Home
Unlabelled
punda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kazi kwelikweli, watu wa haki za wanyama mpo? inabidi muanze kuingilia kati, lakini unguja nafikiri hata sheria za haki za binadamu hakuna sijui kama haki za wanyama itakubaliwa!
ReplyDeleteJamani its OK punda kubba mzigo,lakini hilo zigo alilobebeshwa hapo juu ni mauaji,yaani watu wanafanya vitu bila ubinadamu kabisa,hivi wale watu wa kutete haki za wanyama wako wapo maana hapo ni ukatili wa hali ya juu
ReplyDeleteKama jamaa wa kwanza alivyosema, haki za binadamu zanzibar zinakiukwa ije kuwa hao wanyama. hili jambo sio zuri.
ReplyDeleteinafaa picha hii tuwatumie maafisa wa heathy and safety
ReplyDeletePunda na mzigo yote tisa,kumi ni hayo majina ya Unguja!
ReplyDeleteSebuleni?!!! Mengine hata kuyataja unajiuliza kwanza "may be" umekosea!!!
You know what I am talking about Michuzi!
Huyo punda 'made in Tanzania'babu,mchapakazi halisi!!!sasa kwa nini mnataka nyie kuwaleta hapo hao watetea haki za punda wakati ukweli sisi punda wabongo hakuna wakututetea???
ReplyDeleteHuyo punda anabahati bwana wake anatembea kwa mguuu? huwa hao mabwana punda nao hukaa huu ya mgongo wakati punga akiwa na mzigo,
ReplyDeletejamani imenikumbusha miaka ya 80 huko unguja huo usafiri ulikua wa kawaida sana punda kubeba bagunia ya nazi ikiwa karafuu sufi kuni n.k nilikua na babangu tunatoka shule kijua pyeeee mwenetu sasa tukiwa jiani tukakutana na punda, amebebeshwa mizigo ya kuni ndani ya lile rikwama kiweraaa
hadi mlima na mwenye punda kabebwa juu ya punda na huku anabakora anamtandika kisawasawa yule punda ili atii amri yake .Punda alionekana kuchoka na kua mbishi kwa sababu kago ilimzidi, babangu alivyokiona kile kitendi kilimugusa kwa kumhurumia punda. alishuka toka kwenye gari akamuendea jamaa akamwambia uko chini ya ulinzi twende kituoni malindi Ng'ambo station na alimpeleka, kilichoendelea huko hatukukijua kwani mzee alikua ocd wa kituo hicho, sasa pale mzee kwa kua alikua askari ndio alikua na ufahamu huo kua punda hakutendewa haki.
Sisi raia wengi hatujui sheria hizo basi hata huruma basi hatunaaaa? au kuna fikra kua punda anamgongo wa ngamia wa kubeba nyumba na watu ndani yake na madumu ya maji jangawani?
Nakubali hapo ni ukatili wa hali ya juu. ni sawa na wale tunaofuga mbwa atusaidie ulinzi ila wakati wa kula hatumuhesabu kwenye msosi mpaka anakaribia mezani kuwakodolea macho mnamfurumua "we toka" kama ungempa cha kwake angesogea hapo angelala pembeni akitikisa mkia kwa raha zake kwao hagombwi atiiiii!
kuna baadhi yetu kutokua na huruma wakati tuko ndani ya magari yetu huwa wengine hujiskia raha anapomkuta mbwa na kumgonga kwa makusudi mazima, ukipita utakuta mbwa kagongwa paka kagongwa, nakubali kuna bahati mbaya huwa wanakatiza ghafla ndipo hewezi kumkwepa ila kama umemuona unaweza kuokoa maisha yake ila uangalie na maisha yako pale unapofunga break. roho ni roho hata ya karunguyeye ukimkuta kakanyagwa utajisikia vibaya pengine amewaacha wanawe wachanga shomoni ameenda kuwaokotea chakula.
I must admit Anonimous wa 9:12AM umenigusa sana...mimi si katili kwa wanyama lakini pia hainichukulii muda sana,well kabla sijasoma comments zako...kwamba labda paka/mbwa aliyegongwa ameacha vitoto vyake shimoni kaenda kuvutafutia chakula...mpaka nimetoa machozi (maybe coz am a mother too). PLEASE PEOPLE BE KIND TO ANIMALS!
ReplyDeleteNadhani huyo punda hapo juu hakubeba hilo furushi la mistimu, bali anavuta (anaburuza, yote sawa.).
ReplyDeleteIngawa mwenye huyo punda kama anamtunza vizuri huyo punda wake kama msaidizi wa kazi ngumu, basi angalau ampe mzigo unaowiana na uwezo wa punda.
Prez wa kwanza wa Zenj alipiga marufuku kwa Punda wote kuingia katika eneo la Manispaa ya Zanzibar, Punda na magari ya Punda yalitakiwa kutoingia ndani ya maili tano za halmashauri manispaa. Hata hivyo kuanzia miaka ya tisini sheria hiyo imezidiwa nguvu, ama kutokana na gharama kubwa za vyombo vingine vya kubeba mzigo, kupungua kwa ajila rasmi au kuongezeka kwa Punda hayo.
ReplyDeletekuzaliwa mtu bongo mateso,kusaliwa mnyama pia mateso.nawaonea uruma wanyama waliozaliwa bongo.
ReplyDeletepole dada kwa kuguswa kiasi hicho, but not coz ur a mother2, is normal na huo ndio ubinaadamu unapoona au kusikia kitu cha huzuni ukajisikia huruma ujue bado hujapoteza kile kitu cha thamani ndani yako kiitwacho ubinaadamu, na kwa vile unawatoto tayari unanafasi nzuri pia kuwaelimisha juu ya kuthamini uhai wao na uhai wa wengine, nami ni mama pia, nitawaelimisha wakwangu pia.
ReplyDeletewatu mnapenda kuongea bila hata kutazama kwa umakini,huo mzigo punda hajaubeba juu ya kiuno au mgongo wake,na huyo anaesema Znz hakuna haki za kibanaadamu ana uhakika?have you been there au ni propaganda tu,mradi useme usikike?hata dini zinasema kama huna cha kusema kaa kimya au sema ukweli,kwani dhambi ya oungo huleta chuki,uadui...hujui umewapa picha gani watu wanaosoma hapa na ndani ya vichwa vyao vimejengeka nini,are you so sure???give us vivid examples sio unaandika tu.Zanzibari njema atakae aje.....TUMPELEKE MFEREJI MARINDO,MCHAMBA WIMA,MAGOMENI,KARIAKOO,KIBANDA MAITI,MAKUNDUCHI......
ReplyDeleteNa huyo punda mzigo uko kwenye mkokoteni anauvuta tu,sawa na wale makuli wanavuta mikokoteni kupeleka kwa tajiri