Misupu naomba uitundike hii ili wadau wanielimishe.
Ukinunua muda wa maongezi hapa Tanzania, wa kampuni yoyote ya simu utapewa vocha iliyopangwa bei.

Sasa tatizo langu ni kuwa huwa sielewi kama nikinunua vocha ya shilingi 5000 itakuwa na yuniti ngapi? Mbona huwa hatuelezwi bei ya kila yuniti? Nitajuaje kama shilingi 5000 ninayonunulia muda wa maongezi leo ina thamani sawa na niliyonunulia jana?
Mdau Chuck

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kibaya zaidi hawa watu sina uhakika sawasawa kama wanalipa kodi stahili,hasa VAT.TRA kama mnasoma hii blogu hebu tueleze kodi ya hizi vocha mnaikusanyaje maana tunasikia wakubwa wengine wana mitambo majumbani mwao ya ku print hizi vocha.TRA hivi hamuoni umuhimu wa kubandika stika zenu kwenye vocha kama vile mnavyobandika kwenye chupa za spirits na wine?ni kijiswali tu?

    ReplyDelete
  2. michuzi ya leo kali,computer leo ukitaka kutoa maoni mbona yanakuja maneno ya kijapani?kulikoni?au kwa vile balozi wa japan yuko bongo?

    ReplyDelete
  3. Hio mbona simpo wewe ziro.
    yuniti moja ni sawa na dakika moja
    na dakika moja inauzwa shilingi sitini (muda wa tigo kwa tigo)
    kupata idadi ya yuni unagawa tu hapo mwana wane

    ReplyDelete
  4. Sikiliza Chuck Norris wa bongo,

    Siku hizi hatuko katika mambo ya Yuniti bali tunazungumzia Fwedha.

    Yaan ukiongea watu wanaangalia umeongea Tsh ngapi, au dk ngapi na sio Uniti ngapi.

    Kwanza UNIT maana yake ni kipimo, hivyo hiyo muda utaoongea ndio Unit zako

    Yaan inakua ni Tsh kadhaa per UNIT ambayo ndio muda.

    Kipimo (UNIT) inaweza hata kua hatua, au kitu chochote kinachopimika,

    We hukusomaga Physics ya Geograph nini?

    ReplyDelete
  5. We vipi?

    Kwani wewe unanunua yuniti au muda wa maongezi?

    We angalia kuwa hiyo Tshs 5,000/- inakuruhusu kuongea kwa dakika ngapi ndio utajua kama ni ile ile ama imebadilika.

    ReplyDelete
  6. Bw. michuzi huyu mtu mimi sijamwelewa anachotaka kuuliza ni nini. Wewe mdau uliyepost hili swali uliposema unit ulikuwa na maana gani? Ulikuwa na maana ya ea taimu au? Kama ni air time ( yaani muda wa hewaniau kupiga) nitakuelewa.

    Basi kama ulikuwa na maana hiyo hapo sasa nakupa jibu: Ina maana kuwa kama kuongea kwa sekunde moja gharama yake ni shilingi 5, ukinunua muda wa hewani, yaani unit (kama unapotaka tuseme)wa thamani ya sh 5000 utakaa hewani kwa muda wa sekunde 1000(dk 16.666667).Hizo ndio ndio unit zenyewe.

    Hivyo basi, kama unataka, kuongea kwa muda mrefu zaidi ya hapo itakubidi uongeze unit. Na kwa kuwa mishale ya saa zote inatembea kwa speed inayolingana, kila siku muda wa kuongea unabaki uleule hata kama ukinunua vocha ya aina hiyo leo, kesho, keshokutwa au siku yoyote na wakati wowote ule. Huo ndio ukweli wenyewe.

    ReplyDelete
  7. Hapa Tanzania tunapiga simu kwa kutumia shilingi na sio yuniti, mfano kuna bei ya kila sekunde na dakika, pia inategemea unapiga wapi? kwenye mtandao wako, mwingine au nje ya nchi

    KWA MFANO UKIWA VODA MALIPO KWANZA NA UNATUMIA MALIPO YA SEKUNDE GHARAMA NI HIZI

    SERVICES Prepaid Per Second
    -VAT +VAT
    Vodacom to Vodacom 5
    Peak 4 6
    Off-peak 0.85 4.8
    Late Night 1.02
    Vodacom to National Mobile Networks 5 6
    Vodacom to National Fixed (TTCL) 5 6
    Special Kama Kawaida** rate on calls to Safaricom Kenya 5.55 6.67
    and MTN & UTL Uganda
    International Zone 1 5.83 7
    East Africa (Kenya/Uganda) &
    Vodacom Africa* numbers
    Zone 2 6.67 8
    Burundi, Canada, China, DRC, India, Malawi,
    Mozambique, Oman, Pakistan, Rwanda,
    UAE, USA, Yemen & Zambia
    Zone 3 7 8.4
    Rest of Africa, Belgium, Denmark, France,
    Germany, Ireland, Italy, Lebanon, Netherlands,
    Norway, Spain, Sweden, Switzerland & UK
    Zone 4 11.67 14
    Rest of the world
    45 54
    SMS National
    100
    SMS International 120

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...