Babu Michuzi,
picha hii nimeiona leo kwenye gazeti la mwananchi kupitia mtandao. ila swali langu napenda kujuwa kama kweli mpaka leo hii karne hii ya maisha bora, hivi paka leo wauguzi wetu wameshindwa hata kupatiwa nyezo za kazi mpaka mgonjwa aliefanyiwa upasuwaji wa kichwa anabebwa kama mwizi badala ya kuwekwa kwenye machela? kwakweli hii ni nishai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hi Michuzi kwani hao ni wauguzi au wabeba mizigo pale airport? Mi nilipoiona nilifikiri mlevi mmoja anasaidiwa kunyanyuliwa.
    Serikali yetu haijatulia mpaka taasisi husika. Inasikitisha kuona mgonjwa katika hali kama hiyo bila manesi na wataalamu wa kumshughulikia hapo ndipo wanaposema ilitokea bahati mbaya kweli?
    Sijui kama waziri Mwakyusa na hapo atasemaje?

    ReplyDelete
  2. Halafu hivyo vitanda sio lazima tuagize nje...Tunaweza kufanya welding yetu wenyewe na chuma tulizonazo tukapata vitanda vizuri tu vya kubeba wagonjwa.

    Hii kazi sana

    ReplyDelete
  3. Hawa hawaonekani kama ni wauguzi ni wabeba mizigo pale Airport,ndugu zangu halafu tunasema nyumbani kuzuri we can do better than that.............

    ReplyDelete
  4. Tatizo watu wengi nyumbani Tanzania si wabunifu ( they are not creative). kama alivyosema mdau hapo juu; vitanda au wheelchairs si lazima viagizwe toka nje, kwani hata SIDO wangeweza kutengeneza. Kweli tuna safari ndefu wajameni!!!!

    ReplyDelete
  5. wadau mbona mgonjwa na muathiriwa wa utendaji wa kitabibu bado anaonekana hajapona sawasawa, je ni kwa sababu gani arejeshwe mbindembinde hivyo toka kwa wataalamu India?
    Maanake kuna wagonjwa wengine ambao hawakuathirika vibaya hivyo serikali inaweza kuwabakiza India zaidi ya miezi sita ili kijulikane kama watapona?
    Pia lolote laweza kutokea ambalo hatuliombei kwa mgonjwa hali yake kubadilika ghafla na hata kupoteza maisha, je lawama zitakuwa MOI, India au wizara na serikali kuu ya Tanzania?
    Naomba muongezee mawazo kwa serikali wadau.
    Mdau
    Dublin
    Ireland.

    ReplyDelete
  6. JAMANI HUYO NDO JAMAA WA MOI THEN INDIA WANAMRUDISHA KWA NJIA HII MMH! NGOJA ATEGUKE KIUNO, HAO WALIOMBEBE WATAKOMA

    ReplyDelete
  7. WatAnzania na wadunia wenzangu. Inaelekea lipo tatizo kubwa zaidi limejificha hapo MOI. Hilo ni tatizo la utaalamu wa hao tunaowaita madaktari bingwa wa upasuaji. Tuliambiwa kuwa mgonjwa alipasuliwA kwa kuchanganywa majina kwa bahati mbaya. Hilo tunaelekea tumelikubali.

    Sasa tuambiane inakuwaje huyu mgonjwa apooze kama kweli hao wapasuaji wanajua kazi yao? Inaelekea hata ujuzi wa kupasua hawana ndo maana wanampasua mtu mzima na kumharibu. Inaelekea huko India amekataliwA kwa kuwa wameshaona watatupiwa lawama na kuchafuliwA jina bure kwa mambo ya kizembe. Nadhani waliuliza huyu alipigwa na majambazi au alilipukiwana bomu likamdhuru kichwa. nina hakika kama wapo maofisa waliokwenda naye hawakuthubutu kusema kuwa alipasuliwa na daktari bingwa ili afanyiwe matibabu. nadhani walisema alipata ajali ya gari kuficha aibu.

    Nina shaka kwa wagonjwa waliolazwa hapo MOI/MUHIMBILI wakisubiri upasuaji wa miili yao. Kwanza wajiulize mtu mzima na afya yake amepasuliwa na anayeitwa daktari Bingwa anayesifiwa kuwa ni mzoefu na ameshapasua vichwa zaidi ya 200 lakini matokeo yake anatiwa ulemavu. Sasa mzima yuko hivyo hoi bin taaban kapooza, je ninyi wagonjwa mtapona?

    Lakini pia huyo aliyetuambia huyo alikuwa daktari bingwa mzoefu wa vichwa 200 naushee mbona hakusema hao waliopasuliwa sasa wako wapi? walipona au ndio akina emmanueli mgaya na emmanueli didas. Si ajabu wnegi wamekufa au kupooza na bado tunamsifu lwa kuangalia vichwa alivyokula (msamiati wa daladala) alivyopasua badala ya kuangalia matokeo ya upasuaji huo.

    Tuseme ninyi viongozi mngekuwwa na tatizo la kichwa mtakubali huyo daktari awapasue? Si ni mzoefu kwanini asiwpasue kama mnamuamini. Chukueni hatua msitudanganye tuendelee kupasuliwa wakati walio wazima wanapooza.

    Ile bahat mbaya ingeeleweka kama Emaa Didas angerudia katika hali yake lakini kwamba amepooza hiyo bahati mbaya haisameheki wala kueleweka. Ukweli ni kuwa hao MADAKTARI hawana UJUZI WALA UZOEFU. KAMA mnabisha (NINYI VIONGOZI KINA MWAKIYUSA MNAOTETEA moi NA muhimbili) basi na ninyi mkiuugua nendeni mkatibiwe muhimbili sio mkimbilie nje.

    TUNAOMBA PIA RAIS KIKWETE AKAMTEMBELEE kama alivyofanya kwa yule mwandishi wa habari kwani huyu ana matatizo makubwa zaidi na yanayogusa wagonjwa wote na walalahoi wanaotegemea muhimbili. Vingenevyo labda yule mwandishi alikimbiliwa kulinda maslahi ya vyombo vya habari visiichafue serikali. Na pia sikuona picha ya balozi wa tanzania india au waziri aliyemtembelea DidaS kule India (sijui kama Dar wwalimtembelea) kama walivyofanya kwa kubenea. Au ndio funika kombe?

    Pole Didas. Tunaamini we ni shujaa wetu wa kuleta mabadiliko muhimbili. Endelea kuwa imara na kutetea haki zako na waeleze wazi kuwa umekuwa sadaka INATOSHA. Yasitokee kwa wengine.

    ReplyDelete
  8. hata mi nilidhani ni kibaka, anatiwa kwenye karandinga!! ni Aibu. halafu subiri usikie kuna kuchangia mifuko sijui ya nini, hela kibao zinazochangiwa, haswa wabunge wanapofanya mnada baadhi ya tai, pen au saa na kuchanga hela kibao, instead of mifuko hiyo hiyo pia kuchangia vitu kama hivi!! its a shame for our country!!!

    ReplyDelete
  9. Mdharau kwao ni mtumwa. Hata huko ughaiubuni mambo haya yapo. Kosa popote wadau muuishio Ukerewe msomao magazeti nadhani mtakumbuka mwaka jana mtu kafanyiwa operesheni mguu tofauti na ule uliodhamiriwa. Na kwa wale ambao mna uwezo mkubwa wa fikra na busara badala ya kukandia bongo rudini tujenge taifa letu changa badala ya kulalamika na kusifu utumwa...... Tanzania itajengwa na wenye moyo sio walalamikaji. Changes have to start from somewhere, it is individuals that make a crowed. Everyones efforts counts. Yaani wewe Ano hapo juu unadhani Tanzania hakuna wadunifu wanaoweza kutengeneza kitanda? Watu wengine bwana....!!!!! Akili nywele naona we zako dread lakini bongo hata ukatibukata hawajakupa .....vumilia mwanagu.

    ReplyDelete
  10. ile harambee iliyotembezwa ya kuwapa wachezaji MDEBEWEDO zaidi ya milioni 300 kwa kuifunga BURKINA FASO haiwezi kufanyika tena huko BUNGENI?
    Wale waliokuwa wamevalia jezi za "TANZANIA" na kujifanya WANAIPENDA SANA nchi yao hawawezi kupatikana na kuandaa MAANDAMANO ya kutaka WABUNGE wachange FEDHA za KUSAIDIA hospitali zetu!
    NI HAYO nadhani kuna mengi yanafanyika huko kila kukicha kwa kile kinachoitwa HARAMBEE kwa ajili ya HARUSI na mambo mengine lakini haya ya HOSPITALI NA MADAWA mhhh!

    ReplyDelete
  11. Kila nikifikiria hii hali ya hospitali zetu bongo nakasirika . Sidhani kama kitu kinaweza kufanyika mpaka serikali iiamue . maana mambo haya yapo sikunyingi saana watu wanakufa kwa vitu vya kipumbavu saana. Sijui maisha ya binadamu haya dhaminiwi au vipi? au labda if we have malpractice law and be able to sue these hospitals and doctors then things will change. They say change is going to come ... my question is when I'm tired of waiting

    ReplyDelete
  12. kuna kamsemo kasema mzarau kwao au mkataa kwao ni mtumwa. kwa hali hii mimi bora niwe mtumwa bongo sirudi labda kutembea tu lkn sio kuishi wewe angalia mgonjwa amebebwa kama mlevi alifleti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...