Asalaam Aleikum Wadau wote,
Hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza kuchangia ndani ya malumbano ya kisiasa na hasa kipindi hiki ambacho kimegubikwa na habari nyingi za kisiasa ambazo nyingi ni habari ambazo zimejaa simanzi ama manung’uniko ya kudhulimiwa, kutotendewa haki, na wengine wapo ndani ya shida za ukimbizi baada ya machafuko ya kisiasa.
Kwa kifupi na kwa kuazima maneno ya mwandishi mahiri Chinua Achebe ningelitumia “Hamkani si shwari tena”.
Katika uwanja wa siasa, hakika ni mengi ya kuongea na hata kulumbana kwenye tofauti za kiitikadi ama matashi kwamba wengine hupenda wapewe nafasi “(they need space!!)”.
Nisingependa kuliongelea hilo kwa sababu nina mengine ambayo mimi binafsi nimeyaona ni ya msingi zaidi na ni awali kuayongea labda yanaweza kulandana na mtizamo wa jumla katika kuchangia hoja na hasa hii ya ufisadi uliyotokea katika benki kuu ya Tanzania.
Aliyekuwa Gavana wa benki kuu ya Tanzania, Bw. Balali, ambaye ameshikishwa usukani wa kuliendesha gari la mafisadi wa tuhuma za kutumia nafasi zao na kutafuna mabilioni ya pesa za walipa kodi, ndiye amekuwa tena ameshika nafasi kubwa katika mazungumzo ya takriban nyanja zote za habari nchini Tanzania.
Siwezi kujumuisha yote yaliyokwisha semwa na wengi tuu tangu swala hili liingie katika duru hii ya malumbano. Mimi nitafupisha ili nilenge kuongelea lile ambalo limejiri mimi kuandika katika safu hii, hivyo nitaanza kuangalia taratibu za kazi ambazo nina hakika ndicho chanzo cha mambo yote haya kutokea na kufikia hapa yalipo hivi sasa.
Ninavyofahamu, ni kwamba ni Waziri wa fedha ambaye huchukua taarifa za mahesabu za benki kuu na kuzipeleka bungeni. Taarifa hizi huwa zinakuwa zimekaguliwa na Mhasibu Mkuu, na kupitishwa na Bodi ya wakurugenzi ya BoT. Hivyo utaratibu wa kuwasilisha taarifa za BoT zinafuata ngazi hizo kwamba inapofika taarifa kwa Waziri wa fedha, taarifa hiyo tayari ina baraka za Mhasibu Mkuu, Bodi wa wakurugenzi na mwishowe Gavana wa BoT.
Hakika ni mambo ya ajabu kabisa ambayo tunayaona yanatokea, kana kwamba hakuna taratibu, kana kwamba nchi inaendeshwa na utawala wa amri (hili linaweza kuwa kweli… maana si mara moja ama mbili nimesikia maneno kama “.. Rais amemuagiza… ama Waziri Mkuu amemuagiza….nk”).
Sentensi hizi zina maana nyingine tofauti kabisa katika nchi ambayo inashangilia demokrasia. Na mara nyingi maagizo haya hutokea mara tu panapokuwa na mushkeri na kwamba ni kwa sauti ya mkubwa tu ndipo mambo yatakwenda sawa.
Hii vile vile ina maana unapoagizwa katika hali kama hizi, maamuzi yako hayana uzito na kwamba kuna uzembe wa aina fulani kwako ama wewe hufahamu taratibu na hivyo wenye kuzifahamu ni lazima waache kazi zao na kuja fanya kazi yako ambaoyo utapewa maagizo ya namna ya kufanya.
Hili si jambo ambalo tungetegemea kuliona hapa Tanzania baada ya kipindi chote hiki cha kujitawala. Ni ya kuwa na wasi wasi mkubwa inapofikia kwamba kiongozi wa juu kabisa inabidi aje kuagiza mambo ambayo yana taratibu zinazooeleweka na sheria ambazo zinaongoza shughuli hizo.
Hapa panaweza kuwa na maswali mengi zaidi ya majibu na nina hakika maswali haya ndiyo hasa msingi wa yote hay aambayo tunayaona yakitokea katika nyanja mbali mbali za uongozi hapa Tanzania.
Swala hili linahitaji muangalio wa upeo wa juu katika taaluma za utawala na uongozi kinyume chake kitakuwa haya yalojiri BoT na hata sehemu zingine ambazo zina utata wa aina moja ama nyingine.
Kwa mtazamo huu huu wa taratibu za uongozi na utawala kwenda kuagiza, basi zipo sehemu ambazo serikali na wananchi wamekuwa hawafahamu nini mapungufu ama majaaliwa na sehemu hizo mpaka hapo patakapotokea hisia ya kuagiza, kumbe hili lingeepukwa na watu kufuata taratibu ambazo zitaweka bayana shughuli zote za sehemu hizo.
Kama hiyo haitoshi, nina hakika kwamba kama kweli tunafuata taratibu, basi ripoti ya mapungufu ya BoT ingelijulikana mapema sana tena kipindi kile kile ambacho ufisadi ulianza.
Kimsingi, Gavana asingekubali kusaini taarifa ya hesabu ya kwenda Wizara ya fedha na bodi ya wakurugenzi isingepitisha na wala mhasibu mkuu naye vile vile asingefanya makosa hayo na mwishoni wizara ya fedha ingelifikisha bungeni swala hili likiwa lina taarifa kamili za mapungufu na ni namna gani yametokea na yanashughulikiwa namna gani.
Cha ajabu ni kwamba katika mchakato wote huu hakuna aliyeona haya mapungufu nab ado nina imani kwamba vitengo vyote husika hapo juu vimekuwa vikipitia mara kwa mara taarifa hizi na kinyume chake kuzipitisha kwamba ni sahihi.
Matokeo ya kutofuata taratibu sasa yanavuruga taratibu zingine zote, kwamba Mkuu wa Polisi, Mkuu wa kitengo cha kuzuia rushwa na wengine wengi wameagizwa na Rais kufanya kazi zao BoT na kujipanga kutafuta suluhu la swala hili.
Hii ina maana sasa viongozi hao wafuate maagizo ya Rais na ni lazima wafuate na watafute muda wao wa kufanya kazi nyingine zinazowahusu ila lazima hili la agizo walipe kipao mbele na ikiwezekana hata usingizi iwe kitu cha kama anasa mbaya na hawatakiwa kuuendekeza!!!
Nina hakika kwamba viongozi hawa sasa hawalali na wapo juu juu ili wajinusuru katika kazi zao kutekeleza agizo la Rais.
Hili lingewezekana kufanyika kwa uyakinifu zaidi kama taratibu zingefuatwa, kwamba pindi mhasibu mkuu alipobaini kuna kugushi basi polisi wangepewa nafasi yao na hata vyombo vingine vya sheria na uongozi wa nchi nao kushiriki bila ya kuagizwa kwa kufuata taratibu zao za kazi na matukio husika.
Swala hili la taratibu na uongozi ndilo haswa jipu ambalo linatakiwa kupasuliwa maana hawa mafisadi ni msururu mzima wa watu ambao wamo serikalini na uraiani.
Na wote ama kwa kufahamu ama kutofahamu taratibu wametumbukia kwenye ufisadi bayana na kufanya uharamia ndani ya uwanja mkubwa tu wa wananchi wa Tanzania.
Nitarudia tena maandishi ya Jenerali Ulimwengu kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu vinne; Uongozi bora, Uongozi bora, Uongozi bora!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hapa mdau umeeleza na tumekuelewa na watu wameyafikia na yametuuma sana haya mambo ya ufisadi.Lakini nini hasa kinatusibu?Ni kweli kwamba tunahitaji uongozi bora lakini vilevile tuwe kama wenzetu walioko nchi zilizoendelea.Ni kama hivi ninamaanisha kinachotulostisha bongo ni umwenzetu kiasi kwamba ndio kama mdau ulivyosema mahesabu yapetewi na mhasibu lakini kama kuna mapungufu unafikiri utamwambia mwenzako kwamba hapa pana utata?Kwa hiyo kwa mtazamo wangu mimi nafikiri bongo inabidi tuachane na mambo ya UMWENZANGU ili linapokuja swala kama hili na mwenzako kaleta uzembe isiwe big deal kumFIRE.
    mkereketwa wa philly

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na mtoa mada mia kwa mia.Nchi hii haiendelei kwa sababu ya uongozi mbovu.Na kwa style ya uendeshaji wa nchi ya awamu hii sitashangaa awamu hii ikiondoka madarakani kila mzigo utabebeshwa kwa rais na waziri mjuu.Hii ni kwa sababu viongozi wengine wanaonekana kama wanafanya kazi kwa kusubiri rais au PM wanasemaje,hakuna waziri anayekuja na kitu chake na akakisimamia.
    Tukirudi kwenye hili la tume ya kuchunguza BOT nimeshangazwa sana na hawa makamanda kutaka watu watoe ushahidi.Ushahidi wa nini wanaoutaka????Mambo wanayochunguza ni ya kitaalamu na wataalamu wa Ernst &Young wameshayaweka wazi.Na Mh. Rais ameshatangaza kuwa kuna ufisadi umetokea katika nchi.Mimii nadhani Rais aliwateua ili kuangalia kwa tuhuma walizonazo ni kwa namna gani mashtaka dhidi yao yafunguliwe.Sio kutaka tena ushahidi kutoka kwa wananchi kama hawa mabwan wanahusika au laa.Maana ni kama vie wanataka kumdhalilisha rais kuwa tuhuma ambazo amezitoa kwa kina Balali si za uhakika.Taarifa ya ukaguzi ni ya kitaalamu,kuwa kuna malipo ambayo si halali yalifanyika.Na Rais ameshatengua uteuzi wa gavana,sasa wananchi waje na ushahidi gani.Nachoona ni kitu kile kile,hawajajua Mr. President au PM wanataka nini sasa wanaanza kupoteza muda.Suala lililo mbele yao ni kama kuna kesi ya kujibu,watafikishwaje mahakamani,tutapataaje mali zilizotokana na ufisadi wao nk,ndio maana kwenye tume hii wakawepo AG,IGP,Takukuru nk.Sasa Mie mkazi wa changanyikeni nitajuaje ushahidi wa kuwa Balali alichota fedha BOT na wengineo.Ernst&Young wameshafanya hiyo na inajulikana kuwa fedha zilichotwa.
    MSITAKE KUTUPOTEZEA MUDA,NA ONYESHENI KUWA NI WATU MNAOJITEGEMEA NA MNAJUA MNACHOFANYA!!!

    ReplyDelete
  3. Mdau, you talk too much, are you one of mafisadi??. it is boring to read your contribution.

    ReplyDelete
  4. mdau umemalizia kwa kurudisha mwangi wa kauli ya Jenerali ulimwengu lakini sijaelewa kidogo hebu toa ufafanuzi maana umeandika ili tuendelee tunahitaji vitu vinne(4) uongozi bora,uongozi bora,uongozi bora,akwi - kolazarzar@yahoo.com sasa hilo la nne unamaanisha tunamuhitaji huyo bwana mtajwa hapo mwenye hiyo email pia ama??? usikasirike mshkaji ni kajiswali tu!

    ReplyDelete
  5. Mdau ulichosema ni kweli kabisa hii nchi imekaa kizezeta mno na watu wake pia ndio tulivyo. Hebu waone wenzetu kenya wasiotaka ujinga wanavyowagomea mafisadi wa kura. Hapa kwetu ni nani anayeweza kuthubutu kupinga matokeo yaliyopikwa? Kule zanzibar polisi walinyakua masanduku ya kura mchana kweupe wakatokomea nayo kusikojulikana baadaye wakaibuka na kutaka kura walizokuwa wametokomea nazo zihesabiwe na watu wakakubali bila shari yoyote na hatimaye yule mgombea wao walokuwa wamemkusudia akashinda. Kudadadek!ingekuwa kule kenya hao polisi wangekwishazikwa siku nyingi sana. Kule polisi akihisiwa tu kwamba anataka kuiba kura(na wala sio kunyakua masanduku ya kura kama ilivyotokea zanzibar)wananchi wenye hasira wanaua.
    Ni dhahiri kwamba huo utaratibu tungekuwa nao hapa kwetu nidhamu ingepatikana tu na hakuna polisi koko hata mmoja ambaye angethubutu kusogeza pua yake kunako sanduku la kura!

    Vivohivyo ktk ufisadi pia madudu haya hutokea kutokana na umbumbumbu wa watendaji wetu. Kama ufisadi umeshachunguzwa na Ernst and Young na kiasi cha pesa kilichochotwa kikawekwa hadharani sasa kinachochunguzwa zaidi ni nini? Kama wanachunguza yale makampuni yaliyohusika waone kila kampuni lilichota kiasi gani ili hatimaye yafilisiwe, na ikiwa Ernst and young hawakuonyesha mchanganuo huo ,hapo sawa. Lakini kama watakuwa wanachunguza upumbavu mwingine wanaoujua wao wenyewe,huo ushahidi wanaoutaka basi kumbe wanao. Sasa hapo mwananchi wa kule kibondemaji huo ushahidi wa ziada yeye ataupata wapi?

    Kinachoonekana hapa ni kuendeleza danadana na kuzidi kufuja pesa za wananchi bila sababu yoyote ya msingi. Na kama watawala wajuavyo ni kwamba wanachi tu wepesi wa kusahau na baada ya hiyo miezi sita ya uchunguzi tayari tutakuwa tuliishasahau kila kitu. Si wanajua kwamba vichwa vya wananchi havitofautiani na vile vya kunguru? Yaani ni wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau.Kwani hadi sasa ni nani anayekumbuka wauaji kina ditopile walipo? Si dito wanadunda tu mitaani anauza asali. Raia mnyonge akihisiwa kuiba kuku wa mtu anapigwa jela mvua 30 lakini kina dito wakikamatwa wananyonyoa bata waliomuiba kwa jirani utaambiwa kwamba utoe ushahidi. Kwani kama bata mwenyewe wamemfumbia macho na manyoya alokutwa nayo mikononi hayatoshi kuwa ushahidi? Baada ya hapo unaambiwa kuwa alimuiba huyo bata bila ya kukusudia na kesi yake itafutwa! Huu si upuuzi tu?

    Kumbuka kwamba hata huko kenya enzi za rais moi mabo yalikuwa hivyo lakini hatimaye wannchi wakaja kuchoka na huo upumbavu. Matokeo yake kila mmoja anayaona. Na hawa waTZ ngoja tu waendelee kufuga maovu lakini haima yake itakuja kuwa mbaya kuliko ile tunayoiona kule kenya.

    Naomba kutoa hoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...