mtoto samuel anayesumbuliwa na ugonjwa wa kuathirika ngozi za mdomoni leo ametembelea ofisi zetu za daily news na habarileo akiwa ameongozana na baba yake mzazi immanuel nkya (wa pili shoto) na mratibu wake wa michango ya matibabu david sawe (wa pili kulia) wa ofisi ya rais menejeimenti ya utumishi wa uma ambapo mimi na mhariri wa picha wa habrileo athumani hamisi (shoto) tuliwapokea na kutathmini maendeleo ya michango ambayo wasamaria wema wametoa na kuahidi kama inavyoonesha hapo chini.
vile vile david sawe na baba wa samwel wamesema kesho watafungua akaunti maalumu kwa mtoto huyu mcheshi na kuomba wale wote wenye nia ya kusaidia waendelee na moyo huo. pia wameomba wale ambao wameanza kuchangisha wahakikishe wanawasiliana na hao waratibu ili kuweza kuwa katika njia moja ya kufanikisha kazi hiyo.
kwa mawasiliano yote ya kumchangia samwel tuma ujumbe kupitia davidsawe@estabs.go.tz
hesabu hadi sasa ni kama ifuatavyo:
All costs (USD)

1) Air tickets → Baby 720
→ Accompanying parent 860
2) Medication → 10,200
11,780


Cash available. → Nkya 1,550,000
400,000
100,000
30,000
50,000
2,130,000

KIITEC→ (Pledge ) 3,500,000
5,630,000


Kama ahadi zote zitatekelezwa, basi tuna upungufu wa Shs 6,370,000
kwa maelezo zaidi wasiliana na:

1.Imanuel Nkya(Parent) Cell - + 255 713 616126
+ 255 786 616126
2.David Sawe (President Office-PublicServise Management
Tel.022 2134615,Cell - + 255 754 782175

3.Athman Hamis ( Daily News & Habarileo) Cell - + 255 784 531188
+ 255 713 331188.

4. Muhidin Issa Michuzi (Daily News & Habarileo) Cell +255 754 271 266


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nauliza swali Serikali yetu ipo wapi hapa? Sisi wananchi unalipa kodi kwenye huyu mtoto hawezi hana haki ya kulipiwa na serikali? na kama hana ni kwanini? Ningependa tu kujua mwananchi mwenzenu.

    ReplyDelete
  2. kwa kweli inaleta matumaini,na mimi nitamjulisha kaka michuzi juhudi zangu by end of the week,hata kikiwa kidogo imenigusa sana hali ya mtoto.Nilijaribu ku contact baba mzazi lakini simu zote haziingii,hiyo ya tigo imeita mwanzoni kapokea ikakatika baadae haikukubali kabisa.lakini vile michuzi kaweka contact yake tuta deal na yeye.

    ReplyDelete
  3. Michuzi Ahsante kwa kufanya vitu kama hivi. Serekali na watu binafsi watafanikisha hili jambo kwa kutoa chochote walichonacho umoja n nguvu utengano ni dhaifu. Toeni information za bank account na wawakilishi wa kukusanya hizo pesa zinazohitajika. Wabongo walio ughaibuni wataonyesha upendo wao na wabongo walion ndani ya Bongo wataoyesha upendo wao na moyo wa kusaidia. Blog yako inasomwa na wengi. Nani akusanye pesa kwa Marekani? Au toeni infromation za benki ya nyumbani CRDB au benki yoyote.Inawezekana kutuma kwa Western Union pia. Bila shaka Wengi wasomao Blog yako wataweka mchango wao na kufanikisha matibabu ya huyu mtoto. Haya jamani harambee, tumeni mlichonacho kwa western union au kwa benki account maaalum ya mtoto huyu. bwana Michuzi waambie wazazi wafungue account maalum ya mtoto huyu. Ahsante sana ni mimi Mtanzania mwenzenu kutoka USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...