeleza binafsi pia ni kutenda yale ambayo ni majukumu yetu kwa TAIFA, kwa JAMII....

  ReplyDelete
 6. KAZI KUBWA TULIYONAYO NI KUWABADILI WANA CCM WAACHE KUJALI SANA NGUO ZA KIJANI NA WAJIONE KUWA NI WATANZANIA NA SI WACCM. WAJUE NA WAUKUBALI UKWELI, WAUKATAE UONGO NA WAIPENDE NCHI ZAIDI YA CHAMA. TUKITIMIZA HAYA TUTAIOKOA NCHI YETU KUTOKA KWENYE UFISADI UNAOTETEWA SANA NA WANACCM HIVYO TUTAIONGEA MAPATO NCHI NA MAPATO HAYO YATATUMIKA KWA MASLAHI YA WATANZANIA WOTE HIVYO TUTAFANYA KAZI KWA BIDII KWANI TUTAKUWA TUMEONA FAIDA YA MAPATO YETU, BILA HIVI TUTAENDELEA KUWA NYUMA YA MASIKINI WENZETU.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...