Home
Unlabelled
mama wa shoka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
haya wadau anzeni kutafuta kina mama wote wa shoka, tanzania na madada pia.
ReplyDeleteinaelekea amejitahidi kwa mgogoro wa kenya, alikua na mkapa kule.
ReplyDeleteMafisadi wahaha
ReplyDelete2008-02-19 15:30:42
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Baadhi ya vigogo wanaohusishwa na skendo la utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni hewa ya Richmond, imeelezwa kuwa hivi sasa wanahaha kupoteza kumbukumbu zinazoweza kuwatia hatiani.
Imedaiwa kuwa watu hao ambao ni watendaji tena wenye nafasi kubwa tu Serikalini tangu dili hilo lilipoanikwa wamekuwa bize kuulizia wafanyakazi walio chini yao zilipo baadhi ya nyaraka fulani.
``Yaani kaka watu wanahaha hapa si mchezo. Ukimuuliza mtu anatafuta faili fulani kwa sababu gani, hakujibu,`` chanzo chetu kutoka wizara ya Nishati na Madini kimeliambia gazeti hili.
Kadhalika imedaiwa kuwa mawasiliano ya karibu yamekuwa yakifanywa kwa siri kubwa mno kati ya baadhi ya vigogo wa wizara ya wengine wa Tanesco.
Wakati hayo yakiendelea, inadaiwa kuwa makomandoo walioshupalia sakata hilo hadi ikaundwa tume ya kuchunguza kashfa hiyo, wameapa kupigana kufa na kupona hadi wale wote waliohusika wawajibishwe ama wachukuliwe hatua za kisheria.
``Inasemekana akina Slaa wameapa kufanya kila wawezalo kuhakikisha wale wote waliohusika na kashfa hiyo wanang`olewa madarakani,`` chanzo chetu kimedai.
Sakata hilo la Richmond lilivaliwa njuga na wabunge wa kambi ya upinzani wakiongozwa na mbunge wa Karatu kupitia Chadema, Dk. Wilbroad Slaa.
Kamati ya uchunguzi wa mkataba bomu wa Richmond iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe, ilipendekeza kuwa baadhi ya vigogo waliohusika na kashafa hiyo wawajibishwe.
Katika sakata hilo, aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa aliamua kujiuzulu na kusababisha Rais Jakaya Kikwete kulivunja baraza zima la mawaziri, kabla ya kuliunda upya.
Katika Baraza jipya lililoundwa mawaziri kadhaa walipoteza ulaji huku wengine wakiula.
Grace Machel (aka Graça Simbine and now Graca Machel-Mandela)Ni Mwanamama pekee Africa kuwa "1st lady" kwenye nchi mbili tofauti. Alikuwa mke wa aliyekuwa Rais wa Msumbiji (aka Mozambique)Samora Moses Machel mpaka Rais Machel alipofariki kwenye ajali ya ndege 1986, then akawa wife wa Mzee Nelson Rolihlahla Mandela ("aka Mandiba")na hivyo kuwa 1st Lady wa SA. Inafahamika kwamba Mzee Madiba hakung'ang'ania madaraka, alijing'atua muda wake ulipoisha (have u heard "behind a successful man there is..."?). Nafikiri kuitwa/kupata nafasi ya kuwa kwenye timu ya ushuhulishi wa gogoro la Kenya kunatokana na kuwa nguli kwenye mambo ya siasa ya zone yetu ya Africa. Kwa wale mnaokumbuka, FRELIMO (chama kilichoipatia uhuru Msumbiji) ilizaliwa ndani ya Dar 1962 baada ya muungano wa vyama vitatu:Mozambican African National Union (MANU), National Democratic Union of Mozambique (UDENAMO), and the National African Union of Independent Mozambique (UNAMI)...Edward Mondlane alichaguliwa kuwa Rais wao, ambaye kwa bahati mbaya aliuliwa ndani ya Dar (inaaminika kwamba lilikuwa ni Bomu lilifichwa kwenye kitabu kwenye hoteli moja maaruf mpaka leo).Matokeo ya kuanzishwa kwa FRELIMO ni wao kuongoza nchi na yeye (Mama Machel) kuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni mwaka 1975. Aliolewa na Rais Machel mwaka huo huo (na kumlazimu kujivua u-waziri, na kuanza kufanya kazi na UN kwenye report iliyoitwa " United Nations Report on the Impact of Armed Conflict on Children"). Katika tume hii ya Kenya, anasaidiana na Mzee wetu Ben Mkapa, (ambaye alikuwa Waziri wetu wa Mambo ya Nje 1977-80, then 1984-90). Mzumbiji ilipata uhuru 1975 na wengi mnakumbuka jinsi Nyerere alivyompiga tafu la shoka Samora,it should, then, be logical to think Mkapa alikuwa 'bolizozo" wa shuhuli hiyo nyeti na hatari, and hence kuna mutual understanding and respect between them, and between freedom fighters and democracy keepers ("at any cost")in Africa. Rais wao wa sasa, Armando Guebuza alikuwa Waziri wa Ndani (interior minister) chini ya rais was wa kwanza, hayati Machel. Kwa nini yeye na Kenya?..depend on how you look at the glass (half empty or half full) Kenya mambo yakiendelea kuharibika na pengine kuvuka mpaka wao wa kusini (TZ) mambo yatatuharibikia sisi (as East Africa Community)...so wanatakiwa ma-Heavy weight waliocheza "kamanyola bila jasho" enzi hizo,...that's when Mama Machel, Mzee Ben na Mzee Annan wanapoingia (and it should be logical to think there are others behind the doors sharing minutes)...Bongo yetu imekuwa mstari wa mbele wa kuhakisha ukombozi wa bara la Africa unafanikiwa, na pale wachache wanapolete fyoko-nyoko na demokrasia tutaendelea ku-take charge kuhakikisha waafrika wenzetu wote wana amani. Tutasemezana Arusha aka "Geneva of Africa" (case studies:Rwanda, Burundi, S. Africa) otherwise tutawafuata kwenye ardhi yao wenyewe: case Study:Uganda, Zimbambwe and Kenya as of now. Mungu Ibariki Jamhuri yetu ya Muungano wa TZ, Mungu Ibariki Afrika! Kaka Michu, naomba kuwakilisha. Ndimi Kaka yenu.
ReplyDeleteMumewe Graca inahisiwa kuwa aliuawa na Africa ya kusini baada ya ndege yake kutunguliwa na waafrika ya kusini baada ya siri kutoka zikieleza ndege atakayosafiria.
ReplyDeleteHuyu mama baadaye baada ya kifo cha mumewe akaolewa Huko huko Afrika ya kusini tena na Raisi.
Hivi nani alivujisha siri za Marehemu Samora hadi akatunguliwa na kuuawa wakati safari yake ilikuwa siri? Wataalamu wa historia tusaidiane.
....Sasa basi, kwa sababu hizo zoote we kaka yetu uliyezi-google habari hizo, ndio maana Pres.Mandela au "Madiba" alivyotoka gerezani Roben Island alipewa habari hizo nyeti za ukiukwaji wa habari na unyama uliofanywa na mmoja wa viongozi wa serikali ya makaburu hatimae kusababisha kifo cha "comrade" mwenzake, ndio hapo baada ya kuvunjika kwa ndoa yake!!! akaona ni heshma kubwa kumuomba mama Graca awe kipenzi chake kwa muda uliobakia wa maisha yake.Na faida yake ni kuwa mama Graca ataweza kusamehe/kusahau dhambi zilizosababishwa na Serikali ya A.Kusini ya kifo cha mumewe wa awali kuwa ni ndoto mbaya aliyoiota! :)
ReplyDeletenawasilisha
Mdau,
Ughaibuni
Wadau naomba kutoka nje ya mada.Hivi Condolezza Rice ameolewa? au ana mtoto? Naomba kujua
ReplyDeleteHuyu Mama atamvunja mzee Nelson kiuno,manake anaonekana anahusudu kamchezo.Amejitahidi kenya lakini.Mwenye history ya elimu yake pliiz ai'post'
ReplyDeleteAnon wa 8:23am Thank you very much for the short history very interesting,wengine tumemjua huyu mama kwa kuolewa kwake na Mandela,kuishi nje ya nchi muda mrefu pia ina sababisha kutokujua siasa za Afrika zinaendaje.Kwahiyo watu wenye kujua mambo tuelimisheni sie tulio mbali.
ReplyDeleteAnony wa 3:40pm
ReplyDeleteKondoleza kaolewa na mumewe ni serikali ya Joji Kichaka,na inasemekana kuwa ni mwanamke mtiifu na aliyefundika maana chochote anachotumwa na mumewe huenda kutekeleza haijalishi kama kinaweka uhai wake mashakani au la? sehemu zote zenye vita huwaanaagizwa yeye aende kufuatilia, inasikitisha sana manake inaonekana huyu mumewe hamthamini kama wanawake wengine wengi wanavyothaminiwa. kuhusu mtoto sina hakika. Ila nitafatilia halafu nitakujulisha