aliyekuwa waziri mkuu wetu mh. edward lowassa leo amekabidhi rasmi ofisi kwa waziri mkuu mpya mh. mizengo pinda katika hafla fupi iliyofanyika ofisini hapo mtaa wa magogoni, dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mbona muda kidogo tu Lowassa kachonga kama amepigwa na kipindu pindu.

    Michuzi naku-mind nlikutumia e-mail ya issue fulani ya ASPIRIN zenye HIV,nashangaa huitoi.

    Umeanza ufisadi?

    ReplyDelete
  2. Kama JK angekuwa dj, hapo katoa r&b kaweka reggae. disco lote lina badilika na wengine wanaenda kukaa huku marastafari wakirukaruka kwa furaha

    ReplyDelete
  3. Kaka Angalia Kiti hichooooooo!! Kabla hujakali lazma ufanye jadi..

    ReplyDelete
  4. Mzee Mizengo Pinda kazi unayo na wala siyo lele mama: wananchi tunakutegemea utulize tashwishwi zetu kwa kutowaonea aibu mawaziri wako:wewe ndiye kiranja, angalia suala zima la kuanzisha mchakato wa nguvu kuhusu suala zima la wizara ya Nishati na Madini, zipitiwe upya sheria za kodi zinazotunyima mapato mazuri katika madini,chunguza na kuona nini kifanyike kurekebisha mapungufu hayo ili nchi ifaidi mali zake na siyo wafaidi wawekezaji pekee na watu wachache wizarani.Tusifanye makosa katika mikataba ya utafiti na uchimbaji gesi na kama yatakuwepo mafuta kwani tujifunze matatizo yanayotukumba kwenye mikataba ya madini. Angalia miradi ya uimarishaji miundo mbinu kwani ni ufunguo wa maendeleo kwa wengi hasa wale waishio vijijini,ziba mianya ya wizi wa fedha za umma kuanzia halmashauri za wilaya hadi ngazi za wizara. Waangalie wakuu wa wilaya na mikoa kwani ni ufunguo wa maendeleo katika maeneo yao: hata hivyo chakusikitisha ni kwamba wengi wao hawajui hilo na hawana 'vision' ya kuwaendeleza wananchi; pitia na pima matokeo ya kazi zao usiwabebe wasioweza kazi kwani hali za wananchi huko vijijini zinatisha.Ombi kwa watanzania: tuache siasa zisizo na misingi ya kutuendeleza kiuchumi sisi binafsi na taifa kwa ujumla, tujadili hoja kisayansi kwani nguvu ya hoja ni mkuki mkali kwa watunga sera na hata viongozi wakuu kitaifa.(eg-richmond+BoT)

    ReplyDelete
  5. "BE GOOD TO THE PEOPLE ON YOUR WAY UP
    YOU WILL FIND THEM ON YOUR WAY DOWN"

    ReplyDelete
  6. TANESCO YAENDELEA KULIPA RICHMOND MAMILIONI.

    2008-02-20 10:06:30
    Na Restuta James


    Licha ya Kamati ya Bunge kupendekeza kufutwa kwa mkataba wa Richmond na kutaka malipo ya Sh. milioni 152 yanayotolewa kwa Dowans kila siku yasitishwe hadi jana Shirika la Umeme(TANESCO) liliendelea kuilipa kampuni hiyo.

    Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bw. Daniel Mshana aliliambia gazeti hili jana katika mahojiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kuwa shirika linasubiri maelekezo kutoka serikalini.

    Alitoa ufafanuzi huo alipoulizwa iwapo TANESCO imejipanga kusitisha malipo hayo na pia aliulizwa kiasi cha fedha kilicholipwa kwa kampuni hiyo tangu kuanza kwa mkataba huo uliosainiwa mwaka jana.

    ``Bunge lilijadili suala hili na kupendekeza hivyo lakini hatujasitisha malipo maana serikali haijaanza kutekeleza pendekezo hilo. Nadhani bado ipo katika mchakato wa kuyapitia na kufanya taratibu kwa mujibu wa maelekezo,`` alisema.

    Alipoulizwa lini mkataba utasimamishwa alisema ni jukumu la Wizara ya Nishati na Madini kuamua wakati wa kuchukua hatua hiyo.

    Waziri wa wizara hiyo, Bw. William Ngeleja, alipoulizwa juu ya kusimamisha mkataba huo alisema hatma ya jambo hilo ipo mikononi mwa kamati ya sekta mbalimbali iliyoundwa na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda kupitia na kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo hayo.

    ``Tupeni muda kidogo wakati kamati ile inachambua mapendekezo maana wao watatoa mwelekeo mzuri katika utekelezaji ripoti ya Bunge,`` alisema.

    Alifafanua kuwa hata kama Dowans wataendelea kulipwa hatua za kisheria zitachukuliwa kurudisha fedha iwapo italazimika kufanya hivyo.

    Wiki iliyopita, Bunge lilipitisha mapendekezo 23 yaliyotolewa na kamati yake likiwemo suala la kusitisha malipo ya Sh. milioni 152 kwa kampuni ya Dowans mapema iwezekanavyo.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  7. CHEKI TICHA ANAVYOWACHABO KWA PEMBENI HAPO UKUTANI YANI ROHO YAKE SASA IMERIDHIKA

    ReplyDelete
  8. wasiomjua ex PM huwa anafunga kwaresima full time na hajaanza leo amekuwa akifanya hivyo for years.kwahiyo mashavu lazima yaporomoke. subiri baada ya hapo yatarudi

    ReplyDelete
  9. THAS GOOD MZEE MWENZAGU LOWASSA KAMA ULIVYOAMBIWA USANZE KUMTAFUTA MCHAWI KAA CHINI 'MEDITATE ALONE" while sobber sio on brandy !!! uangalie ulikosea wapi na wapi pa kurekebisha you are still very young na wenzetu huwa wanasema when "ONE DOOR CLOSE THE OTHER ONE......."

    JAMANI TUSAIDIANENI SAKATA LA RICHMOND LIMEMPA BUKUKU katibu mkuu SIO MZEE WA SUMO ! ILA CHA KUSHANGAZA KAFUNGA OFISI MIUNDO MBINU NA MWENZAKE ALIYETEULIWA HAJAWEZA KUINGIA BADO ANATUMIA OFISI YA ZAMANI, JK KAZI UNAYO KUBWA SANA !!!!!!

    ReplyDelete
  10. Kitakachofuata masomoni Ulaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...