Home
Unlabelled
kp
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Wewe KP, unastahili uchapwe viboko vya matakoni hadharani kwa ajili ya ile katuni ya Beauty & the Beast!
ReplyDeleteSAWA KP!
ReplyDeleteWadau wa Holland runaona mambo yako mabaya na mazuri (mengi mazuri-yadumishe)
KG.
Kipanya mwenyewe umefanana na Pinda mtu akikuangalia vizuri. So, na wewe ni beast pia??
ReplyDeleteMmh we KP nadhani unacheza na moto...unamwita mtumishi mwadilifu wa kitalu namba 1 kwa miaka 22 The Beast...jiandae, kama si mwaka huu basi kabla ya 2010 utapata u the beast wako. Labda vijana wake waamue kukuonea huruma...sometimez cheza kwa step si wote wanavumilia utani kwi kwi kwiiii
ReplyDeleteWe Michuzi, ile t-shirt yetu haikukauka tena? Mbona umerudisha shati la zamani?
KP ndugu yangu huwa nakubali sana kazi zako lakini ile katuni yako ya hivi karibuni khs PM mpya pia imenifanya nikose hamu kabisa na kazi zako...
ReplyDeleteHivyo basi kwa kututendea haki sisi mashabiki wako nakushauri uombe radhi kwa mheshimiwa na pia kwa Watanzania wote manake ile si tu inamdhalilisha PM bali hata wananchi anaowaongoza wanafedheheka kuona kiongozi wao akitolewa kasoro ambazo Pia ni kutokana na Uumbaji wa Mola.
Vinginevyo Kipanya una kipaji kutoka kwa Mungu hivyo usiikosoe kazi yake ya uumbaji wa sura ya mtu mwingine ilhali unamshukuru kwa kazi yake ya kuumba kipaji ndani mwako, kazi ya Mola haipaswi kukosolewa..
Kaka KP, naomba nikushauri kitu kimoja juu ya katuni zako. Ni kwamba unatoa katuni nzuri ila angalia sana kuna lugha nyingine huwa unatumia sijui ni kuwa unajua hujui maana au unafanya makusudi. Mfano ile ya "The Beauty and the Beast". Nakumbuka kuna movie inaitwa hivyo niliwahi kuona title ya namna hiyo, lakini unapoleta jina kama hilo kwenye katuni kama ya juzi wadau tunashindwa kuelewa unamaanisha nini?? Kwamba PM ni beast na JK ni beauty au ulikuwa unamaana nyingine. Tunaomba ufafanuzi. Otherwise, waandishi wa habari mkibaniwa na govt msilaumu kwamba unanyanyashwa maana mnavuka mipaka kw amtindi huo.
ReplyDeleteMdau Brussels
Mbona kipanya kafanana na Beast?
ReplyDeletehapo juu acheni ushamba, ile ndio inaitwa freedom of speach
ReplyDeletetukiogopana hatutafika kokote.
halafu kama hamjawahi kuona magazeti ya ulaya vile wanavyochora makatuni,
Ubaya wako unawaita wenzako "Beast"
ReplyDeleteLakini kwa Ujumla unaielimisha jamii. (Jihadhari usijemwagiwa Tindikali).
jamaa wee ni beast kuliko yule ulomtaja kihivyo!! Hivi yule masoud alowahai kushindana na dr remmy kwenye shindano la mr sura mbaya ndo baba yako?? naona kama unafanana nae sana!!
ReplyDeletehuyu anayesema ni freedom of speech sawa, lakini sio kwa kosoa sura za watu?? huyu masoud mwenyewe ashukuru mungu yuko mjini kwa hiyo atleast anaonekana mtu otherwise ni hao ho tu
ReplyDeleteJamani naona tumemuelewa vibaya kaka KP hakuwa akimaanisha maumbile wala urembo wa mtu kwenye ile cartoon. Ile cartoon aliitoa baada ya uozo wa kazi iliyofanywa na baraza la mawazili lilio pita, alikuwa akimaanisha JK alikuwa anawaremba na kuwabeba mawaziri waliopita ndio maana akaweka beaut na beast ana maanisha PINDA atakuwa mkali na mwenye msimamo katika kazi ya kujenga taifa. Wandugu tukiona cartoon inabidi tujue imetoka wakati gani alafu ndio tuanze kuhoji. Pongezi Kaka KP.
ReplyDeleteOOOh God kumbe Pk mwenyewe ni bonge la Beast!!!!! brother you realy realy to apologize to our MP wewe mwenyewe ni mbovu kinoma...let me tell you wanaume wenye sura kama MP ndiyo wenyewe kwa sisi wakina dada tunawaita maHB but you...mmm you are ga dem BEAST
ReplyDeleteSASA NIMEKAA KIMYA NAONA NIWAJIBU, ME NDO KP MWENYEWE!! KWANZA KABISA POLENI KWA KUNIELEWA VIBAYA, PILI SIWEZI KUOMBA MSAMAHA KWA VILE SIJAFANYA KOSA LOLOTE, TATU SIKUJUA KUWA MNA AKILI PUNGUFU HIVYO, NNE MKIENDELEA KUONGEA PUMBA NAWACHORA NA NYIE!!! KUDADAKI...!!!
ReplyDeleteNIMETAJA WAPI JINA LA MTU? TUMIENI AKILI JAPO KIDOGO SIO MNABWABWAJA TU, MP NI BABANGU MDOGO NDO MANA TUNAFANANA, NEED I SAY MORE?? YES, NINA FILE MILEMBE..KWIKWIKWIIIII.. KWA HIYO ANAYEBISHANA NA CHIZI NAYE NI CHIZI...ENDELEENI KUCHIZIKA!!
Kwa kweli Kipanya umeniudhi sana na katuni yako ya Beauty na Beast!!
ReplyDeleteSikupenda hata kidogo utani wako hapo ulivuka mpaka. Hakuna elimu hapo ni udhalilishaji! Sio uandishi huo!!!
Mbona hizi post zinazolalamikia cartoon ya KP ya the Beauty and the Beast hazina hoja? Hawa wanaozituma wana viwango gani vya uelewa? Jamani hii ni art! Matokeo ya art ni kuwapa fursa kila mtu atafsiri kulingana na uwezo wa kufikiri aliomjalia Mwenyezi Mungu. Wakati mwingine kwa kuandika kwako unatusaidia sana kukufahamu wewe na uwezo wako kuliko unachotuambia kuhusu KP.
ReplyDeleteKumbe Kipanya unafanana na panya ... he kumbe wewe ni beast namba wani
ReplyDeleteHatukufagilii kaka
unaonyesha utulivu ni zero
Here come a real beast
ReplyDeleteKipanya repent for what you described our Prime Minister
HAKUNA UHURU USIONKUWA NA MIPAKA
ReplyDeleteHAKUNA KAZI YENYE THAMANI YA MAISHA YAKO
FREEDOM OF THE SPEECH NI NENO SAHIHI ILA LIMETOMIKA NDIVYO SIVYO NENO SAHIHI NI PRESS FREEDOM
KP STORY IS MIGHTER THAN A SWORD BE OBJECTIVE
BEAUTY AND THE BEAST, TRY TO READ BETWEEN THE LINE AND YOU WILL UNDERSTAND WHATS BEHIND THE CURTIAN...
KP WHAT ABOUT POTRAYING THE GOOD THINGS ABOUT THE GOVERMENT?
ngoja nikawaonyeshe vijana wa usalama ambao Pinda ni mwenzao wa miaka mingi.
ReplyDeleteafu we endelea kusubiri hapo uone utakavyotulizwa kimyakimya.
Jamani mi nadhani ile katuni alikua analenga baraza la mawaziri kama sijakosea..wala sio PM.Yani mawaziri wazuri kiutendaji na wabovu kiutendaji.
ReplyDeleteNi mtazamo wangu..msinitie kucha za jicho
MWTYM
THE BEAUTY AND THE BEAST SI LAZIMA VIWE VIUMBE VIWILI TOFAUTI, INAWEZEKANA IKAWA KIUMBE KIMOJA LAKINI CHENYE SURA MBILI NDANI YAKE KAMA TULIVYOSHUHUDIA MTU MWENYE SURA NZURI, MCHA MUNGU LAKINI FISADI KAUTAFUNA UCHUMI WA NCHI.
ReplyDeleteMdada hapo juu ukitaka kuenjoy zaidi muombe kp (mouse) atoe makaratasi yake hapo usoni upate burudani zaidi ukiyaona masikio yake utanipa jibu anafanana na nanihino naogopa kusema ntapata dhambi kama yake.
ReplyDeleteJamani watanzania mbona tunajirudisha nyuma namna hiyo?mbona tunakuwa na upeo mdogo wa kuelewa na kufikiria?Mdada kwanza MP cjui ni nini ila najua niMP ni Member of Parliament,na kama ulikuwa unamaanisha PM ni Prime Minister.
ReplyDeleteKP hajakosea lolote na katuni zake ila tafsiri ni kuwa anamaanisha baraza la mawaziri lililopita lilikuwa na uozo(Ufisadi) na sasa JK kaamua kuweka baraza jipya chini ya Mh PINDA akimaanisha litakuwa la KUCHAPA KAZI na sio kulea uozo kwa kuwa na mvuto mbele za wananchi na kuwadhulumu haki yao.TUELEWE na TUTAFAKARI kwa makini.
People! Cartoon ya KP si zaid ya humor at it is very best! hapo kuna
ReplyDelete'sinema' mbili. Ni ajabu hiyo sinema ya 'From Boys to Men' watu hawaipigii kelele kwamba KP amemdhalilisha Mheshimiwa Raisi kwa kumuita Mvulana!! ama ni kwa vile jina ni la wanamuziki mashuhuri wa marekani? Kama mmeelewa 'Boyz to Men' kiasi cha kutoipigia kelele, iweje msiielewe 'The Beauty and the Beast' kwamba si zaidi ya art at it is best inayohitaji mtu kutafakari tu kwa ziada na kuugundua kuwa haimdhalilishi kwa namna yoyote PM wetu??
Sasa nimekubali kwamba nchi hii watu ni majoga kishenzi.Hodari wa kubwabwaja tu.Wengi wamekurupuka na kuanza kutoa tafsiri potofu ya ile Cartoon ya KP.Aliyesema kinacho maananishwa hapo ni uzuri wa sura na ubaya wa sura wa viongozi hao wawili ni nani?Kama huwezi kutafsiri katuni correctly better shutup!Usianze kugonganisha vichwa vya watu.Tafsiri sahihi ya ile katuni ni kwamba KP alikuwa analinganisha 'BEAST' na uozo au ubaya wa CABINET iliyopita hata ikalazimika ivunjwe kwa tuhuma nyingi zilizopo sasa na zinazoendelea kujadiliwa na Bunge letu NA 'BEAUTY' ikimananisha CABINET ya sasa ambayo itatarajiwa kuwa nzuri zaidi na itatenda mema na adilifu zaidi kuliko ilivyokuwa huko awali, period!Sasa hizo tafsiri zenu mbovu zimetokana na hisia zipi?Pleeeeeeeeeeeeeeeeeaase!
ReplyDeletemimi ningependa kuichukulia hii katuni katika mtazamo tofauti, yaani Beauty ni baraza letu jipya la mawaziri tukiamini kuwa ni zuri kuliko lililopita na Beast ni baraza la mawaziri la zamani ambalo limeonekana kuwa bovu. hizo picha mbili hapo naona zimetumika kama tu ni viwakilishi vya mabaraza mawili niliyoyazungumzia mwanzo, kama si hivyo basi hapo tungemuona mmoja amewekewa mvi kichwa kizima. Just think out of the box. Hata hivyo kama bwana Kp ulikuwa na dhamira ya kumnanga muheshimiwa mpya utakuwa umemkosea sana kwani juwa pia wewe una kashfa ya BOT (Indirect, wenye akili hasa wakifuatilia zile trip zako za China watakuwa wamenielewa). tulia mtoto usije kuundiwa tume bure.
ReplyDeleteHoyaaaaaaaaaa! Nyinyi vp mbona mnapayuka tuu hamuelewi maana ya katuni nini? Kama tungesimama juu ya mitazamo yenu basi kauti zisingekuwepo kabisa!! Hacheni mitazamo ya kale nyiee! KP big-up sana mtu wake kama Kenya, kaaaaaazi iendeleeeeeee!
ReplyDeleteWe anonymous 11:28, acha kujishaua. Kwani alichoandika ni kiswahili, nasi sote watanzania ni waswahili. Kama huna la kuandika kalale.
ReplyDeleteKipanya acha ubishi wa kitoto ... OMBA MSAMAHA UONEKANE GENTLEMAN
ReplyDeleteWANAOKUSHARI NI WAKUBWA ZAKO, WASOMI, NA WANAUELEWA USIBISHE TU.
KUOMBA MSAMAHA NI SEHEMU YA MAISHA
YOU WILL LOOSE NOTHING BUT GAIN RESPECT WHICH YOU ARE NOW STARTING TO LOOSE.
Angalia usije ukaanza kuwa Public enemy utosa hata hiyo michongo inayokuweka hapa mjini na kukufanya ujisikie matawi ya juu
Kipanya kumbuka
ReplyDeleteKIBURI SI MAUNGWANA NA HEWALA SI UTUMWA
Kwahiyo kama beast ina maanisha ni baraza bovu la mawaziri lililopita, sasa mbona picha iwekwe ya muheshimiwa PM mpya? hapo sijaelewa kidogo!
ReplyDeleteHII NI DALILI YA TOTO LILILOKUZWA KWA MAZIWA YA KOPO NA KULELEWA NA HOUSEGIRL ALIYEKUWA ANAIBA UNYUMBA KWA BABAKE.....KWA HIYO WAKATI WA NANII LINAEGESHA PEMBENI WAHUSIKA WAKIDHANI LIMELALA KUMBE LILISHAAMKA ZAMANI LIKAWA LINAWOCHI MUVI.....kha!!!!! liangalie lilivyoumbwa na uso usiokuwa na haya....Mwee
ReplyDeleteWewe jamaa hapo juu acha ushamba, eti ngoja nikawaambie wana usalama.
ReplyDeleteEnzi za kutishana zimekwisha.
kila kitu kwenu kibaya nyie wabongo,
Sijui uchapaji wa kazi wa huyu mr Pinda kama waziri mkuu, na hio ndio tutamjaji.
Bora awe sio handsome lakini akawa na uchungu wa nchi kuliko kutuletea mr handsome lakini anakula mali za nchi.
Kuongezea ni kweli Pinda sio handsome lakini bahati kuna wanaompenda.
kwahio wewe jamaa mwenye vitisho sijui wana usalama, hivyo vitisho kawatishe wakenya kuho.
tumechoka sasa.
Kipanya kumbuka
ReplyDeleteKIBURI SI MAUNGWANA NA HEWALA SI UTUMWA kweeeeliiii!!!
isitoshe we ni mchora katuni tu si mwandishi wala mtangazaji!
We dogo, kama ulishangaa ya "Tindikali" utaona ya "Kemikali".
ReplyDeleteHao wanaokupa kichwa sijui ni akina nani vile? Na wengine wanajaribu kukutetea hata kwenye hii blog ya michuzi.
Michuzi na wewe unampa kichwa huyu dogo. Mbona unabanaga baadhi ya maoni yetu, lakini huyu dogo anamuita PM Beast nawe unamuachia tu?
Tuwaheshimu Viongozi wetu.
LOH.. WABONGO KWELI MNAMATATIZO.. LINI MTAENDELEA? KP SIO MPUMBAVU KUTOA CARTOON ILE, KWANI HAJUI MADHARA YAKE? YEYE KAMAANISHA UTAWALA WA ZAMANI NA MPYA, SASA NYIE WENYE AKILI ZILIZOJAA VICHWA VYA DAGAA MMEMKAMIA, MARA MUMUITE BEAST,WAEGO WEWE WALA SIO BEAST HUO NI WIVU TU.. SOMENI, TEMBEENI MUONE MAMBO DUNIANI.. NA USIKUTE WEWE NI MTU MMOJA UNAYEANDIKA PUMBA HUMU KTK BLOG.. EEBOO
ReplyDeleteEwaaaaa Mjomba Mpoto Pandu Jecha wa feb 15 12:21 Natena Wahenga walisema,
ReplyDeleteMaji ukiyavulia nguo lazima uyaoge,
usipoziba ufa utajenga ukuta,
usitukane wakunga na uzazi ungalipo,
na lisemwalo lipo kama halipo likuja mjomba,
kwa mwoga hwenda kicheko na kwa chuja hwenda kilio.
Pia wamesema kumla nguru si kazi kazi kumwosha
Na mchezea matopee humrukia
AU ndo mwanamaji wa kale kufamaji mazoweaaa? na ulivyonyamaa kimya mjomba unanipa nikumbuke tena chambile cha kale cha ujeuri chasema :- MWAMBA NA WAKO HUKUTUMWA UMWAMBIEEEE? (komeni hamkutumwa mukamwambieee?)
HIZI NI SALAMU ZANGU MJOMBA KP
ndimi shangazilo.
KP mimi nakukubali sana na kazi zako ni za muhimu sana katika kuwaelimisha watu wote Tanzania na hata nje ya nchi. Tunakupa pia hongera kwa kazi yako ya ubunifu wa mavazi.
ReplyDeleteHata hivyo niruhusu niseme yafuatayo:
Hii si mara ya kwanza KP anatoa kazi yake hadharani.
Siku zote zimesifiwa na wengi kama si wote maana ni kazi nzuri inayofurahisha na kufundisha pia.
Sasa alipokosea mara moja ameambiwa wazi na hii haina haja ya kuwa mtaalamu wa ukaragosi au uandishi kuona kuwa kakosea. Toka aje na upuuzi wa kumdhalilisha PM kwa kigezo cha sura watu wenye akili zao na taaluma mbalimbali hapa kwa Michuzi, BC, Jiachie, Darhotwire, ktk magazeti mbalimbali n.k wamepinga vikali na kumsahihisha. Kp najua umeingia mitandaoni na kuona comments za watu mbalimbali walivyoandika kupinga kazi yako ya siku hiyo.
Usitegemee tuje na constructive criticisms kama hata baada ya kukueleza kwa lugha nzuri na upole bado wewe mwenyewe au washikaji zako wanakuja hapa kwa kukutetea unconstructively kwa kutoa rejea za anayofanyiwa Bush na Putin na kupindisha maana ya freedom of press isiyo na mipaka wala kiasi!
KP sikiliza, binadamu si Mungu. Sote tunafanya makosa. Ukigundua makosa yako ni kuomba msamaha na kufanya marekebisho kwa siku zijazo, huna haja ya kung'ang'ana na kujitetea au kutufanya sisi washabiki zako na wengine humu na mitandao yote niliyokutajia na kwingineko kuwa ni wajinga au kuwa tulikurupuka kutafsiri kikaragosi chako visivyo.
Kwanza tunapaswa kujua kuwa hata kama nia ya KP ilikuwa nzuri lakini kwa sababu ya nyenzo au maneno au alama alizotumia, ujumbe haukueleweka au umetafsiriwa vibaya bado, yeye mhabarishaji ana jukumu la kuomba msamaha maana nia yake ni ujumbe kueleweka na sio kutoeleweka kwa kutafsiriwa visivyo!
Aidha mimi sioni haja ya kumtisha Masoud, eti sijui ATASHUGHULIKIWA na vijana wa Usalama wa Taifa n.k maana idara hiyo haikuanzishwa kwa sababu hiyo!
Badala yake, Kwa kutotaka kukubali kosa lake na kwa kutotaka kuomba msamaha ATAJISHUGHULISHA YEYE MWENYEWE hapa duniani!
Mfano mwingine ni huu ambao watu wengi wamekuwa wanaadika na kumchora kwa namna mbalimbali EX-PM kuhusiana na sakata la Richmond hadi kujiuzulu kwake.
Wengi tumekuwa tunakubaliana na jumbe hizo maana hakika zilitakiwa kutolewa kuonyesha Serikali na hata wananchi wengine makosa au mapungufu makubwa aliyokuwa nayo EX-PM, ambayo hayajawahi kuwekwa hadharani.
Lakini sasa leo baadhi ya watu wameendeleea mpaka wanajaribu sasa kuwasilisha jumbe zao kwa kutumia photoshop, corel n.k 'kumtundika' EX-PM na wenzake eti msalabani na kunukulisha maneno kama aliyotoa Yesu Kristo pale gholgota!
Binafsi na wengine hatufurahishwi na hilo kwani katika tamathali zote za semi na maandiko hatuoni haja ya kumuhusisha EX-PM na Yesu Kristo maana sasa hata inaweza kupoteza maana ikawa kama yeye EX- PM alionewa tu, kwamba yeye ilibidi atolewe au ajitoe kafara kwa ajili ya dhambi au makosa ya wengine. Au mbaya zaidi ni pale Yesu kristo anaweza kusomeka kuwa naye alisulubiwa kwa sababu makosa yake kama aliyoyafanya LOWASA; inaleta kichefuchefu ndani dini yangu (yetu)!
Mimi kama Mkristo na mdau wa blogu na vyombo vinevyo vya habari sikubaliani kamwe na matumizi ya MSALABA KUFIKISHA UJUMBE WA KUANGUKA KWA KIONGOZI KAMA LOWASA!
NAWASHAURI WACHORAJI WATAFUTE PICHA ZA HERODE AGRIPA ALIYEJIKWEZA NA KUJINYANYUA, AKAKAA JUU YA KITI CHA UKUU NA PALE PALE MUNGU AKAMWADHIBU KIFO HADI KUOZA KWA KULIWA NA MINYOO.
Wasilisheni jumbe zenu kwa mifano iliyo hai na inayoshabihiana.
Ahahhh!! Basi Nyie Ndo Mshatibua kila kitu! Si-tulitaka tumnanihiii,nyie mara ohhh Usalama wa..,sijui Mizengo ngoja akusikie, omba msamaha,maneno kibaoo!!sasa hata akijikwaa tu watasema....
ReplyDeleteWabongo bwana,Kila mtu Usalama wa Taifa siku hizi....hebu na mimi nijaribu ku-'Apply'...ngoja niwaulize wenyewe..Eti Braza MICHUZI taratibu zikoje katika ku...
Man!! Since when did Tanzanians become so uptight. Lighten up people, you gotta have a sense of humor.
ReplyDeleteAnd rememebr, any work of art can tell a million stories, the interpretation is left up to the reader/viewer... a bright mind never takes anything by face-value and ponders before speaking.
And for the person that asked about the good things the government does... well it is KP's choice wether he wants to sing the government praises or not. And perharps he has not found a reason to. How about you find a way to do it. Beside, have you seen all of KP's work to conclude that he never mentions the good things?
Kaka Michu napenda kuchangia hapa kwani huu ni uwanja wangu.Tukumbuke kwamba sanaa nchini kwetu toka enzi za mababu, ilitumika kama njia ya kuliwaza, kufrahisha, kukanyana au kukosoana, kuhamasishana na pia kukatisha tamaa.Hivyo msanii alionyesha umaili wake kwa lengo mojawapo kati ya hayo hapo juu.Sasa jamii husika, ilitafakali sanaa husika na kupata ujumbe uliokusudiwa na msanii.Mpaka hapa bado hakuna aliyefanya kosa si KP wala watoa maoni.Hata hivyo mwenye ukweli ni kp kwani anajua ni lengo lipi alilokusudia.Wasomaji sisi tunaweka hisia zetu kutokana na ufahamu wetu na tafsiri zetu juu ya sanaa. SANAA JUUUUUUUUUUUUUUUU KP JUUUUUUUUUUUUUUUUUUU na wasomaji JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUZAIDI.
ReplyDeletemichu! tunaomba photo ya kipanya akiwa hajaficha masikio tafadhali.
ReplyDeleteKwa wale waliangalia vizuri sinema ya beauty and the beast au kusoma kitabu na kukichambua vizuri wanaweza kumwelewa vizuri kipanya, Kwanza kabisa beast alikuwa ni kijana mzuri aliye laaniwa akawana sura ile lakini ndani mwake alikuwa pia ni kijana mwenye roho nzuri na mpendwa na watu alinyanganywa himaya ayke na mjuvi mmoja lakini beauty alipomlilia machozi yake yaka mdondokea ndipo alipojidhihirsha uzuri wake. Sasa kama unajua fasihi unganisha mwenyewe maelezo niliyo yatoa na tukio kamili lililo tokea, lakini kama mnakumbuka vizuri Pinda hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake miaka miwili iliyo pita sijui ikawaje ikageuka lakini riziki ya mtu huipanga mungu, itachelewa lakini itakufikia tu.
ReplyDeleteKP ni msanii mzuri sana na jinsi sanaa inavyo zua gumzo basi ujue lengo lake limetimia (kwa wale wanojua vizuri maana ya sanaa watanielewa)
jamani watu wengi wemebloo hii katuni ya beauty and the beast out of proposheni. KP keep up the good work !!
ReplyDelete