jk akimpa pole mhariri wa mwanahalisi saeed kubenea alipomtembelea hospitali ya taifa ya muhimbili leo. kubenea na mwandishi mwandamizi ndimara tegambwage walishmbuliwa na watu wasiojulikana ambapo kubenea alimwagiwa tindikali wakati tegambwage aliyekuwa anamsevu alikatwa na mapanga. hali ya kubenea inaendelea vizuri ingawa bado anaona kwa shida
jk akimpa pole mhariri wa mwanahalisi saeed kubenea alipomtembelea hospitali ya taifa ya muhimbili leo. kubenea na mwandishi mwandamizi ndimara tegambwage walishmbuliwa na watu wasiojulikana ambapo kubenea alimwagiwa tindikali wakati tegambwage aliyekuwa anamsevu alikatwa na mapanga. hali ya kubenea inaendelea vizuri ingawa bado anaona kwa shida

Kwa kweli, inasikitisha sana sana sana. Tanzania yetu hiyooo, duh, balaa.
ReplyDeleteMbaya zaidi, sasa hivi kila mtu atatoa pole tena kwa masikitiko na kuomba uchunguzi na sijui sheria ifuate mkondo wakena maushauri kibao!. Sasa jamani, kama sisi wote ni sympathaser, then nani muhusika wa balaa hili?
Na pole wataenda kumpa hospitali. Kweli unafiki kitu kibaya sana. Wanakuja kusikitikia rohoni kwa nini jamaa bado yupo hai after all the attempts to kill him!
Jamani mi natoa ushauri kwa bwana Kubenea akipona na Waandishi wengine. Chonde chonde jamani, Better safe than sorry......, Hao unaodai/mnaotaka kuwaumbua Tanzania yetu hii hamtaweza, na sisi wananchi mnaotutetea ni vizuri lakini mh, Your own safety kwanza jamani, Uhai hauji mara mbili, utakufa kile ulichokuwa ukipigania kisipatikane, tutakusahau ati, ohoooo.
Achaneni na mentality eti unakuwa umekufa kishujaa, nani kasema? Jalini uhai wenu kwanza jamani, sisi wananchi mtuone hivi hivi, hatuchelewagi kuwageuka ati. Hebu jaribuni kuomba mchango wa matibabu toka kwa sisi uliokuwa ukitutetea, i bet hupati!
Sina nia ya kukataza watu wasifunue ukweli sijui madhambi ama vyovyote vile, lakini kwa Bongo yetu, waandishi na wengineo wenye the so called uchungu na nchi sijui Uzalendo sana I will advice you to use your head, hii ndio Bongo lAND.
Pole sana Baba, ndio ukubwa huo na majukumu.
Walau rais wetu anajali wananchi wake, maana si mara ya kwanza kumuona akienda hospitali kusalimia wagonjwa!! hongera sana rais!!!
ReplyDeletePili nimtolee uvivu huyo anayejiita "Najificha" we ndugu yangu, watu wanafanya kazi kwa uzalendo na maadili, kama si watu wachache waliojitolea maisha yao kwa ajili ya uhuru wa nchi hii, unafikiri Tz ingekuwa leo hivi??? Mfano rahisi tu, je we utamwacha mke wako akibakwa au kupigwa na majambazi na wewe kulala mbele eti kwa madai unajali afya yako!!!! Huo ni ubinafsi!!!Na km wewe ni baba wa familia AIBU kwako!!!!!
Umeniudhi sana!!!!!!!!
By Mavere
Aisee inatisha na kusikitisha,jinsi watu tulivyo roho mbaya,tuko tayari kutoa roho ya mtu kwa sababu binafsi,Mungu amsaidie hayo matibabu anayoenda kufanyiwa India yamsaidie kurudisha sight yake.Loo Mungu atawadidimiza walio tenda haya.
ReplyDeleteWaliohusika bila shaka ni kama huyu 'najificha'. Hata hivyo ajue kwamba amani na upendo tulionao sasa ni matokeo ya watu kujitoa bila woga katika kuhakikisha kwamba jamii yetu inaishi katika hali ya amani. Kuna waandishi wa habari, wanajeshi, polisi na wengine wengi ambao wanafanya kazi za hatari kwa ajili yetu, na matunda yake tunafaidi wote.
ReplyDeletevitendo kama hivi vya kujaribu kuwakatisha tamaa havitafanikiwa na waovu kama akina 'najificha' watafichuliwa tu!
Nakuhakikishia kwamba watanzania ni wakarimu sana. Machinga, mama ntilie na wengine wenye vipato duni nao wangechangia ili mashujaa hawa waweze kupata matibabu. Serikali imeamua kutumia pesa ya walipakodi kwa sababu inajua hakuna atakayelalamika katika matumizi kama haya. Shame on you 'Najificha'!!
Najificha we endelea kujificha. Na ninakuhakikishia utaishi si zaidi ya mwezi mmoja utaanza kuugua na utakufa Tarehe 9/1/2008 saa tatu na nusu asubuhi. Humwagiwi tindikali na mtu lakini ndo mwisho wako ulivyoandikwa.
ReplyDeleteMbona Mheshimiwa Rais haonyeshi masikitiko kwenye hiyo picha? Ni macho yangu tu au ni kweli anatabasamu?
ReplyDelete