Home
Unlabelled
maadili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Sijui niseme nini zaidi ya..NO COMMENTS!!!!
ReplyDeleteMMHHH HII KALI SASA ANAMAANA UKIINGIAN NA MWANAMUME LAZIMA MANANIHII.AFADHALI WAKATI WA ADAM NA HAWA KULIKUWA AKUNA CHETI CHA NDOA, SIJUI NANI MWENYE WIVU MKUBWA KAANZISHA CHETI CHA NDOA.VIPI IANANKANA ILO ENEO AKIONEKANA BATA AU KUKU ANANANIHII NI KOSA LA JINAI MAANA MPAKA WAWE NA CHETI CHA NDOA
ReplyDeletenzuri sana
ReplyDeleteKuingia wanaume kwa wanaume yaani mashoga mbona hawajaandika? Au ujumbe huo una maana kuwa mashoga tu ndio wanaruhusiwa kuingia hapo
ReplyDeletehii imetulia laiti kama hotel na gesti zote zingekuwa na kanuni hizi basi uasherati ungapungua kwa kiasi kikubwa na wizi wa wake au waume za watu ungepungua kabisaaaaaa. safi sana!
ReplyDeleteVery Sorry,inasikitisha sana!Mwenye hoteli ukifikia hatua hiyo ya kuanza kutoa masharti fyongo kiasi hicho basi ujue wewe umekwisha hufanyi biashara ya hoteli bali akili zako zote ziko kwenye uzinzi!Ukiweka masharti hayo ndiyo nini?Utasifika kwamba wewe ni muumini kwelikweli wa dini fulanifulani,ebo!Ukiwazuia watu wasifanye uzinzi kwa njia hiyo si ndiyo kabisa utazidisha matatizo kwa kuwafanya wanaotenda matendo hayo wajifiche kabisa na kuyatenda mafichoni na wewe usipate fursa hata ya kusaidia kwa kutoa ushauri wa ana kwa ana!Kwa maoni yangu huo ni ujinga ulioje.Tumpe Binadamu Uhuru kamili wa kujiheshimu yeye mwenyewe bila kusukumwa ili aone haya kutenda maovu kwa mujibu wa utashi wake na tamaduni za kijamii.Tusiige tamaduni toka nje kama vipofu bila kufikiri tukadhani tunajenga au kumtendea Mungu mema anayostahili.Mwenyezi Mungu asinge umba MUME NA MKE.Na asinge mpa binadamu UTASHI wa kuelewa MEMA NA MABAYA.Usilazimishe utashi wako wewe uwe utashi wa kila mtu kwa mujibu wa tamaduni zetu za asili siyo za watu wengine kutoka nje wenye mazingira na historia tofauti na ya kwetu.HOTELI YENYE MASHARTI KAMA HAYO KWAFUNGULIE WAJOMBA ZAKO NA SHANGAZI ZAKO,lakini siyo katika miji yenye mchanganyiko wa watu wenye hulka mbalimbali.Ni ushauri tu japo mchungu.Biashara hiyo itakufa,labda kama kinauzwa kitu kingine humo,hatujui!Chui aliyevaa ngozi ya Kondoo.Moto unawasubiri Kiama kitakapo wadia.Shauri yako.
ReplyDeleteNyumba zote za wageni Tanzania zingekuwa na utaratibu kama huu, na kuufuata, nina hakika kwa kiwango kikubwa tu tungepunguza majanga mengi yanayotusumbua, hasa UKIMWI! Hongereni sana wenye hoteli!
ReplyDeleteDuh!!! safi sana,yaani "Tanzania Bila ukimwi" ingewezekana kama guest House,hotels n.k wanangefuata nyazo hizi.
ReplyDeleteJaribu kufirikiria Tanzania bila uzinzi,uasherati,usagaji,ushoga na "ufisadi jamii" kwanza kiuchumi kuna madhara makubwa sana mfano kampuni za cm,bars,maduka ya nguo,vyumba ya kupanga,maduka ya samani n.k HUYO JAMAA ANAFAAA SANA!! MUNGU IBARIKI TANZANIA
Hawa ndiyo wazinzi wakubwa sana!
ReplyDeleteSasa Michuzi ulipoenda Pemba ilikuwaje? Maana ninavyokujua, sijui ulilala wapi?
ReplyDeleteTueleze wengine tunaopanga safari za Pemba tuahirishe au twendelee na mipango ya kutembelea Pemba.
Nafikiri nimeelewa kwa nini watalii wengi hawaendi Pemba!!! Kila nikijitahidi kuinadi Pemba naona watalii hawataki kwenda na ukiwauliza hawasemi kwa nini hawataki kwenda,wanaishia kusema, thank you for the offer!Kumbeeeeee!!!! kuparamiana marufuku!!!!
Hivi kila mtu akipanga chumba chake halafu usiku mkanyemeleana vyumbani kuparamiana hapo jamaa michuzi wanasemaje?
Au hiyo hoteli ni kama Msikiti? kuna upande wa wanawake na wanaume? Maana kama vyumba vinatazamana vya wanawake na wanaume lazima mwanake aparamiwe tu hata kama kitandani qurani imewekwa kwa jinsi wengine tulivyo na nyege.
Watu wanaparamiana Makka wakienda hija itakuwa na Pemba?
Duuuuuuuu hapa jamaa kachemsha biashara imemshinda, afadhali ageuze nyumba ya ibada. Kisha inaonyesha yu mzinzi kiasi gani yaani kutembea watu wa jinsia tofauti kwake yeye ni haramu mshamba kweli. aende asome social business.
ReplyDeletemuelewemi mwenye hoteli amekataza ili kupunguza tatizo la ukimwi na sio kuiga tamaduni za nchi nyingine unzinzi ukizibitiwa kiasi hichi basi tazania itawezekana bila ya ukimwi lakini watanzania wenyewe tukiwa tunachukiwa na hatua kama hizi basi vijana wengi watateketea
ReplyDeletehawa watu sijui kama ni wafanyabiashara kweli.Kwanza kuna wanandoa wangapi nchini tanzania wana vyeti vya ndoa?Nadhani ni chini ya 10% wenye hivyo vyeti,wengi wetu tunachukuwana kimakubaliano kati pande mbili.kwa nini nchi ya Tanzania kuna sheria za ajabu?Serikali ya muungano inasema haifungamani na dini yoyote,lakini ona haya.
ReplyDeletesijui kama tutafika
hapa kuna kutetea ushoga(usenge) na usagaji.
ReplyDeletehuyu mwenye hii hotel basi alale humo yeye na mkewe na ndoa yao!!!
ReplyDeleteHow ignorant is this?
Aje na huku majumbani mwetu atupangie wageni wetu wanaokuja kututembelea wawe wamefunga ndoa!!!
ANON WA 11:08AM WEWE NDIO UNASIKITISHA,NAFIKIRI MAONI AMBAYO UNGEMPA NI KUA BIASHARA HAITOKUA NZURI KWASABABU KAZI KUBWA YA WENGI WETU NI UZINZI NA TUNATUMIA HOTEL NA GUEST HOUSE KWA HAYO,IDEA YA JAMAA NI NZURI NAFIKIRI ANAHITAJI PONGEZI KUFIKIRIA KITU KAMA HICHO KATIKA KUPUNGUZA UZINZI NA MARADHI.TAMADUNI UNAZO ZIZUNGUMZIA NA SEXUAL ACTIVITY ZETU NDIO ZINAZO TUPONZA.
ReplyDeleteKWA WALE WANA NDOA WENYE KUJALI AFYA NA KUPUNGUZA UZINIFU WAMPE SUPPORT HUYU JAMAA KWA KUTUMIA HUDUMA HII SIKU KAMA ZA VALENTINE, ANNIVERSARY AU JUST TO GET AWAY FROM YOUR FAMILY FOR A DAY, BASI WATUMIE HUDUMA YAO KWANI MAFISADI WENGI HAWATO WEZA KURUHUSIWA NA ITAKUA SABABU YA KUFUNGA BIASHARA HII.
Kwa mamneno mengine, tembeeni na vyeti vyenu vya ndoa hasa mkiwa safarini. Ila nahisi kapunguza wateja asilimia 50 kwa kuweka masharti hayo.
ReplyDeleteNaam,Mashaalah bado nchi yetu mema yapo...wahenga wasema...itachukua watu wema kutokufanya chochote ili mabaya yaenee!!!Hayo sio mawaidha ya kidini bali ni 'common sense'
ReplyDeleteHebu waangalie wahindi,ujamii bado strong...na sisi wanyaturu...kila kitu kiholela tu...aibu,hadhi,heshima ni maneno tu,wala hayazingatiwi.
Huyu biashara ataifunga si muda maana wapemba wenzake wanaomuunga mkono hawana aja ya kukodi vyumba hapo ukifuatilia wana maskani yao. Wageni wa kutoka nje asiwategemee maana sidhani kuna mtu anayetembea na vyeti vya ndoa kila aendapo.
ReplyDeleteUsusani kuna watu wengi ambao wameolewa kijadi na wanajulikana kihalali na familia zao kama mke na mume. Au anamaanisha watu wa group hii inabidi waende polisi kutafuta kitambulisho kabla ya kwenda kwenye guest yake basi polisi hawana kazi za maana za kufanya.
Hawezi kuzuia ukwimu kwa njia hii wakati tuliopo kila mtu anafahamu madhara ya ukimwi na asiwageuze watu kuwa watoto wadogo kila mtu anatumia akili. Hii siyo njia ya kuzuia magonjwa wala uasherati.
Nafikiri huyu angetafuta biashara nyingine na siyo ya guest maana naona haimfai hata kidogo.
Mazee, hiyo hapo ni nyumba ya wageni na siyo nyumba ya starehe. Kwa mgeni mwenye nia ya kutafuta mahala pa kulala tuu masharti hayo siyo magumu. Kwa wale ambao wana mahitaji mengine zaidi ya kulala ndo watakaosumbuka ma hayo masharti.
ReplyDeleteha ha ha ha sasa mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke? wao wataruhusiwa?
ReplyDeletesheria hazisaidii kama watu wanataka kuibiana wataiba tu...na ndoa za mkeka nazo zina marriage certificates?
kwanza wabongo hata siku moja uwaone wanawapeleka wake zao sehemu za kustarehe ni miujiza...
Je wachangiaji wanaelewa kwamba maambukizi ya UKIMWI visiwani Zanzibar na Pemba kwao hawa tunaowaita wamechelewa kuwa ni asilimia 0.7 wakati sehemu nyengine "zilizoendelea" nchini Tanzania maambukizi ni zaidi ya asilimia kumi?
ReplyDeletemtasema sana mradi mtasema na litawaumaa...mwenye kuchukia na apasuke..!!
ReplyDeletehiyo ni nyumba ya wageni na kwa mgeni mwenye kutafuta mahali pa kulala hiyo sheria si ngumu km kuna mmoja alosema juu hapo!haikukusudiwa kuwa sehem ya kustarehe.its as simple as that..
keep it up PEMBA oyeee...
na ndo mana maambukizi ya ukimwi ni kidog sana PEMBA ukilinganisha na sehem nyengine zenye waharibifu na mafisadi nchini mwetu.
alonuna na apasuke na hotel ndo kwanza inaendelea uhudumia wala haijaanza jana hiyo ni siku nyingi tuu inaendelea na huduma..
mtajiju haters...
SAFI SANA MOYO WA IMANI KWA MWENYE HOTEL/GESTI LAITI UNGEIGWA NA WENYE MAGESTI:
ReplyDeleteLazima ukiingia huko kufanya mavituuz vinakuwa vitamu. Vya kuiba vitamu au siyo?
ReplyDeleteuku kwetu Tandale baba na mama pekee ndo wana chumba.mimu na dada zangu tunalala sebuleni.Baba na mama inabidi na sie mtutafutie vyeti vya ndoa kwa kutulaza chumba kimoja.teh teh teh
ReplyDeletePemba itafika wakati hata kuingia kwenye boti yenu mpaka uwe na vyeti vya ndoa.
Mpemba wangu hataki kubeba dhambi za watu!!!
ReplyDeleteRaha mule nyinyi dhambi hapati yeye, no way, kagoma!!!
Mimi nimependa hiyo ili wenye wake tu ndio tufike hapo!!!
Wahuni kaeni chonjo.
Huyo mwenye hoteli mpemba kweli au wa kufoji?Msiwapakazie wapemba wangu jamani.Ushawahi kusikia ile hadisi ya Mpemba aliyesafiri behewa moja na Mchaga wakitoka DSM kuelekea Mwanza,kila mmoja kaketi pembezoni kabisa mwa chumba akimhofia mwenzake?Kama hujasikia basi ulizia kwa wenzio waliokuzidi maarifa.Kalaga Baho na Ubozi Wako,Mwee!Ukiona kibao kama kile nje ya hoteli basi ujue jamaa wa Bushi bado anashangaa Mataa ya mjini!
ReplyDeleteJmbo lolote lililo zuri hupongezwa, mimi ninamsifu mwenye hoteli hiyo kwani mbali na kuwa anafanya biashara hana tamaa ya pesa na anajali utu.
ReplyDeleteKama walivyotangulia wachangiaji wengine masharti hayo kwa wageni ni mepesi kabisa lakini kwa waasherati na walevi ni magumu. Kama kweli unakwenda kama mgeni na umeongozana na mumeo au mkeo mnachotakiwa ni kuwa na vielelezo vya kumridhisha mpokea wageni. Kama una aina yeyote ya kileo basi hapo sio mahali pako.
Jitihada za kutokomeza maovu zinahitaji mchango wa kila mwanajamii popote pale alipo.
Hii bomba sana maadili lazima yalindwe hata kama wengine hawataki, na anaesema huyo jamaa hafanyi biashara kachelewa, nazijua hoteli kubwa kubwa hapa ughaibuni ambazo zimeamua kuweka "dry policy" yaani no pombe na biashara imewachanganyia kinamna ingawa milevi inalalamika.
ReplyDeleteWatu kama hawa ndio wawe wa kuigwa sio celebrities wakueneza uozo kwa jamii.
Kitu kizuri kinabaki kuwa kizuri hata kisiposifiwa na yeyote. Na kitu kibaya kinabaki kuwa kibaya hata kama kikihusudiwa na watu wote.
ReplyDeleteNampongeza mwenye hoteli kuonesha ujasiri wa kuogelea dhidi ya mkondo kwani zuio lake litasifiwa na wachache kama sio kuwakosa kabisa kabisa.
Afadhali kuwasha mshumaa mmoja (ukapata mwanga kidogo) kuliko kubaki gizani ukilalama. Shikilia uzi huo huo, ndugu, wengine watafuata baada ya kuona faida yake; na wengine baada ya kuonja madhara ya maisha ya ufuska.