BUSH AMESHATUA DAR NA KAPIGIWA MIZINGA 21 NA KUKAGUA GWARIDE. HIVI SASA ANAPOKEA SALUTI TOKA KWA GWARIDE ALILOANDALIWA RASMI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. I am happy to be tanzanian leo CNN ni Tanzania tu ...benin hakukaa sana lakini bongo wameionyesha toka asubuhi na mabango hayo...yaani raha raha tu sasa hivi Najifeel niko home.....

    Halafu bahati wanaonyesha tu sehemu nzuri kidogo hapa nimeona ngima na mabango apo sehemu nzuri tu....


    wanasema joto mbona joto la huku summer ni kali kuliko la bongo...labda hiyo humidity ya hapo Dar

    yaani I am so happy nikiona nchi yangu kwenye news

    Mdau NJ

    ReplyDelete
  2. Ni kweli mdau hapo juu, hao jamaa wanakasumba tu joto la washington dc ni kali sana wakati wa summer ukilinganisha na la bongo. mimi mdau wa DC

    ReplyDelete
  3. Mheshimiwa raisi, amchombeze Raisi Bush ili wawape vile vichwa vyetu vya Mzumbe na Ilboru nafasi(walau mbau tu) waje waji-mix Harvard, Brown na Stanford (UDSM wanajua kuwapa watu "disco" tu wakidhani sifa). "Asiyeomba kitu, hapewi kitu", au? Nafasi ndio hiyo!
    Babao

    ReplyDelete
  4. INANIKUMBUSHA MWAKA 2000 CLINTON ALIVYOKUJA, WELL DONE MKAPA FOR PUTTING TZ BACK ON THE MAP AND FOR JK FOR CONTINUING

    ReplyDelete
  5. Wewe Anony wa February 16, 2008 8:07:00 PM EAT, acha ushamba! Mzumbe na Ilboru ndo ni wewe kuna shule bwana! wewe ongelea TZ na siyo hivyo vishule vyenu.

    ReplyDelete
  6. Karibu Bush Bongo,iwe ni kwa namna yoyote ile lakini naamini leo Amana Hospital ni zaidi ya hospitali! Sipati picha usafi uliofanywa pale. Ila leo Michuzi mende kadondosha kabati pale anifidi. Yani katikisatikisa kabati kule mwanawane...Natabiri Benitez leo anatoka nduki utasikia tu...

    ReplyDelete
  7. MIMI NI MTANZANIA PIA, LAKINI SIWEZI KUSEMA JOTO LA USA WAKATI WA SUMMER NI ZAIDI YA DSM. NAONA SIYO KWELI. TOFAUTI ZILIZOPO NI KUWA DSM INA JOTO NYEVU WAKATI USA SEHEMU NYINGI ZINAKUWA NA JOTO KAVU HIYO SUMMER.

    JOTO LA DSM LINAKUWA KERO SI WAKATI WOTE. NI PALE TU UNAPOKUTA LESO HAISAIDII KUMALIZA JASHO MWILINI MWAKO PALE UWANJA WA NDEGE. NIMESHUKA MWAKA JANA AIRPORT KUKIWA HAMNA AIR CONDITION WALA FAN. NDIYO MAANA WAWEKEZAJI WANAPEWA BAADHI YA HUDUMA BADALA YA KUENDESHA SISI WENYEWE. NI AIBU SANA. KUNA WASAFIRI HUKATIZA TU TZ KUPITIA AIRPORT TU, HIVO TUNAPOSHINDWA KUWA NA VIPOZA JOTO NINAONA SI UMASIKINI BALI TU UZEMBE FULANI. KWANI BIASHARA NI NINI KAMA HUWEZI KUJILINGANISHA AU KUSHINDANA KIMATAIFA?

    SIWEZI KUSIFIA HOME KWA HILO. I AM SORRY!

    ReplyDelete
  8. Joji Bushi katia timu tumemwona,ila misupu leo Barnsley kamchinja mtu kwa panga butu! Oldi trafodi mvua inanyesha ile ya mawe imelowesha mzinga 3 hadi hafu taimu wanaulizana Goli la 3 kafunga Nani? Hawajui au hawakumwona,he Nani?. Historia ya Grimandi kukaa mkoba inaweza kujirudia tukatupia sita

    ReplyDelete
  9. Anony Saturday, February 16, 2008 8:29:00PM EAT. Maada umeikubali au umeikataa? Wenzio wakitoa mjadala huwa wanaweka na data kidogo. Hizo shule zilizotajwa zilikuwa zinaitwa "special school"; mwandishi akitoa mfano wa shule zenye vijana wenye uwezo mkubwa. Ila mjomba inaonekana umepania! Haya ugua pole!

    ReplyDelete
  10. IM PROUD TO B TANZANIAN. FINALLY WE R KNOWN AROUND THE WORLD. NAISHI UK NA UKIMWAMBIA MTU UMETOKA TZ ANAULIZA NDIO WAPI LAKINI NOW EVERYONE KNOWS WHERE IT IS.
    KIKWETE APEWE PONGEZI.

    ReplyDelete
  11. Bado Tanzania haitambuliki duniani leo kwenye Aljezira wametangaza Bush is visiting west African country -Tanzania.Tanzania Bado. watu wengi wanajua mlima Kilimanjaro uko Kenya, Mbuga ya serengeti iko Kenya. Tanzania Zii sababu ya ufisadi.

    ReplyDelete
  12. Jamani Bush alishatoa nafasi ya Havard na Sumaye ndiye aliyekwenda kusoma huko sasa mnataka nini tena,kwani hamjui Sumaye ni product ya Ilboru.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...