bush akitembelea shule
bush akiwa na kinamama wa kimasai
bush akipokewa a-taun
bush akisalimiana na wafanyakazi wa hospitali ya mount meru
bush na laura wakiwa na baadhi ya wagonjwa waliofuata huduma hospitali ya mount meru



bush akiwa na wamasai
bush akipiga stori na dk. aziz msuya wa hospitali ya wilaya ya mount meru


Kaka michuzi,
Naomba kushea na wadau jinsi dege lililomleta Bush bongo linavyoonekana kwa ndani. Yeye akiwa kwenye ndege kazi huendelea. Hapo akiongea na Senator Johhny Isakson anayeawikilisha jimbo la Georgia kupitia chama cha Republican tokea mwaka 2005. Pia kuna picha akiwa a-taun
Mdau US
PS: Endapo wewe au mtu mwingine angependa kuifuatilia hotuba zenyewe, basi zinapatikana:






Subi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. ALL I CAN SAY ABOUT THAT PLANE IS DAMN !!!!
    THAT IS A RICH COUNTRY

    ReplyDelete
  2. Hivi Bush hajatoka na gonjwa kweli hapo?

    Na DSM si ajabu katoka na malaria.

    ReplyDelete
  3. Hebu acheni upuuzi wenu ninyi hapo juu cha muhimu ni amani ambayo tunayo nchini kwetu kwanza hata ninyi wenyewe mnaweza kuona rais wa bonge la nchi jinsi alivyo relax, yaani ni vakesheni in Tz au vipi bro misupu!!!!!!!!!!.

    ReplyDelete
  4. THESE ARE REALLY LOVELY PHOTOS FOR HIS HOLIDAY ALBUM,EMAIL HIM.

    ReplyDelete
  5. Atleast tunapata kuona his soft side,maana bila picha kama hizi tunamuona jangili fulani hivi.

    ReplyDelete
  6. Bush anaonekana mtu pouwa sana. Inafaa aje Bongo kuishi akishamalizana na mikiki ya White House

    ReplyDelete
  7. tuplionyu, i was thinking about the same thing....lol. something is gonna come out of him...

    ReplyDelete
  8. Hiyo hospitali aliyotembelea nadhani ni Arumeru, sio Mount Meru. Ninavyopajua mimi Mount Meru hapako hivyo, na si hospitali ya wilaya, ni ya mkoa.

    ReplyDelete
  9. Kaka Michuzi

    Kwa upeo wangu mdogo wa saikologia nafikiri Rais Bush ataikumbuka Tanzania mno kwa mapokezi makubwa ya kiungwana na kikarimu aliyoyapata. Alikuwa ni mtu mwenye furaha mno kila alipokuwa akipita na ni kwa kitambo kidogo hajapata mapokezi kama haya ya kushangiliwa(watu kwa exited), kushiriki na watu wa caliber zote.Nchi nyingi alizopita huko duniani wengi walimuona kama jangili fulani hivi.
    Kwa ajili ya furaha aliyokuwa nayo na ukarimu wa watanzania ameonyesha kumbe na yeye na upande wa pili wa shilingi ambao ni laini.
    Bado nasisitiza katika usimamizi thabiti wa matumizi ya msaada alioutoa ($700M) japo sifahamu ni nini haswa marekani itafaidika in return.
    Mungu wabariki watanzania wawe wakali katika hili.
    Mungu ibariki Tanzania.
    Mdau Dommy

    ReplyDelete
  10. HIYO PESA YA MSAADA INATOSHA KABISA NA KUBAKI,KUMNUNULIA JAKAYA NDEGE MPYA KAMA YA BUSH

    MAONI TU

    ZEROOOOO

    ReplyDelete
  11. Tutakumbatiwa sana,hii inanikumbusha enzi hizi za mababu zetu jinsi walivyukumbatiwa na toba wakaingia mkenge!! Mtaka cha uvunguni shurti ainame na Bwana Bush hili analijua na anatekeleza! jamani tujipange hatujachelewa kama tunaona game! huwa namkumbuka Rais mstaafu alivyokuwa anatutusi kwa ukosefu wa kufikiri!!
    JK alicheza ngoma yake alivyomuaga rafiki yake(Bush), je sisi! Ngoma tutacheza lini!
    Wananchi tuamke! Eti vacation bomba!picha bomba!

    ReplyDelete
  12. Hospitali ilikuwa inaitwa Arumeru lakini imebadilishwa jina na inaitwa MERU DISTRICT HOSPITAL. I humbly submit.

    ReplyDelete
  13. Ama kweli masikini akipata! Yaani kwa kuwa yuko Bongo basi atatoka na maradhi? Hivi nyie ndio mnaosambaza upuuzi kuwa nchi zetu za Africa ni maradhi matupu! Kweli masikini akipata...........!

    Hao wamasai kwa taarifa yenu wala sio watu wa kuugua hovyo kutokana na system yao ilivyo. Na tena kuna wazungu kibao wanaofanya kazi za kujitolea Africa na kuishi maisha ya vijijini kabisa. At least ameonyesha kuwa ni mtu kuliko hata sie waafrika wenyewe tunaojidharau. Wewe mdau unayesema maradhi nafikiri hata kijijini kwenu kwa asili hujaenda unaogopa kuambukizwa maradhi na babu na bibi zako! Na ungekuwa ndio umepewa hiyo cnance naona ungewadhali kweli watu maskini na hata usingewapa mkono watu kama hao wa kwenye picha eti MARADHI! (huku umebana pua)

    Kama huko mliko hakuna maradhi kuna hospitali za nini?

    ReplyDelete
  14. Yeah!
    One thing I noticed, he is a genuine guy! He obviously hates POVERTY !!! period.I think he was sort of emotional after given the statistics about number of kids that are dying of stupid disease of malaria that can be preventable! and he had a privilege to decided right there and then that he will buy mosquito nets for 5 million T'zanian kids! it's employees were happier of course of guaranteed employment that will keep them busy for a long while ;).
    Personality: He is a people person! he wants to relate to people wherever he goes, and sometimes he likes to make them laugh! but not necessarily a comedian, he better keeps his day job to be more effective to a greater audience ;)
    Dr.Phil
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  15. Hii inadhihirisha kwamba TANZANIA tumepiga hatua kubwa kwa uongozi wa JAKAYA KIKWETE anajua kucheza kete maana rais wa MAREKANI kukaa nchi moja siku nne siyo mchezo anaweza kufanya hivyo nchi chache duniani kama UINGEREZA N.K hivyo watanzania tujivunie kwamba nchi yetu imekubalika duniani kwamba ni amani na utulivu, mnajua mpaka HIS EXCELENCE G W BUSH kukaa siku zote hizo Tanzania ni kwamba wameshachunguza kuwa shwari na hakuna vurugu yaani tambarale, je mnajua kwamba ni nchi mbili tu ambazo marekani anaziamini katika AFRIKA mojawapo ni TANZANIA ndio maan kuna ubalozi mkubwa kuliko seheme nyingine za AFRIKA, mmesahau kwamba mlikuwa mnakwenda AFRIKA KUSIN kuomba viza ya Marekani.Pili mbona sijawaona viongozi wa vyama vya upinzani wakimpokea BUSH?

    ReplyDelete
  16. Anko Bushi nae kumbe BITOZI!
    yaani kakaa a-tauni siku moja lakini kavaa mashati mawili tofauti...

    Dah, mwenyewe anajiona mseeelaaaa...

    Misoup,
    hivi hizo nguo alibadilishia hoteli gani. Alivyokuwa Arusha dinner tya mchana aliipatia wapi? au ndio mambo ya ea-fosi-wani hayo???? kila kitu mumo humo!!!...

    ReplyDelete
  17. tena bora akiondoka nayo hiyo malaria atapata test yake kwani sikuzote anaisikia tu, pambafu weee
    kuwa nje unasahau kina mbuya na mahabobo wako ulowaacha huku. Najarubu kukisia umri na matamshi yako, kama ni mkubwa unahasara maana sijui utakua mzazi gani asiyekuwa na mawazo ya busara ya kufikiri ila kuongeo pumba hizi ninazozisoma hapo juu

    ReplyDelete
  18. Kwa mapokezi yale hata ingekuwa mimi ningetoa mijihela jamani...wabongo kwa usanii!!!sasa wanakuja wengine..naomba watanzania tuzidishe usanii ili wamwage mijihela...big up sana wabongo!!! Bush mwenyewe alichoka akasaini mkataba bila kujua..maanake akigeuka huku anakuta tabasamu akigeuka huku vicheko na vigelegele..kugeuka nyuma akamkuta KK analimimina sebene...weweeeeeee..

    ReplyDelete
  19. Hizo ndizo siasa za Mataifa makubwa Watanzania wenzangu!Wengi walivyomfikiria Bush sivyo alivyo.Yeye pia ni binadamu kabisa mwenye hisia za kibinadamu kama sisi sote.Anazo hisia za kuona huruma,kujiwa na majonzi,kukerekwa na hali duni ya maisha,maradhi,ujinga na umaskini,hisia za kuchukia serikali dhalimu zilizokithiri kwa rushwa na ufisadi,ukandamizaji wa mawazo na uhuru wa binadamu,kutotendewa na kunyimwa haki na binadamu kupoteza kabisa matumaini ya hali bora ya maisha!Vyote hivyo vilidhihirika kumgusa Rais Bush katika zunguka yake na kupeana mikono na watanzania wa rika na tabaka mbalimbali bila kuhofia usalama wake!Unapokuwa Rais wa nchi tajiri na yenye nguvu kama Marekani basi unakuwa siyo wewe yuleyule waliekuzoea marafiki zako.Utajikuta ukisukumwa utekeleze sera na mikakati itakayo linda maslahi ya Makampuni Makubwa yenye hisa na kimaya kote ulimwenguni ambayo ndiyo yanayo changia zaidi katika Pato la Taifa na la kulifanya Taifa liwe jeuri na lenye nguvu mbele ya mataifa mengine.Nchini Tanzania Rais Bush alikuwa nyumbani kabisa.Wala hakuhitaji walinzi wa karibu sana kila aliposalimiana na mtu au kila alikokwenda.Alijisikia yuko huru kabisa tofauti na jinsi ambavyo angekuwa katika mitaa ya nchi za Mashariki ya Kati au Europa na kwingineko.Nadhani kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu sana nchini Tanzania alifanikiwa kupata usingizi wa kutosha 100% bila ya kuhofia uvamizi wa aina yoyote.Rais Bush siyo yule 'shetani'ambaye siasa za Marekani zilitufanya sisi Watanzania tumuelewe hivyo.Baba wa watu mkarimu,mnyenyekevu,mpenda watu asiye na chembe ya dharau au maringo ya kujikweza.Ni mtu Poa kabisa.Watanzania tumemkubali.VIPI MAMBO!Waliomchukulia kama katili na muuaji sasa watakuwa wameulewa ukweli wenyewe.Siyo yeye bali ni siasa za Mataifa Makubwa katika kujihami na Matishio yoyote!Wakati mwingine hata tishio lenyewe basi halipo,bali woga tu!Kuyakimbia Mataifa makubwa kama Marekani kwa kutokuwa na mahusiano nayo kwa sababu hizi na zile ambazo sio zetu moja kwa moja bali zinawahusu wengine siyo uamuzi busara hata kidogo na hautalisaidia Taifa la Tanzania kwa vyovyote vile.Kwa kuwa karibu na Mataifa hayo Makubwa yenye migogoro ya kimaslahi na Mataifa mengine yataifanya Tanzania kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuwa Wasuluhishi Wazuri wa migogoro na Watakao kubalika na pande zote zilizopo katika migogoro.NI KUTOKANA NA HILO KWAMBA nalazimika kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Kikwete kwa ushindi mkubwa sana wa KIDIPLOMASIA alioupata kwa Rais Bush kuweza kukaa hapa nchini kwa SIKU NNE MFULULIZO!Wanaosema kaja kwa mambo yake binafsi,sawa hata yeye ni binadamu vilevile.Naomba na kusisitiza tena na tena kwamba UJIO WAKE BUSH UTUZINDUE WATANZANIA KUTOKA KATIKA UJINGA WA KUTOAMINIANA baadhi yetu kujiona wao ndio wao waliosoma zaidi nchi hii kuliko wengine na ndio wenye haki na milki ya kufikiri kwa niaba ya watanzania wengine.Watanzania wengine ni wa kuja wa kuburuzwa na kufuata mkumbo tu!Zama hizo zimekwisha.Mageuzi ya kweli kisiasa na kiuchumi bora yaanze sasa.Pasitokee Richmond nyingine,wala EPA-BENKI KUU nyingine.Ukifanikiwa kupita kwenye tundu la sindano shukuru Mungu,usirudie kupita tena!Watanzania tujivunie uhuru tulio nao kuna wenzetu hawajafika hapa tulipofika,kubali usikubali!

    ReplyDelete
  20. Jamani mimi nahishi Congo huku jimbo la Katanga(mji jina nalihifadhi!).Wacongolee wanadai huyo bush hajaja kuleta Misaada Africa,amekuja kuwagombanisha waDRC amepita Tanzania kama 'zugaling' akaingia Rwanda kutuma sms kwa Nkunda!!Mimi nahapa simo!!

    ReplyDelete
  21. Mdau Anon Feb 20, 3:57 pm, Umetema point tupu. Nakubaliana nawe kabisa na ningependa kuwasihi watu wanaoandika tuhuma zisizo vigezo kureconsider. Heshima tuliyopewa si ndogo. Si mmemwona Mzee Bush alivyokaa na Mmasai hapo kama yuko nyumbani hata Lowassa hujawahi kumwona kukaa na Ole Saitabau namna hiyo. Asante Bush, Asante Marekani, Haya wabongo twende kazini!!! Long Live the Friendship between the People of the United States and the Tanzanian People. Ninachojiuliza sijui Jakaya alimwomba skolashipu Bwana Bush ili wale wakali wetu wa point 3 wawe wanakwenda Harvard, Cornell, Yale na MIT kuongeza ujuzi... Anyway, tunashukuru kwa tulichopewa sasa viongozi mle kidogo tu jamani!!!

    Mdau - Boston, US

    ReplyDelete
  22. Anon wa 3:57 umesema ukweli nchi kubwa kama hizo raisi ni kutekeleza sera za serikali tu kwa faida ya nchi kiuchumi... kiubinadamu ni mtu mwingine kabisa hii ni sawa na ma-actor wengi wanaonekana makatili kwenye filamu zao lakini kiubinadamu ni watu kama mimi na wewe...ikumbukwe kuwa Marekani kuna sera za kiulinzi ziko bega kwa bega na CIA..watakavyoamua raisi ni kufuata tu....asante

    ReplyDelete
  23. I like the way Bish was simple and his wife tu.Angekuwa mama wa kwanza wetu na mumewe mhhhhhhhhh.

    Ama kweli mwenye nacho hajidai.

    ReplyDelete
  24. MR.PRESIDENT BUSH IS THE REAL DEAL...GOD BLESS YOU AND YOUR FAMILY AND THANKS FOR THE WONDERFUL DONATIN TO OUR COUNTRY MR W BUSH...THE PEOPLE OF TANZANIA LOVE YOU SO MUCH, COME BACK AGAIN TO SEE US MR. BUSH..MUAAAHHHHHH!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...