RAIS Thabo Mbeki wa Afrika Kusini juzi (Jumatano, Januari 2, 2008) alimtembelea hospitali na kumjulia hali Balozi wa Tanzania nchini humo, Emmanuel Mwambulukutu.
Balozi Mwambulukutu alilazwa hospitalini mjini Pretoria/Tshwane wiki iliyopita baada ya kuwa amevamiwa na kuumizwa na majambazi.
Kabla ya kumtembelea Balozi, Rais Mbeki alimpigia simu na kuzungumza na Rais Jakaya Kikwete, akimwelezea masikitiko yake juu ya tukio hilo la kuumizwa kwa Balozi Mwambulukutu.
Rais Mbeki pia alimweleza Rais kuwa hadi juzi hiyo, mmoja kati ya watu wanaosadikiwa kumshambulia Balozi Mwambulukutu, alikuwa tayari amekamatwa na polisi.
Rais Mbeki alimweleza Rais kuwa majambazi wengine watano bado wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo. Aliahidi kuwa Polisi wa nchi yake watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa wote wanapatikana na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Balozi Mwambulukutu aliumizwa wiki iliyopita wakati watu wasiojulikana walipovamia nyumba ambako balozi huyo alikuwa anafanyiwa hafla ya kumwaga, na wakajaribu kuiba gari.
Balozi Mwambulukutu anatarajiwa kurejea nyumbani karibuni baada ya kuwa amemaliza muda wake wa utumishi wa ubalozi wa Tanzania katika Afrika Kusini.

hizi 'party'jamani...anagharimia nani?si jasho letu walalahoi ???sasa kama jambazi la kisauzi limewapora...si ajabu manaake ' easy come easy go'!!!
ReplyDelete