jk karejea toka dodoma jioni hii na kupitiliza diamond jubilee moja kwa moja ili kuongea na wzee wa dar ambao walimwandalia mkutano. picha ya juu jk akiongea na kushoto kwake ni mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa dar mzee athumani mwinyimvua na rais mstaafu alhaji alio hassan mwinyi. chini ni baadhi ya viongozi wa kidini na kisiasa walioketi naye haitebo.
jk kaongea mengi ila moja lililowakuna wazee ni pale aliposema kwamba yeye aalikuwa na mpango wa kufanya mabadiliko la baraza la mawaziri mara tu baada ya kikao hiki kinachoendelea cha bunge na baada ya rais george bush kumaliza ziara yake. ila kwa bahati mbaya ama nzuri saga rhumba la richmond likampiku na mambo yakawa mambozzzz
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Namuona hapo muheshimiwa (oopssii.. Mchungaji) kakobe... sijui anawaza nini!

    ReplyDelete
  2. Namuona Mzee Ruksa kwa raha zake kapozzy... huyu baba mungu ampe maisha marefu hana makuu mzee wetu...I Love you Grandapaa

    ReplyDelete
  3. Namouna Kakobe hapo! Light bluu suti.

    ReplyDelete
  4. Amepata extra days to clean the cabinet na kuwaweka more sharp sharp...naona bush amedelay safari yake...kwa sasa


    Lakini ni vizuri watu waenjoy hivyo vizuri vilivyowekwa kwa ajili yake tu. Manake angekuja na kuondoka basi vizuri vyote vingetolewa right away.

    ReplyDelete
  5. Michuzi alichofanya JK ni KUHUTUBIA wazee na si kuongea na wazee. Kuongea ni 2-way conversation kuhutubia ni 1-way. Wazee walikuwa wanasikiliza tu hakukuwa na maongezi hapo!

    ReplyDelete
  6. umekosea michuzi, useme JK kaongea na wana ccm dar
    Nashangaa bwana JK kila anakokwenda basi rais wa nchi wanamuona kama kawakilisha ccm

    wazee wa dar ni wa ccm na vyama vingine, kwahio kama tunavyoona kwenye picha yuko maskani hapo.

    ReplyDelete
  7. Nilibahatika kusikiliza mazungumzo haya pale Diamond Jubilee,nilisikitika sana.Yale yaliyozungumzwa pale na pande mbili yaani waalikaji na mualikwa,aisee sikuamini kama ni mazungumzo yanayoonesha kuna dalili za maendeleo ya kweli. Nafikiri taswira iliyopo kwenye vilabu vya Simba na Yanga ni ileile iliyopo serikalini.Timu zile ni tegemezi hadi kesho,licha ya kua na rasilimali kibao kama ilivyo nchi yetu. Unajua ni kwa nini?Ushabiki na maneno mengi umetawala sana kuliko kitu kingine chochote,najua post hii haitatolewa lakini nasema kweli hamna la maana lililosemwa pale zaidi ya kuoneshana tu mimi ni CCM damu! Kidumu chama cha mapinduzi na fikra za mwenyekiti! Heee,hadi leo hii halafu wanasema ni wazee wa Dar es Salaam?Nilitaraji Rais atakumbana na hoja nzito kutoka kwa wazee na si kumpongeza na kumpamba,si wakati wake huu.Kwa lipi hasa? Maana yaliyosemwa pale yalishatamkwa mwaka 2006 mwanzoni kabisa mwa serikali yake sio jana.Rais ni sawa na kutuongopea aliyozungumza kuhusu baraza la mawaziri,kwani kina Msabaha na Kalamagi ilikua wawajibishwe mwaka jana,na si kusubiri hadi ripoti za uchunguzi zisomwe. Namalizia kusema kwamba kitakachofuata ni kuwasahaulisha watanzania mambo haya na kamwe hamna atakayewajibishwa kiuchumi kati ya wote waliohusiwa kutokana na dhana ileile ya kishabiki na kuoneana haya,kadhalika kulindana

    ReplyDelete
  8. Hotuba ya Raisi haikuandaliwa kitaalamu au Raisi inaelekea hakuipitia kabla ya kusoma au Raisi hakujipanga vizuri kujua anataka aseme nini.Alikurupuka tu Sababu.

    1.Raisi Kasema hakutarajia kufanya mabadiliko sasa hivi ila baadaye ina maana kalazimishwa kufanya mabadiliko bila hiari yake! Hii ni sawa na kusema kapinduliwa hayuko madarakani kuna wengine wanaoongoza nchi sasa hivi nay eye kabaki kama national symbol tu! Wenyewe wenye nchi wako nyuma na remote controls zao.Statement hii kutolewa na raisi ni aibu kwake na hao walioandika hiyo hotuba.

    2.Kasema Lowasa Historia ndiyo itamhukumu!! Jamani hivi Rais huyu vipi? Lowassa hatakiwi kuhukumiwa na Historia anatakiwa ahukumiwe na Mahakama.Aburuzwe mahakamani siyo aachwe eti historia imuhukumu? Hivi Raisi haoni kilichofanyika kwenye Richmond kinatakiwa kiende mahakamani na siyo kiachiwe historia? Mabilioni yote hayo yaliyochukuliwa tuachie historia tu ihukumu? Jamani Raisi asitupandishe hasira wananchi.Hapa tulipo tuna hasira kama nini nay eye anazidi kuchochea hasira zetu.

    3.Anasema alifanya mabadiliko hayo ili mambo yasichafuke!!!!! Yaani anataka kusema yalikuwa hayajachafuka? Mambo yalishachafuka.Angekosha sana wananchi kuwa kafanya mabadiliko kusafisha uozo na uchafu ulioichafua serikali ili kujenga imani kwa wananchi.

    Kwa ujumla hotuba yake kwa sisi wataalamu wa saikolojia Kiini cha hotuba yake kilijaa kujikosha mbele ya akina Lowassa,Karamagi na Msabaha kuwa wasimwone mbaya kwa sababu uamuzi alioufanya ulikuwa uamuzi mgumu, kalazimishwa tu wasimchukie n.k.Alitumia hadhira ya wazee wa Dar es salaam kuongea na Lowasa,Kalamagi na Msabaha ! Kwa sisi wandengereko lugha za kujikomba kuomba msamaha mbona tunazijua! Labda awaeleze watu wa kuja toka bara, wandengereko hatudanganyi.

    ReplyDelete
  9. JK HAKUWA ANAZUNGUMZA NA WAZEE WA DAR ES SALAAM BALI UKWELI NI KUWA ALIZUNGUMZA NA WAFUASI WA CCM KWANI TULIWAONA KWA MACHO KWENYE MKUTANO HUO WALIKUWA SI WAZEE KAMA INAVYODAIWA, HII NIKUJITAKIA UMAARUFU WA KISIASA KUWA WAZEE WOTE DAR WANAIPENDA CCM TU. TULIONA JEZI NA MAPAMBO YA CCM UKUMBINI NA HUO MKUTANO ULIKUWA NI KWA AJILI YA WANACCM KUPONGEZANA! MAMBO HAYO YA BONGO, HUKO WENZETU WOTE HAO WANGEFURUMISHWA MADARAKANI SISI TUNAFANYA UTANI.

    ReplyDelete
  10. MHE JK HII MIKUTANO YA KUPONGEZANA HAINA MANUFAA YOYOTE KWA TAIFA, WANANCHI TUNACHOTAKA HIVI SASA NI WEWE KUTUELEZA HATUA ULIZOCHUKUA ILI MAPESA YOTE YAREJESHWE NA HATUA ZA KISHERIA ZIMECHUKULIWA.

    ReplyDelete
  11. INAONEKA KIKWETE KWENYE MAWAZO YAKE ANAJUA KWAMBA YEYE BADO NI KIJANA ... ONA ALIVYOKUWA AKIHUTUBIA BADALA YA KUSEMA WAZEE WENZANGU ANASEMA NYINYI WAZEE HALAFU AMEMU"OFFEND" RAISI MWINYI, NA MARAISI WENGINE WALIOPITA KWA KUJIFAGILIA KWAMBA HII NI MARA YA KWANZA KWA RAISI WA MAREKANI KUFANYA STATE VISIT ... WE UNAFIKIRI MWINYI NA MKAPA WALIJISIKIAJE ALIPOSEMA MARAISI WALIOFANYA ZIARA WALIKUWA WANAFIKA KISHKAJI NA KUANZA ZAO ... KIKWETE NAKUSHAURI UWE UNAANDAA HOTUBA NA KUSOMA KAMA MWENZIO MKAPA HUWEZI KUFANYA CLEAN SPEECH KAMA NYERERE INGAWA UNAJITAHIDI KUMUIGA LAKINI HUWEZI ..... HALAFU NAKUSHAURI UWE UNASOMA VITABU MAANA NAONA HUNA PHILOSOFIC IDEAS ... KIFUPI UKO SHALOW SANA



    MICHUZI NAOMBA USIFUTE CHOCHOTE KWENYE HII COMMENT YANGU

    ReplyDelete
  12. Kikwete you look like msanii and unadharau wazee ... you think you can think and fool around people but to tell you we smell everything we know were you are playing dramma and dont bulldose your vice ... vice President Shein due to his low profile status

    ReplyDelete
  13. Kwa hotuba ya jana ya Rais wetu Mh.J.K nimeingiwa na mashaka makubwa juu ya umakini 'seriousness &commitment' aliyonayo mkuu. S ikutarajia kauli kama zile za Rais,kwa uwazi kama ule wa ripoti ya Richmond na mapokeo yake kwa jamii yetu,yeye kutoa hotuba ile inayoonesha juhudi binafsi za kujikosha na kuwasafisha mafisadi eti historia itawahukumu.Mr. President kauli zile zinajenga ujasiri kwa mafisadi wengine kuchomoza na kuitafuna nchi yetu si wanajua hakuna noma tutajiuzulu na pesa inabaki mfukoni na jela hatuendi. Mheshimiwa tuna imani na wewe lakini kamba za viatu vyako zinaweza kukuadhiri na kukuharibia sifa kama umeamua kutoa uhuru wa haki itendeke,shikilia hapo hapo ila huko unapotaka kuelekea ni kuchafua pale uliposafisha. Ushauri wangu hawa watu acha waadhibiwe kama wabunge na wananchi na wadau wote wa Tanzania waliokuweka madarakani wanavyotaka vinginevyo kauli zako zitakuharibia harakati zako mwaka 2010. Si mbali kutoka sasa. Wapinzani hawana tena shida na Richmond walisha ifikisha walipopataka sote tunakumbuka,kusema kwamba wanaitumia kupata umaarufu si kauli nzuri kutoka kwako.Chamsingi tulichojifunza kutoka kwao si njaa kama CCM inavyowabeza bali ni juhudi zao katika kumtetea mwananchi

    ReplyDelete
  14. Wewe anony wa 8:28:00 AM kote umeenda vizuri. Ume-comment vizuri kwa kweli. Ila umekuja kuharibu mwishoni. Eti uwaongopee hao hao watu wa kuja? Bila wao kwa taarifa yako wala usingejua sakata la Richmond.Usithubutu kamwe kuwalinganisha na Wadengereko. Wao wameenda shule na wana uelewa mpana kuliko unavyofikiri!

    ReplyDelete
  15. Kutokana na matukio haya ya Richmond,Benki Kuu,Buzwagi ,OGL NA IMPORT SUPORT,nk.,KWANZA KABISA nawaasa WanaHarakati wote,Vyama vya Siasa kambi ya Ushindani/Upinzani,Taasisi za Kidini,NGOs na Watanzania wote ndani na nje ya nchi kwamba wakati sasa umefika ili kumuokoa Rais wetu asije akatumbukia kwenye Kashfa za Rushwa au hata kuhusishwa tu na maovu ya aina hiyo,ambayo yanaweza kulitumbukiza Taifa letu katika machafuko makubwa kama ilivyo tokea nchi za jirani SISI SOTE KWA PAMOJA TUANZE KUTOA SHINIKIZO ILI MAREKEBISHO YAFANYIKE KATIKA KATIBA YETU HARAKA IWEZEKANAVYO,ili kutenganisha Vyeo hivi viwili vya MKUU WA NCHI(Head of State) ambaye kwa kawaida atapaswa awe RAIS WA NCHI,na MKUU WA SERIKALI(Head of Government) ambaye kwa kawaida atapaswa awe WAZIRI MKUU.Faida ya mfumo huo ni kwamba Rais wa Nchi hatahusika kabisa na kwa namna yoyote ile katika uendeshaji wa shughuli za kila siku za Serikali.Na kwa njia hiyo ataepuka mitego mbalimbali itakayo weza kumtumbukiza katika Mikataba iliyozingirwa na Ufisadi wa aina yoyote.Na Waziri Mkuu atakapo kumbwa na Kashfa yoyote ya rushwa,litakuwa jambo rahisi kwa Bunge 'lililo huru' kupiga kura ya pamoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu huyo pamoja na Serikali yake.Kwa ajili hiyo,Rais wa Nchi atalazimika kuivunja Serikali iliyoko madarakani na kukiomba Chama chenye wabunge wengi zaidi Bungeni kiteue Kiongozi mwingine kutoka Chama chao watakaye ona ana sifa na anastahili kuthibitishwa na Rais na hatimaye kupigiwa kura na Wabunge wote ili aweze kuunda Serikali nyingine.Hilo litaweza kufanyika kila mara Serikali itakapo dhihirisha uzembe na kujitumbukiza katika Ufisadi BILA YA KUHATARISHA UMOJA WA KITAIFA na nchi kuwa hatarini kutumbukia katika machafuko.HILI SI SUALA LA WALIOKO MADARAKANI HIVI SASA WATUAMULIE.HAPANA.Hawa watu watapenda waendelee kubakia madarakani mpaka hapo Mungu atakapo wachukua.Hili limethibitishwa kwa vitendo.WAZEE WAMEANZA KUBANJULIWA MMOJA BAADA YA MWINGINE kutokana na shinikizo za nyakati na siyo kwa hiari yao wenyewe kama wanavyotaka kutufanya tuamini.Mabadiliko hayo ya Katiba ni vyema yakaja kwa HIARI ya pande zote mbili,CHAMA TAWALA NA UPINZANI,bila ya kusubiri Shinikizo za Nyakati.WAKIENDELEA KUWA WABISHI AMINI USIAMINI,kwa jinsi upepo wa mageuzi ya kisiasa yanavyo endelea hapa nchini hivi sasa,WATAPOTEZA VYOTE!mkaidi hafaidi hadi siku ya iddi!

    ReplyDelete
  16. majuzi kuna mheshimiwa mmoja amesema kuwa huu sio wakati wa watu kugombania hoja ya kwamba ni nani aliyeanzisha hoja ya Richmond. ajabu ni kuwa rais wetu kaenda kule kule kwa kugombania hoja na wapinzani. kaaz kwel kwel.

    ReplyDelete
  17. Kikwete ungefungua moyo wa Kawawa wakati unahutubia ... usingeendelea kuhutubia ... wazee wanakuangalia lakini wanakuonea huruma na wanashindwa la kufanya

    DONT PLAY DRAMA WITH MATURED PEOPLE HAPO ULIPO WAO WASHAPITIA LONG TIME AGO NA WATANZANIA WA SASA SIO WALE WA ENZI ZA NYERERE SIJUI KAMA UNALITAMBUA HILO

    ReplyDelete
  18. kwa kweli watanzania tuendelee kufunguka macho,ningependa kuandika lakini mengi ningekuwa narudia,huwa najiuliza tatizo nini?tunaongea sana lakini kesho ni yale yale!labda ndio hicho wanachokuwa na imani nayo kwamba tutaongea na mwisho tutalala!!!
    Zaidi ya kujikosha kwa wazee wa ccm, anataka kuwaambia wakawafunge midomo wananchi kwa ziara ya Fisadi Bush baba yao!

    ReplyDelete
  19. Richmond belongs to Rostam Aziz - MP

    2008-02-15 09:48:40
    By Bilham Kimati, Dodoma


    The MP for Mbozi East, Godfrey Zambi (CCM) has said that the proprietor of Richmond, the controversial power generating firm, is Igunga MP Rostam Aziz.

    The MP made the remarks during a debate on findings of the House Select Committee that had probed the Richmond emergency power generating contract.

    During the debate, MPs said that some fellow legislators had disgraced the nation in the eyes of the donor community and members of the public by misappropriating public funds that would have been spent on development projects.

    Zambi likened Richmond to a monster created by fellow legislators, currently exploiting national resources mercilessly at the expense of poor tax payers.

    ``Richmond belongs to Rostam Aziz. This is an open secret. There is nothing to hide about this. Why fumble looking for owners of Richmond while there is straight forward answer given by the report? Rostam Aziz, the Igunga MP, is the proprietor of Richmond,`` Zambi said, flashing a copy of MwanaHALISI newspaper with its bold headline `Richmond belongs to Rostam Aziz.`

    Zambi said it was reported by MwanaHALISI that the current State House Communication Director, Salva Rweyemamu, had informed the select committee on December 18, 2007 that he knew Richmond since December 2006 and that it belonged to Rostam Aziz.

    He said former Prime Minister Edward Lowassa, was absorbed into Richmond by Rostam Aziz.

    Lowassa and two ministers, Nazir Karamagi and Ibrahim Msabaha, who were also implicated in the Richmond scandal, resigned last week, just hours before President Kikwete dissolved the cabinet.

    ``It is not enough for those implicated in the scam to resign and be left off the hook, even those who had been slightly involved. They should be taken to task and legal measures taken against them,`` said Zambi.

    He recalled another nasty experience last year when members of the Parliamentary Committee on Infrastructure visited the Tanzania International Container Terminal Services at Dar es Salaam port.

    They learnt that after five years of operation out of the agreed ten, the company was granted a 15 - year contract extension even before expiry of the first agreement.

    ``We came to discover that some of the owners of this company are those who recently resigned from public office.

    We need to clean up this kind of mess and help people fight poverty in the real sense of the term,`` he said, adding, ``This shows how politicians and entrusted leaders abuse the power to advance individual interests. They should be taken to court,`` the MP said.

    Saidi Nkumba (Sikonge?CCM) said Richmond and other companies which had entered into dubious agreements were still draining national resources.

    He commended the IPP Executive Chairman, Reginald Mengi, whom he said had for many years continued to help various social groups, ranging from income generating groups, the disabled and other disadvantaged members of the society without aspiring for political posts.

    ``Why is it that for some businessmen, it has become necessary to aspire for political positions for them to further their business dealings? In this country, we have clean businessmen like Mzee Mengi who is absolutely philanthropic. He is helping people fight poverty but has never shown any ambition to join politics,`` Nkumba added.

    He named other reputable veteran businessmen like Mzee Rupia, Amir Jamal; Sykes whom he has said had maintained clean business.

    ``Is it true that one needs to be a councilor or a legislator in order to serve the nation more appropriately? They use political positions to cover up their dirty deals. The 152m/- paid to Richmond on daily basis by the power utility company?Tanesco? would have been spent on other development projects. This money has to be recovered,`` Nkumba said.

    Kabuzi Rwilomba (Busanda?CCM) said: ``Our leaders used to tell us that the government didn?t have sufficient funds to finance people`s projects, while all the money was going into their pockets, leaving us with nothing. We will support you Prime Minister Pinda if you are determined to fight corruption.``

    Grace Kiwelu, (Special Seats?Chadema) advised the government to confiscate travel documents of all those implicated in the Richmond deal so as to make sure that they remained in the country to face justice.

    ``Inflated power rates have rendered many people jobless as they cannot afford to use electricity to run small projects. Consumption of charcoal which implies destruction of the environment has increased dramatically.
    This is not fair. Legal measures should be taken against all causing these hardships to the people,`` said Kiwelu.

    Tatu Ntimizi, (Igalula?CCM) said Tanesco collected 30bn/- per month but spent 21bn/- to pay power generating companies which were hardly contributing anything to the national economy.

    Charles Keenja (Ubungo?CCM) said the Richmond suspects had no valid excuse for all that had happened because they acted deliberately in spite of warnings, advice and proposals from Tanesco officials that the contract was full of ambiguities.

    ``Tanesco has been forced to increase power tariffs by 23 per cent. This is too much for our people, who are forced to make all that payment for the benefit of a few individuals. Let the money be recovered to help improve social services for the country,`` said Keenja.

    Beatrice Shelukindo, Ruth Msafiri, Magdalena Sakaya, Chrisant Mzindakaya, Mgana Msindai said the government should go deeper to expose all details relating to Richmond operations.

    Other MPs suggested that those who had been implicated, including junior government officials who facilitated the process, should be taken to court to answer charges and have their property confiscated.

    They commended the unity among MPs, irrespective of their ideological differences, which was manifested by fighting together for people`s rights.

    The MPs suggested that all the money stolen through the Richmond contract and other similar agreements should be recovered so as to restore people`s trust in the government.

    With regard to Prevention and Combat of Corruption Bureau, the legislators suggested total overhaul of the institution, which they said had lost its credibility, especially after clearing the Richmond contract of corruption.

    The Parliamentary Select Committee report, which was tabled in Parliament, last week, revealed that Richmond which was awarded the tender by the government to generate power in 2006, had no expertise in energy matters and was financially incapacitated.

    ReplyDelete
  20. Da amna kitu nilicho furahi kama kumuona Mtu kama kakobe akimsikiliza Jakaya inaelekea ule usemi wa Jk mtu wa watu ni kweli coz kakobe ni mtu aliyemchachafya sana Ben wakati wa awamu ya Tatu!basi tugange yajayo na tumshukuru sana mungu kwa mema juu yetu na taifa letu kwa ujumla.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...