Waziri mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda
Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda kabla ya kutangazwa kuwa kaula
wabunge wakimpongeza waziri mkuu mpya Mizengo Kayanza Peter Pinda

Wapendwa wahariri, waandishi, wanahabari wote,

Napenda kuwafahamisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, leo saa 5 asubuhi, anatarajia kumuapisha Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda, kushika rasmi wadhifa wake mpya wa Waziri Mkuu wa Tanzania katika Ikulu ndogo ya Chamwino.

Nachukua fursa hii kuwaalika na kuwakaribisha waandishi na wawakilishi wa vyombo vyote vya habari.

Tunawaomba mtakapofika katika lango kuu mjitambulishe kwa kuonyesha vitambulisho vyenu rasmi vya vyombo vya habari mnavyowakilisha na kufanyia kazi.

Asanteni na karibuni,

Wenu,

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
8 Februari, 2008

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Haya shughuli imeanza jamani!
    Ndugu zangu tuombe MUNGU aibariki TZ kwani huyo anayeapishwa si malaika anyetarajiwa kumaliza matatizo ya nchi yetu......!Tusaidiane sote kuwaumbua MAFISADI!!!!

    MTANZANIA, MD-USA

    ReplyDelete
  2. Jamani lakini tuacheni utani..huyu Pinda sura yake haijatulia kabisa...duh!

    ReplyDelete
  3. Mheshimiwa Mizengo Pinda tunakupa pongezi kwa kukabidhiwa wadhifa huo mkubwa wa kuwa Waziri Mkuu.
    Baada ya pongezi hizo, kufuatana na historia yako ya kikazi kuwa ulikuwa Ikulu ofisi ya katibu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa TZ miaka mingi takwimu hapo chini:
    Mh JK Nyerere miaka 7
    Mh AH Mwinyi miaka 10
    Mh BW Mkapa miaka 3
    ulikuwepo na kushuhudia hapo Ikulu viongozi wengi waandamizi waliokuwa wanakula kiapo kuwa watatekeleza majukumu yao vizuri mbele ya hao waheshimiwa marais wastaafu.Pia tulikuona ktk picha lukuki za magazeti ktk matukio hayo nyeti pamoja na wateuliwa wakiapa kiapo mbele ya Rais Ikulu.
    Kutokana na hilo utakuwa unaufahamu mkubwa kuhusu nani atafaa kuwapo na wewe ktk baraza la mawaziri. Hivyo utatumia uzoefu wako na busara kumshauri Rais wa sasa Mh Rais Kikwete ni kina nani watafaa kuwapo ktk baraza jipya kwani umeshaona utendaji wao baada ya viapo. Yetu Macho Tutatazama mwanzo wako wa jukumu hili zito la nani atakuwemo ktk baraza jipya la mawaziri.
    Mdau
    Senior Junior
    London.

    ReplyDelete
  4. Kaka Michuzi nakusifu sana kwa habari ulizotuletea kweli unajituma hata mpaka wakati wa usiku sana!
    Lakini naomba nikusahihishe moja tu ambalo ni nyeti hapa.

    Umeandika hivi

    "Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda kabla ya kutangazwa kuwa kaula"

    Kweli nimesikitishwa sana na hii kauli maana laiti ungefikiri kidogo ungeona kuwa ni kwa ajili ya neno hilo la KUULA, Umma kupitia mifumo ya nchi leo umemkataa EL na kusababisha huyu Pinda kupatikana!

    Kama ametangazwa ili aule basi JK hajafanya kitu wala kamati makini ya bunge haikufanya kitu wala wananchi kushangilia, mnashangilia mauti yenu tena!

    Ni kwa mtazamo huu baadhi ya wananchi huwa wanalazimisha kukarimiwa kupita kiasi na wagombea mfano ubunge, udiwani n.k kwani husema tunampa kura akaule hivyo tumalizane mapema.

    Kama kweli tuko serious na kuupiga vita ufisadi basi wananchi tuanze kwa kubadili mtizamo wetu juu ya viongozi wetu. Tuwaone kuwa ni wenzetu ambao tunawapa dhamana ya kututumikia zaidi kuliko kuwa mabosi, ya kuhudumia zaidi kuliko kuhudumiwa, ya kutoa zaidi (alichonacho)kwa nchi yake kuliko kuchota toka nchini.

    Michu nasema tena kuwa samahani kwa sahihisho hili na pengine wengine waweza kutofautiana nami. Sina haja ya kukwambia kuwa usinibanie maana hujawahi kunifanyia hivyo.

    ReplyDelete
  5. MPWA MICHUZI SI UNIPE ID NIKAWAKILISHE BULOGU MSHKAJI?

    ReplyDelete
  6. Kazi imebakia baraza la mawaziri sasa. Sidhani kama ana haja ya kuunda baraza kubwa tena kama last time maana likiwa kubwa hata ufuatiliaji wa mambo hauwi wa ufanisi kama ilivyosemekanika kuwa mawaziri ni wengi ili kuleta ufanisi.Mi naona ni hakuna ufanisi na matumizi ni makubwa zaidi. Nchi ni nyingi tu zenye mawaziri si zaidi ya 20 na wana mafanikio makubwa mno. Ni jinsi ya kujipanga tu na hizo wizara chache then wakatumia wakurugenzi au makamishina au hata ma-PS ndani idara za wizara badala ya kuweka mawaziri wa ziada, kwani hili pia litasaidia kukata mishahara minono wanayolipwa mawaziri wasio na shughuli. Wenzao kama japan ndo wanafanya hivo na hebu uone maendeleo waliyonayo ni ya aina gani nadhani kila mtu anajua hilo na hata wabunge wanajua hilo pia ila sielewi ni kwanini inakuwa ngumu kufuata mifano ya nje na yenye mafanikio.

    Mdau mpenda nchi

    ReplyDelete
  7. Duh!! huyu ataweza kasi mpya? na uzee wote huo?

    ReplyDelete
  8. aaah mbona ni mtu mzima sana huyu bwana mkubwa? babu huyu ataweza kwenda na sayansi na teknojia? cha msingi afanye yale anayotakiwa fanya.. mungu ibariki bongo yetu..

    ReplyDelete
  9. ASANTE MDAU KWA KUIKATAA NENO "KUULA", NILIKUWA NAINGIA HAPA KUKEMEA HILO, KINGIA KZINI SIO KUULA, NI KUJENGA NCHI. TNATAK MBADILIKO YA KWELI.

    ReplyDelete
  10. michuzi nauliza yule kamanda wapolisi TIBAIGANA ni ndugu na huyu PINDA waziri mkuu mbona wamefanana sana.

    ReplyDelete
  11. BUTT KISSERS! Sasa atapata na mabibi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...