Michuzi,
Nami pia nachukua fursa hii kuchangia mawazo yangu katika hili
kwa mdau alochangia na kaka michuzi kuna mnanishangaza sana
mimi ni mdau katika sekta ya afya.
kwa mdau alochangia na kaka michuzi kuna mnanishangaza sana
mimi ni mdau katika sekta ya afya.
La kwanza la ajabu ni kwa nyinyi kupotosha jamii kuwa upasuaji umetokea hospitala ya taifa muhimbili wakati sio kweli bali ni hospital ya mifupa ya MOI(MUHIMBILI ORTHOPAEDIC INSTITUTE) ambayo haina uhusiano kabisa WA KIUTAWALA NA KIUTENDAJI na MHN ,kweli hamuwezi fanya utafiti wa kina kama ili mkawa informed kabla ya kuandika habari ????
Ni kweli kuwa majengo yamechukua muda sana kwisha kwani yalianza kukarabatiwa tangu 2002/2003 na hadi leo hayajaisha lakini ni majengo ya muhimbili national hospital na sio MOI japo MOI inatumia wodi mbili za MNH kwa makubaliano maalumu.
Lakini kwa ufupi kinachosababisha wagonjwa wa tatizo kama la mgonjwa wa ubongo kufa sio majengo tu bali zaidi ni utamaduni wetu wa kutotafuta huduma za afya mapema zaidi tunmasubiri hadi baadae sana hali ikiwa mbaya ndio tunaibuka hospital na ugonjwa ushasambaa hata majengo ya kiwepo ni tuu leiti.
Siwatetei madaktari waliosimamishwa kwani jambo lishatokea na linashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za sekta hii lakini pia hilo la kusema mgonjwa kauwawa na madaktari mwandishi wa mwanzo kashalifafanua vizuri
CHONDECHONDE TUWE WEPESI WA KUFUATILIA HABARI ILI TUWE INFORMED NA TUSIKURUPUKE NA KUPOTOSHA JAMII BILA SABABU NI AIBU MTU UPO DAR MIAKA YOOOTE TATIZO LIMETOKEA MOI TANGU NOVEMBER LEO ZAIDI YA MIEZI MIWILI BADO WEWE UNADAI TU NI HOSPITAL YA TAIFA WAKATI NI TAASISI TU YA MIFUPA MUHIMBILI INAYAOJITEGEMEA KILA KITU
Mdau wa afya
MDAU WEWE WANENA... NI MUHIMBILI BAAAASI!!! MOI ikifanya vizuri mnasema ni sehemu yenu ikivurunda mnadai si yenu KWIIISHAAAA!!!!
ReplyDeleteWEWE BWANA UNAYEJIITA MDAU WA AFYA NA KUWEKA UJUMBE HAPO JUU, NAKUJIBU KIFUPI IFUATAVYO.
ReplyDelete1. USIWAPOTOSHE WATANZANIA KWA KUWEKA MIPAKA KATI YA NENO TAASISI YA MIFUPA NA HOSPITALI YA MOI. TOFAUTI UNAZOTUELEZA NI NDOGO MNO. MAGAZETI KIBAO MFANO HUWA YANASEMA KUWA MGONJWA KAFIKISHWA HOSPITALI YA MUHIMBILI, NA DR. ALMASI ALITHIBITISHA KUPOKELEWA KWA MAJERUHI HAO. NA HUJAWAHI KUWAKOSOA. KWA MAANA UNAJUA SI KITU CHA KUTOFAUTISHA SANA, NA WATZ WANGAPI WANATAKA HILO? INAONEKANA UNGEKUWA MTAWALA WALA USINGEPENDA HATA HABARI ZA HAO MADAKTARI ZIANDIKWE.
2. UMEMTUHUMU HATA MICHUZI KAMA VILE YEYE NDIYE ANAWEKA HABARI ZOTE KATIKA BLOG HII, KUMBE NI SISI ZAIDI, NA YEYE KAZI YAKE NI KUTUNDIKA TU ILIMRADI HABARI HAINA MATUSI. HILO LA UTAWALA TOFAUTI YEYE HALIMHUSU, SAWA?
3. ILI USIWAPOTOSHE WASOMAJI, NITAKUPA MFANO. PALE UDSM, IDS, KITENGO CHA UTAFITI WA KISWAHILI NK. NI TAASISI, NA ZINA UTAWALA WAKE, NA ZINAJITEGEMEA VILEVILE. JE, TUSISEME JAMBO LIMETOKEA CHUO KIKUU CHA DSM MFANO, SABABU TU NI TAASISI ZINAZOJITEGEMEA? WE MWENZETU VIPI?
4. ACHA KUTUELEZA HABARI ZA MAJENGO YA MOI NA MUHIMBILI BWANA. MBONA WATU TUNAPENDA KUZUNGUKA MBUYU? UNAJIBU KAMA YULE BWANA WA WESTERN UNION ALIYEJIBU KWA KUIFAGILIA OFISI YAKE, WAKATI WADAU WANAONGELEA MATATIZO. HEBU NA WEWE CHANGIA MADA INAYOHUSU WAGONJWA KUPASULIWA KIMAKOSA, NA SI KUTUELEZA MGAWANYO WA KIUTAWALA. KWANZA TUNAWEZA HATA KUILAUMU WIZARA YA AFYA WALA TUSITAJE MUHIMBILI AU MOI. MAJINA HAYANA UZITO SANA KAMA UNAVYOKAMIA WEWE!
Mdau unaleta porojo, Moi nini, na MNH ni nini hizo zote nafikiri zinaanza na neno Muhimbili! Sasa unaposema ni Moi sio Muhimbili una maana gani? kumbe wewe ndo hujafanya utafiti. Huyo mwingine ni subset na mwingine ni set nzima! Usituongopee!
ReplyDeleteMdau wa afya,nadhani watu wengi wanacholalamikia ni kile kitendo cha ku-"switch" wagonjwa.Hata kama mgonjwa alikuwa kwenye "final stage" ndio waache kuwa makini kwa sababu tu,hana muda mrefu wa kuishi?
ReplyDeletePia ni wachache wanaotofautisha kati MOI na MNH kutokana na vyombo vyote vya habari vinavyo-present habari.
Na mdau mwingine ameeleza kuwa hiyo imechangiwa na uhaba wa vyumba vya upasuaji,mbona kesi kama hii ilitokea kwenye hospitali kubwa tu Marekani?Labda nako kulikuwa na uhaba wa vyumba vya upasuaji!Uzembe umeshafanyika,tuangalie jinsi ya kuzuia usije tokea tena.
Kwani hata hao wahusika sidhani kama watashitakiwa kwa mauaji.
Anyway I have gotten confused a bit with the discussion,however,I would like to comment using Configuration and Structure wise of the Muhimbili organisation.
ReplyDeleteThere is range of organisation structures with their scope of service rendering along with decision making system
Cha muhimu hapa watu wasichanganyikiwe na tofauti hizi,inachotakiwa mfanye upembuzi yakinifu kwamba je muhimbili mgawanyiko wa madaraka na utendaji wake upoje kwa ujumla.
I mean the hierarchical: Does the national Hospital control, monitor and supervise the MOI, if so ,how, where, what and when such control are exercised, is it in the form functional, multifunctional, matrix organization system. Then we can be on the right side of arguing evidently.
Nia yangu ni kuweza kuzuia mijadala isiyo kwenye form ya broad vichwa wala migu bali kiwiliwili tu,kwa hiyo huwezi tambua nini hasa cha bishaniwa ama kujadiliwa.
Kwa hiyo nawapa homework mnaobisahana,fanyeni uchunguzi huo ndio muanze kukosoa kila upande.
Kwa sababu inawezekana hata waliotolewa hawana kosa kosa lipo kwenye uandaaji wa taratibu za opareshenbi,ama hata motisha kwa watendaji,who knows!!Manake bwnana ukiwa kazini lakini huna uhakika wa kesho kama walivyo wanasia na watu wa kada nyingine unaweza hata ukatia onge puani ukifikiria unaweka mdomoni siyoi masihara wala utani.
Am remains
Huyo anaye jiita mdau wa afya hana jipya la kutueleza. Atake asitake ni Muhimbili ndiko kosa liliko fanyika, mambo ya mipaka mtajuwa nyiyi, end of story!!
ReplyDeleteKuhusu kuwalaumu wagonjwa kwamba hawaendi hospitali mapema hadi hali zao zinapokuwa mbaya ni kutaka kupotosha ukweli uliopo. Watu wanakufa siku hizi Tanzania kwa kukosa pesa za kuwahonga madaktari ili waweze kutibiwa. Naongea kulingana na uzoefu nilio nao. Miaka michache iliyopita nilifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Temeke. Nilikuwa na tatizo la muda mrefu tumboni lililohitaji upasuaji. Baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu na hali yangu ilikuwa mbaya sana daktari alisema kuwa kama nilikuwa nahitaji kufanyiwa upasuaji haraka basi nilitakiwa kulipa pesa. Katika hali niliyokuwa nayo sikuweza kukataa. Nilitafuta Tsh 40,000 na kumpelekea. Daktari alikataa na kusema 'bila Tsh 60,000 sitaweza kushika utumbo wako'. Ilibidi nitafute pesa zaidi na zilipotimia ndipo nilipofanyiwa upasuaji.
Kwa hivi sasa nina ndugu yangu anaye umwa na amefanyiwa upasuaji hivi juzi juzi tu ingawa yalifanyika makosa na atahitaji upasuaji tena. Lakini hadi uamuzi wa kupasuliwa ulpofikiwa alishatozwa pesa ambazo hadi sasa naweza kusema zinafikia hadi laki mbili hivi. Kuombwa chai na manesi na watu wa masijala ndiyo usiseme. Ni kwa vile najitahidi kumsaidia mdogo wangu lakini isingekuwa hivyo tungekuwa tunasema mengine. Kwahiyo kuwalaumu wagonjwa si vyema kabisa tatizo ni hospitali zetu na wafanyakazi wake.
Naomba kutoa hoja.
Ndugu zangu,
ReplyDeletenimefuatilia kwa karibu mjadala huu na kuona nami nichangie labda nitaweza kuwapanua mawazo wenzangu. Lengo siyo kutetea wala kusifia makosa yaliyotokea Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI).
Kuna watu hapa wanachangia kwa jazba pengine landa kwa sababu ndugu zao waliwahi kukutwa na mikasa isiyofurahisha au inayotia maumivu yasiyofutika moyoni.
Kuna mmoja wetu ambaye amenisukuma pia nichangie, pale aliposema tufanye utafiti tujue chanzo. Kwa bahati mimi nimesoma Muhimbili kwa miaka mitano na kufanya kazi pale, na bahati zaidi nimewahi kushuhudia kwenye vikao mbali na kusoma documents mbali mbali za ndani zikielezea jinsi mashirika ya MOI, MNH na sasa Chuo Kikuu MUHAS kiking'atuka kutoka pote MNH na UDSM. Ni kwamba nina uhakika kila shirika katika niliyoyataja hapo juu yana utofauti wa kila kitu, na yote yanaunganishwa na vitu vichache tegemezi kama vile kwenye facilities na utendaji wa baadhi ya staff. muunganiko huu ni wa makubaliano maalumu (Memorandum of Understanding, MOU). Kwa mfano ni wazi kabisa mashirika haya yana uongozi separate, watendaji separate, boards separate na sera na mipango separate kabisa. Sema kwa mfano MUHAS ina wataalamu wengi na wenye qualifications za juu kuliko vyote, hivyo inabidi watumike kutoa huduma kwa wananchi wanaokuja kwenye hizi hospitali mbili, na pia MUHAS hawana hospitali ya kufundishia wanafunzi wao, hivyo watatumia MNH na MOI! Ni mambo mengi ambayo wanahusiana kimfumo na siwezi kuyataja yote hapa, nitawachosha wasomaji.
Suala la Mix up, japokuwa silihalalishi, ni la kimfumo (systemic) zaidi na kwamba hutokea sehemu yoyote ile ya kazi, hata kwenye dunia ya kwanza, na ndo maana mashirika yanayotoa huduma kwa wagonjwa hufanya utafiti kabisa kuhusu ni jinsi gani watazuia mix ups zisitokee. Kwa bahati mbaya imetokea kwetu na imeathiri sana maisha ya ndugu zetu hawa. Pia mix up hutokea kwenye sekta nyingine pia na siyo hospitali tu pekee yake. Kwa mfano fundi wa magari au ndege anapomix mambo yake na ajali kutokea na kuua watu wengi! Hizi zote ni stori zilizowahi kutokea duniani!
Pia suala la media houses kulivamia na kulikuza hili suala bila hata utafiti wa habari na issue zenyewe halikubaliki vile vile. Kuwalaumu madaktari na kutukana taasisi pia haikubaliki, maana kuna watu wanafanya kazi masaa 24 bila kulala na wanapewa 10,000 sh, wakati kuna wengine wanapewa 100,000 kwa masaa kadhaa waliyofanya mkutano wakiwa pale pale ofisini kwao! Hii haileti morali, na endapo tutaendelea kuwalaumu na kuwadharau wale wachache walioamua kubaki kwenye sekta ya afya wakiwatibu ndugu zetu, basi nao watakimbia na tutakosa hata hao wanasababisha mix ups!
Kwa mfano mmoja wa madaktari aliyesimamishwa, ni daktari bingwa wa magonjwa ya kichwa (neurosurgeon). Inachukua miaka mingi sana kumsomesha, na ameshawahi kufanya operesheni zaidi ya 300 successfully. Na kwa hakika alikuwa ni mwenye elimu kuliko wote katika fani hiyo pale MOI. Hata kama atashinda kesi na kuamuliwa arudishwe kazini sidhani kama atarudi tena pale, tayari tutakuwa tumempoteza....kwanza mshahara tunaompa hapa nyumbani kwa taaluma na uzoefu wake ni mdogo mno, pili matusi na dharau, wakati amekesha akisoma ili afike hapo alipo!
Kwa hiyo ndugu zangu kuna ishu nyingi sana za kuangalia na siyo tu kutukana na kurushia madongo wafanyakazi wa sekta ya afya. Kuna ishu za kukosekana kwa morali miongoni mwao kutokana na kutolipwa mishahara inayovutia, kutolipwa posho, mazingira mabovu ya kufanyia kazi na ndiyo maana madaktari wengi vijana siku hizi wameishia kuspecialize kwenye masomo ya utawala, research na kuendesha miradi ya afya! Japokuwa haya pia ni ya muhimu sana kwenye sekta hii, lakini ni indicator ya vijana kuyadharau na kuona hayalipi masomo ya uzamili ya tiba (kama upasuaji, kinamama, macho etc.) Hivyo tusishangae siku moja tukijikuta hatuna kabisa madaktari hawa nyeti wa hizi sekta. Hebu kwa mfano angalia ukienda huko mawilayani mikoa tulikotokea utakuta madaktari wenye digrii walau moja tu wawili hadi wanne kwa mkoa mzima, unafikiri wanaohitimu wameenda wapi? wakati vyuo vimeongezeka, namba ya kuingia vyuo vikuu imeongezeka????
Naomba kuwasilisha.
Dr. Hamisi Kigwangalla, MD, MPH, MBA