Hi friends! 
Those who need scholarship for further studies (Masters and Phd) here is your chance to apply for ford foundation IFP scholarship. You dont need to know anyone, just fill the forms and if you have the right credentials, the scholarship is yours. 
If you feel that this is not for you please pass on to your friends who might need this scholarship. 
Kind Regards 
Mdau Naima 


 
Asante sana mdau Naima. Kwa muda mrefu sana scholaship nyingi kwa bahati mbaya zimekuwa za masomo ya sayansi ya jamii, mazingira, uchumi, sanaa, utawala, nk lakini za uhandisi sijawahi kuziona kwa hiyo mwelekeo ni wazi kuwa scholarships kama za mechanical engineering, civil engineering nk hazina maana kwa nchi zetu zinazoendelea!
ReplyDeleteAsante sana Naima kwa taarifa yako,naona hawa jamaa wamebadilisha masharti yao,mwaka jana niliona kwenye web yao kuwa hawamfadhili mtu aliyewahi kusoma nje ya nchi, lilikuwa sharti la ajabu sana, naona sasa wamebaini kuwa watu wanabidi kupimwa kwa uwezo wao na sio vigezo vya kipuuzi kama hivyo. Hili suala la uzoefu wa kazi nalo ni sharti lisilo na maana yoyote, ni vizuri watu wakasoma wakiwa na umri mdogo ili waweze kulitumikia taifa kwa muda mrefu zaidi,kuna baadhi ya nchi hapa afrika ni jambo la kawaida kuona mtu ana phd kabla ya kufikisha miaka 30, lakini sisi bado tunaamini kuwa phd lazima ziendane na uzee. waambie waondoe sharti la "uzeefu" wa kazi ili wapate vijana wenye uwezo
ReplyDeleteConstantin nashukuru kwa ujumbe wako, ila mie sina uwezo wowote juu ya masharti yao. Mie niko shule nasoma kwa scholarship ya hiyo hiyo IFP. Nilivyoona kuwa wametoa fomu kwa ajili ya watu kuomba kusoma nikaona nivyema watu wengi wapate hii habari na wajaze wajaribu bahati yao. Maana kama umeona kitu na wewe hukihitaji yanini kukibania wakati watu wengine wanaweza nufaika nacho. The more we have educated people in our counrty the better ukizingatia mabadiliko ya dunia hivi sasa.
ReplyDeleteNaima
Hey @ 9 45 ...hilo sharti lipo bado. watakaochaguliwa ni watu ambao hawajasoma nje ya nchi na wanaishi bongo kama sitakosea . Nimezipitia haraka haraka nikaona hyyo nikashangaa. Hilo sharti liliningia katika akili nikashangaa kidogo ..
ReplyDeleteWe annon Jan 18 9;28 kwanini ushangae?! Wewe kama uko nje ya nchi unahitaji scholarship ya nini? Beba mabox huko na ujisomeshe. Hii ni kwa wale ambao wako TZ na hawajawahi kutoka nje ya nchi. Nadhani scholarship zote wangefanya hivi ingekuwa safi sana. Walioko nje waache huko huko na wa ndani watoe nje! Safi sana IFP
ReplyDeleteWe Constantine na wenzako wote, ni budi mkaelewa kuwa kila mtu nayefadhaili huwa ana mashrti yake. Vinginevyo, wewe tafuta hela yako jifadhili mwenyewe. Kumwita mupuuzi mtu mwenye hela yake ni sawa sawa na kujitukana wewe usiye na hela kabisa. Sharti la kwamba mtu aliyesoma nje si kwamba wewe uliye nje ndo una akili kuliko wa ndani. kwani wewe uliendaje huko nje! Wenyewe wanataka kuwa-expose watu waweza kufahamu hali halisi ya nchi zingine. Wewe kama umesoma nje shukuru Mungu na waachie na wengine wajaribu nao kwenda huko.
ReplyDeleteUsithubutu kuyaita masharti ya wezako ya KIPUUZI. Hata aliyekupeleak huko nje alikupa mashrti ambayo wenzako waliyashindwa wewe ukaweza.
thanks naima, naomba tuwasiliane, i would like to apply for the similar course kama uliyooipata.
ReplyDeletekelvin_kafita@hotmail.com
Hii ni kwa ajili ya watu wa IFP.
ReplyDeleteMwaka uliopita niliomba nafasi katika hii programu.
Mara baada ya kujaza form nilizileta hapo ofisi kwenu kama mlivyokuwa mmeagiza.
Nilipofika ofisi nilipokelewa na mlinzi getini aliyeniambia kuwa kwanza hajui kama kuna kitu kama hicho.
Nilipojaribu kumfafanulia alikuwa mkali kupindukia akisema nisimfundishe kazi, nilibaki nimepigwa butwaa.
Baada ya sakata hilo aliniambia kuwa niache form zangu getini na yeye atazipeleka ndani ili kufuatilia kama kuna kitu kama hicho lakini alikataa kata kata kuniruhusu kwenda ndani wala kuwasiliana kwa simu na mtu aliyekuwa ndani kwa njia ya simu.
Sasa wasiwasi wangu ni kuwa inawezekana hata form zangu yule bwana hakuzipeleka.
Ushauri wangu ni kuwa IFP lazima ijiangalie kwani miongoni mwa watumishi wake hawana kauli nzuri kwa wageni.
Ni vyema IFP ikazingatia kuwa kama inataka kutoa elimu ya juu katika mambo ya haki za binadamu na mengineyo je....wenyewe ndani wanayafata hayo wanayoyahubiri?