Habari kutoka Dodoma zinapasha kwamba Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi la aliyekuwa Waziri Mkuu,Edward Lowassa la kujiuzulu na pia amelivunja Baraza la Mawaziri.
Redio mbao zinadatisha kwamba huenda JK akamtangaza Waziri Mkuu mpya Jumamosi hii na kumuapisha Jumapili huko Chamwino, kabla ya kutangaza baraza jipya la mawaizi Jumatatu.
Wadau, nasema tena, halahala bin chonde; hii ni kutoka redio mbao na haijathibitishwa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. Ni lazima ilikuwa akubali.There was no other way.Sasa atueleze anamfikisha vipi mahakamani na kumfilisi vipi.

    Waliobaki je inakuwaje?Wakina karamagi,Msabaha,Mwanasheria mkuu,Mkurugenzi wa TAKUKURU???

    ReplyDelete
  2. KWA KWELI HIZI NI HABARI TULIZOKUWA TUNAZISUBIRI KWA HAMU KUBWA SANA

    UKWELI NI KWAMBA RAISI ASINGEKATAA KWANI TAARIFA ZA UKWELI ZINASEMA YEYE RAIS NDIYE ALIYEMUAMURU LOWASSA AJIUZURU KABLA HAJAPATA AIBU; KWANI MH. JK ANGELAZIMIKA KUMTOA MADARAKANI AMBACHO KINGEKUWA KITU CHA AIBU SANA;

    NA KAMA MLILITAZAMA SAKATA VIZURI NDG.LOWASSA ALIPOTOA TAARIFA ZAKE ZA KUJIUZURU ALIKUWA KAMA NI MWENYE KUTAKA KUTOKWA NA MACHOZI;
    MKEWE PIA ALILIA KWA UCHUNGU
    HAWAKUWA NA JINSI;

    NAMPENDA SANA KIKWETE NA NINGEPENDA AEENDELEE NA MOYO HUO HUO MILELE ; NA NAPENDA AWE RAIS WA TANZANA DAIMA MILELEE KAMA INGEWEZEKANA!!!

    MUNGU IBARIKI TANZANIA
    MUNGU MBARIKI JAKAYA KIKWETE
    MUNGU MBARIKI DR.SLAA
    MUNGU MBARIKI ZITTO
    MUNGU MBARIKI DR.MWAKYEMBE .. NISHUJAA MKUBWA SANA ANAYESTAHILI SIFA ZOOTE

    ReplyDelete
  3. Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeehh!! Pinaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!! Cheleaaaaaaaaaaaaaa pinaaaa!! Isishio hapo inabidi wafikishwe kizimbani kama walivyofanywa wakina Aden Rage na FAT.

    ReplyDelete
  4. Heko mwanangu. Sasa sheria ifuate mkondo wake. Tunataka pesa zetu. Vilevile, watuhumiwa wachukuliwe hatua za kisheria. Ahsante Yesu.

    ReplyDelete
  5. safi sana, kwa hiyo hivi tunavyoongea NCHI HAINA UONGOZI...afanye mambo upya, sasa CCM walivyo, utashangaa Pius Msekwa,Kingunge,Malecela wanapewa uwaziri, wakati vizee vishakuwa spana mkononi...sasa Vasco Da Gama tulia uweke mambo sawa huko nyumbani, natumaini safari yako ya Finland next week, utaifuta, mana mwenzio Sitta sijui alidokezwa na mtu kuwa kuna kasheshe la Richmond, akafuta safari yake ya Marekani juzi, sasa na wewe tulia nyumbani baba...mana huku Finland tushapigiwa tarumbeta kuwa unakuja, kwakweli sintafurahi kukuona huku wakati home mambo ni hovyo kwa sasa...weka mambo mswano, mapema kabla Mr.Kipori(Bush) hajafika....

    ReplyDelete
  6. Ndugu zangu mimi bado sielewi... wakati wa biashara ya richmond. Mheshimiwa kikwete si alikuwa waziri wa mambo ya Nje?? na yeye ndio alisign cheki ya Richmond. sasa mbona yeye akujihuzuru??? au yeye ni kama nani? Arafu mbona kesi ya BOT imekuwa kimnya??? Michuzi tupe Brother.. kama nawaona vile mavi yamewabanaaaaa mtakunya heno heno...

    ReplyDelete
  7. TANZANIA PM TO RESIGN OVER GRAFT

    Mr Lowassa told MPs his decision had not been an easy one
    Tanzania's Prime Minister Edward Lowassa has tendered his resignation after being implicated in an energy deal corruption scandal.
    He has denied that his office was involved in improperly awarding a contract to US-based electricity company Richmond Development in 2006.

    The firm failed to provide emergency power during a power crisis in 2006.

    Following Mr Lowassa's announcement to parliament, two other ministers linked to the scandal resigned.

    The BBC's Africa analyst Mary Harper says the offer of resignation from such a senior member of government for alleged links with corruption is unprecedented in Tanzania, and unusual in Africa.

    But Tanzania has been getting more serious about corruption since President Jakaya Kikwete was elected in 2005.

    Just last month, the governor of the central bank was sacked following the disappearance of public funds from the bank.

    'Lacked expertise'

    The BBC's Vicky Ntetema in Dar es Salaam says Richmond was contracted to bring in generators to provide 100 megawatts of electricity each day after a drought early in 2006 left low water levels in dams leading to severe power cuts.

    I've offered my resignation... to register my disagreement with the manner in which the committee misled parliament

    Edward Lowassa
    Tanzanian prime minister

    But a parliamentary inquiry, launched in November, found that the generators failed to arrive on time and when they did, they did not work as required.

    By the time the company was ready to start operations, Tanzania's power problems had been resolved.

    Despite these failings, the government was contracted to pay Richmond more than $100,000 a day.

    Mr Lowassa's office later influenced the government's decision to extend Richmond's contract despite advice to the contrary from the state-run energy company Tanesco, the inquiry alleges.

    Richmond "lacked experience, expertise and was financially incapacitated", ruling party MP Harrison Mwakyembe, who headed the investigation, is quoted by Tanzania's Guardian newspaper as telling parliament on Wednesday.

    Richmond transferred its tender to another company, Dowans, last year.

    Emotion

    Mr Lowassa, who has denied any links to the scandal, has suggested the parliamentary committee investigating the energy deal was given the wrong information.

    "I've thought long and hard about this issue. I've offered my resignation without any ill motive," he said in an emotional speech to parliament on Thursday morning.

    "I've done it to as a sign of my responsibility and to register my disagreement with the manner in which the committee misled parliament."

    Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi and Ibrahim Msabaha - a former energy minister and now in the East African Community ministry - resigned on Thursday afternoon.

    Our correspondent says Mr Lowassa, who entered politics in the 1980s, is a very close ally of President Kikwete.

    But the president is likely to accept his resignation in light of public anger over the scandal, she says.

    This is not Mr Lowassa's first brush with controversy.

    Under President Ali Mwinyi, he was relieved of his duties as a land minister because of allegations of corruption - a scandal that reportedly infuriated Julius Nyerere, Tanzania's respected independence leader.

    ReplyDelete
  8. michuzi utafikiri nimevuliwa nguo zote halafu nikawa exposed katika baridi kwa jinsi ninavyosisimka...
    is this really happening to our country???
    hii ni historia ya aina yake!
    sijui nifurahi, au nisikitike...
    kwa kweli tusubiri itakuwaje,
    Watanzania tuutumie wakati huu kuiombea nchi yetu kwa uamuzi wowote atakaouchukua Rais wetu, basi ukalete manufaa kwetu sote.
    Mungu ibariki Tanzania.
    SOLIDALITY FOREVER
    AND
    ALUTA KONTINUA!!!

    ReplyDelete
  9. Aminiaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  10. Hili ni somo muhimu sana kwa JK. Na ajiulize kwa kina kwa nini watu wanafurahia viongozi wao nyeti wanapojiuzulu? iko kasoro. aache kuteua kishikaji na utamaduni wa uwajibishaji uendelee. hali ya maisha imezidi kuwa ngumu...JK sio ahadi yako hiyo!!!!

    ReplyDelete
  11. That's nice! ila hatutaki re-cycled cabinet, he better bring totally new faces, nasiio hawa vizee wafujaji!!

    ReplyDelete
  12. are u killing me mchuzi?ahaaaa safi sana .ndio kazi ya rais wetu na bado wataumbuka wengi tuuuuu safi sana .jk

    ReplyDelete
  13. KUMEKUCHAAAAAAAAAAAAAA!!! MAFISADI MTATOKA TU NA MTAKE MSITAKE.... NITAMPONGEZA RAIS KAMA ATATUMIA NAFASI HII KUUNDA SERIKALI YA MSETO CHINI YA WAZIRI MKUU MPYA DOKTA SLAA NA BILA KUMSAHAU ZITTO KABWE KATIKA KIKOSI HICHO!MUDA WA KUJENDA NCHI YETU NI SASA, HIVYO NI MUHIMU SANA TUKASAHAU TOFAUTI ZETU NA KUWEKA MASLAHI YA TAIFA MBELE.HAPA NILIPO NASOMA REPORT YA RICHMOND HUKU MACHOZI YAKINITOKA NA NIMEPANDA NIENDE HOUSTON, TEXAS ILI KUONANA NA WAHUSIKA ILI KUJUA MTAZAMO WAO BAADA YA KUGUNDULIKA UFEDHULI WALIOTUFANYIA SISI WANYONGE. NI MIMI MDAU MWENYE UCHUNGU NA NCHI YANGU
    KIDUME, USA

    ReplyDelete
  14. Mzee Michuzi, kazi yako ninaiheshimu sana. Lakini leo nimekuheshimu zaidi kutokana na habari hizi zinazoingia haraka! Sijui nisemeje..yaani ni kama nasikiliza RTD nyumbani; halafu mijadala ya Bunge live.

    Shukrani.

    ps: Inabidi uanze kutengeneza hela kutokana na kazi hii...

    ReplyDelete
  15. kazi sasa kwa kikwete rafiki zake ndio mafisadi,swali atamchagua nani kuwa waziri mkuu? mimi nampendekeza prof. mwandosya

    ReplyDelete
  16. kaka michuzi,
    kazi ni ngumu sana kwa jakaya ktk wiki hii na kipindi chote ambacho mkataba mwingine wa bunzwagi na ule ufisadi wa BOT...hivi itakuwa vipi kama baraza atakaloliunda jakaya mawaziri wake wakaja kutwa na scandal ktk hiyo mikataba inayochunguzwa?
    hapa mi naona inabidi jakaya atafute wasomi wasiokuwa na majina na ambao hawana scandal awape kazi ya uwaziri,kwani kama atawang'ang'ania hao ambao wanaona kazi ya uwaziri ni zao basi kila siku atakuwa anavunja baraza la mawaziri.kwa kifupi aweke sura mpya kuanzia makatibu wakuu na huu ndio mwanzo mzuri wa jakaya kuunda baraza la mawaziri lililosafi na viongozi wasiowafanya biashara!

    ReplyDelete
  17. hii ni historia mpya kwa nchi yetu, shukrani kwa JK, wabunge wa upinzani { kwa kuwaamsha wabunge wa CCM ], NA PIA SIFA kwa Lowasa. mimi naona PM mpya awe Keenja, na Magufuli arudi miundombinu. Chenge toa kabisa, sitaki kusikia kabisa. Seif Khatib, Mungai, tupa nje.Mwanyika nje. arudi Magufuli na waziri wa Utalii Maghembe. Mkurugenzi TAKUKURU ashitakiwe kwa kusema uongo, kwamba uongo wa Richmond ulikuwa ukweli. Na pia JK naye aseme kwa nini alitetea Richmond ? nakumbuka aliwahi kutetea Richmon { wanahabari fanyeni kazi yenu hapa }nakusema bei ni ndogo na mambo kama hayo.

    ReplyDelete
  18. Na yeye mwenyewe arudishe funguo arudi kwao!
    Wasije wakatufanya tuane kama Kenya bure kwa ajili ya chuki.
    The sooner the better.

    ReplyDelete
  19. Kwishaaaaaaaaaaaaaaa.......!
    Wazanzibar walishayaona haya kitaaaaaaaaaaaaaaaambo, nyie wabara ndo mwaamka leo, ha ha ha mnakumbuka shuka kumekucha (ndo basi tena, umekula kunguru wasema umekula kuku..!). Lau kama msingekuwa mnakubali kupelekwa zanzibar kipindi cha kura ilikuongeza idadi (hata hivyo huwa hamshindi)basi leo yasingefika hivi mpaka ikawa umeme unaonekana lakshari, maana wengekuwa hawapo tena zanzibar na huku bara wangekaa kwa nidhamu, lakini wapi, sasa mtaamuwa moja nyie wadanganyika, mtakubali kuendelea kuwa kichwa cha mwandawazimu 2010 au mtaungana na wazanzibar kuwang'oa kiujumla.
    kubadilisha baraza sio dawa nisawa na kuweka bodi mpya wakati injini kongwe na mbovu.. suluhisho liko mkononi mwako wewe mdanganyika.
    Natamani nyerere angekuwa hai loooh, sijui labda hili ndo lingempeleka ahera kwa presha!Yaani mie ningekuwa kikwete ningejiuzulu coz hao wezi wote kawa weka yeye madarani, sasa mtoto akiiba anaelaumia kwanza ni nani? si wazazi wanaomlea halafu ndo atalaumiwa nayeye mtoto mwenyewe. Sasa kikwete anangoja nini? Lakini naona muda wakuiita nyeupe nyeusi na njano kuiita nyekundu umekwisha, sasa kijiko kitaitwa kijiko sio chepeo dogo na chepeo litaitwa chepeo sio kijiko kikubwa.

    Michu najuwa kada na sihasha hii ukaibania lakini hata wewe si utakuwa umeisoma!

    ReplyDelete
  20. Hapo Sawa JK.
    Lakini uangalie usivuke majivu ukavaa moto. I hope mpaka sasa unajua wema na wabaya katika timu yako. Chaugua wema

    ReplyDelete
  21. Hata wikijiuzulu na hela warudishe na pia jela walione...Nimesikiliza leo bunge ...wamenifungua macho...kweli wafisadi ni wengi...Raisi ana kazi kubwa sana...Hizo LTD nyingi wanazo hao hao viongozi. Kutupia tenda kwa wanao wajua na biashara zao..mapaka wanajisahau wanatumia anuani za barua pepe za makampuni yao kuwasiliana na watu wengine na hapo hapio wanaswitch kuwa ni kampuni nyingine na kujibu matenda mengine...

    halafu ni nini kuwaoa 10 days kutangaza hiyo zabuni...what is this?

    Mlo ulikua mzuri sana...bado BOT wote nao wajiuzulu..

    ReplyDelete
  22. Tarehe Thursday, February 7, 2008 8:45:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Mkereketwa

    "Kutoka kwenye katiba Kifungu 57 (2)(e) Waziri Mkuu Akijiuzulu serikali yote (Baraza la mawaziri) wanatakiwa wajiuzulu. Hii ndio Hoja aliyotoa Iddi Simba kuwa alijiuzulu ili kuepusha waziri mkuu (Sumaye) na serikali nzima kuvunjwa. Kwa hiyo hapo JK atavunja Baraza la Mawaziri na Kuunda upya. Sijui kwa nini Bunge bado linaendelea wakati Serikali haina kiongozi Bungeni (Waziri mkuu amejiuzulu, yeye ndio kiongozi wa serikali Bungeni) "

    ReplyDelete
  23. Hii michuzi ni breaking news kweli. What a revolution in Tanzania. Watu wamebanwa kwenye angles!! Wana literature hii wanaita "THE FALL OF THE GIANT" JK hapa anatega vitendawili, but big up saana!!!

    ReplyDelete
  24. The news is very encouraging.at last our leaders have learned how to take responsibility.corruption should not be tolerated in way because it hinders any country's economic development.it gives a way for only a few individuals to benefit from the country's resources.president kikwete now should bring very hardworking and serious people to his new cabinet.we need ministers who can contribute to improving the standard of living of all tanzanians who have been struggling since their independence.

    ReplyDelete
  25. Mie naona Mh Jakaya Kikwete angeteua mawaziri kutoka kambi ya upinzani, hii inaweza kusaidia ktk uongozi wake. Maana CCM sasa inazidi kuonyesha uozo wa hali ya juu. Then kama vipi jamani hawa jamaa uchaguzi ujao kwanini tusiwanyime kura tu!! Maana this is too much, au kama vp basi JK nae aachie ngazi kama kashindwa kuihandle nchi.

    ReplyDelete
  26. Napenda kutoa pole kwa JK, maana inaonekana uongozi wake sasa unaonekana kimeo labda kuliko walio mtangulia.
    Pole baba, kazana, ila next term lazima tukupige chini.

    ReplyDelete
  27. Yaaaaaaaaap!!!!
    Manyanga chini safari hii, ujinga huu na ufike mwisho wake, nchi yetu wote iweje wengine waiburuze tukiwaangalia hivi hivi, ebo!!!
    Ndo kwanza Mechi kabla ya kuanza lazima wachezaji wapya wapatikane ama sivyo mpirA Hauchezeki hapa!!!
    Hongera nd. Rais, nchi lazima ikusilize, chagua wachezaji wenye uwezo kiakili, ki-maadili, wenye busara, hekima, waadilifu, heshma, na wenye kusikiliza wananchi!!!
    Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  28. MICHUZI PAMOJA NA HAWA JAMAA KULA PESA YOTE HIYO WEWE KAMA MTU WA KARIBU NA KIKWETE HAWAKUKU KATIA HATA SENTI MOJA? KWELI DUNIANI KUNA MAFISADI HURUMA HAKUNA KABISA. WALAU WANGEKUPA KIASI FURANI CHA KUKUFUTA MACHOZI KAKA YETU LABDA KA BLOG KAKO ONE DAY NAKENYEWE KANGEINGIA KWENYE TENDA FULANI FULANI HUMU INCHINI AMA UNASEMAJE MJOMBA MICHUZI?HATUNA UZALENDO WABONGO!!!

    ReplyDelete
  29. Asante michuzi kwa updates. Japo uko Zenji lakini unajitahidi kutu-update kwa kila kinachotokea. Kama JK naye hutembelea humu globuni, ushauri au ombi langu ni kumkabidhi Bw. Mwakyembe aiongoze "Takukuru". Naamini rushwa itaisha. Ameonyesha ujasiri wa hali ya juu kabisa.

    ReplyDelete
  30. Bro Michu, kweli blogu yetu hii chini ya uwenyekiti wako ni zaidi ya CNN, BBCworld n.k katika kutuhabarisha na kutushirikisha ktk maoni ya matukio muhimu kwetu sisi tulio hata ughaibuni, maana vyombo hivyo vya habari vikubwa haviandiki au kutoa breaking news zisizo za umwagaji damu.
    Baada ya kusema hayo nachukua dhana shirikishi ktk kuwasaidia viongozi wetu waelewe kuwa tunafuatilia kila jambo lihusio Taifa letu yaani mama Tanzania. Hivyo tunaomba waziri mkuu mpya atakayeteuliwa pamoja na baraza lake la mawaziri wawe viongozi waadilifu ktk utekelezaji wa sera kusudio ya kumwezesha mtanzania atumie kila awezalo kuanzia nishati,maliasili, ardhi,mifugo, ubongo wake na nguvu zake kutuondoa ktk umaskini uliokithiri Tanzania ambao kwa kweli hatukupaswa kuwa taifa mojawapo masikini sana ulimwenguni.
    Mdau
    SeniorJumior
    London

    ReplyDelete
  31. Kuna suala moja hapa limedokezwa na naomba tuliangalie kwa makini! huenda JK akatangaza baraka la mawaziri katika kipindi kifupi;na tukumbuke kwamba kuna kamati njingine ya kuchunguza mikataba ya madini! SWALI: sasa iwapo itatokea hao watakaoteliwa na rais kama mawaziri wapya wakahusishwa tena kwenye sakata la mikataba ya madini itakuaje? watawajibishwa na kuwekwa wengine katika kipindi kifupi? wadau natoa hoja naomba majibu. Those who have involved in energy deal corruption scandal not only need to resign but also to face the justice!!!kama alivyosema "ndesa" katika serikali za nchi kama china mafisadi hawa walistahili dealth penalty !!!.

    ReplyDelete
  32. HONGERA TUME..SASA HAPA WABEBA BOKSI WANA USEMI GANI??

    ReplyDelete
  33. RADIO MBAO....waziri mkuu mpya, WASSIRA...TYSON.

    ReplyDelete
  34. Kaka michu hata mie nimeguswa sana na kinachoendelea nchini mwetu.Naona vile vile ant-corruption beaural nayo ingeondolewa kabisa kuwa chini ya raisi maana labda ingefanya kazi ipasavyo. Kuhusu tuhuma zote hizo hakuna anaye mtaja mkapa? hivi wanamwogopa? nakama ningekuwa kikwete ingemtoa kafala mkapakwanza.tuliyo ughaibuni tuwe makini tusiwe tunawakaribisha wafuja mali za uma.

    ReplyDelete
  35. jamani na wengine pia aliowateua hivi karibuni, hata robo wengine hawafai kabisa, ni balaa tu wanalosababisha kwa watu, kweli timu mpya iwe makini sana kwa kufuatia ushauri wa wananchi.

    ReplyDelete
  36. Kinachonikera zaidi ni watu kumpa big up JK, kwani yeye kama rais hajui haya?? Isitoshe kuna kashfa nyingi tuu hata yeye pia anahusika hata kabla hajawa rais, so pia yeye ni mhujumu mkubwa tu. Anatutolea kale kasmile ila he is just killing us softly. Wake up ppl. If the govt is very active, this would have happened long time ago. wote wanabebana tu. We will see Lowassa atakua nani later on, yangu macho na masikio.

    ReplyDelete
  37. Bongo moto sasa ivi. Watu tumechoshwa na vimeo na madili ya wakubwa.Dr.Asha-rose Migiro ndio awe our new PM. Mama yule yupo makini na kazi yake. Achana na akina Membe na Pinda, ni old wine kwenye new bottles.

    ReplyDelete
  38. kweli madhambi yao yameanikwa, na bado iyo ofisi ya serikali uko us, laana tupu bora hata ya wasomi wa uko, yaani ni bure kabisa, wasomi usa, bora, maana kujinufaisha tu uko us.

    ReplyDelete
  39. HIVI HUYO ANAE ONGELEA ATI WAZENJI WALIONA ZAMANI HANA HATA HAYA! HIYO MBALI WALIYO IONA MATOKEO YAKE YA MAENDELEO YAKO WAPI? MSHAMBA SANA LAZIMA ATAKUA MUIMBA TAARABU TU UPEO HAMNA USWAHILI TU NA KUANDIKA ASICHOKIELEWA. TUNATAKA POINT SIO BETI ZA TAARABU HAPA!

    ReplyDelete
  40. hivi ile kesi ya afia mzengo sijui us iliishia wapi?? pale us nako, wajiuzulu wote.

    ReplyDelete
  41. haya michu tunasubiri kwa hamu hiyo redio mbao,betri papai,antena mnazi naiamini kupita maelezo

    ReplyDelete
  42. Mtoto wa pwani(JK) sijaona bado, kinachofuata mahakamani, kumfilisi kisha jela, ukafanya kwa viongozi kama watano hivi, waliobaki watataadabu,vingunge, vinjekitile,watajigenguwa wenyewe, nao wataacha kula pesa za paki,maana nchi tajili lakini watu masikini sana,na nchi masikini watu wana maisha mazuri, kwa sababu ya uongozi bora, lakini vingozi wengi wa Afrika wabinafsi wanapenda kujilimbikizia pesa wao wenyewe na watoto wao na kuwa na dogodogo kibao.

    ReplyDelete
  43. JK waangalie sana, sali sana, na kwa babu pia usiache kwenda mwakwetu we, maana wasije wakakukolimba ndugu yangu,lakini namini Bwagamoyo sio mchezo,Komaa nao funga kwanza uvunje recodi ya kuwa Tanzania viongozi hawafungwi wanajiuzuru tu, halafu wanaendelea kutumbua mapesa kama kawaida, na ndio maana watu siku hizi wengi wanaingia kwenye siasa wanasema kuna pesa za bure.

    ReplyDelete
  44. Poormond alaah Richmond kanikumbusha sana wimbo huu wa Marijani Rajabu:

    CHORUS: DUNIA SASA IMANI IMEKWISHAA
    NYOYO ZA WATU ZIMEBADILIKAAA
    WALA HAKUNA UAMINIFU TENAA
    SI WANAUME
    SI WANAWAKEE
    SI MAWAZIRI WALA SI WABUNGEEEE
    WOTE TUNAKWENDA KWA RICHMONDIII
    KWENYE WATU KUMI BINAADAMU MOOJAAA!

    "BWANA FULANI KAACHIWA NCHII
    MWENYEWE JK=KAENDA UGHAIBUNIII
    HUKU NYUMA NCHI IKAFILISIWAA
    KAUA TANESCO NA MITAMBO FEKIII
    ALIPOULIZWA EE BWANA KULIKONI?
    KAJIBU 'MU JENGO' WOOWOO NINAONEWAA!!

    CHORUS: DUNIA SASA....

    ReplyDelete
  45. Kwanza hongera michuzi mimi pamoja na kuwa nasafisha vibibi lakini nina kacomputa kangu, nikirudi nyumbani nakawasha naangaliami mambo yanaendeleje nyumbani asante kaka.Pili nasema hivi JK kazi unayo maana viongozi wa bongo wengi ni maselfish, kwa hiyo wewe bahatisha tu kupanga safu ya mawaziri wako upya, na cha maana uwe mkali, na mfano kwa uadilifu labda inaweza kusaidia walala hoi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...