Nachukua fursa hii kuwatakia wadau wote heri ya mwaka mpya na wakati huo huo kuwatangazia kuwa kitabu kipya kuhusu simulizi za Kombe la Dunia kitakuwa mitaani katika muda mfupi ujao.
Nina furaha kuwa baada ya kazi iliyonichukua takribani mwaka mmoja hatimaye nimemaliza kazi ya kutafuta, kutafiti, kuhakiki na kuandika kitabu kuhusu Kombe la Dunia kwa lugha yetu ya Kiswahili.
Najaribu kutafuta wadhamini watakaoniwezesha kukichapa na kuweka matangazo yao na hivyo basi kiwe cha bei nafuu sana na kiwafikie Watanzania wengi zaidi wapenzi wa soka. Hii ni zawadi yangu ya Mwaka Mpya kwa Wapenzi wa Soka wa Tanzania na hata Afrika ya Mashariki na Kati kuna kozungumzwa lugha ya Kiswahili. Naangalia uwezekano wa wapenzi wa soka mlio nje ya Tanzania na mtakaokihitaji, kuweza kukinunua kitabu hicho on-line.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. SIJUI ULICHOTAFITI HUMO NDANI YA KITABU CHAKO LAKINI NAONA KAMA UMECHELEWA?
    KOMBE LA DUNIA UNALOTAFITI NI LA MWAKA GANI NDUGU YANGU MJENGWA. WAKATI HUU KILA MTU HIVI SASA ANAZUNGUMZIA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA HUKO GHANA MWEZI HUU.
    NDIYO! KILA AFUATILIAYE SOKA ANAJUA UMUHIMU WA MICHUANO NA JINSI INAVYOATHIRI LIGI KUU ZA ULAYA KWA KUKOSA WACHEZAJI WAO MUHIMU WANAORUDI KWENYE TIMU ZAO ZA AFRIKA. JARIBU KUTOA KITU KINACHOKWENDA NA WAKATI SIYO KUKURUPUKA TU NA VITABU VILIVYOPITWA NA WAKATI!

    ReplyDelete
  2. hivi "zawadi" si zinakuwa za bure,sasa unaposema unatumaini "kiwe cha bei nafuu sana" una maana gani?
    Mtu umeshasema kitakuwa ni zawadi yako ya mwaka mpya,kwa nini usikitowe bure tu.

    ReplyDelete
  3. we anoni wa kwanza kwani nchi za ulaya au amerika ya kusini wanafanyaje? je wao hawaathiri timu zao? je ligi ya ulaya haiwezi kupisha kombe la dunia? je ulaya na afrika hawawezi kupanga skejo nzuri.

    ReplyDelete
  4. Ndugu anony wa kwanza hapo juu usikurupuke tu kuponda.

    Mi nilivyomwelewa Ndugu Majjid ni kwamba anawalenga sana Wapenzi wa soka ambao hawana internet, na pia analenga Kombe la Dunia la 2010 Afrika Kusini. Kitabu bado hakijatoka ndio kwanza anatafuta wadhamini. Kwa hiyo kikitoka inaweza kuwa baadae kidogo mwaka huu. Sina uhakika kama "homa" ya kombe la dunia itakuwa imeshaanza, labda kikitoka mwanzoni wa 2009 hivi utakuwa wakati muafaka.

    Hata hivyo ni hatua nzuri na inaweza kumsaidia majjid kupata mialiko mingi kwenye vyombo vya habari kama Dokta Rikki.

    ReplyDelete
  5. SAWA MJENGWA NIMEKUELEWA NA MAONI YAKO HAPO JUU UNAYEJIFANYA ANNONY.
    LAKINI UKWELI WA MAMBO UPO PALE PALE. KOMBE LA DUNIA UNALOTANKA KUZUNGUMZI NI LA MWAKA GANI AU LILILOFANYIKA NCHI GANI?
    KUMBUKA UMESEMA KATIKA MAELEZO YAKO MAFUPI UKIDAI moja kati ya mambo unayozungumzia ni kwamba UMETAFI,KUHAKIKI na KUNADIKA!
    NADHANI UNGETAFUTA MAANA YA NENO kuhakiki, kutafiti na kuandika NDIYO UNGEJIBU HOJA YANGU KIUNGWANA.
    UMEKUWA NA TABIA YA KUTOKUBALI KUKOSOLEWA HATA KAMA UKIWA NJE YA MSTARI UNAJIONA (WENGI TU HATA MICHUZI) KUWA MPO SAWA NA HAMUKOSEI KITU!(MIUNGU WATU).
    NAWEZA KUKUPA WAZO NA UTATENGEZA HELA KIBAO NA HATA WADHAMINI WATAFURUMUKA KUTAKA KUKUSAIDIA KAMA UNGEANDIKA KITABU CHA:-
    "TAIFA STARS juu ya safari yao ya kutaka KWENDA GHANA" (SAFARI YA STARS GHANA ILIPOISHIA DAR).
    HUMO UNGECHAMBUA, KUHAKIKI NA KUTAFITI YALIYOSABABISHA NA HATA KUIFANYA TIMU HIYO ILIYOKUWA NA UHAKIKA WA ANGALAU ASILIMIA 70 YA KWENDA KWENYE FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA HUKO GHANA MWEZI HUU.
    TUJARIBU KWENDA NA WAKATI NA TUKUBALI KUKOSOLEWA KWANI SIYO KILA MTU ANAJUA ATAAMKA VIPI KESHO!
    WATUNZI WENGI HASA WA SINEMA WANAFAIDIKA SANA NA WATU WANAOITWA "FILM CRITICAL" AMBAO KAZI YAO NI KUKOSOA KILA AINA YA SINEMA HATA KAMA ITAPENDWA VIPI LAKINI WANA UTAALAM WAO WA KUTAMBUA MAKOSA AMBAYO MTU WA KAWAIDA HAWEZI KUYAONA AU KUYAGUNDUA.
    NI HAYO TU KAMA UTAPENDA UTAMEZA KWA MAJI NA KUBWIA SUKARI KIDOGO KUZUIA HII CHLOROQUINE (4X4X2).

    ReplyDelete
  6. Michuzi mbona hatukusikii na zile "Bwawa la maini" stuff.Mkiambiwa looserpoop mna gundu hamkubali.Sasa mtatowaje draw na timu kama wigan?

    ReplyDelete
  7. Hivi huy jamaa Maggid kakurupuka huko katoka na kitabu chenye uchambuzi wa kombe la dunia...timu yake imeshagusa hata raundi ya kwanza? Badala akae aanze kuchambua Challenge mwezi uliopita imeendaje au kama walivyosema wengine African Cup hapo Ghana kipi kimetufanya tusiende anaanza na kombe la dunia..!!Angalia mbeleya macho yako usiangalie mbali ya upeo wa macho yako hutaona kitu...!!Hizo habari zenyewe mpaka uzi-google halafu ndio utuletee....fanya uchambuzi wa vitu ambavyo timu yetu inashiriki hatutaki kujua Brail au Germany kajiandaaje..au walikuwaje miaka 30 iliyopita...tunataka kujua kunamipango gani inafanyika juu ya sisi kuweza kupata hata chance ya kushiriki mataifa ya afrika mwakani 2009,kushinda challenji 2008 na mengineyo sio World Cup.

    Siongei kwa kuponda bali naweka vitu Clear.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...