wadau kunradhi.
awali ya yote naungama kwamba kumekuwepo na zaidi ya mdau mmoja aliyeibuka wa milioni 3 katika ile mechi ya kuwania dola 500. kwa unyenyekevu mkubwa naomba radhi ili mnipe nafasi na muda nifafanue nini kilichotokea.

ni kwamba muda ulipokaribia wa mil. 3 zaidi ya wadau 4,000 walikuwa wanaposti na kufanya kaunta ichelewe kusogea mbele haraka kwa kila hit, hivyo mgando huo ukasababisha idadi ya waliopatia wawe zaidi ya mmoja kwa mpigo.

nimempataje rehema? katika kucheki IP address yake na muda wa kuingia nikakuta yeye aliingia mapema kuliko wote na ndio nikampa ushindi. naomba ieleweka kwamba Rehema ni mama wa nyumbani, na mumewe Chesi Mpilipili ilibidi aitwe ili kufanya litakiwalo la kuleta ushuhuda kwa kupiga picha na kutundika kopi ya ukurasa wa ushindi. hapo kilichoangaliwa sio muda wa kutuma ushahidi bali saa ya IP address iliyoonekana, ambapo kwa huku Bongo ilikuwa saa tano na dakika moja. hivyo sijamaanisha kwamba wengine ni mafisadi ila kutokana na matatizo hayo ya kiufundi jopo likakubaliana lichague mtu wa kwanza kuliko wote kuingia ndio awe mshindi. kwa bahati nzuri ama mbaya mdau huyo alikuwa Rehema. Hongera zake.

ni kweli kwamba ufumbuzi ungeweza kupatikana kwa njia ya kuchezesha droo ambapo kila aliyepatia angejumuishwa, lakini pia si uwongo kwamba hatua hiyo haikuwemo kwenye masharti ya mchezo tokea awali (hapa naomba nikili udhaifu wa kutootea jambo kama hilo kwani kwa uzoefu wa alivyopatikana mdau wa mil 2 ambapo hakukuwa na hilo tatizo, mdau yeyote asingeota kutokea hayo). hivyo hatua iliyochukuliwa ya kumchagua mdau wa mil. 3 haikuwa ya ufisadi ama njama za makusudi.

wadau watukufu, asilani siwezi kufanya ufisadi mbele ya wadau kama nyie ninaowaheshimu na najua fika kwamba nikikosea naweza kuudhi wadau, jambo ambalo niko makini nalo sana. ndio maana ilinichukua masaa zaidi ya manne kufikia hatua hiyo.

samahani sana wadau watukufu kwa usumbufu mlioupata na naahidi kulifanyia kazi swala kama hilo huko mbeleni. Na kama alivyodokeza mdau mmoja awali mshindi si Rehema peke yake bali ni wadau wote wa globu hii ya jamii.

Hivi sasa nafanya juu chini kuweko na dola 500 za mara kwa mara ili wadau wengine wengi wanufaike. Kuna fununu kwamba kuna mfadhili yuko tayari kutoa hizo dola 500 angalau mara moja kwa mwezi ili kuendeleza libeneke. panapo majaaliwa nitaweza kumtangaza wiki ijayo pamoja na namna ya kuzipata hizo dola 500 kila mwezi...
naomba kuwasilisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi,

    Umejitahidi sana kuweka sawa wasiwasi wa watu. Imefahamika na mimi nimekubali ingawa jibu la saa 10:32 kwenye saa ya kompyuta ya mshindo halijakuwemo kwenye maelezo. Labda ukifafanua watu watazidi kuridhika.

    Tuko wote!

    ReplyDelete
  2. michuzi

    3000002

    ilipatikana around saa 11:23am tz

    2999997

    ilikuwa around just after 11:20am tz

    sasa wewe wasema eti ilikuwa 11:01am tz

    huu ni uongo

    mie sikuamini

    status ya waingiamo humu ipo leo asubuhi more than mtu mmoja walikuwa wanaingia dakika hiyo hiyo

    sema uliamua kuchukua mtanzania alieko bongo

    ReplyDelete
  3. Masaa ya computer ya mshindi yanadanganya kabisa.

    nimepata namba 3000000 yangu inaonyesha saa 4:12:33AM kwa masaa ya marekani ilikuwa ni saa 10 asubuhi,wakati napiga picha hiyo
    lakini ushindi niliupata kwenye saa tisa usiku.

    Huyo dada computer yake inaonyesha saa 4:32 PM haimainishi chochote

    hata kwa kiswahili kwa kiswahili ni saa kumi jioni?????si kweli
    kwa kiingereza ni saa kumi jioni asubuhu????? haiji kabisa Bwana Michuzi.

    Nilazima ufanye uchunguzi kabla ya kutoa hiyo pesa,make itakufishika mahakamani

    mimi ndio Mshindi,na ushahidi ninao
    Nitawasiliana na Extreme Tracking
    nimekwisha anza uchunguzi wangu

    Hii blog inatembelewa na watu zaidi ya 8000 kwa siku
    kwa hiyo kuwa makini kwa kuwa makini.

    huu sio uwanja wa kutaniana
    Ahsente.

    ReplyDelete
  4. Sawa,

    Lakini unapaswa uwe muwazi ndugu MIchuzi. Unaposema Rehema kaingia mapema kuliko wengine, yeye kaingia saa ngapi? Na uko wapi ushahidi unaoonesha kuwa yeye ndio kaingia mapema. Na hao washindi wengine waliingia saa ngapi?Unajua unaweza kuomba radhi sana lakini as long as huweki mambo bayana, hatutakuelewa.
    Pili kwa kuwa hii ni blogu ya jamii, mbona umejichukulia madaraka ya kuamua nani mshindi harakaharaka. Yaani ni sawa na Kenya. Walivyofanya haraka kumtangaza na kumwapisha Kibaki.
    Unajua katika maelezo ya shindano hukusema kabisa kuwa kama akipatikana mshindi zaidi ya mmoja utafanya nini. Nadhani katika utaratibu wa kutoa haki, ilikuwa useme kabla ya kutangaza kuwa "jamani mpaka sasa kinyume na nilivotarajia, amepatikana mshindi zaidi ya mmoja, sasa wadau naomba ushauri kifanyike nini ili ionekane kuwa umetenda haki.Lakini sasa wewe ulikurupuka tu kusema kuwa mshindi keshapatikana na baadae ukenda kumtangaza chapchap.Sasa unafikiri sisi tutafikiria nini? Hapa Michuzi hukutenda haki na hukututendea haki wadau wa blog yako ambayo unataka iwe ya jamii.Haki inatakiwa itendwe na ionekane kuwa imetendwa.
    Bado una kesi ya kutueleza kilichotokea Michu.Hapa kuna mchezo umechezwa.

    ReplyDelete
  5. Hizi ni fix tu zinazokubalika bwana Michuzi. Hatuna jinsi. Hivyo ndivyo ilivyo kwa rangi yake. Huwezi chubua.

    ReplyDelete
  6. Mambo ya kutuambia ni mke wa mtu hatuelewi. Kwani wewe si mme wa mtu!!? Kwa hiyio hakuna hatari yoyote hapo.

    Ila tu, UMAFIA uliofanya kwenye hii rafle, kwa kweli ni wa hali ya juu kabisa!

    Pamoja na hayo, tunakupa tano za nguvu sana. Unastahili kuwa ulivyo. Sisi ni member wa hii blog kwa kuwa mwendeshaji ni bonge la analyser pia FISADI wa nguvu. Mwanaume huwezi kuwa legelege au easy tu na ukaitwa mwanamme. Lazima watu wakulaumu sana na wachache wakusifie. Ndo maana na mwanaume.

    VIVA blog yetu!

    ReplyDelete
  7. wewe michuzi kama kweli unakubali maoni ya wadau basi yaweke na haya: Wewe bwana ni mnafiki na mashindano yako ni batili kwanini kila mara kunakuwa na malalamiko ya watu kutoridhika na nasibu bahati zako?kulikoni? wewe ukishaona wadau wanakuhama na kuhamia Blog zingine basi unakuja na kamtindo kako ka mdau wa milini sijui nagapi....ili kuwavutia kwako,acha hizo ni bora ukome kuleta mashindano yasiyokuwa na kichwa wala miguu,unatufanya sisi kama watoto wadogo kulikoni?.Itafika wakati tuta-boycot kuingia katika Blog yako ohhh shauri yako.Na nyie wenzangu na mimi muache tabia ya kupenda dola za burebure tafuteni zenu kwa jasho lenu sio kukaa nakungoja za michuzi...yeye ana ndugu jamaa marafiki na vimada kibao wa kuwapa hizo dola!si mmeona wenyewe tayali kaisha zigawa.NYAMAZENI FUNGENI VINYWA VYENU.

    ReplyDelete
  8. Binafsi nimekuelewa vema "michu"! Na nina imani wale wepesi wa kuelewa kama mimi pia watakuelewa. Naamini kwamba kwa kadri unavyoandaa shindano hili na ndio unavyopata uzoefu na kurekebisha mapungufu, hongera mkuu kwa hilo; aidha ni imani yangu kwamba shindano hili nitakuwa la kiwango cha juu zaidi na zawadi nono zaidi katika siku za mbele panapo wajaliwa. However, jiandae kaka kwa madongo toka kwa waosha vinywa !!! just take it easy kwani watachoka na hatimaye watalala !! usijali wenye akili tumekuelewa.

    ReplyDelete
  9. Michu pole na hili sakata ambalo sasa limefananishwa na la tume ya uchaguzi wa Kenya.

    Unajua unapotangaza shindano na zawadi ya fedha kiasi hicho lazima nawe uwe tayari kuandaa mazingira muafaka juu ya taratibu za shindano na hata namna mshindi atakavyopatikana bila kusababisha utata, vinginevyo ndio matusi yanaanza kwa wasio na simile.

    Binafsi sina haja ya kuwa na wasiwasi juu ya uamuzi wako maana sijawahi kukufahamu kuwa uanaweza kupika matokeo, isipokuwa kama kuna watu walioshiriki shindano hili ambao wana vigezo vya kulalamika wao wataendelea kusema tu.

    Nakushauri kuwa kwa siku zijazo:-

    1. Kwanza shauriana na watu (wataalamu katika fani husika) na hata waendesha bahati nasibu wazoefu ili kuweka mazingira ambayo hayataleta utata. Mfano, sasa counter iliposimama je hapo shindano lilikuwa katika hali gani, Linaendelea au Limesitishwa n.k. Tena afadhali kama nilivyokuwa nimekushauri mwanzoni kuwa mtu anapotuma comments katika shindano kama hili zijiposti sekunde hiyo hiyo maana wote wangekuwa wanaona. Unapotaka comments zikuijie kwanza halafu ndipo wewe unaziruhusu, kweli mfumo huo hautofautiani na yake mazingira ya Tume zetu za uchaguzi ambapo mashaka ya kupika matokeo lazima yawepo kwa washiriki.


    2. Pamoja na kwamba hii ni blogu yako yako binafsi unapohusisha jamii katika kuwashindanisha na kuwaahidi zawadi uliyofadhiliwa na mtu au asasi fulani basi ulitakiwa si tu kuunda kamati ya waamuzi bali kuitangaza hapa waziwazi ijulikane na ikiwezekana wasifu wa watu hao. Hili nalo husaidia kutokufikiria vilivyo sivyo!

    HAKUNA SHINDANO DOGO HUSUSANI UNAPOHUSISHA NA ZAWADI YA FEDHA.

    Mshindi hongera, Washindwa poleni na mjaribu kipindi kingine mazingira yakirekebishwa

    NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO.

    ReplyDelete
  10. Ha chesi mpilipili huyo tajiri namjua sanaaana...wacha kutudanganya michuzi ...this is very low..

    hata hao walioshinda wengine ni mama wa nyumbani pia....be fair....chesi mpilipili na mjua

    ReplyDelete
  11. Michuzi,
    Hapa umeishatufanyia zengwe. Counter haiwezi kutoa namba sawa kwa watu ambao watakuwa wame-access karibu wakati mmoja. Kila mtu au kompyuta inapofungua wavuti counter ina increment haijali muda inajali zaidi hit.
    Sasa kama kweli una ushahidi huo kwamba huyo Da Mpilipili ndio ameshinda, ebu tupatia hizo "IP address" na details zote weka wazi hapa tuzifanyie tathmini.
    Hayo maelezo yako uliyoweka hapa kumchagua mshindi hayajitoshelezi.
    Kurahisisha ungekiri tu kwamba kuna mshindi ulikuwa umemwandaa.

    ReplyDelete
  12. Michuzi. Nadhani wakati unaweka sheria za kugombania dola 500 ni kwamba wote tulijua kuwa counter haiwezi toa namba moja kwa zaidi ya computer 1. Hivyo baada ya hilo kutokea ilibidi kwanza uwachukue wale wote wanaodai walikuwa wa mil. 3. Halafu uchambue ili uwatoe wale waliotoka "sayari nyinginezo". Baada ya hapo utuulize wadau utaratibu gani ufuate. Sasa ile wewe kujichukulia uamuzi wa sijui kuangalia IP ya aliyeingia mapema. Pengine ni uamuzi uliofanya kwa makusudi yako, na pengine kumpatia mdau toka bongo ili ku-balance mambo kwa kuwa yule wa mil 2, alitoka US nadhani. Sasa muda wa computer ya huyo dada "uliyemchagua" unaonyesha ilikuwa 4.32, inawezekana IP address ilimtambua huyo ni wa mapema kutokana na muda wake kukosewa. Tunaomba utupe ufafanuzi hapa, maana hata ingekuwa saa inasoma kiswahili, mshindi alipatikana baada ya saa 5 asubuhi. Hivyo usifute uwezekano kwamba huyo dada pengine ni mmoja wa wanaotoka "sayari nyingine", ambapo mtu wa mil 3, aliingia mapema kabla ya mtu wa "sayari" ya dunia. Anyway, ulisema uamuzi wa kwako ni wa mwisho tunakubali na tunampa hongera mshindi, lakini next time inabidi uwe muwazi ili kuondoa dhana kuwa kuna ufisadi ndani yake.

    "Mimi ni mmoja wa watu wa 3000000 kwa blog yako"

    ReplyDelete
  13. Tunaombeni picha jamani...haya maneno yanachosha kuyasoma!! hii ni glob ya picha!!! mwenye nayo ni mpichapiga!!

    ReplyDelete
  14. Michuzi una kesi ya kujibu.

    Rehema unayedai ni mkazi wa Magomeni saa ya computer yake inasomeka 4:32 PM. Mimi ni mkazi wa Dar es Salaam na muda niliopata hit ya 3,000,000 ilikuwa saa 11:22 AM

    Hapo kuna walakini mkubwa sana. Labda utuoneshe huyo rehema, tena na kitambulisho chake, ikiwezekana mpaka nyumbani kwake ndio nitaamini kweli Rehema ana-exist.

    Na atuambie ilikuwaje akapata hit ya 3,000,000 saa kumi jioni?

    //Fred

    ReplyDelete
  15. INSIDE GAME!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. Kaka Michuzi nina amini kuwa umejieleza vizuri kabisa na asiyetaka kukuelewa atajijuu. Tena its your 500 dollars and you can give it to whom ever you feel ata kama angekuwa mdau wa 3,000,001. It doesn't matter. I believe you are a honest man and that you have made a just choice. Walioshindwa wanyamaze.

    ReplyDelete
  17. Hello Mr Michuzi, mimi binafsi siku shiriki, nimesoma analysis zako ulizota. I want to remind you this, most of us tunaingia blog yako sababu you always keep simple and less politics. However in recent time you been bias on several things, ni ushauri wangu kwamba it is better ukawa same Michuzi wa 2006 to mid 2007. Just keep it simple and less political. Ni ushauri tuu

    ReplyDelete
  18. Ndugu Michuzi,

    Maelezo yako Michuzi, kwa kweli hayajaeleweka, kama wadau wengine wanavyojieleza, kwamba, hit ya mdau wa milioni tatu ilikua ni 11:21am-Bongo time, na mimi binafsi nimepata hit ya mdau wa milioni tatu saa 8:21am, kama vielelezo vya picha na video nilivyokutumia.

    Sasa tukija kwenye maswala ya kwamba dada Rehema, kaingia mapema at 11:01am, katika address blog yako, mimi nimeingia hiyo blog saa 6:30am kwa saa za Ireland ni sawa na 9:30am kwa saa za BONGO.

    Nimefurahi umejaribu somehow kujieleza, lakini maelezo yako hayalingani na FACTS zilizokuwepo na zinazojionyesha.

    Mimi nakubaliana na wadau wengi ya kwamba wengi wamepatikana kuwa wadau wa milioni tatu, yaani zaidi ya mmoja. lakini judgement yako na hao majaji unaosema wapo wemekwamba mramba juu ya decision yao, hususan hasa katika maswala ya timings, kama comment na ushahidi wa wengi unavyojieleza.

    Hata hivyo hii ndio comment yangu ya mwisho juu ya hilo, nimekutumia video, picha ya kupiga na picha ya paint, ambayo kwa maelezo yako na vielelezo vyako umesema ndio njia pekee, lakini kutokana na hisia zetu mambo kama haya yatatokea, ndio tumeambatanisha na kujitahidi kuchukua hatua hiyo ya kuchukua picha-snap shot.

    Hata hivyo, Kwa sababu mshindi ameshatajwa naye ni Rehema, I will settle with that.

    Nawakilisha.

    Shukran

    ReplyDelete
  19. Salaam,duh naona kazi ipo.Michuzi hapa unaweza jikuta unafikishwa mikononi mwa Pilato.

    Kwanza suala la saa sio la kutilia maanani sana,mfano kama mimi nilibahatika kuwa wa Mil 3 lakini saa yangu niliset tofauti kabisa na muda wa hapa nilipo.

    Ukiwa unafanya installation ya window unaweza set zone ya saa unayotaka mwenyewe.Unaweza kuwa upo Magomeni ukaset zone ya Alaska an majira yako yakasoma upo Janeau-Alaska.Mfano mimi nilipopata namba ile hapa ilikuwa saa 1:30pm hivi.Lakini PC yangu nilipochukua picha ile inaonyesha saa 10:53pm.Ni muda sawa nilipofungua blog hii jana na leo(pungufu dakika 4 kwa leo).

    Kwa hiyo suala la muda sidhani kama lina uzito sana.

    IP address,hili naweza kukubaliana na bwana Michuzi na liko ndani ya uwezo wake kama atapenda anaweza kuwaeleza.

    Hongera dada Rehema.

    ReplyDelete
  20. MICHUZI NA KIBAKI SAWASAWA!

    ReplyDelete
  21. Michuzi pamoja na hotuba kubwa ya kueleza mambo ... cha msingi ni kwamba "umechemsha". Umebadili sheria baada ya mchezo ili ushindi huo wa mezani ukubalike. Kama hiyo counter kweli iliganda basi ulitakiwa ugawe hiyo 500 dollars kwa wote waliyopata.

    ReplyDelete
  22. Ok nimegundua kinachowauma watu hapa sio fedha zaidi bali hisia ya kuwepo uongo na dhuluma katika shindano ambalo watu walishiriki kwa moyo wa upendo juu ya blogu yako.
    MICHU angalia; muda wa post ya huyo Mama uliyempa ushindi na pia kusema kuwa kulikuwa na watu zaidi ya mmoja waliokuwa wa 30000 ni utata tosha usiopingika.

    Nakushauri (kwa vile kamwe huwezi fananishwa na Kibaki kwa jinsi tunavyokufahamu) kuwa kama huyo Mama hajapokea hizo fedha jasti nalifai hili shindano kwa sababu zilizo wazi kabisa hapa na hata yeye ataelewa na kisha kwa hizo fedha sasa utangaze atakayebashiri mshindi wa Afrikan kapu ovu neshens. Yaani ataje timu, pointi zake, magoli ya kufunga na kufungwa NA UWEKE MSTARI MFU MTU KUTUMA mfano Post za watu wote ziwe tayari ndani ya wiki mbili kutoka sasa (ili kuleta ugumu wa kutabiri)kisha watu tusubiri tuone. Ikitokea mshindi zaidi ya mmoja (kitu ambacho uwezekano wake ni mdogo) basi majina yao yawekwe kwenye kapu na ifanyike droo iliyoenda shule chini ya timu ya kampuni fulani inayoaminika ambayo inabidi tuijue kuanzia sasa. Kama hakutakuwa na aliyepatia in all counts basi tunachukua mshindi mwenye counts nyingi kwa mfuatano wa Timu, point, magoli ya kufunga na kisha kufungwa.

    Vinginevyo sasa hii kuwasha matairi katikakati mwa barabara ya tovuti sijui itaisha lini au nayo itabidi sasa tusumbilie Koffi Annan aje au pengine watu wanaweza anza sema kama Odinga tususie bidhaa inayohusiana na ..... kazi kweli kweli hapa!

    Bro. Issa naomba uchukulie maanani ushauri huu maana you can't afford to loose your credibility on such an event!

    ReplyDelete
  23. MICHUZI DAWA YA KUONDOA UTATA NILIKUFUNDISHA SIKU NYINGI TU, WATAALAM WA KOMPYUTA WANAIJUA, NAYO NI ALARM KWA MDAU WA 3M. KAMA HESABU NI SAHIHI ANATAKIWA AWE MMOJA TU ALARM INALIA KWA KELELE KWENYE PC YAKE NA NYIE YA KWENU FULLSTOP.

    NILIVYOSHAURI HAYO NILIJUA TU SIYE WA KABILA LA WALALAMA HATUTAKUBALI MATOKEO. PANAPO USHINDANI LAZIMA APATIKANE MSHINDI MMOJA HAIWEZEKANI WOTE TUWE WASHINDI. NASHUKURU MUNGU HATA HIYO SIKU SIKUINGIA MTANDAONI KWANI SIKUTAKA KUSHINDA KWA KUOGOPA MAKOMBORA NA KUDHALILISHWA SIMPLY TU UMESHINDA!

    YAANI HAWA WALALAMA HATA UFANYEJE NDUGU YANGU HUWEZI WARIDHISHA, SASA KILA MTU ANADAI YEYE NI WA 3M HII WEB YAKO VIPI INAWEZAJE KUWA NA WATU WA 3M ZAIDI YA MMOJA?

    WEWE USIYUMBISHWE NA HAYO MANENO YAO MSHINDI KAPATIKANA BASI. HII NI BAHATI NASIBU AU SADAKALAWE MWENYE KUPATA APATE MWENYE KUKOSA AKOSE WASIKUPE UGONJWA WA MOYO BURE.

    HALAFU WA 2M WABONGO WALIPIGA KELELE WEE KWA NINI KAPATIKANA KUTOKA NJE KWA NINI ISIWE BONGO SASA KAPATIKANA KUTOKA BONGO SASA IMEKUWA KAPATIKANAJE? KAPATIKANA SAA NGAPI? MBONA MIE TAYARI NILIKUWA WA 3M? SIJUI SAFARI HII HUYU ANGETOKA NJE KAMA WABEBA MABOX WANGEPONA KWA MATUSI YA KUTOKA BONGO.

    MPIRA UMEKWISHA, NA MSHINDI KESHAPATIKANA MPE KOMBE LAKE TUANGALIE USTAARABU MWINGINE. KILA SIKU KURUDI NYUMA BADALA YA KWENDA MBELE NDIO MAANA HATUENDELEI!!!!

    ReplyDelete
  24. Wabongo njaa zitawaua!!!

    Hi guyz! Still am confused the way of presenting my critical analysis in view of the raffle and responses from range of bloggers.

    Hivi michango yote hii ni kuboresha ama ni dalili za usongo wa njaa kutoka kila upande wa dunia.Labda basi iteuliwe tume ya uchunguzi wa suala hili halafu iwe inalipwa kiasi cha dola 10 kila inapokutana,tume ijumuishe watu wa nyanja mbalimbali.Bloggers,wanasheria, waandishi na mlalahoi,ha ha ha ha ha!!!!


    All in all, ever since the announcement of the second winner, 2,000,000 blogger, much of current debate on fairness and transparency is firmly centred on the procedures to followed to get the winner!!

    But what lesson do we learn over here!! This pace of technological change has stimulated the change of human behaviours towards their rights, currently , societies are in high level of understanding the right of being considered in the benefits.

    Lakini yote tisa,njaa inachangia kiasi kikubwa kuleta,munkari,usongo na mabishano ya kila kona.Ushauri wangu ni kwamba hii ni blog yenye muelekeo wa kutambua mchanho wa jamii ya wanablog therefore is branded as Blog ya jamii na Umma, kama ndivyo basi haya masuala ya raffle yatengenezedwe sera kamili na operation manual hivyo ieleweke vigezo,na kama mtu akisiporidhika ni hatua zipi za kufuata.

    La sivyo, isiwepo kabisa raffle, kwani hakuna anayelaziomishwa kuingia humu ila ni kutokana na wingi wa habari na zinazocover at least every angle.

    Acheni Njaa, acheni majungu, muwe na hekima na Busara.

    Am tired
    Dr. Confusion.

    ReplyDelete
  25. Michuzi,

    To most of the people na wapenzi of this blogs, it has never been about money but about INTEGRITY, your own integrity.

    Which it seems, you single handedly place it in a BIN, it will never been the same after this event. Your decision and your luck of judgment was blurred or somehow never been anticipated given the circumstances. Yes there was a technical hitch with counters, full of bugs, which it has never been perfect by getting more than winner, however your rushing judgment of declaring the winner followed that, which makes things matters worse. You would have waited and respond to all potential winners by addressing the issue to your blog. You have waited for several weeks to address the winner of the football match, this could have waited a few more weeks to do the same, but you didn't, and thats the issue of INTEGRITY and never being about money.

    Try to think hard, what is your next step, you need to restore your integrity.

    My advice to you, find a good cause or charity and award the money onto that, particularly of Samuel Nkya, will satisfy everyone, and issue a public apology to all wadau and personally to Rehema, the incumbent winner, as I might call it.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  26. Watanzania wenzetu, Salamu. Tumesikitishwa na kusononeshwa mno na kauli za baadhi ya Wadau wa Blog yetu hii kuhusiana na ushindi wa mama, pamoja na mmiliki wa Blog kujitahidi kuutolea maelezo.

    Labda tu tuseme hivi, si kila mtu ni mtaalamu wa Computer na kosa kubwa la mama, kama ni kosa kweli, ni hilo la kujua kuingia tu kwenye mtandao wetu huu na kuangalia picha, basi. Na ahukumiwe kwa hilo.

    Na ndio maana jana alipoingia kwenye mtandao na kukuta counter inasoma tarakimu Milioni tatu, ikabidi anipigie simu huko nilikokuwa kwenye mibangaizo.
    Nilimpigia simu Michuzi kumfahamisha hili na nikarudi haraka nyumbani na kuupiga picha ukurasa kwa kamera ya simu.

    Mama aliupata ukurasa saa 5 DK 01 za asubuhi na kuutunza chini ya screen na mimi nilipofika na kuupiga Picha na Video nilizomtumia michuzi ulikuwa unasomeka saa 11 DK 25.

    Baada ya hapo, niliurudisha tena ukurasa chini ya screen na kuendelea na mihangaiko yangu hadi alasiri Michuzi aliponipigia tena na kuomba niutume tena ukurasa kwa vile picha nilizomtumia kwa kutumia kamera ya simu yangu zilikuwa hafifu (sikutaka kumuambia
    kuwa pengine hii ilitokana na kuzipiga nikiwa nimehemka!) na ndipo nikafika nyumbani na kuiibua tena ule ukurasa na kisha kuutuma kwa njia iliyoelezwa kwenye Blog.

    kwa maana hiyo, saa iliyosomeka ilikuwa ni ile iliyokuwa pale chini wakati huo ambayo wadau wengi wameonyesha kuihoji lakini ukurasa ulikuwa ule wa asubuhi niliokuwa nimemtumia Michuzi.

    Kwa hakika, ni hayo tu na tunakosa amani kabisa wadau wanapodai maelezo ya ziada ushindi wetu, maana hatuna zaidi ya hayo.

    Sana sana tunasononeshwa mno kauli za wadau dhidi YETU na MMILIKI WA BLOG ambapo yupo mdau aliyedhibitisha kabisa kuwa HATUPO magomeni kwa kuangalia saa tu!

    Tumeshitushwa mno pia na mdau aliyeandika kuwa mama sio mama wa nyumbani kwa vile ni mama gani wa magomeni atakuwa na flat screen!! Hivi huku ndiko watanzania
    tulikojifikisha kwa kuamini kuwa baadhi ya vitu ni maalumu kwa maeneo fulani tu?

    Naomba nimhakikishie mdau mwenzangu
    kwamba tupo Magomeni Mapipa na kwamba kuwa na Flat Screen ni mipango na maamuzi ya mtu tu. mwingine anaamua kuanza na Gari na mwingine anaamua kuanza na TiiVii na mwingine Flat Screen.

    Mwingine pia ametushangaza kwa kusema kuwa mimi ni rafiki wa Michuzi. Kwa hiyo? Idadi kubwa ya walioshiriki shindano hili ni marafiki wa michuzi na kwa vile kulikuwa hakuna katazo la hili, ina maana hata mdogo wake Michuzi ana haki ya kushiriki na kupewa zawadi yake iwapo angeshinda.

    Naomba Wadau wenzetu muwe na IMANI na AMANI tu na ushindi wa Mama. kwamba kulikuwa na matatizo ya Counter na Washindi wengi, hilo Michuzi aneishalitolea maelezo.

    ReplyDelete
  27. Michuzi is Balali in another form.

    Na nyie washindi feki ushauri wa bure. Vile hiyo hela hamkuitegemea sana, basi walau toeni kamchango hata ka $ 100, kwa mtoto Nkya, Mungu atawabariki. hayo maelezo ohhh, flat screen mnatafuta ujiko tu, maelezo yanayotakiwa ni ushindi wenu una walakini, sio kutukumbusha mna flat screen!

    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  28. Pole bwana Chesi na Bi Rehema, poleni sana, hata ningekuwa mie ningefadhaishwa na kitendo hicho kilichotokea na kinachoendelea. Inaonyesha ni jinsi gani siku hizi binadamu utu na imani zilivyotutoka kwa ajili tu ya pesa.

    Basi watu wamesema maneno mengi mengine ya kashfa bila kujali kuwa nanyi pia mna feelings hilo lote ni kwa ajili ya huyu ibilisi aliyelaaniwa PESA! Hakuna lolote hapo hao wanaojidai integrity sijui nini hakuna kitu kama hicho ni PESA tu ndiyo inayumbisha ubongo na akili zetu. Hali hii shindano lenyewe ni la ka dola 500 je ingekuwa ni dola 100,000? Tumeshuhudia humu watu wakileta hiyo namba 3m hata kabla ya muda. Yote ni nini jamani? Hii kitu was supposed to be fun and not otherwise. Kama ameshinda Rehema basi ni bahati yake subiri next time. Kwani ilikuwa lazima tu ushinde wewe unayedai kuwa ulishinda na Rehema kapendelewa? Ulishapanga matokeo au? No jamani hebu tuacheni kabisa hizi tabia za ajabu kabisa ambazo zinaendelea kunishangaza. Sasa bwana Michuzi ili kuondoa ulalamishi acha hayo mambo ya mashindano ya kupeana PESA maana ni ibilisi mkubwa huyo PESA.

    Tafuta kitu kingine kama mtu atakayeshinda basi zawadi yake akapate mlo na watoto Yatima kwa pesa yake uone kama watu watashededea nimeshinda nimeshinda! Au tafuta kitu kingine chochote lakini si pesa. Loh!

    NA HUO UCHAGUZI WA 2010 WATU WAJIANDAE KUTOLEWA NGEU DALILI ZISHAANZA KUONEKANA!

    ReplyDelete
  29. Bwana Chesi hao wanaosema hamuwezi kuwa na flat screen Magomeni ni washamba na wameanza kuziona hizo flat screen recently naona. Hivi unawezaji kumjudge mtu kwa vitu kweli kama flat screen, sijui TV sijui Frigde, feni, khee! Makubwa basi. Kwa taarifa yenu sasa hivi computers ziko bwereree wengine utakuta ndani ya familia watoto wana PC yao ambayo desktop, mama ana laptop yake na baba naye ana laptop yake. Tanzania gani mnayoishangaa nyie? Tanzania hii ya watoto wa darasa la kwanza kuwa na simu za mkononi? Tanzania hii hii ambayo watu wana computer mpaka vijijini na wanafanya business za photocopy na typing? Tanzania ipi inayowashangaza kwa mtu wa Magomeni kuwa na Flat Screen. Au kwa vile nyie tangu mlivyotoroka makwenu hamjarudi mpaka leo mnafikiri ndiyo zile enzi za watu kushangaa Fridge mtaa mzima wanakuja kuomba maji baridi nyumbani kwenu. Tanzania hii watu wana mafridge double door na ma home theatre huko Magomeni na Kinondoni sio Tanzania ile mliyoiacha ambako mafriji yalikuwa kwa wajomba zenu Masaki na Osterbay. Kwanza mkirudi sijui kama mtaweza kupanga nyumba Magomeni kwa sababu ni downtown na kodi yake ni kubwa. Shikeni adabu zenu na muache kutukana watu! Mie nakaa Magomeni hiyo flat screen ni kwa ajili ya watoto wangu kufanyia mazoezi ya masomo yao ya computer huko shuleni na kucheza games!

    ReplyDelete
  30. MICHUZI HATA UELEWEKI KABISA,SISI TUNATAKA KUSOMA TU NEWS ZAKO LAKINI NASHANGAA UMEKALIA $500 KAMA BIG ISSUE,SISI WENGINE ATUJALI KABISA WALA KUJUA INACHEZWA LINI,LABDA WALALA HOI,NAONA KAMA UNATUUMIZA KICHWA NA KILA SIKU DORLA 500 DORLA 500.KAMA UNALISHIA NDOGONDOGO WATU WAONE LABDA HUKO POA SANA BONGO UJINGA WAKO KWANI HUNA UWEZO WOWOTE WA KIPESA TUNAKUJUA KAMA MPIGA PICHA TU WA MITAANI.

    ReplyDelete
  31. WEE MNYONGE MNYONGENI, ACHA HIZO!
    NYI NDIO MMEKOPA HELA KWA WATU MKITEGEMEA KUZILIPA KWA ZAWADI YA MICHU!
    JAMAA KESHAPATA, BASI. WATAJIJUA YE
    NAMUNGU WAKE, HAYO MAMBO YA KUMPANGIA PA KUIPELEKA HELA YAKE NI YA NINI? WE UMEISHATOA SHIING' NGAPI KAMA MCHANGO KWA MTOTO NKYA???
    HAYO MAELEZO YA FLATSKRINI AMEYATOA
    BAADA YA KUONA MTANZANIA MWENZAKE, KAMA WEWE, ANAONA MAGOMENI HAKUWEZI
    KUWA NA FLATSKRINI..NA SIO KUTAFUTA
    UJIKO.
    KAFANYENI KAZI, ACHENI KUPIGIA KELELE DOLA MIA 5 AMBAYO IMEISHAKWNDA NA MAJI. MNANIUZI SANA!! NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  32. MDAU WA JAN 26 01:20 MI NAKUUNGA MKONO INGAWA LUGHA ULIYOTUMIA NI KALI NA INAMDHALILISHA MICHU. LAKINI NI KWELI SASA TUNACHOKA NA KELEL ZA DOLA MIA TANOOO, DOLA MIA TANOO!! SIS TUWEKEE PICHA BWANA TUANZE KUCHANGIA NA TUACHANE NA MJADALA WA HELA AMBAYO IMEISHAPATA MWENEYWE IWE KWA HARAMU AMA KWA HALALI!!
    PIA NAUNGA MKONO USHAURI WA MDAU ALIETAKA TUACHANE NA MAMBO YA ZAWADI YA HELA KESHI MAANA WATU WATAKUJA KUTOANA ROHO.
    KAMA ALIVYOSEMA MDAU, ZAWADI IWE KWENDA KULA LUNCHI NA YATIMA KWA GHARAMA ZAKO,, TUONE KAMA WATU WATAMLALAMIKIA MSHINDI!!! MNANIUZI.

    ReplyDelete
  33. wabongo bwana! kweli njaa inatusumbua. laiti haya mahasira ya kuhoji ushindi wa mtu wa dola 500 tu wangeyaelekeza kwenye kuhoji
    wizi wa dola BILIONI 133 huko BOT, nchi ingekuwa mbali. lakini waapii.
    wanamuandama michuzi na mshindi wake wa dola 500...#@&(*&%#@# kabisa nyie!!!

    ReplyDelete
  34. ...'Michuzi is Balali in another form'!
    Mdau, umenifanya nitabasamu peke yangu na screen. Punguza hasira na maisha,khakhaa! Michuzi amefanya alichoona ni haki.period. usimpangie mtu nini cha kufanya na zawadi yake. usilete matatizo yako ya nyumbani kwenye Blog yetu, bwana!

    ReplyDelete
  35. PEOPLE!! GET REAL, PLEEAASEEE!!
    Yaani wewe hasira zako za kukosa Dola mia 500 ndio unataka umpangie matumizi aliyezipata!! wewe huna tofauti na yule mwingine aliyesema kuwa alimuandikia meseji michuzi kwamba alikuwa amepanga kutoa dola 100 kwa mtoto Nkya iwapo angepewa yeye ushindi! au ndio wewe??Jamani mwe, KHA!
    Hivi alifikiri akisema hivyo ndio Michuzi atampa ushindi?? REALLY?
    KOMENI kumtumia mtoto Nkya kwenye njaa zenu! Serikali yenyewe imebung'aa kumsaidia na badala yake inakimbiza
    waandishi waliomwagiwa MAJI machoni India! (hivi mnajua Tindikali nyie?) halafu nyie mnataka kushinikiza watu wamchangie! Acheni watu wachange kwa roho zao wenyewe sio kwa sababu
    wameshinda zawadi ambayo nyinyi mmeikosa!! waangalie kwanza nyuso zao!! peace.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...