Kwa wadau wote wa blogu hii, tunapenda kuwapeni ofa ya bure ya wimbo wa Ras Nas, "Dar-es-Salaam".
Wimbo huu ndio unaobeba jina la albamu mpya ya Ras Nas yenye mseto wa muziki wa dansi na reggae. Ofa hii ni kampeni ya kuitambulisha albamu kwa kutumia teknologia ya kileo, yaani mtandao.
Katika albamu hii Ras Nas amewashirikisha wanamuziki mahiri toka Dar, Keppy Kiombile (mkung'utaji wa besi) na Norman Bikaka (mkali wa gitaa la solo). Jumla ya wanamuziki waliohusika ni 24 toka mataifa tisa.
Bonyeza linki hii na pata kopi yako ya wimbo (mp3):
http://www.garageband.com/artist/rasnas/songs
Pichani ni Ras Nas akiwa pamoja na injinia Jack Loveband (ambaye ndiye aliwamiksi Special AKA zamani zile!) kwenye studio ya Urban Sound, Oslo.
http://www.garageband.com/artist/rasnas/songs
Pichani ni Ras Nas akiwa pamoja na injinia Jack Loveband (ambaye ndiye aliwamiksi Special AKA zamani zile!) kwenye studio ya Urban Sound, Oslo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...