Mr Michu,

Nimesikitika sana kwa matukio ya mioto yanayoendele kutokea hapa nchini. Takwimu zinonesha kuwa fedha nyingi sana zimepotea kwa majanga ya moto, na zaidi maisha ya watu. Nakutumia picha hii nilipokuwa natoa mafunzo kwa tenants (wapangaji) wa PPF tower jinsi ya kutumia vifaa vya kuzimia moto. Vifaa hivi ni bei rahisi sana, na vinapatikana kwa urahisi sana.


Kwa kweli mioto mingi mnayoiona ingeweza kuzuiwa kama kungekuwa na FIRE EXTINGUISHERS.


Kwa mahitaji ya training na vifaa vyenyewe

nipigie +255 784 442 806.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Unajua watu tunachulikia sio kitu serious lakini jamaa anafanya la maana angalia hapo kuna watu wapo tu hawasikilizi body language tells everything my cousin last week he lost everything alichofanikiwa ni uhai wao tu na nimtu ambae alijitahidi sana kujenga nyumba yake kwa maisha ya shida sana ni mtu mwenye kipato cha chini hakuweza kutoa kitu na ni umeme ulisababisha .anyway tunashukuru ni wazima

    ReplyDelete
  2. Big up sana kwa kutufahamisha. ni kweli watu wengi hawaoni umhimu wa kuwa na hivyo vifaa vya kuzimia moto, vina saidia sana kwa huduma ya kwanza, jamii ya kitanzania haijatilia kwa makini sana vifaa hivyo, serikali ni muda muafaka sasa kufuatilia kwa ukaribu sheria inayosisitiza umuhimu wa kuwa na hivi vifaa vya kuzimia moto. ninakufahamu sana bwana mdogo na kampuni yenu iko juu kwa usambazaji wa vifaa hivyo, endeleeni kujitangaza watu wapone dhidi ya janga hili.

    ReplyDelete
  3. yes kwani mnapatikana wapi nyie. watu walazimishe kuwa na hizo fire extinguisher kilia sehemu mpaka majumbani kuweza kuzibiti hiyo mioto.

    ReplyDelete
  4. KAMA KILA MTANZANIA ANGEFANYA HOMEWORK YAKE(KUTOA MCHANGO WAKO KWA JAMII KUTOKANA NA UJUZI AMA TAALUMA ULIYONAYO)KAMA HUYO BWANA ANAVOFANYA HAPO BASI TUNGEKUA MBALI SANA! AKSANTE MDAU
    mdau ufini!

    ReplyDelete
  5. Duu! Huyo dogo mi namjua nilisha mwona kwenye TV akimwaga utirio kuhusu mambo ya usalama wa moto. Ni kweli vitu hivyo ni muhimu sana nilimsikiliza ikabidi nikatafute kwa ajili ya gari yangu. Wadau kazi kwenu mi gari yangu kwa sasa iko poa.

    ReplyDelete
  6. Jamani mioto ni kiswahili fasaha?

    ReplyDelete
  7. HUKU UINGEREZA WATU WANA HAMASISHWA KUTIA SMOKE ALARMS,INFACT COUNCILS ZINA WATILIA WAPANGAJI WAO HIZI SMOKE ALARMS FOR FREE,NAJUA KWA NYUMBANI SERIKALI ITAKUA HAIWEZEKANI KUWAWEKEA FOR FREE,LAKINI INGE FANYA CAMPAIGN YAKUELIMISHA WATU UMUHIMU WA SMOKE ALARMS NA KITENDO WANACHO FANYA HAWA JAMAA NI MUHIMU SANA NA PIA HONGERENI.PIA NINGEPENDA KUONGEZEA JUU YA HAO WAZIMA MOTO NAFIKIRI HUDUMA HIYO HAIFANYI KAZI KAMA INAVYOTAKIWA,NAFIKIRI WAZIMA MOTO NA POLISI WA TANZANIA HAWANA TOFAUTI WANAWADIA MWISHO WA TUKIO,KWA MAONI YANGU MIMI WANACHANGIA HALI KUA NGUMU.

    ReplyDelete
  8. Duh...kuna jamaa wenye tai na vitambi wamsikiliza kwa makini huto instrakta...huko tairi likiungua,lakini je hilo tairi likipamba moto,wenzangu mtaweza kupiga sitini???

    ReplyDelete
  9. Safi Sana Moshi!! Kazi nzuri! Jamii inahitaji watu wa namna yako. Maisha ya wengi yanapotea kila siku na pengine ni kwa vile elimu ya namna hii haitolewi kwa jamii yote. Katika nchi zilizoendelea somo la kuzima moto lazima lifundishwe shuleni na mara nyingi huwa kunakuwa na marudio ya mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa watu wanakumbuka. Mimi napendekeza hili suala livaliwe njuga na elimu hii iwafikie watanzania wote kwani moto hautoi taarifa. Unaweza kutokea wakati wowote. Chombo cha taifa cha kudhibiti moto mara nyingi hakipo tayari majanga yanapotokea! huenda ni ukosefu wa vifaa elimu, uvivu au uzembe mimi sijui. Kwa hiyo kuliko kutegemea njia hiyo moja tu ambayo haina uhakika sana ni heri watu wafundishwe namna ya kuzima moto na namna ya kupata vifaa vya kuzimia moto kwa gharama watakayoimudu ili kuokoa maisha.
    najua wengi wa watanzania hawana bima ya moto hivyo ni bora basi wafundishwe namna ya kuuzima ili wasipate hasara ya mali na maisha
    Naomba kuwasilisha

    ReplyDelete
  10. waswahili bwana,kwani hakuna sehemu wanayoweza kuunguza hilo tairi mpaka wachafue barabara...uchafu mtupu!

    ReplyDelete
  11. Nina appreciate hayo mafunzo kwa sababu siku elimu inaweza kuwa kinga ila huyo mwalimu naye kaniangusha kwa kitu kimoja.

    Hakuvaa nguo rasmi za zima moto, kama hayuko serious kuvaa vazi linaloendana na somo vipi tutegemee wanaomsikiliza wawe serious?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...