Home
Unlabelled
mdau wa washington dc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Sasa Michuzi hapo ni kwamba wewe u mfupi sana au jamaa yu mrefu sana?
ReplyDeleteLo! angalia Michuzi huyo jamaa atakumeza, hahahahaaaa!
ReplyDeleteMbona hukusema anaitwa nani maana anafanana na Flavian tuliyepoteana tangu Tambaza miaka ya 1982 form 2K
ReplyDelete...
Michuzi iyo inakaaje mbona wewe kiatu kinashine wakati chake vumbi,ilikuaje kuaje
ReplyDeleteKweli bongo tambarare, Nikilinganisha ndula mlizovaa za mshikaji ya maboksini zimechoka vumbiiiiiiiiiii zako michu zinangara kama za afande kiimbi pale Mgulani.
ReplyDeleteSijawahi kuona mtu akicheka kama huyo tangu nizaliwe..yaani unaweza kuhesabu meno yote...Michuzi ulimuahidi nini? He he he he he eh eh...hicho kicheko..ona hayo meno..ha ha ha.....!!
ReplyDeletehuyu jamaa mdomo wake ndo ulivyo, au pozi za picha tu??
ReplyDeletemhh, yani mdau kachekelea kweli kweli, hivi amefurahi kukuona michuzi au ni aje,
ReplyDeletehaya siku njema
Tehe teh tee!
ReplyDeleteNyie Michuzi hamumjui kwa kupenda DEZO?
Hapo mwenzenu alitoka ku-brashi viatu vyake kwenye zile mashine za kubrashi viatu bure zinazokaa mahotelini.
Ndio maana kanayanyua mguu makusudi ili yuone reflekshen.
Kwa hali ya kawaida mtu huwezi kusimama hivyo.
Alitaka tuone polish ya dezo hiyo!
Hongera lakini. Wewe ni M-bunifu.
Tehe teh tee!
sio vumbi,si mnajua tukishuka huko tunajua ni vumbi tupu kwa hiyo tunakuja na boots sio viatu vya maana kwa sababu tunakuja kwenye mbuga,na si mnajua michuzi kavaa mng'alo sababu kaitwa kempinski na hajazoea zoea sasa anaogopa ogopa inabidi apendeze
ReplyDeleteMichuzi huyo jamaa anaitwa Flavian nasikia ni Telecom Engineer huko Marekani miaka mingi.Jamaa very bright. Mimi pia tulikuwa naye Tambaza miaka hiyo. Ila tumepoteana siku nyingi. Michuzi naweza kupata contact za jamaa?
ReplyDeleteduu afadhali hapo michuzi kabadili shati....na viatu
ReplyDeleteKaka Michu duu huyo kaka mlimchekesha wakati picha inapigwa, hilo si tabasabu anyway anapendeza sana. Naomba unieleze kama ameoa, mwenzio natafuta jamaa aliyepanda anitoe
ReplyDeleteTruly the guys is known as Flavian,I remember him as one of the brilliant mathematician in science, I spent a year with him at Mazengo High School.I have got told is one of the most succseeful engineer in USA.
ReplyDeleteWhilst other has managed to prosper in life and career, Am still remaining confused. It is better to benchmark from the best performer like Flavian.I remember him whwn he was doing PGM, with other colleagues, like Honorata now is a PhD. Holder, Inno,is a pilot and many others.
O poor me still suffering confused life of studying.
Dr.Confusion.
Duuh bongo kuna sehemu inaitwa Washington Dc nini manake mchizi choka ile mbaya.
ReplyDeletewe mtoa maoni january 17, 9.45
ReplyDeleteacha ubishoo, ni kawaida yenu kuvaa hivyo. Nani kakumbia ni mavumbi tanzania, Hilo tishet imechoka ka nini sio hata yakuenda kukata majani haifai. Mbaazi akikosa majani husingizia jua. Endelea tu kufuta mavi au kubeba mabox.
Dah kweli huko maboksini maisha tabu mshkaji kavaa nguo za bei cheap halaf hata saa tu kashindwa kununua ..hahaha
ReplyDeleteBongo tambarare kwa sana tuuuuuuuuuu bwa michu LOL
nasikia huko majuu mtu mweusi haruhusiwi kukanyaga sehemu zenye status kama ya movenpick ndio maana jamaa kafuraaaahi kukanyaga for the 1st time sehemu bomba
ReplyDeleteBongo tambarare..sibaguliwi kwa rangi yangu wala kabila popote nikanyagapo
Meno thelathini na nje yote mbili LOL
Labda huyo jamaa ajiunge na timu yetu ya taifa ya 'basketibolu',mnasemaje jamani?
ReplyDeletewabongo wameniuwa nimecheka mpaka mbavu sina .hii ndio inanifanya nione raha ndani ya roho kuwa mbongo asilia .yaani jamaa amepigishwa box nawanyapaaa kafika bongo anaenda kula movienpick kweli maisha wakati huku siku zote mnaenda kula chinese au mcdonald na KFC hapo roho inamuuma kweli fikiria hiyo hela amejipinda masaa mangapi warehouse
ReplyDeleteNi hakika huyo jamaa ni mrefu, yaani michu hata bega hujalifikia! kisturi pia tukikupandisha huwezi kumpita urefu. picha inafurahisha ukiitazama kwa makini kwa muda mrefu.
ReplyDeleteYoh! people have to grow up! dress code kwani ipo hadi mtaani! jamaa kavaa casual hana mkutano na hayuko ofisini! sasa ajipigilie misuti na joto la december Dar hajipendi. Dar watu tuna over dress bila sababu. Kuvaa kivipi ni option ya mtu! sio unavaa hadi ukaazime cha jirani ili uonekane uko juu kumbe hata pa kulala huna! wengine walishamaliza mavazi wanafocus kwenye kuwekeza.
ReplyDeleteDah mnaomcrash huyu jamaa labda hamjui cv yake,, Huyu jamaa anaitwa Flavian jamaa yupo juu sana asee si mbeba box huyu maana ni kijana msomi na shule imepanda haswa si kitoto na mkwanja anao si wa kitoto na mke wake ana deal na sumercamp pogram na wanauraia wa marekani sasa nyie mnaaona jamaa anabeba box mh kalaga bao
ReplyDeleteHAKUNA WATU WANAFIKI DUNIANI KAMA SISI WATANZANIA.MABITOZI WAKIPIGA MAPAMBA WAKIWEKA PICHA MNAWAPAKA KWAMBA KAZI NI KUVAA TU MAREKANI NA KUPIGA BOKSI,SASA JAMAA KAVAA SIMPLE MNAKUJA JUU KWAMBA KACHOKA.JAMAA ENGINEER NA SIO KWAMBA HANA HELA YA KUVAA HIO NDIO STAILI YAKE KUWA SIMPLE HANA MAKUBWA HATA KAMA NGUO NI CHEAP LAKINI KAWEZA KURUDI NYUMBANI KUWATEMBELEA NDUGU ZAKE.ACHENI UJINGA KUWENI HAMNA MTU ANAISHI HILI KUWARIZISHA NYINYI KILA MTU ANAISHI MAISHA YAKE. " THE NICER THEY LOOK THE BROKE THEY ARE". ALAFU MTU AKIWA HANA KITU NDIO ANAKUWA ANAOGOPA JAMII ITAMUANGALIAJE NDIO MAANA WANAENDA KUFORCE MAMBO WASIO YAWEZA MWISHO WAKE MNAANZA KUINGIA KWENYE MADILI YA AJABU MNAISHIA JELA.
ReplyDeleteduuuh huko kucheka si mchezo,chapati hakunji huyu!!!!
ReplyDeleteJamani, Flavian namfahamu ni jamaa mmoja yupo very simple lakini anafanya matusi ile mbaya pote hapa USA na bongo. Huyu jamaa kama kuna kubeba box kwa ubongo/akili ndio huyu hatumii msuli mnofu. He is very strategical na hajionyeshi. He is doing very fine. Jamaa mpaka ana boat, weekend summer huwa ana kwenda kuvua burudani. Jamaa katulia yani hana tabia za kibongo za kujionyesha onyesha onyesha. Wabongo wengi huku majuu wanakopa pesa alafu wanafanya vitu vya hovyo hovyo. Huyu jamaa anafanya anafanya vitu vya maana sana . Iwapo wabongo wengi walio majuu wangekuwa na tabia ya Flavian mambo yangekuwa tofauti. Lakini wengi wanapenda ushamba wa ulimbukeni, huyu jamaa hababaishwi na kitu. Anajiamini sana na ndio maana hathamini mavazi.
ReplyDeleteJamani huyu jamaa hamumjui ! ana mkwanja si wa kawaida na kama kuna mtu anayeweza kuwa role model kwa wabongo USA ni huyu.
ReplyDeleteLakini huwezi kumjua kabisaa kwa jinsi alivyo simple, ukielezwa matusi yake/vitu anavyo fanya ndio utashangaa. Michu muombe jamaa CV yake uitundike humu. Jamaa ni anatesa.
kweli nimeamini hii ni blog ya waosha vinywa (Michuzi) yaani sina hata la kusema. Wamemchimba kaka wa watu maskini mpaka basi. Mavazi sio suluhisho la maisha!! Ametoka simple kaka wa watu maskini. Hivi naomba mnieleweshe, kuwa majuu ndio kuvaa vizuri ama? Kwa hili nashindwagwa kupata maelezo kamili kila nitembeleapo blog hii, especially wakiona mtu wa ughaibuni, watamchambua weee kuanzia mavazi mpaka sura. Jamani tuelemike kwa ufupi kuwa majuu sio kuvaa vizuri na kuwa na sura nzuri kama mtakavyo nyinyi wabongo. Mnaninchosha kwa ufupi!! Mbeba kikobsi - london
ReplyDeletethat is real african people. michuzi hapo unatoka mara mmoja na nusu.
ReplyDeleteThank you for BIG BIG smile bro.hou make me smile too
Jamani eeh hebu telewane! kuwa SIMPLE sio lazima uwe mchafu. Nakubaliana kabisa na wadau waliosema wabongo tumezoea kuwa over dressed....lkn bado haibadili dhana nzima ya UCHAFU na USAFI...hivi vile viatu alivyovyaa mshirika(msomi flavian) mmevia assess kwa kina au mnakimbilia kwenye u SIMPLICITY tu....kwanini tusiwe wakweli tu jamani, vile viatu sawa ni simple lkn kuna mtu anaebisha kuwa vile viatu ni vichafu? najua wengine mtasema muda labda kwa kuwa yupo busy..na atokee mtu mwingine adumbukize picha yake kwenye blog hii akiwa na viatu visivyozingatia matunzo kama vile kati ya nyinyi juu mliotoa maoni ya kuunga mkono huyu bwana....cha msingi hapa ni USAFI sio suala la ku OVER DRESS au KUWA SIMPLE
ReplyDeleteeti hana saa ya mkononi wa bongo bwana taaabu sana. Kama saa ndio maendeleeo basi bongo yote ingekua mabillionear. kila mtu ana saa za mkononi lakini life imewapiga chenga sana tu . Kutwa kucha wanapendeza lakini hawana hili wala lile. Mngejua kuingia hotel kama hiyo huku ni uamuzi wako na wala sio big deal. Huku kula nje jambo la kawaida na watu wanakua proud wakipika msosi nyumbani. Huku inacost more na it is os much time consuming to prepare a meal at home than to eat out jamani
ReplyDeleteKwanza saa za mkononi ni thing of the past siku hizi. Ukiwa unavaa saa ni accessories tu siku hizi kwenye party, casual wear saa ya nini kila gadget ulionayo ina saa. Kama hudrive kila subway, bus na kila mahali unapokwenda kuna saa..... bongo hiyooooo listerine wako wengi sana lakini midomo haiachi kunuka. Majungu tuache.
Anony wa jan 18, 09:02, mshikaji inaelekea unamaindi sana mambo madogo madogo. hivyo viatu vya jamaa inawezekana sio uchafu bali jamaa ametinga 'Hush Puppies' ama 'Clarks' za brown za bei mbaya!
ReplyDeletehapo, vipi?
bro michu: mi natamani kuleta salamu na kuambatanisha na picha ,ila kwa mtaji huu? kila nikiangalia naogopa hayahaya mana kaka ametusalimu hapo yamekua maneno dada cynthia katutaarifu biashara yake manenoooo pamoja na uzuri wake, mhabeshi wawatu kalapozi nawewe kule ooh mronjo kama mfyonza ukwaju, kaka teri katusalimu kwa upendo pereperepere hee jamani mtima nyongo huoooo!
ReplyDeleteSasa mi ntaleta salamu zangu nitafanya kama yule aloweka tv mbili ila alificha sura yake mimi ntaleta taulo nyeupe toka dukani leo ,haina lable wala picha plain, pia watasema:- "lo hiyo taulo chafu inatoa harufu hapo pooo"! jamani jamani,
{SOLO}: wivu
WOTE: ah! ah!
{SOLO}:wivu
WOTE:wawakereketa X2
WASHINGTONIAN UNAWAAMBIA WABONGO HUYU JAMAA ANA BOTI, UNAFIKIRI WABONGO WANAELEWA MAANA YA KUWA NA BOTI HUKU JUU?
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteWADAU KUNRADHI KUWAINGILIA KWENYE UKUMBI HUU WENU AMBAO MIE HUJA MARA CHACHE SANA, HASA KAMA KUNA DHARURA KAMA HII.
ReplyDeleteMARA NYINGI NIMEKUWA NIKILAUMIWA KWAMBA NABANIA MAONI YA WADAU, JAMBO AMBALO SI LA KWELI ENDAPO KAMA MAONI HAYO HAYAHARIBU HALI YA HEWA.
MFANO WA MAONI NINAYOBANIA NI HUYO MDAU HAPO JUU YA HII.
JE NIACHIE MANENO KAMA HAYO AMA NIENDELEE KUBANIA. HII NIMEWEZA KUWEKA KWA SABABU MUATHIRIKA NI MIMI, HIVYO SINA MATATIZO. SASA MANENO KAMA HAYO AMBAYO NDIYO NABANA MNGEPENDA NIYAACHIE YAENDE KWA WADAU AMA YAJE KWAKO EWE MDAU?
NAFURAHI KUONA HUYO MDAU AMETUMIA HAKI YAKE YA KIDEMOKRASIA YA KUSEMA KILICHO MOYONI MWAKE NA NAAMINI ROHO YAAKE ITAKUWA IMESUUZIKA SASA. NA NAKUHAKIKISHIA KWAMBA NDIO MWANZO UMENITIA MOYO KUENDELEZA LIBENEKE MARA MBILI YA HAPO...
ASANTE MDAU MIE NAOMBA MUNGU TU NA ATANILIPIA MOLA KWA MANENO HAYO - AMINA!
Ninyi waswahili hamtandelea. mnatumia muda mwingi na teknolojia hii adimu kuzungumza utumbo. Badala ya kuungelea masuala ya muhimu kwa maindeleo yeinu. Mtabaki kunyonywa na watu wingine milele, mnabaki kutukana tukana na kusema ovyo.
ReplyDeleteMzungu Mtanzania
BWANA MICHUZI, MIMI NDO YULE MDAU NILIYEKUTUKANA, NIMEJISIKIA VIBAYA KWA NILICHOANDIKA NA NINAOMBA MSAMAHA AS GENTLEMAN,ILIKUWA NI FRUSTRATION YANGU KWAMBA I TRIED MORE THAN 4 TIMES TO COMMENT UP HERE BUT ALL WAS REJECTED THUS WAS MY DISCRETION. SO PERSONALLY NINAIPENDA BLOG NA KAZI YAKO ILA NILISHINDWA KUELEWA WHY KWA NINI HATA CLEAN VERSION YA COMMENT UNA REJECT?THAT'S THAT.KWA MANTIKI KWAMBA WEWE NA MIMI TUTAKUBALIANA KITU KIMOJA KWAMBA SOTE NI WACHA MUNGU SO NAOMBA MSAMAHA WAKO NA NINAONGEA HII KUTOKA MOYONI KWANGU HAMNA SHINIKIZO LOLOTE LILE CAUSE I DON'T HOLD GRUDGES ON ANYBODY SO FORGIVENESS IS YOUR CHOICE AS I CURSED YOU OUT BUT THAT'S ALL I ASK BRO..PEACE
ReplyDeleteMungu wangu, kweli huyo mwandishi (Jan 18th, 4:41:00PMEAT) ni mzima? I doubt he is/was sane when posting that.
ReplyDeletePole sana kaka Michuzi. Nakuomba uondoe comment zake. Huu ni uchafuzi wa hali ya hewa, mi nakuunga mkono; maoni ya nmna hiyo endelea kuyabania!
Michuzi,
ReplyDeleteNafsi zao zimejaa chuki binafsi wala hazieleki(Mkanye mjinga akuchukie na mipango yako akuharibie).
KAKA SHIKAMOO,TAFADHALI HIYO COMMENT TUSHAIONA IONDOE TU SASA,KAMA MAMBO YENYEWE NDIO HAYO,,WE ENDELEA KUYACHUJA TU KAMA KAWAIDA, WE MTU MZIMA UNAJUA MEMA NA MABAYA,,,YAMENIUMA SANA HAYO MANENO----
ReplyDeleteBIBLIA YASEMA:..KWA MAANA BWANA NI MUNGU WA KISASI, HAKIKA YAKE YEYE ATALIPA...
WE ULIYEANDIKA MANENO HAYO KWA KAKA MICHUZI, TULIA KIMYA, UMUOMBE RADHI MUNGU WAKO, LA SIVYO YATAKUJA YAKUTOKEE MABAYA SIKUMOJA, MARK MY WORDS.
Pole sana ndugu yangu michuzi. Kwenye jamii watu kama huyo aliyetuma hayo maoni ya matusi wapo tena wengi tu.
ReplyDeleteNafikiri hapa usijali lawama za kubania hoja zisizo kuwa heshima, weka maoni yanayositahili katika jamii.
Pole sana
Jamani, watu tuko na akili zetu tunakaa apa kujadili mavazi kama vile tuko form one, can we have some other constructive discussion, ooh please we need more than this. Mavazi sijui kavaaje, kiatu kiko upande tuwaachie ma receptionist na secretaries maana wao ndo kioo cha ofisi,. Huyu kaka labda alitoka zake site kuangalia jumba lake analojenga huko Mbezi akaamua akapate lunch! na hicho kiatu huenda ni rangi! hata mjini kuna jeans za rangi chafu kama vumbi vile, zinauzwa na ni expensive pia! u dont have to shine to look expensive, na kwa taarifa yenu huenda hicho kiatu chake kina bei mara kumi ya cha kaka Michuzi, kwa ajili ya hiyo sura (mnayoiona) mbaya! come on, grow up people!
ReplyDeleteWe anon friday 18 4.41pm.
ReplyDeleteKwanza kabisa safisha mdomo na lugha yako. Lugha gani hii kwani unadhani watu wako wapi hapa, maneno machafu yanatia aibu, kweli ulizaliwa na kukuzwa na wazazi au ulikulia mitaani?
MICHUZI TAFADHALI COMMENT ZA STUPID PEOPLE LIKE THIS DON'T BOTHER EVEN TO PRINT. PUT THEM IN THE BIN. NO MANNERS AT ALL, Unajua unachokifanya na kama atachukia aanzishe blog yake na wajinga wenzie. HE/she need to apologize.
SIKUTENGEMEA KAMA KUNA WATANZANIA WENYE LUGHA CHAFU KAMA HII
MDAU UNAYEUNGAMA KWAMBA NI WEWE ULIYECHAFUA HALI YA HEWA HUMU NAKUSAMEHE NA PIA NAKUSIFU KWA HATUA HIYO KWANI NI WACHACHE WASIO WASTAARABU AMBAO WANGEFIKIA HATUA HIYO.
ReplyDeleteSINA KINYONGO NA WEWE ILA NAKUSIHI UELEWE SI TU HII BLOG INASOMWA NA WATU WENGI WAKIWEMO WATOTO NA WATU WAZIMA WENYE HESHIMA ZAO.
NAMI PIA NISAMEHE KAMA NIMEBANA MAONI YAKO ILA ELEWA HUENDA NI KWA NIA ILE ILE YA KUOGOPA KUCHAFUA HALI YA HEWA. NA HALI YA HEWA HUCHAFUKA KWA MAONI YANAYOLENGA KUJERUHI NAFSI YA MTU AMA WATU KAMA ILIVYOTOKEA BAINA YANGU NA WEWE. HIVYO SHIME NA TUWE NA SUBIRA NA WENYE KUWAZA MARA MBILI KABLA YA KOSHA KINYWA.
MUNGU NA ATUSAMEHE WOTE KWA LOLOTE BAYA TULILOFANYA. KWA NIABA YA WADAU WOTE NAKUBALI OMBI LAKO LA MSAMAHA NA TUENDELEZE LIBENEKE BILA CHUKI WALA HASIRA.
NAWASILISHA HUKU NIKIONDOA ULE UCHAFUZI WA HALI YA HEWA. ASANTE NA SHUGHULI NJEMA...
MDAU UNAYEUNGAMA KWAMBA NI WEWE ULIYECHAFUA HALI YA HEWA HUMU NAKUSAMEHE NA PIA NAKUSIFU KWA HATUA HIYO KWANI NI WACHACHE WASIO WASTAARABU AMBAO WANGEFIKIA HATUA HIYO.
ReplyDeleteSINA KINYONGO NA WEWE ILA NAKUSIHI UELEWE SI TU HII BLOG INASOMWA NA WATU WENGI WAKIWEMO WATOTO NA WATU WAZIMA WENYE HESHIMA ZAO.
NAMI PIA NISAMEHE KAMA NIMEBANA MAONI YAKO ILA ELEWA HUENDA NI KWA NIA ILE ILE YA KUOGOPA KUCHAFUA HALI YA HEWA. NA HALI YA HEWA HUCHAFUKA KWA MAONI YANAYOLENGA KUJERUHI NAFSI YA MTU AMA WATU KAMA ILIVYOTOKEA BAINA YANGU NA WEWE. HIVYO SHIME NA TUWE NA SUBIRA NA WENYE KUWAZA MARA MBILI KABLA YA KOSHA KINYWA.
MUNGU NA ATUSAMEHE WOTE KWA LOLOTE BAYA TULILOFANYA. KWA NIABA YA WADAU WOTE NAKUBALI OMBI LAKO LA MSAMAHA NA TUENDELEZE LIBENEKE BILA CHUKI WALA HASIRA.
NAWASILISHA HUKU NIKIONDOA ULE UCHAFUZI WA HALI YA HEWA. ASANTE NA SHUGHULI NJEMA...
Pole sana kaka michuzi.Umejitolea kutpatia taarifa za nyumbani ila ndio hivyo tena.Kama ulivyosema na walivyokwisha sema wengine,usiweke kamwe lugha zenye kuharibu hewa huku.Asante.Ubarikiwe
ReplyDeleteJAMANI MIMI JANA SIKUFUNGUA COMPUTER YANGU LAKINI INAONYESHA MTU ALIJISAHAU AU JAZBA ILIMZIDI,KAKA MICHU POLE SANA,MAELEZO YAKO YAKUKUBALI MSAMAHA YANAONYESHA WEWE NI MTU WA AINA GANI,COOL,PATIENT AND EDUCATED MAN.WATU WA CUSTOMER CARE INABIDI WASOME KUTOKA KWAKO.ENDELEZA LIBENEKE
ReplyDeletethis is a GENTLE GIANT watu kama hawa inabidi wafurahi kila saa ama sivyo, binadamu wengine hawatapata amani!!! looking good bro, keep up!!!
ReplyDelete